SIMBA SC ITAFANYA MKUTANO WAKE WA WANACHAMA JUMAPILI WIKI HII
Klabu ya Simba itafanya mkutano wa
wanachama wake Jumapili (Machi 16 mwaka huu) kwa ajili ya kuifanyia marekebisho
Katiba yao.
Nachukua fursa hii kuwatakia kila la
kheri katika mkutano huo ambao ni muhimu katika kuhakikisha klabu yao inapiga
hatua katika maendeleo ya mpira wa miguu na ustawi wake kwa ujumla.
TAARIFA KUTOKA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI TFF LEO
SEMINA YA
WAAMUZI YAANZA DAR
Semina ya siku mbili kwa waamuzi wenye beji za
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na wale wa ngazi ya juu nchini
(elite) kwa robo ya kwanza ya mwaka huu inaanza kesho (Machi 15 mwaka huu)
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
BREAKIN NEWZZZ:- RAIS AWAAPISHA RASMI VIONGOZI WA BUNGE LA KATIBA SASA HIVI LIVE!!
Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Bw, Yahya Khamis Hamad akiapa mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete Leo Mjini Dodoma. |
Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Yahya Khamis Hamad akisaini Kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete Leo Mjini Dodoma. |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akisaini kiapo baada ya kumuapisha Katibu bunge Bw. Yahya Khamis Hamad (mbele aliyesimama) |
UHURU WA KUPENDA NA KUPENDWA UNAVYOATHIRI PENDO HURIA
Uhuru
wa kupenda au kupendwa ni moja ya haki binadamu ambayo kama zilivyo
haki yoyote ile inatakiwa iheshimiwe kwa sababu kila mmoja ana haki ya
kuoensha hisia zake katika kile ambacho moyo wake unaouhusudu.
Uhuru huu wakati mwengine
hutafsiriwa kutokana na Dini, kabila au utamaduni wa jamii kwa mujibu wa sheria
za nchi au eneo husika.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOANI IRINGA LEO
Kamanda
wa polisi mkoani Iringa Kamishina Msaidizi Ramadhan Mungi akitoa
taarifa kwa waandishi wa habari asubuhi hii mjini Iringa wakati
alipozungumza nao katika ofisi zake zilizopo jengo la mkuu wa mkoa huo.
……………………………………………………………………………
Ndugu waandishi wa habari , kwa niaba ya askari Polisi wa Mkoa wa Iringa, nitumie fursa hii kuwakaribisha hapa ofisini kwetu.
Ndugu zangu tumeitana hapa asubuhi hii ili niweze kuwapa
taarifa ya usalama katika Mkoa wetu wa Iringa hususani katika Jimbo la
Kalenga katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi wa Jimbo la Kalenga
na usalama wa siku ya uchaguzi wenyewe.Ili iwe rahisi kueleweka taarifa
hii nitaitoa kwa kifupi sana kwa kuigawa katika maeneo matatu.
HELKOPTA MARUFUKU KWENYE ANGA LA KALENGA SIKU YA UCHAGUZI, WALIOTUMWA KUFANYA FUJO KUKIONA
Kamanda Mungi akizungumza leo |
Na Bashir Nkoromo, Iringa
JESHI
la Polisi, limepiga marufuku chama chochote kurusha helkopta kwenye
anga la jimbo la Kalenga, na limeahidi kushughulikia kikamilifu kundi au
yeyote atakayejaribu kusababisha au kufanya vujo wakati wa uchaguzi na
matokeo ya uchaguzi huo.
Onyo hilo limetolewa asubuhi hii na Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi, wakati akieleza Polisi ilivyojiandaa kuhakikisha uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, unafanyika kwa amani na utulivu, Jumapili hii, ya Marchi 16, 2014.
Onyo hilo limetolewa asubuhi hii na Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi, wakati akieleza Polisi ilivyojiandaa kuhakikisha uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, unafanyika kwa amani na utulivu, Jumapili hii, ya Marchi 16, 2014.
Wafanyabiashara na wachimbaji Tanzania walifikia soko la madini Kimataifa
Wafanybiashara
na Wachimbaji waliowakilisha wenzao katika Maonesho ya 53 ya Bangkok
Gems and Jewelry Fair’ wakiwasikiliza wageni waliotembelea banda la
Tanzania kuona aina mbali mbali za madini ya Vito na Usonara
yaliyowasilishwa katika maonesho hayo.
Mthamini
wa madini kutoka idara ya Uthamini wa madini ya Almas (TANSORT) Bw.
Edward Rweymamu (katikati), akiwaeleza jambo wageni waliotembelea banda
la Tanzania katika maonesho hayo. Wanaoshuhudia wa kwanza kushoto ni
Mratibu kutoka Kituo cha ‘Tanzania Geomological Center’ (TGC), Bw. Musa
Shanyangi na wa kwanza kulia ni Mthamini wa Madini kutoka Idara ya
uthamini madini ya almsi (TANSORT), Wizara ya Nishati na Madini Bibi.
Teddy Goliama.
Mwandishi
wa habari hii (Kushoto) Asteria Muhozya, akifanya mahojiano na
wafanyabiashara wa madini walioshiriki maonesho ya Vito na Usonara ili
kutaka kujua namna walivyofaidika na ushiriki wao katika maonesho hayo.
Anayeongea ni Bw. Jeremiah Simioni Mfanyabiashara kutoka Kampuni ya Tom
Gems na katikati ni Mfanyabiashara Mhe. Dorah Mushi kutoka Kampuni ya
H.B Mining Company.
…………………………………………………………………..
Na Asteria Muhozya, Bangkok
Wafanyabiashara
na wachimbaji wa madini Tanzania wameelezea kufurahishwa na ushiriki
wao katika maonesho ya 53 ya madini ya vito na usonara, Bangkok,
kutokana na kupata fursa ya kulifikia soko la madini kimataifa.
Subscribe to:
Posts (Atom)