MARTIN KADINDA: ‘KUMMENEJI’ WEMA SHUGHULI PEVU

MARTIN KADINDA: ‘KUMMENEJI’ WEMA SHUGHULI PEVU

April 19, 2014

MENEJA wa Wema Isaac Sepetu, Martin Kadinda amekiri kuwa kumsimamia ‘kummeneji’ staa huyo ni shughuli pevu kwani ana tabia ya kubadilika.

Meneja wa Wema Isaac Sepetu, Martin Kadinda akiwa na na Staa huyo.
Alisema Wema anahitahi hesabu kwani kuna vitu unaweza kupanga naye lakini akashindwa kutimiza kutokana na hisia zake binafsi.
“Kuna wakati unaweza kumwambia usitoke hadi nikuruhusu lakini cha ajabu unakuja kushtukia mwenzio yupo mtaani jambo ambalo hamkukubaliana, ni ngumu we’ acha tu,” alisema Martin Kadinda ambaye pia ni mbunifu wa mavazi.

AZAM FC WAKABIDHIWA MWALI WAO...PATI LINAENDELEA CHAMAZI

April 19, 2014


Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) akimkabidhi Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Nahodha wa Azam FC, John Bocco jioni hii baada ya kuifunga bao 1-0 JKT Ruvu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Mabingwa wakisherehekea na taji lao, sherehe za ubingwa zinaanza sasa Complex hadi usiku wa manane
Mwenye timu; Mmoja wa Wakurugenzi wa Azam FC, Yussuf Bakhresa akifuarhia Uwanja wa Azam Complex leo
Watoto Said kulia na Idha kushoto wakiwa Uwanja wa Azam Complex

COASTAL UNION YAKUBALI KICHAPO TOKA KWA KAGERA SUGAR UWANJA WAO WA NYUMBANI HII LEO,YALALA 1-0

April 19, 2014
KOCHA MKUU WA TIMU YA COASTAL UNION YA TANGA,YUSUPH CHIPOO AKITETE JAMBO NA WACHEZAJI WAKE WAKATI MECHI KATI YAO NA KAGERA SUGAR IKIENDELE LEO KWENYE DIMBA LA CCM MKWAKWANI.

DAKTARI WA TIMU YA COASTAL UNION AKIMTOA NJE YA UWANJA RAZACK KHALIFANI LEO MARA BAADA YA KUUMIA KWENYE MECHI YAO NA KAGERA SUGAR IKIWA NI LALA SALAMA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA AMBAPO KAGERA WALIIBUKA NA USHINDI WA BAO 1-0

HAPA AKIPATA MATIBABU

*DIDA, MANULA, SAMATTA, ULIMWENGU NI MIONGONI MWA 19 WALIOITWA KUUNGANA NA 16 WA TAIFA STARS

April 19, 2014

Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Salum Mayanga ametangaza wachezaji wengine 23 watakaoingia kambini kesho (Aprili 20 mwaka huu) kuungana na 16 waliotajwa awali kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi itakayochezwa Aprili 26 mwaka huu.
Wachezaji walioitwa ni makipa Aishi Manula (Azam), Deogratias Munishi (Yanga) na Mwadili Ali (Azam). Mabeki ni Abdi Banda (Coastal Union), Aidan Michael (Ruvu Shooting), Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Hassan Mwasapili (Mbeya City), Kelvin Yondani na Said Moradi (Azam).
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Frank Domayo (Yanga), Himid Mao (Azam) na Jonas Mkude (Simba).
Washambuliaji ni Athanas Mdamu (Alliance), Haruna Chanongo (Simba), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Khamis Mcha (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Markhiya, Qatar), Ramadhan Singano (Simba), Simon Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
Wachezaji walioitwa kutoka katika kikosi cha maboresho ni kipa Benedicto Tinoko Mlekwa (Mara), mabeki wa kati; Emma Namwondo Simwanda (Temeke) na Joram Nason Mgeveje (Iringa). Walinzi wa pembeni ni Omari Ally Kindamba (Temeke), Edward Peter Mayunga (Kaskazini Pemba) na Shiraz Abdallah Sozigwa (Ilala).
Viungo ni Yusuf Suleiman Mlipili (Temeke), Said Juma Ally (Mjini Magharibi), Abubakar Ally Mohamed (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magona (Shinyanga), Omari Athumani Nyenje (Mtwara) na Chunga Said Zito (Manyara).
Washambuliaji ni Mohammed Seif Saidi (Kusini Pemba), Ayoub Kasim Lipati (Ilala), Abdurahman Othman Ally (Mjini Magharibi), Paul Michael Bundara (Ilala). Wachezaji wa U 20 ni Mbwana Mshindo Musa (Tanga) na Bayaga Athanas Fabian (Mbeya).

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaingia kambini kwenye hoteli ya Kunduchi Beach.