JK AOMBA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA KUKABILI UJANGILI

JK AOMBA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA KUKABILI UJANGILI

November 07, 2014
GU9A8625
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye ufunguzi wa mkutano mkubwa wa kudhibiti ujangili na hifadhi endelevu ya wanyamapori uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha. (Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog)
Na Mwandishi Wetu
RAIS Jakaya Kikwete ameitaka jumuiya ya kimataifa kushirikiana na Tanzania katika kukabiliana na majangili wanaomaliza tembo kwa lengo la kupata pembe zao. Alisema kutokana na biashara nzuri ya pembe hiuzo duniani majangili wamekuwa na soko tayari kiasi cha kuendeleza vitendo vyao.
Alisema mitandao iliyopo inawezesha kuuawa kwa tembo hao na kufikishwa bidhaa za pembe katika soko haramu ambalo lipo duniani na hivyo bila ushirikiano wa kimataifa wanyama hao ambao ni urithi wa dunia watatoweka kabisa katika miaka ijayo. Amesema takwimu zilizopo sasa nchini za tembo zinatisha.
Alisema mathalani kwa ujangili pekee kwenye mfumo wa ekolojia wa Selou-Mikumi tembo waliobaki ni 13,084 kwa mwaka jana kutoka Tembo 109,419 waliokuwepo mwaka 2006.
Alisema mfumo uliopo wa ujangili na soko la bidhaa hizo unafanya vita inayoendeshwa na Tanzania kuwa ngumu kama haitapata ushirikiano na mataifa mengine.
Alisema kutokana na ukweli huo wanataka mataifa jirani na jumuiya ya kimataifa kuingia katika mapambano ya kudhibiti biashara hiyo na hivyo kuwamaliza majangili na kuendelea kuhifadhi Tembo. Katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kwenye ufunguzi wa mkutano mkubwa wa kudhibiti ujangili na hifadhi endelevu ya wanyamapori, alisema serikali ya Tanzania imeanzisha mchakato wa kulinda wanyama pori.
GU9A8723  
Baadhi ya wadau kutoka nchi mbalimbali wanaohudhiria mkutano huo akiwemo Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto).
Mchakato huo ni pamoja na kuimarisha doria , kuendesha operesheni za kukabiliana na ujangili.
Alisema pamoja na kuwapo kwa juhudi za makusudi za kukabiliana na ujangili serikali ya Tanzania imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za kifedha na raslimali watu. Aidha kumekuwepo na ushiriki mdogo kutoka kwa wananchi katika vita dhidi ya ujangili.
Alisema kutokana na haja ya kukabili ujangili na kuwa na hifadhi endelevu, Februari mwaka huu mataifa ya Botswana, Chad, Garbon na Ethiopia yalitiliana saini mkataba wenye lengo la kupunguza mahitaji ya bidhaa za wanyamapori, kuimarisha sheria zilizopo dhidi ya ujangili na pia hifadhi na kusaidia maendeleo ya maeneo yanayokabiliwa na changamoto ya uwindaji haramu.
Rais Kikwete alisema katika hotuba yake kwamba kuwepo kwa mataifa hayo katika mkutano huo ni kuendeleza makubalino ya kutojishughulisha na biashara za bidhaa za wanyamapori kwa miaka 10 au hadi hapo tembo waliopo bara la Afrika watakapokuwa wameondoka katika hatari ya kuangamizwa katika uso wa dunia na majangili.
GU9A8943
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akizungumza kwenye mkutano mkubwa wa kudhibiti ujangili na hifadhi endelevu ya wanyamapori uliofunguliwa rasmi leo jijini Arusha kwenye ukumbi wa mikutano wa makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Aidha rais alisema kwamba mkutano huo wa Arusha unatarajiwa kuona namna ya kuendelea utekelezaji wa makubaliano ya London, Uingereza ya hifadhi ya wanyamapori walio katika hatari ya kutoweka akiwemo Tembo. Alisema kutokana na mfumo wa ikolojia na hifadhi ya wanyama na majirani zake, Tanzania inataka majirani kushiriki katika kulinda na kuhifadhi ikolojia hiyo na wanyama waliopo na sio kuiachia Tanzania pekee.
Tanzania ikiwa na eneo la kilomita za mraba 943,000 asilimia 30 ya eneo lake na 15 imetumika kwa hifadhi ya wanyamapori na misitu. Amesema eneo hilo hutumiwa zaidi kwa ajili ya utalii wa wanyamapori ambapo asilimia 17 ya pato la taifa linatokana na utalii huo. Wakati huo huo Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez ,ameipongeza Tanzania kwa kuitisha kikao cha kujadili ujangili na uhifadhi endelevu wa misitu.
GU9A8824
Mwenyekiti wa mkutano mkubwa wa kudhibiti ujangili na hifadhi endelevu ya wanyamapori ambaye pia ni Makamu mwenyekiti wa ICCF Group, Dr. Kaush Arha akiwakaribisha wadau wanaoshiriki mkutano huo kutoa maoni yao katika udhibiti wa ujangili ulioshika kasi.
Akizungumza kwa niaba ya mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo Kenya na Msumbiji alisema Umoja wa Mataifa unajisikia furaha kuona mataifa wanachama yanakabilian na changamoto ya ujangili na uhifadhi wa misitu kwa namna ambavyo itasaidia kizazi kijacho. Mratibu huyo alisema kwamba ujangili unatishia maendeleo, mazingira na usalama kitu ambacho Umoja wa Mataifa unakipiga vita.
Anasema biashara ya bidhaa za wanyamapori zinahatarisha uwepo wa wanyama ambao tayari wapo katika hatari ya kutoweka, unasababisha rushwa na migogoro ambayo inahatarisha maihsa ya watu. Alisema kwa sasa dunia imekuwa ikipungukiwa na tembo wa Afrika kwa kasi isiyokubalika kutokana na vitendo vya majangili na hivyo kutaka jamii kushirtikiana kukabiliana na vitendo hivyo. Mratibu huyo amesema uhalifu unaofanyika kwa wanyamapori na misitu ni lazima ukomeshwe kwa manufaa ya wananchi .
GU9A9238
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Tonia Kandiero akizungumza katika mkutano huo.
 
Alisema Tanzania inastahili kupongezwa kwa kuitisha mkutano wa kujadili ujangili Mei mwaka huu na sasa kuwa mwenyeji wa mkutano wa kikanda wa kukabiliana na ujangili. Alisema Umoja wa Mataifa utaendelea kuimarisha ushirikiano wake na mamlaka mbalimbali zinazoendelea kukabiliana na ujangili na kupotea kwa misitu duniani ili kuhifadhi urithi wa dunia.

Alisema Umoja huo kupitia mashirika yake mbalimbali watawezesha mambo mbalimbali ili kukabiliana na ujangili na uharibifu wa misitu. Alisema itaendelea kusapoti programu zinazokuza uchumi wa wananchi waliopo karibu na hifadhi za wanyamapori na misitu ili waone umuhimu wa kushiriki kuhifadhi wanyama na misitu husika.
GU9A9173
Balozi wa Finland nchini Tanzania, Mh. Sinikka Antila pamoja na Balozi wa Ujerumani nchini, Egon Kochanke nao ni miongoni mwa wadau wanaohudhuria mkutano huo.
GU9A9016
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano),Ummy Mwalimu akishiriki mkutano huo.
GU9A9099
Mwenyekiti wa mkutano mkubwa wa kudhibiti ujangili na hifadhi endelevu ya wanyamapori ambaye pia ni Makamu mwenyekiti wa ICCF Group, Dr. Kaush Arha akiteta jambo na mgeni rasmi Waziri wa Mali asili na utalii, Mh. Lazaro Nyalandu.
GU9A9278
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP) Bw. Philippe Poinsot (katikati) akimsikiliza mdau kutoka AWF akitoa maoni yake kwenye mkutano huo uliofunguliwa rasmi leo jijini Arusha.
GU9A8659  
Pichani juu na chini ni washiriki mbalimbali wa mkutano wa kikanda unaozungumzia ujangili na hifadhi endelevu uliofunguliwa rasmi leo jijini Arusha.
GU9A9041 GU9A9042   GU9A9175 GU9A9072 GU9A9304

KAULI YA WAZIRI MEMBE BUNGENI KUHUSU BIASHARA HARAMU YA PEMBE ZA NDOVU.

November 07, 2014
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe
Mheshimiwa Spika,
Siku ya Jana Vyombo vya Habari mbalimbali vya Ndani na Nje ya Nchi vilitoa habari kwamba ujumbe wa Rais wa China uliokuja nchini Miezi 18 iliyopita ulijihusisha na ununuzi wa pembe za ndovu nchini. Chanzo cha habari hizo ni taarifa ya taasisi isiyo ya kiserikali ya nchini Marekani ijulikanayo kama Environmental Investigation Agency (EIA). Habari hiyo imekwenda mbali zaidi kuituhumu nchi yetu na viongozi wake kutojali, wala kushughulikia tatizo la biashara haramu ya pembe za ndovu.

Mheshimiwa Spika,
Ninapenda kupitia Bunge lako tukufu kuutaarifu umma wa watanzania na dunia kwa ujumla kwamba madai yaliyotolewa na NGO hiyo ya Marekani ya kuihusisha ziara ya kihistoria ya Rais wa China kutembelea Tanzania kama nchi ya kwanza toka aingie madarakani na biashara ya pembe za ndovu hayana ukweli wowote. Vilevile, madai ya kwamba Serikali ya Tanzania haijali na wala haichukui hatua dhidi ya wanaojishughulisha na biashara haramu ya pembe za ndovu sio kweli.

Taarifa za EIA ni za kupikwa na kuungwa kuungwa ili kuchafua heshima ya nchi yetu, pamoja na kuchafua heshima ya rafiki zetu Taifa la China. Ni taarifa iliyoandaliwa na kutolewa wakati huu ili kukidhi ajenda mahususi ambayo tunaifahamu fika.
Mheshimiwa Spika,
Kabla sijaelezea kwanini ninasema taarifa hii sio ya kweli ningependa kwanza kulielezea Bunge lako tukufu mambo sita yafuatayo ambayo hayana ubishi:
1) Moja, ni kweli soko kubwa la pembe za ndovu lipo China. Wanaofanya biashara haramu ya pembe za ndovu hutafuta soko China;
2) Ni ukweli usiopingika kwamba pembe za ndovu nyingi zinazouzwa kwenye masoko haramu zinatokea Afrika, Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi zinapotoka pembe hizo;
3) Biashara hiyo haramu inahusisha wahalifu/ na mitandao ya waalifu ambao wana uraia wa nchi mbalimbali zikiwemo China na Tanzania;
4) Serikali ya Tanzania na Serikali ya China hazifanyi biashara haramu ya pembe za ndovu na wala hazihusiki na mitandao haramu.
5) Kwa kutambua ukubwa wa Tatizo la biashara hiyo haramu, Serikali zetu mbili zimekuwa na ushirikiano wa karibu kabisa katika kukabiliana na mitandao inayofanya biashara hiyo haramu. Vyombo vya dola vya nchi zetu mbili vimeshirikiana kwa karibu na kupashana habari kila wakati zilizowezesha kuwakamata wahusika wa biashara hiyo. Isitoshe wakati wa ziara iliyomalizika hivi majuzi Serikali zetu mbili zilisaini mkataba wa kutupatia vifaa vya kusaidia operesheni ya kupambana na ujangili wa wanyamapori – (China Aided Equipment for Forest Resources and Wildlife Conservation). Vilevile kwenye ziara hiyo tulisaini Mkataba wa kutupatia mitambo ya kisasa ya kufanya ukaguzi wa mizigo bandarini- ambayo itasaidia kubaini mizigo inayosafirishwa.
6) Tanzania na China zilishiriki kikamilifu kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Kudhibiti Biashara Haramu ya Pembe za ndovu (London Confrrence on Illegal Wildlife Trade) uliofanyika mwezi Februari 2014. Moja ya mafanikio makubwa ya mkutano huo ni kwa nchi za China, Botswana na Tanzania kusaini mkataba wa kupambana na biashara hiyo haramu. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa China kusaini Mkataba wa aina hiyo, jambo linalodhihirisha umakini wa Serikali ya Rais Xi Jinping kushughulikia tatizo la biashara haramu. Vilevile kabla ya mkutano huo wa London, Serikali ya China ilichoma moto hadharani shehena ya meno ya tembo haramu yaliyokuwa yakishikiliwa nchini humo.
Mheshimiwa Spika,

ZAIDI YA ABIRIA 37 WANUSURIKA KIFO BAADA YA BASI LA HAPPY NATION KUACHA NJIA NA KUPINDUKA IGURUSI MBEYA

November 07, 2014


Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo wakisaidia kuokoa majeruhi 

Basi lenye namba T281 ARR mali ya Happy Nation likiwa limepinduka eneo la Meta Igurusi kilometa 54 kutoka Mbeya




Moja wa majeruhi aliyenusurika akisubiri usafiri kupelekwa hospitali ya Chimala

Kamanda wa Polisi Mkoa waMbeya Ahmed Msangi akiwa eneo la tukio 

Majeruhi wakikumbatiana hawaamini kilichotokea na kuwa wapo hai

Kamanda wa Polisi Mkoa waMbeya Ahmed Msangi akiwatembelea majeruhi Katika Hospitali ya Chimala Mission

Moja wa askari aliyekuwa akisafiri katika basi hilo ambae alimuonya mara kadhaa dereva kutokana na mwendo kasi 


Wauguzi pamoja na madaktari wakiendelea kuwahudumia majeruhi

Watu 37 wamenusurika kifo baada ya basi la abiria lenye namba za usajili T 281 ARR aina ya Scania linalofanya safari zake kati ya Mbeya na Dar es Salaam linalomilikiwa na Kampuni  ya Happy Nation kuacha njia na kupinduka eneo la Meta Kata ya Igurusi wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi amesema ajali hiyo imetokea leo majira ya saa moja asubuhi  basi hilo likitokea Mbeya baada ya kupasuka gurudumu la mbele kulia kisha kupoteza uelekeo  na baadaye kumgonga mpanda baiskeli na kupinduka.

Msangi amesema baada ya ajali hiyo Dereva wa basi hilo aliyefahamika kwa jina moja la Shabani alikimbia ambapo Jeshi la Polisi linafanya juhudi za kumtafuta ili kueleza sababu za ajali hiyo.

Aidha Msangi amesema katika ajali hiyo kulikuwa na majeruhi 37 wanaume 26 wanawake 10 na mtoto mmoja wa kiume.

Baada ya ajali hiyo majeruhi walikimbizwa katika Hospitali ya Misheni ya Chimala ambapo mjeruhi 10 bado wamelazwa na wanne wamekimbizwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya kwa matibabu zaidi.

Kwa mujibu wa Daktari Mkuu Mahenge wa Hospitali ya Chimala amesema kuwa waliolazwa Hospitalini hapo ni wanaume sita na wanawake wanne na walohamishiwa Rufaa ni wanaume wanne.

Daktari Mahenge amesema kuwa hali za majeruhi 10 walipo Chimala hali zao zinaendelea vema ingawa wanakabiliwa na upungufu wa damu na wameomba msaada katika kitengo cha benki ya Damu salama Mbeya.

Hata hivyo baadhi ya abiria wamelalamikia mwendo kasi wa basi hilo kwani baada ya kutoka kituo kikuu cha Mabasi lilianza kwenda kwa mwendo wa kasi na mara kadhaa walikuwa wakimuonya Dereva lakini alikuwa akikaidi.

Pia walikuwa wakifukazana na mabasi mengine yaliyotokea Mbeya kuelekea Jijini Dar es Salaam hali iliyosababisha basi hilo kupasuka gurudumu la kulia likiwa katika mwendo kasi na kona kali kisha kupinduka.

Wakati huo huo Kamanda Ahmed Msangi amesema  watu wawili wamefariki dunia wilayani Mbozi baada ya roli la mizigo kugongana uso kwa uso na gari linalomilikwa na NSSF.

Msangi amesema bado majina ya waliofariki hayajapatikana na kwamba Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha ajali na miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Serikali Mbozi.


Na Mbeya yetu 

LINNAH ATUMBUIZA KAMPENI YA MWANAMKE NA UCHUMI MKOANI TANGA.

November 07, 2014
Msanii wa muziki wa kizazi kipya ,Linah Sanga jana alikuwa kivutio cha aina yake baada ya kuamua kujaza fomu za kujiunga na mfuko wa pesheni wa GEPF na kusababisha wanawake waliokuwa wamehudhuria mafunzo ya kampeni ya mwanamke na uchumi na kumfuata.

Linah ambaye pia ni balozi wa Angels Moment inayoendesha kampeni ya mwanamke na uchumi alijaza fomu za uanachama wa GEPF katika banda la maonesho lililowekwa Naivera Jijini Tanga yalikokuwa yakifanyika mafunzo  hayo.

Msanii huyo aliamua kujiunga na mfuko huo mara baada ya maafisa wa GEPF wakiongozwa na Meneja wa Mkoa wa Tanga,Silvanus Kuloshi kumweleza juu ya faida za uanachama wa mfuko huo pamoja na mafao yanayotolewa .

Nimeamua kujiunga na GEPF kwa sababu nimevutiwa na mafao yanayotolewa na natoa wito kwa wanawake wengine wakiwamo mashabiki wangu kujiunga nao”alisema Linah.

Kabla ya kuujiunga na mfuko huo,msanii huyo alikonga nyoyo za
madshabiki wake kwa kuimba nyimbo za kuwahamasisha wanawake kuendesha shughuli za ujasiliamali kwa kujiamini .

NSSF YAWAKABIDHI NYUMBA WASANII WA ORIJINO KOMEDI

November 07, 2014


Meneja Mipango na Uwekezaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abdallah Mselly (kulia) akimkabidhi msanii wa Orijino Komedi, Mjuni Silvery ‘Mpoki funguo ya moja ya nyumba za gharama nafuu walizokopeshwa wasanii  wa kikundi hicho na NSSF wakati wa hafla fupi ya kukabidhi wasanii hao zilizopo Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam hivi karibuni, mkopo huo utalipwa kwa kipindi cha miaka 15. (Na Mpiga Picha Wetu)

ya nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kukopeshwa wasanii wa kikundi cha Orijino Komedi Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Taifa la Hifadhi
ya Jamii (NSSF) zilizopo katika mradi wa ujenzi wa Mtoni Kijichi jijini
Dar es Salaam.

Mac Reagan ‘Kipara’ na Mjuni Silvery ‘Mpoki wakiangalia moja kati ya nyumba walizokabidhiwa na NSSF baada ya kukopeshwa na Shirika hilo na mkopo utalipwa kwa kipindi cha miaka 15.
Kushoto, Mac Reagan, Joti na Mpoki wakiangalia nyumba zao walizokabidhiwa na NSSF.
Meneja Mipango na Uwekezaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abdallah Mselly akimkabidhi funguo ya nyumba msanii wa Orijino Komedi.  
Msanii Isaya Mwakilasa ‘Wakuvwanga’ akipokea funguo ya nyumba yake.

Muandaaji wa vipindi vya Orijino Komedi, Sekioni David ‘Seki’ akipokea funguo ya nyumba yake kutoka kwa Meneja Mipango na Uwekezaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi
ya Jamii (NSSF), Abdallah Mselly (kulia)
Meneja Mipango na Uwekezaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi
ya Jamii (NSSF), Abdallah Mselly akifafanua jambo wakati wa hafla ya kukabidhi nyumba kwa wasanii kikundi cha Orijino Komedi.
Msanii Mac Reagan akizungumza baada ya makabidhiano ya nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NSSF Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam.

Muandaaji wa vipindi vya Orijino Komedi, Sekioni David ‘Seki’ akifafanua jambo wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa nyumba.

TIKETI ZA ELEKTRONIKI KUTOUZWA KWENYE MAGARI

November 07, 2014


Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea wikiendi hii ambapo tiketi za elektroniki hazitauzwa tena kwenye magari, hivyo washabiki wanunue tiketi hizo kwenye mtandao au kwenye maduka ya CRDB Fahari Huduma.

Kesho (Novemba 8 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kutakuwa na mechi kati ya Yanga na Mgambo Shooting wakati Uwanja wa Chamazi kutakuwa na mechi kati ya Azam na Coastal Union. Jumapili ni mechi kati ya Simba na Ruvu Shooting.

Viingilio kwenye mechi za Uwanja wa Taifa ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani na bluu, sh. 8,000 (viti vya rangi ya chungwa), sh. 15,000 (VIP B na C) wakati VIP A itakuwa sh. 20,000. Mechi za Uwanja wa Chamazi kiingilio ni sh. 3,000 kwa sh. 10,000.

Mechi nyingine za VPL kesho ni kati ya Stand United na Mbeya City (Uwanja wa Kambarage, Shinyanga), Mtibwa Sugar na Kagera Sugar (Uwanja wa Manungu, Morogoro).

Raundi hiyo ya saba itakamilika Jumapili kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam kwa mechi kati ya JKT Ruvu na Ndanda kutoka Mtwara.

Wakati huo huo, mchezaji bora wa VPL kwa mwezi Oktoba, Salum Abubakar wa Azam atakabidhiwa zawadi yake kesho (Novemba 8 mwaka huu) kabla ya mechi kati ya Azam na Coastal Union.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

WALIOWEZESHWA NA TBL KUPITIA PROMOSHENI YA SAFARI LAGER WEZESHWA WAPATA MAFANIKIO MAKUBWA

November 07, 2014

 Valerian Luzangi (kushoto) ambaye ni Mkurugenzi wa Kiwanda cha kuzalisha shampoo za binadamu na wanyama hasa mbwa cha L & V Intergrated Firm akimuonesha Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha Mushi,  shampoo  ambayo iko tayari kuuzwa. Tbl kupitia Promosheni ya Safari Lager Wezeshwa ilimpatia  mfanyabiashara huyo chupa 20,000 za kuwekea shampoo. Kiwanda hicho kipo Mikocheni Dar es Salaam.

 Valerian Luzangi (kulia) ambaye ni Mkurugenzi wa Kiwanda cha kuzalisha shampoo za binadamu na wanyama hasa mbwa cha L & V Intergrated Firm akimuonesha Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha Mushi,  shampoo ya kuoshea mbwa ambayo iko tayari kuuzwa. Tbl kupitia Promosheni ya Safari Lager Wezeshwa ilimpatia  mfanyabiashara huyo chupa 20,000 za kuwekea shampoo. Kiwanda hicho kipo Mikocheni Dar es Salaam.

 Mmoja wa wafanyakazi walioajiriwa na kiwanda hicho akiweka maji kwenye pipa tayari kuchanganywa na dawa wakati wa kutengeza shampuu.