Uhamiaji waanza kuwaandikisha walowezi wa Malawi na Msumbiji.
Na
Oscar Assenga, Tanga.
IDARA
ya Uhamiaji Mkoa wa Tanga imeanza kuwaandikisha walowezi wa Malawi na Msumbiji waliokuja
mkoani hapa katika kipindi cha miaka ya nyuma ambao walikuwa wakifanya kazi
kwenye mashamba ya mkonge na kazi za majumbani.
Akizungumza
na blog hii, Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Tanga, Sixtus Nyaki alisema uandikishwaji
watu hao unafanyika baada ya kuzungumza nao katika mkutano wa kuwaelimisha kwa
kushirikiana na wenyeviti wa mitaa, vitongoji na maafisa watendaji wa kata na vijiji.
Nyaki
alisema wakati wakiwa wanaendesha zoezi hilo wanakumbana na changamoto
mbalimbali ikiwemo baada yao kutokukubali kuandikishwa kwa kuona kama
wanafukuzwa hapa nchini hali ambayo inapelekea kuwa na ugumu kiasi.
Alisema
katika kupambana na wimbi la uhamiaji haramu mkoani hapa idara hiyo imefungua
ofisi ya uhamiaji wilayani Korogwe lengo likiwa ni kuzibiti ongezeko la
wahamiaji wanaoingia mkoani hapa kutoka nchi mbalimbali duniani.
Ofisa
huyo alisema ofisi hiyo itakuwa na kazi ya kuwahudumia wilaya ya Korogwe na
wilaya ya Lushoto wakati idara hiyo ikiendelea kujipanga kwa ajili ya kufungua
ofisi nyengine wilayani humo ikiwa ni mkakati wa kupambana na wahamiaji haramu.
Aidha
alisema tayari wameshapata ofisi hiyo na ukarabati wake unaendelea ambapo
unatarajiwa kukamilika muda sio mrefu ili iweza kufanya kazi zake ambapo
aliongeza kuwa idara hiyo pia imeweka vizuizi katika barabara za
Tanga-Horohoro, Tanga-Arusha na Tanga-Dar.
Hata
hivyo aliogeza kuwa wataendelea kutoa elimu ya uhamiaji shirikishi kwa wananchi
katika maeneo mbalimbali lengo likiwa ni kupunguza wimbi la wahamiaji haramu
mkoani hapa pamoja na kuweza mikakati ya kupunguza uwepo wapo.
Mwisho.
KLABU ZA ENGLAND ZIARANI ASIA
MAN UNITED, CHELSEA, ARSENAL, CITY, SPURS, LIVERPOOL, SUNDERLAND NDANI YA NYUMBA!!
KABLA
MSIMU MPYA wa 2013/14 kuanza Klabu kubwa za England zitatirirka Barani
Asia kwa Ziara zao za matayarisho lakini pia lengo ni kuteka Soko kubwa
huko kwa Klabu zao kwa kujitangaza kwa kishindo.
Arsenal wataanza Ziara yao huko Asia kwa
kucheza Jakarta Indonesia Julai 14 na Siku 3 baadae wataenda Vietnam na
kumalizia Ziara huko Japan, hii ikiwa Ziara yao ya kwanza Nchini Japan
tangu Mwaka 1968.
Huko Japan, Arsenal watacheza na Nagoya
Grampus 8, ambayo ni Klabu iliyofundishwa na Meneja wao Arsene Wenger
kabla hajatua Arsenal Mwaka 1997, na Mechi hiyo itakuwa Julai 22.
Kisha Arsenal watacheza na Urawa Reds kugombania Saitama City Cup hapo Julai 26 na baada ya hapo kurudi London.
Nao Chelsea, hapo Julai 17 watakuwa huko
Bangkok, Thailand kucheza na Kombaini ya Thailand na Tarehe 21 Julai
watacheza huko Kuala Lumpur, Malaysia na Julai 25 kucheza Jakarta,
Indonesia.
Liverpool watakuwa Australia kucheza na
Melbourne Victory na baada ya hapo watapitia Bangkok, Thailand kucheza
Mechi moja hapo Julai 28.
Hong Kong itashuhudia Mashindano ya
Klabu za Ligi Kuu England kugombea Asia Cup na safari hii washiriki ni
Manchester City, Tottenham Hotspur na Sunderland ambao watacheza Mechi
zao za Kombe hilo Julai 24 na 27.
Mabingwa wa England, Manchester United,
wao watakuwa na Ziara ya Wiki mbili itakayoanza Julai 13 huko Bangkok,
Thailand na kisha kuruka kwenda Sydney, Australia na Japan, kucheza na
Yokohama F. Marinos na Cerezo Osaka, Timu aliyotoka Shinji Kagawa, na
kumalizia Ziara yao huko Hong Kong kucheza na Klabu ya hapo Julai 29.
Subscribe to:
Posts (Atom)