CAMPUS VYBEZ YA TIMESFM YAKUTANISHA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU KUJADILI CHANGAMOTO ZA AJIRA

July 09, 2016
Watangazaji wa Kipindi cha Campus Vybez kinachorushwa na Kituo cha redio cha TimesFm ya jijini Dar, Sandra Temu na Raheem wakiongoza mjadala maalumu wa utakaoibua hoja ya kutatua changamoto ya ajira nchini, ambapo mjadala huo umeandaliwa na Kituo cha Timesfm redioni ndani ya kipindi cha Campus Vybez kinachorushwa kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 kamili usiku. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
  BAADHI ya wanafunzi wa elimu ya Juu kutoka katika vyuo mbalimbali jijini Dar es Salaam, wakimsikiliza kwa makini Mtangazaji wa kipindi cha Campus Vybez katika mjadala maalumu wa utakaoibua hoja ya kutatua changamoto ya ajira nchini, ambapo mjadala huo umeandaliwa na Kituo cha Timesfm radion ndani ya kipindi cha Campus Vybez kinachorushwa kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 kamili usiku.
  Mc Pilipili akitoa kibwagizo mara baada ya kukaribishwa.
 Mc Pilipili akijitambulisha kwa vijana, pembeni yake ni Ron Fidanza, Naibu waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Anthony Mavunde.
Msimamizi Mkuu wa radio ya TimesFm  Ron Fidanza.
 Mhadhiri wa Lugha wa Chuo cha Ualimu DUCE, Mhe. Ruben Ndimbo akijitambulisha.
 Mmoja wa waalikwa akijitambulisha.
 Meza mkuu.
-- ---- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.blogspot.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''

DC GONDWE ATAKA WAFANYABIASHARA KUWEKEZA KWENYE KILIMO KIKUBWA WILAYANI HUMO

July 09, 2016
MKUU wa wilaya ya Handeni Mkoani Tanga,Godwin Gondwe  amewataka wafanyabiashara kuhakikisha wanawekeza kwenye kilimo kikubwa cha kisasa ambacho kitakuwa na tija kwao ili kuweza kusukuma gurudumu la maendeleo na kukuza uchumi.

Gondwe alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wafanyabiashara, viongozi wa dini ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka kuona umuhimu wa kutumia fursa ya uwepo wa rutuba nzuri ya ardhi iliyopo wilayani humo kujikita kulima kisasa ili kuweza kupata mafanikio.

Alisema kuwa lazima wafanyabiashara watambue kuwa kilimo ndio njia pekee ambayo inaweza kuwainua kiuchumi na kuharakisha kasi ya ukuaji wa maendeleo iwapo watazingati na kukipa kipaumbele kila wakati

  “Niwaombeni suala la kilimo mlipe  msukumo mkubwa sana kwani hii ndio njia pekee ambayo inaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kusukuma gurudumu la maendeleo kwa wilaya yetu “Alisema.

Aidha pia alisisitiza umuhimu wa wananchi wa wilaya hiyo kutilia mkazo kulima mazao yanayostahimili ukame ikiwemo Alizeti, Ufuta,Viazi na Mihogo ili kuweza kukabiliana na tatizo la kutoku patikana mvua za uhakika kwa ajili ya kilimo cha mahindi.

 “ Ninajua katika kipindi hiki tumelima kwa wingi lakini hali ya hewa sio nzuri na mvua nazo zimekuwa hazipatikana kwa uhakika hivyo lazima wakulima tubadilike kwa kuanza kupanda mazao yanayostahimili ukame ili kuweza kuepukana na baa la njaa “Alisema DC Gondwe.

Sambamba na hayo,Mkuu huyo wa wilaya alizishauri taasisi za kibenki wilayani humo kuhakikisha zinatoa kipaumbele kwa wawekezaji wa kilimo ili waweze kuzalisha kwa wingi mazao ambayo yataweze kuinua kiuchumi lakini pia kuchangia pato la Taifa.

Hata hivyo ,Mkuu huyo wa wilaya alitumia pia fursa hiyo kuwaasa wakulima waliopata mazao kidogo kuhakikisha wanayatunza na kuacha kuyauza kwani kufanya hivyo kutaweza kusababisha hali ya njaa kwao

Naye Sherhe wa wilaya ya Handeni, Shabani Mohamed alisema kuwa wao watamuombea dua Mkuu huyo wa wilaya ili mungu amuwezeshe kuweza kutimiza majukumu yake ipasavyo na kusaidia kuchangia juhudi za maendeleo kwa wananchi.

 “Nikuambie Mh Mkuu wa wilaya ujio wako hapa Handeni watu wengi wamefurahi sana kwani uchapakazi wako unafahamika tokea ulipokuwa unafanya kazi kwenye kituo cha ITV na tunaamini uhodari huo pia utasaidia kuinua uchumi wetu “Alisema.

Alisema kuwa wao watahakisha wanampa ushirikiano wa hali ya juu ili kumuwezesha kutekeleza vema majukumu yake ya kuipa maendeleo wilaya hiyo.