COASTAL UNION:MCHAKATO WA KOCHA MPYA BADO UNAENDELEA

October 29, 2013


Na Oscar Assenga, Tanga.
UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga umesema hivi sasa hauna mpango wa kutafuta kocha mpya badala yake wataendelea na kocha Joseph Lazaro mpaka kumalizika mzunguko wa kwanza.

Kauli hiyo ilitolewa leo na Mwenyekiti wa Klabu hiyo,Hemed Aurora “Mpiganaji”wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi kuhusu mikakati ya kumleta kocha mpya baada ya Hemed Morroco kubwaga manyanga.

Morroco alibwaga majanga baada ya mkataba wake kumalizika huku timu hiyo ikiwa inasuasua kufanya vizuri katika michezo yao ya ligi kuu Tanzania bara hali ambayo wakati mwengine ilikuwa ikimuweka kwenye wakati mgumu hasa kwa mashabiki.

RC GAWALA ATEMBELEA KIWANDA CHA RHINO CEMENT

October 29, 2013


MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI MSTAAFU CHIKU GALLAWA KATIKATI AKIPATA MAELEKEZO KUTOKA KWA MKURUGENZI MTENDAJI WA KIWANDA HICHO ALIYEKAA KUSHOTO NA KULIA NI MKUU WA WILAYA YA TANGA,HALIMA DENDEGO



BAADHI YA MITAMBO MIPYA INAYOJENGWA KWENYE KIWANDA HICHO





MWENGE FC YAONYESHA NIA YA KUCHEZA LIGI KUU ZANZIBAR MSIMU UJAO

October 29, 2013
Na Masanja Mabula -Pemba
Timu ya soka ya Mwenge imeanza kuonyesha nia ya kutaka kurithi nafasi ya Timu ya Jamhuri kucheza ligi kuu ya Zanzibar kwa msimu ujao baada ya kuifundisha soka timu ya Maendeleo Manta (Wazee wa Kununua ) mabao 2-1 katika mfululizo wa michezo la ligi daraja la kwanza Taifa Pemba uliofanyika kwenye uwanja wa Polisi Finya .
Mwenge ambayo kwa sasa inashika nafasi ya Pili kwenye msimamo wa ligi hiyo kwa kufikisha alama 16 ikiwa nyuma ya wanajeshi wa H/Rock wenye alama 19 iliutawala mchezo kwa dakika zote .

Katika Mpambano huo uliochezeshwa vyema na mwamuzi Asaa Ali ilishughudia mchezaji Idd Ramadhaman akiinyima bao la kuongoza timu yake ya mwenge manao dakika ya 25 baada ya kushindwa kuunganisha vyema mpira uliopigwa na Mchezaji Ali Salim  .

Wakiutumia msemo wa kwamba "Penye fungu ndipo paongezwapo " Mwenge walifanikiwa kuandika bao la kwanza katika dakika ya 42 ya kipindi cha kwanza kupitia mchezaji Idd Ramadhaman baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Maendeleo Manta .

Mwenge walifanikiwa kuongeza bao la pili katika dakika ya 53 kwa bao la kichwa lililofungwa na mchezaji Ali Salim Kareka  ambaye alifunga bao hilo baada ya kuunganisha vyema  kona iliyochongwa na Madenge kutoka winga wa kushoto .

Nalo bao la kufutia machozi la timu ya Manedeleo Manta lilipatikana katika dakika 66 likifungwa na Mchezaji Massoud Ali kwa shuti kali la Mguu wa Kushoto kufuatia uzembe uliofanywa na walinzi wa Timu ya Mwenge .

MECK MEXIME KUFUNGWA NI SUALA LA KAWAIDA.

October 29, 2013
Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar,Meck Mexime akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mechi kati yao na Coastal Union ambapo Mtibwa walikubali kichapo cha mabao 3-0.


Mashabiki wa Coastal Union wakifurahia ushindi huo

PAMBANO LA SIMBA, AZAM LAINGIZA MIL 64/-

October 29, 2013
Na Boniface Wambura,Dar es Salaam.
Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Azam lililochezwa jana (Oktoba 28 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 64,261,000.

Washabiki waliohudhuria mechi hiyo namba 76 iliyomalizika kwa Azam kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 walikuwa 10,728 ambapo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.

Mgawo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 9,802,525.42, gharama za kuchapa tiketi sh. 3,793,490 wakati kila klabu ilipata sh. 14,946,170.45.

Wamiliki wa uwanja walipata sh. 7,599,747.49, gharama za mchezo sh. 4,599,848.61, Bodi ya Ligi sh. 4,599,848.61, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,279,924.31, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,773,274.46.

SIMBA, KAGERA SUGAR KUUMANA ALHAMISI

October 29, 2013
Na Boniface Wambura,Dar es Salaam.
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaanza raundi ya 12 keshokutwa (Oktoba 31 mwaka huu kwa mechi kati ya Simba na Kagera Sugar itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.

Viingilio katika mechi hiyo itakayooneshwa moja kwa moja na Azam Tv kupitia TBC 1 vitakuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A.

Nayo Yanga itashuka uwanjani Novemba Mosi mwaka huu katika mechi nyingine ya ligi hiyo dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Novemba 2 mwaka huu kutakuwa na mechi nne; Mgambo Shooting na Coastal Union (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Tanzania Prisons na Oljoro JKT (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).

Raundi hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7 mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashani United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, Rhino Rangers vs Tanzania Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar.

Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City wakati Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

KONGAMANO LA WANASALAMU NCHINI LAFANYIKA TANGA.

October 29, 2013
 Mkuu wa wilaya ya Tanga,Halima Dendego akiwahutubia wanaalamu katika risala yake

Mkuu wa wilaya ya Tanga,Halima Dendego akifungua mfano wa cheti cha umoja  wa wanasalamu Tanzania.

 MKUU wa wilaya Tanga,Halima Dendego akicheza mziki ikiwa ni kuahisiria ufunguzi wa kongamano la Wanasalamu hapa nchini

Meza ya watangazaji wa radio za mkoani Tanga ,Mwanza na Dar es salam wakisikiliza kwa makini mgeni rasmi


YANGA, MGAMBO KUUMANA UWANJA WA TAIFA VPL LEO

October 29, 2013

Na Boniface Wambura,Dar es Salaam.
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inakamilisha  raundi ya kumi na moja leo kwa mechi tatu huku Yanga ikiwa mwenyeji wa Mgambo Shooting kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mbeya City na Tanzania Prisons. Rhino Rangers na JKT Ruvu zitacheza katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.

Raundi ya 12 ya ligi hiyo itaanza Oktoba 31 mwaka huu kwa mechi kati ya Simba na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Novemba Mosi mwaka huu kutakuwa na mechi kati ya Yanga na JKT Ruvu kwenye uwanja huo huo.

Novemba 2 mwaka huu kutakuwa na mechi nne; Mgambo Shooting na Coastal Union (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Tanzania Prisons na Oljoro JKT (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).

Raundi hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7 mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashani United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, Rhino Rangers vs Tanzania Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar.

Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City wakati Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.