MAJALIWA AONDOKA NCHINI KWENDA MOURITIUS KUMWAKILISHA JPM KATIKA UZINDUZI WA JUKWAA LA UCHUMI LA AFRIKA

MAJALIWA AONDOKA NCHINI KWENDA MOURITIUS KUMWAKILISHA JPM KATIKA UZINDUZI WA JUKWAA LA UCHUMI LA AFRIKA

March 18, 2017
MAKO
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kwenye uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam kabla ya kuondoka nchini kwenda Port Louis, Mauritius kumwakilisha Rais John Magufuli katika Uzinduzi wa  Jukwaa la Uchumi la Afrika (The Inaugural  Session of The African Economic Platform) , Machi 18, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
UFUNGUZI WA MASHINDANO YA MAJESHI VISIWANI ZANZIBAR

UFUNGUZI WA MASHINDANO YA MAJESHI VISIWANI ZANZIBAR

March 18, 2017
ASOU
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Wachezaji wa Timu ya SMZ katika Ufunguzi wa Michezo ya Majeshi ya 1i kwa mwaka 2017 (BAMATA) yaliyofanyika Uwanja wa Amaan Mjini Unguja leo.
ASOU 1
 Maaskari wa Vikosi mbali mbali vya Ulinzi na Usalama wakiwa katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja katika sherehe za Ufunguzi wa Michezo ya Majeshi ya 17 kwa mwaka 2017yaliyofunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
ASOU 2
Maaskari wa Vikosi mbali mbali vya Ulinzi na Usalama wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wakati alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa Michezo ya Majeshi ya 17 kwa mwaka 2017 katika  uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja katika sherehe zilizofanyika leo.
ASOU 3
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) wakiangalia ratiba Ufunguzi wa Michezo ya Majeshi ya 17 kwa mwaka 2017 (BAMATA) na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance S. Mabeyo (kushoto) katika  uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja katika sherehe zilizofanyika leo (kulia) Waziri wa Ulinzi Majeshi ya Kujenga Taifa Mhe,Dkt.Hussein Mwinyi.  
ASOU 4
Kikosi cha Maaskari Kanda ya JKT wakipita mbele ya Mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na kutoa heshima wakati ufunguzi wa Michezo ya Majeshi ya 17 ya mwaka 2017 (BAMATA)katika  uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja katika sherehe zilizofanyika leo. 
ASOU 5
Maaskari wakiimba wimbo maalum wakati wa ufunguzi wa Michezo ya Majeshi ya 17 ya mwaka 2017 (BAMATA)katika  uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja katika sherehe zilizofanyika leo.
ASOU 6
 Kikosi cha Maaskari Jeshi la Wananchi JWTZ Kanda ya Ngome  wakipita mbele ya Mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na kutoa heshima wakati ufunguzi wa Michezo ya Majeshi ya 17 ya mwaka 2017 (BAMATA)katika  uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja katika sherehe zilizofanyika leo. 
ASOU 7
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa Michezo ya Majeshi ya 17 kwa mwaka 2017 leo katika  uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,Mkoa wa Mjini Magharibi.
ASOU 8
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa Michezo ya Majeshi ya 17 kwa mwaka 2017 leo katika  uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,Mkoa wa Mjini Magharibi, [Picha na Ikulu] 18 /03/2017.

WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA WATAKIWA KUMTUMIKIA MUNGU NA KUACHA KUTENDA MABAYA

March 18, 2017
Mlezi wa wanafunzi Umoja wa wanafunzi wajumbe wa Kristo kutoka Shule ya Wasichana ya St.Christina Mwl Boaz Lazaro akizungumza na wanafunzi wakati wa sherehe ya kuwaaga wale wanaomaliza kidato cha sita kwa shule hiyo na Galanosi uliofanyika kwenye Kanisa la Pentecoster Tanzania(KLPT)
Mwenyekiti wa CASFETA shule ya sekondari ya Wavulana Galanosi  na Makamu Mwenyekiti wa wilaya,Anderson Mtalemwa akitoa neno kwenye sherehe hizo mapema leo
Mwalimu Nelson Kato ambaye ni Mlezi wa Vikundi vya Kikisto shule ye Sekondari ya Wavulana ya Galanosi (CASFETA, UKWATA,ASSA na TYCS akiwapa nasaha wanafunzi hayo
Wanafunzi wa shule ya Sekondari St,Christina wakiimba nyimbo za kuwaaga wenzao kwenye umoja huo
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Masechu wakiimba kwenye sherehe hizo
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Wavulana ya Galanosi wakiimba kwenye Shehere hizo

Wanafunzi wa shule ya Sekondari St,Christina wakiimba nyimbo za kuwaaga wenzao kwenye umoja huo
Wanafunzi na wageni wengine waalikwa wakifuatilia kwa umakini hotuba ya mgeni rasmi

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Galanosi wakiendelea kutoa burudani wakati wa sherehe hizo



Mama Hosea akifuatilia matukio mbalimbali kwenye sherehe hizo leo

Muonekana wa wanafunzi na wageni waalikwa wakifuatilia matukio mbalimbali

Muonekana wa wanafunzi na wageni waalikwa wakifuatilia matukio mbalimbali
Muonekana wa wanafunzi na wageni waalikwa wakifuatilia matukio mbalimbali
Wanafunzi wa shule ya shule ya Sekondari  St.Christina wakitumbuiza kwenye sherehe hizo



Wanafunzi wa shule ya shule ya Sekondari  St.Christina wakitumbuiza kwenye sherehe hizo


Mlezi wa wanafunzi Umoja wa wanafunzi wajumbe wa Kristo kutoka Shule ya Wasichana ya St.Christina Mwl Boaz Lazaro wa pili kutoka kushoto akiwaongoza wanafunzi hao kuingia ukumbini

Mlezi wa wanafunzi Umoja wa wanafunzi wajumbe wa Kristo kutoka Shule ya Wasichana ya St.Christina Mwl Boaz Lazaro wa pili kutoka kushoto akiwaongoza wanafunzi hao kuingia ukumbini
Wanafunzi wakiingia ukumbini

Mlezi wa wanafunzi Umoja wa wanafunzi wajumbe wa Kristo kutoka Shule ya Wasichana ya St.Christina Mwl Boaz Lazaro wa pili kutoka kushoto akiwaongoza wanafunzi hao kuingia ukumbini
Wanafunzi wakifanyiwa maombi kabla ya kuanza sherehe hizo ambazo zimefanyika leo kwa ajili ya kuwaaga wanafunzi wanaohitmu kidato cha sita
Wanafunzi wakiendelea na maigizo

MD KAYOMBO AWAONYA MAAFISA WATENDAJI WA KATA NA MITAA KUTOPOKEA RUSHWA

March 18, 2017
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akitoa ufafanuzi wa muongozo wa ukusanyaji wa mapato kwa Maafisa Watendaji wa Kata na Mitaa
 Maafisa Watendaji wa Kata na Mitaa wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo
 MD Kayombo akisisitiza jambo


Na Mathias Canal, Dar es salaam

Maafisa Watendaji wa Kata 14, Watendaji wa Mitaa 91 pamoja na Wahasibu wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo wameonywa kutopokea Rushwa wala hongo ya aina yoyote kutoka kwa wamiliki wa biashara mbalimbali katika Manispaa hiyo kwani kufanya hivyo watadhoofisha ukusanyaji wa mapato ya serikali kama ilivyokusudiwa.

Kauli ya onyo imetolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo wakati akitoa ufafanuzi wa muongozo wa ukusanyaji wa mapato na kutoa maelekezo ya majukumu ya kazi kwa Maafisa Watendaji wa Kata na Mitaa kwenye kikao cha kazi kilichofanyika leo Jumamosi Machi 18, 2017 katika ukumbi wa Ofisi za Manispaa hiyo ilipo Mtaa wa Kibamba CCM.

Kayombo ameeleza kuwa kwa mtumishi yoyote wa Manispaa kwa ngazi yoyote atakayebainika kujihusisha na ubadhilifu kwa kuchukua Rushwa kwa walipa kodi atachukuliwa hatua Kali za kisheria kwa kuiibia serikali kwani kuihujumu serikali kwa kuiibia mapato au kuzuia ukusanyaji wa mapato ni kosa kwa mujibu wa taratibu na sheria.

"Nina amini kwamba mnaishi vizuri na wananchi wenu kwahiyo mnawafahamu vizuri wafanyabiashara wanaokwepa kulipa Kodi lakini hata walipaji wazuri hivyo jambo la ukusanyaji mapato litakuwa jepesi sana kwenu kutokana na uzoefu mlionao" Aliongeza Kayombo

Mkurugenzi huyo amewasisitiza Watendaji hao kusimamia vyanzo vyote vya mapato ikiwemo Hotel Levy, Service Levy, Mabango makubwa na madogo (Bill Board), Leseni za biashara na Vileo, Upimaji afya kwa ngazi za Mitaa hususani katika Migahawa.

Hata hivyo amewataka Watendaji hao kufanya kazi kwa ushirikiano, Uaminifu, na Weledi mkubwa kwani kufanya hivyo kutasababisha ukusanyaji mkubwa wa Mapato kwa mwaka 2016/2017.

Kayombo Amewataka Watendaji wote kukagua Maduka yote katika maeneo yao ya kazi ili kubaini Maduka yasiyokuwa na leseni na Yale yenye leseni kuwa na Leseni za Manispaa ya Ubungo kwani wafanyabiashara wa Maduka mengi wamekuwa na kisingizio cha kukata leseni na Kodi mbalimbali katika Manispaa ya Kinondoni na kutaka kulazimisha kuitumia leseni hiyo kama halali kwa Manispaa ya Ubungo.

Sambamba na hayo pia MD Kayombo amewataka Maafisa biashara kutochelewesha leseni za wafanyabishara waliokamilisha taratibu zote za kumiliki leseni kwani kufanya hivyo ni kuchelewesha huduma kwa wananchi na kuongeza makwazo kwa wafanyabishara kwa sababu tu ya kuchelewa kusaini leseni.

Alisema kuwa litakuwa ni jambo la aibu na lisilovumiliwa kwa kuruhusu sheria zitungwe kwa umakini mkubwa lakini utekelezaji wake uwe hafifu.

MD Kayombo aliongeza kwa kusema kuwa hakuna Haki bila wajibu hivyo Watendaji hawapaswi kufanya kazi kwa mazoea lakini pia kutofanya kazi kwa kuongozwa na tamaa.

MD Kayombo amesema kuwa Oparesheni hiyo ya itakayodumu kwa miezi mitatu ya ukusanyaji wa mapato itaanza jumatatu Machi 20, 2017 kwa ushirikiano baina ya watendaji kutoka Makao makuu ya Wilaya, Watendaji wa Kata, Watendaji wa Mitaa na wenyeviti wa serikali za Mitaa.

WANANCHI WAMPONGEZA MKUU WA WILAYA YA UBUNGO JIJINI DAR ES SALAAM

March 18, 2017
Na Dotto Mwaibale

WANANCHI wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam wamempongeza Mkuu wa Wilaya hiyo, Kisare Matiku Makori kwa kuweka utaratibu wa kusikiliza kero zao kwa ajili ya kuzitafutia utatuzi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti  jijini Dar es Salaam jana walisema utaratibu anaoufanya mkuu huyo wa wilaya unapaswa kuigwa na viongozi wengine kwani unakwenda na kasi ya kazi ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli ya hapa kazi tu.

MBINU HIZI ZITAKUSAIDIA KUKABILIANA NA MVUA JIJINI DAR ES SALAAM

March 18, 2017
Na Jumia Travel Tanzania

Hivi kuna mkazi yeyote wa jiji la Dar es Salaam ambaye ni mgeni wa adha zitokanazo na mvua zinazonyesha? Sidhani kama kuna mtu yeyote hafahamu ya kwamba mvua ikinyesha kutakuwa na foleni zisizokwisha, barabara na mitaa tofauti jijini kujaa maji, mafuriko na matamko kadha wa kadha kutoka kwa viongozi wa serikali kuwataka wananchi wahame mabondeni.

Lakini ni wangapi wametafakari watawezaje kukabiliana na mvua zitakaponyesha? Zipo mbinu nyingi tu ambazo Jumia Travel inakushauri uzizingatie ili kipindi cha mvua nyingi za Dar es Salaam kwako kiwe ni cha kawaida katika mwaka. 


Amka mapema kukabiliana na foleni ili uwahi shughuli zako
Hakuna wakati ambao kunakuwa na foleni kubwa na zisizopungua kwa muda mrefu jijini Dar es Salaam kama kipindi cha mvua! Lakini jambo hili sio la kushangaza kwa sababu kila mwaka hali hii inajirudia. 

Na hiki ni kipindi ambacho mabosi wengi huchukia sana pengine kuliko vipindi vyote vya mwaka maana visingizio vya wafanyakazi wao kuchekelewa kazini kwa sababu ya mvua huwa haviishi. Kwa hiyo unakabiliana vipi na hali hiyo? 

Kwanza kabisa lazima uwe makini katika kuwahi kuamka mapema na pia njia ya usafiri utakayoitumia. Inakubidi kuwahi kuamka mapema sana kama unategemea usafiri wa umma au binafsi. Kwa sababu ukifanya hivyo kama kutakuwa na foleni barabarani basi utaziwahi ukilinganisha na ukichelewa kuingia barabarani. Lakini pia kama unategemea usafiri wa umma, mabasi ya mwendokasi ni mkombozi mkubwa kwenye kipindi hiki. Hivyo kwa maeneo ambayo usafiri huu unapatikana ni vema kuutumia ipasavyo kwa sababu yenyewe hayakai foleni kutokana na kuwa na njia zao pamoja na kupewa kipaumbele.    

Nunua vifaa vya kujikinga na mvua
Kutokana na jiji la Dar es Salaam kuwa na vipindi virefu vya jua na joto kali, imekuwa ni nadra sana kuwakuta wakazi wake wana vifaa vya kujikinga na mvua kama vile mwamvuli, koti, sweta au viatu vya mvua. Inashauriwa kuwa na vifaa hivi nyumbani kwako ili kujikinga ifikapo kipindi cha mvua na sio kuanza kufikiria kununua kwani inawezekana usiwe na bajeti hiyo pindi unapovihitaji. Vifaa hivyo ni muhimu kwani hukukinga na baridi, kutolawana, magonjwa na hata kutunza mavazi yako kutokana na maji ambayo huweza kusababisha kuharibika.
Umakini kwenye chombo chako cha usafiri 
Kwa wenye vyombo vya usafiri wanajua wenyewe ni kadhia gani wanayokumbana nayo ikifika kipindi cha mvua. Kipindi hiki ni jambo la kawaida kukuta magari kadhaa yamezimika au kukwama barabarani kutokana na sababu mbalimbali za kiufundi. Lakini pia barabara nyingi huharibika na kutopitika kabisa hivyo kulazimisha chombo chako kupita ni kujitafutia kuingia gharama zisizohitajika siku za usoni. Kama inawezekana tafuta njia mbadala ya usafiri katika kipindi hiki au pita kwenye njia ambazo una uhakika ni salama kwa chombo chako.

Kuwa makini na vifaa vyako vya umeme
Siyo vifaa vyote vya umeme vimetengenezwa vikiwa na uwezo wa kuzuia maji kutokuingia ndani yake. Licha ya makapuni mbalimbali kuja na teknolojia hiyo lakini unashauriwa kuwa makini sana aidha kwa kuvivika vifaa maalumu vya kuzuia maji au kuvikinga kabisa na maji. Kipindi hiki ndicho ambacho wengi hupatwa na majanga ya kuharibikiwa na simu, kompyuta, radio pamoja na luninga huko majumbani.

Kuwa makini na vyakula utakavyokula
Kama huwa unakuwa makini na aina ya vyakula unavyokula basi kipindi hiki inabidi uwe makini zaidi. Mvua zikinyesha jijini Dar es Salaam ndiyo kipindi ambacho pia kunakuwa na mlipuko wa magonjwa kadha wa kadha kama vile kipindupindu. Inashauriwa kula chakula sehemu ambayo unaiamini na inayozingatia usafi wa hali ya juu au kama inashindikana uwe unabeba chakula unachopika mwenyewe au kutokula kabisa.  

Tumia muda wako kusoma vitabu
Sio watu wote wana utaratibu wa kusoma vitabu kwenye siku zao za kawaida badala yake wanatazama filamu, kusikiliza muziki, kutoka wikendi au kupendelea kutembea. Lakini katika kipindi hiki ambacho mvua zinanyesha, barabara hazipitiki, hali ya hewa ni baridi na sehemu nyingi za starehe au kutembelea zinakosa watu ni vema ukajaribu kusoma vitabu. Amini usiamini kuwa hata kutazama filamu na kusikiliza muziki hufikia mahala vinachosha, hiki kinaweza kikawa ni kipindi kizuri cha kujaribu kitu tofauti, nunua vitabu na usome ili uongeze maarifa. 

Hivyo basi tusiifanye mvua ikawa ni kisingizio cha kutofanya shughuli zingine au majukumu mengine yanayotukabili. Kila kipindi huja na changamoto pamoja na fursa zake, ni vema kupambana nazo na kuzitumia ili kusonga mbele.