RAIS JAKAYA KIKWETE AMETANGAZA MABADILIKO HAYA YA MABALOZI…

RAIS JAKAYA KIKWETE AMETANGAZA MABADILIKO HAYA YA MABALOZI…

August 11, 2015


kasemaje-com-rais-jakaya-kikwete-ametangaza-mabadiliko-haya-ya-mabalozi_a291c5fa449d6f450ddc6acf36b8325d5e3ac509.jpgJioni ya Aug 11 Rais Jakaya Kikwete ametangaza mabadiliko ya Mabalozi kadhaa pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Mabadiliko hayo yamenifikia pia mtu wangu na barua hiyo imeandikwa hivi.
UTEUZI NA UHAMISHO WA MABALOZI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Joseph B. Masikitiko kuwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Kabla ya uteuzi huo Ndugu Masikitiko alikuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo (TBS).
Aidha, Rais Kikwete amefanya uteuzi wa Balozi mmoja na kuwabadilishia vituo vya kazi Mabalozi wawili kama ifuatavyo:
(i) Lt. Gen. Charles L. Makakala, ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe. Kabla ya uteuzi huo Lt. Gen. Makakala alikuwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (National Defence College).
(ii) Balozi Wilson Masilingi aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi amehamishwa kwenda kuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Liberata Mulamula aliyeteuliwa hivi karibuni kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa. Atakuwa pia anaiwakilisha Tanzania nchini Mexico
(iii)Balozi Irene Kasyanju aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi kushika nafasi inayoachwa wazi na Balozi Wilson Masilingi.
Taarifa iliyotolewa leo, Jumanne, Agosti 11, 2015 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue mjini Dar es Salaam inasema kuwa Uteuzi na uhamisho huu unaanzia tarehe 07 Agosti, 2015.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
11 Agosti, 2015
SOURCE - Millard Ayo
KAMATI KUU YA CCM YAFANYIKA LEO MJINI DODOMA

KAMATI KUU YA CCM YAFANYIKA LEO MJINI DODOMA

August 11, 2015

unnamed (85)
Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati kuu ya CCM kilchofanyika katika ukumbi wa White house, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo.(Picha na Freddy Maro)
unnamed (86)
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifungua kikao cha Kamati Kuu ya CCM, leo Agosti, 11, 2015 katika ukumbi wa Jengo la White House Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. (Picha na Bashir Nkoromo).
unnamed (87)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa katika Kikao cha Kamati Kuu ya CCM, leo Agosti, 11, 2015 katika ukumbi wa Jengo la White House Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. (Picha na Bashir Nkoromo).
unnamed (88)
Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Steven Wasira na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Adam Kimbisa wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza kikao cha Kamati Kuu ya CCM leo mjini Dodoma. (Picha na Bashir Nkoromo).
unnamed (89)
Wajumbe wa Kamati Kuu, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Adam Kimbisa na Dk. Emmanuel Nchimbi, wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza kikao cha Kamati Kuu ya CCM leo mjini Dodoma. (Picha na Bashir Nkoromo).
unnamed (90)
Wajumbe wa Kamati Kuu, Dk. Maua Daftari na Samia Suluhu Hassan, wakibadilishana mawazo ukumbini, kabla ya kuanza kikao cha Kamati Kuu ya CCM, leo mjini Dodoma. (Picha na Bashir Nkoromo).
unnamed (91)
Mjumbe wa Kamati Kuu, Adam Kimbisa akiwasalimia wajumbe wenzake ukumbini kabla ya kuanza kikao cha Kamati Kuu ya CCM leo mjini Dodoma. Kutoka kulia ni Shamsi Vuai Nahodha, Zakia Meghji na Dk. Salim Ahmed Salim. (Picha na Bashir Nkoromo).
unnamed (92)
Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Zakiah Meghji na Dk. Asha-rRose Migiro wakibadilishana mawazo ukumbini kabla ya kuanza kikao cha Kamati Kuu ya CCm leo mjini Dodoma. (Picha na Bashir Nkoromo).
unnamed (93)
Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Ameir Pandu Kificho akibadilishana mawazo na mjumbe mwenzake, Khadija Adood, kabla ya kikao cha Kamati Kuu ya CCM kuanza leo mjini Dodoma. (Picha na Bashir Nkoromo)
unnamed (94)
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akibadilishana mawazo na Mjumbe mwenzake wa Kamati Kuu, Zakiah Meghji kabla ya kikao cha Kamati Kuu kuanza leo mjini Dodoma. (Picha na Bashir Nkoromo)
 Kampuni ya Tigo yapata Tuzo ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa Mkoani Lindi

Kampuni ya Tigo yapata Tuzo ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa Mkoani Lindi

August 11, 2015
unnamed (79)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete akikabidhi tuzo ya ushindi wa kwanza ya kipengele cha mawasiliano kwa Meneja wa Mauzo wa Tigo mkoani Lindi, Eric Stephen kwenye maonesho ya Nanenane yaliyofanyika kitaifa Mkoani Lindi mwishoni mwa wiki.
unnamed (80)
Meneja wa Mauzo wa Tigo mkoani Lindi, Eric Stephen(kulia) na Afisa Utawala Tigo Lindi, Jacob Masawe  wakipozi na kombe walilopata la tuzo ya ushindi wa kwanza ya kipengele cha mawasiliano kwenye maonesho ya Nanenane.
unnamed (81)
Afisa Utawala Tigo Lindi, Jacob Masawe(kushoto),Meneja wa Mauzo wa Tigo mkoani Lindi, Eric Stephen(katikati) na Meneja wa Tigo kanda ya Pwani Kusini mikoa ya Lindi na Mtwara,  Nderingo Materu wakipozi kwenye picha ya pamoja.
unnamed (82)
Meneja wa Mauzo wa Tigo mkoani Lindi, Eric Stephen akinyanyua kombe juu.
unnamed (83)
Meneja wa Mauzo wa Tigo mkoani Lindi, Eric Stephen akiwa kwenye picha ya pamoja na kikundi cha burudani
the 3rd Annual Cyber Defense East Africa Summit held in Dar Es Salaam on 11-08-2015

the 3rd Annual Cyber Defense East Africa Summit held in Dar Es Salaam on 11-08-2015

August 11, 2015

SONY DSC
The Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA) Director General Dr. Ally Yahaya Simba (left), addresses the 3rd Annual Cyber Defense East Africa Summit held in Dar Es Salaam on 11-08-2015. The event was opened by e-Government Agency Chief Executive Officer (CEO) Dr. Jabiri Kuwe Bakari (right) on-behalf of the Chief Secretary, Ambassador Ombeni Sefue. . (Photo by  Courtesy  TCRA)
SONY DSC
The Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA) Director General Dr. Ally Yahaya Simba (right), e-Government Agency Chief Executive Officer (CEO) Dr. Jabiri Kuwe Bakari (centre) and of Dar Es Salaam  Teknohama Business Incubator (DTBi)CEO, Eng. George Mulamula  address a news conference during the 3rd Annual  Cyber Defense East Africa Summit held  in Dar Es salaam on 11-08-2015. Dr. Bakari opened the summit on-behalf of the Chief Secretary, Ambassador Ombeni Sefue. (Photo by  Courtesy  TCRA)

WLAC YAENDESHA KONGAMANO LA UHAMASISHAJI KUPIGA KURA KWA WANAWAKE WALIO KATIKA MAKUNDI MAALUMU

August 11, 2015

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake na Watoto (WLAC), Theodosia Muhulo Nshala, akizungumza na wanahabari katika kongamano hilo.
 Mwanaharakati wa masuala ya haki za binadamu, Gema Akilimali, akitoa mada kwenye kongamano la uhamashaji upigaji kura lililofanyika Dar es Salaam leo asubuhi. Kongamano hilo liloandaliwa mahususi kwa watu wa kundi maalumu liliandaliwa na Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC)
 Mmoja wa washiriki wa kongamano hilo, Kuruthum Dindili (katikati), akizungumza na wanahabari katika kongamano hilo.
 Kongamano likiendelea.
Kongamano likiendelea.
……………………………………………………………………………
Na Dotto Mwaibale
 
WALEMAVU wenye mahitaji maalum wameonekana kusahaulika na serikali kwa kuwawezesha kufikia haki zao kama mchakato wa kupiga kura kutokana na kukosekana kwa miundombinu rafiki.
 
Kauli hiyo imetolewa Dar es Salaam leo asubuhi  na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake na Watoto (WLAC), Theodosia Muhulo wakati wa mafunzo kwa wanawake walemavu wenye mahitaji maalum kuelekea uchaguzi.
 
Lengo ikiwa ni ushiriki wa wanawake wenye mahitaji maalum katika kushiriki na kujitokeza  katika mchakato wa uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25,mwaka huu pamoja na kujenga na kukuza uelewa.
 
“Kundi hili limesahaulika kwa serikali yetu hivyo kwa kuwapa semina hii kunawafanya wasionekane kutengwa na jamii ndiyo maana tumeona tuwaite na kuwaongezea uelewa wao katika kushiriki uchaguzi mkuu ikiwa ni pamoja na kushiriki,kuchagua na kuchaguliwa,”alisema
 
Alisema serikali inapaswa kujua mahitaji ya walemavu kwenye michakato ya jamii,kwani hakuna sehemu maalum ya watu wa kundi hilo kwa kuwawekea miundombinu kama sehemu zenye ngazi ili kuweza kufika bila tatizo lolote.
 
Muhulo alisema wanawake wanapaswa wajitokeze kupiga kura ili waweze kuchagua na kuchaguliwa kwa kumshagua rais, wabunge na diwani  ili waweze kuletewa maendeleo na mabadiliko  katika jamii zao na si kubaki nyuma.
 
Kwa upande wake  Mbunge wa viti Maalum kupitia Umoja wa Wazazi nchini wa Chama cha Mapinduzi,Kuruthumu Dindili, alimpongeza rais Kikwete anayemaliza muda wake kwa kuwa ni mpenzi wa watu lakini walikosa wa kuwawakilisha bungeni kwani anaamini wangefaidika.
 
“Kwa bunge lilikopita hatukuwa na mwakilishi bungeni wa kuweza kutusemea malalamiko yetu hasa kwa watu wenye ulemavu wa viungo  kwa maana wangekuwepo tungefaidika na mambo mengi sana, walikuwa wamekaa tu kimya bungeni wenzetu wananufaika wao…sisi walemavu hakuna tuanachokipata kupitia wao ndio maana tumeona tuingie na sisi kwenye mchakato,”alisema 
 
Alisema wanapojitoa kugombea nafasi mbalimbali za kiuongozi wanaonekana ni kichekesho kwa wale wasiokuwa  walemavu na kuwabeza kwa kukosa fedha za kufanyia kampeni, aliitaka serikali kwa kutoa nafasi nyingi za wawakilishi walemavu  katika bunge lijalo ili kuwe na sauti nyingi za kuleta maendekeo ya kupata mahitaji ya kimsingi kuanzia ngazi za afya, elimu.
Aidha semina hiyo ilihudhuliwa na Chama cha walemavu wa viungo(Chawata), Chama cha Walemavu wa Ngozi(Tas), Chama cha Wasioona (TLD), Chama cha Viziwi Wasioona(Tasodep), Chama cha wazazi wenye watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi(Asbat) pamoja na Chama cha Afya na Akili(Tuspo).
 
IBF Africa, Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred waandaa ngumi za kulipwa kuchangia albino

IBF Africa, Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred waandaa ngumi za kulipwa kuchangia albino

August 11, 2015

unnamed (95)
Rais wa IBF Africa, Onesmo Ngowi (wa kwanza kulia) akizungumzia mapambano ya ngumi ya kulipwa yaliyopangwa kufanyika Novemba 28 jijini kwa ajili ya kutafuta fedha za uchangia watu wenye ulemavu wa ngozi(albino), wa pili kulia ni Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred na wa Rais wa TPBO Limited, Yasin “Ustadh” Abdallah.
unnamed (96)
Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred (wa pili kushoto) akiwa na viongozi wa juu wa ngumi za kulipwa nchini, Onesmo Ngowi (Rais wa IBF Africa, wa kwanza kushoto), Emmanuel Mlundwa (rais wa PST) na Yasin Abdallah (Rais wa TPBO-Limited) mara baada ya kutangaza mapambano ya ngumi ya kulipwa yaliyopangwa kufanyika Novemba 28 jijini kwa ajili ya kutafuta fedha kwa ajili ya kuchangia watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino).
………………………………………………………………………………………
Na Mwandishi wetu
Shirikisho la Ngumi za kulipwa la Afrika (IBF Africa) kwa kushirikiana na Taasisi ya Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred Foundation (BAF) na kampuni ya Kango wameandaa mapambano ya ngumi ya kimataifa kwa kushirikisha mabondia nyota duniani.
Mapmbano hayo yamepangwa kufanyika Novemba 28 kwenye ukumbi wa Mlimani City na lengo lake kubwa ni kutafuta fedha za kusaidia watu wenye ulemavu wa ngozi (albino).
Rais wa IBF Africa, Onesmo Ngowi alisema kuwa siku hiyo imepewa jina la  “knock out albinos killers” (piga wanaua albino) ambapo bondia kutoka Denmark, Lolenga Mock atapigana na bondia nyota wa Zambia, Chioctha Chimwemwe  katika pambano la uzito wa super middle la  IBF continental Africa super.
Pambano hilo limepangwa kuwa la raundi 12 na litafuatiwa na pambano lingine la kulipiza kisasi kati ya bondia kutoka Afrika Kusini, Phillip Ndou atakayepambana na Mtanzania, Ramadhan Shauri kuwania ubingwa wa IBF-Continental Africa welterweight  ambalo pia litakuwa la raundi 12.
Bondia nyota wa Tanzania, Cosmas Cheka naye atapanda ulingoni kupambana na Gottlieb Ndokosho wa Namibia kuwania ubingwa wa IBF continental Africa super-feather.
Mabondia wa Kenya, Geoffrey Munika na James Onyango nao wataingia ulingoni kupambana na mabondia kutoka china na Iran ambao watajulikana baadaye.
Pia kutakuwa na pambano mengine ambayo yatawakutanisha mabondia wanawake, Lulu Kayage dhidi ya bondia atakayetangazwa baadaye kuwania ubingwa wa IBF Africa flyweight.
“Lengo ni kutafuta fedha za kuchangia kununua vifaa maalum kwa albino na mpaka sasa maandalizi yanaenda vizuri, hii ni tukio kubwa sana kwa ngumi za kulipwa hapa nchini,” alisema Ngowi.
Alisema kuwa wameamua kushirikiana na Brigitte kutokana na kutambua juhudi zake za kutetea albino baada ya kuwajengea bweni eneo la Buhangija, Shinyanga na taasisi yake kwa kushirikiana na Junior Achievements (JA) wanatoa elimu ya ujasiriamali kwa jamii hiyo.
“Brigitte akiwa mwenye mashindano ya urembo ya dunia, 2012, aliweka rekodi ya kushika nafasi ya tatu katika mashindano ya ‘urembo wenye malengo maalum” au Beuty with purpose”, alipeleka kazi yake ya ujenzi wa bweni la albino mkoani shinyanga, imetupa faraja sana na kuamua kumuunga mkono katika vita hiyo,” alisema.
Brigitte alishukuru kuungwa mkono na kuomba wadhamini kujitokeza kusaidia shughuli hiyo ambayo baada ya ngumi, pia kutakuwa na mbio za marathon mkoani Kilimanjaro zenye lengo hilo hilo.
“Tumeandaa mbio za Marathon mkoani Kilimanjaro wiki moja baada ya ngumi, mbali yam bio hizo, pia kutakuwa na zoezi la kupanda mlima Kilimanjaro, lengo ni kutafuta fedha na vile vile kutangaza utalii wetu, naomba makampuni yajitokeze,” alisema Brigitte.

MENEJIMENTI YA OFISI YA MKUU WA MKOA WA RUKWA YAMPONGEZA MKUU WA MKOA HUO ENG. STELLA MANYANYA KWA USHINDI WA KISHINDO KURA ZA MAONI CCM JIMBO LA MBINGA MAGHARIBI

August 11, 2015


Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa ambaye pia ni Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Ndugu Erasmus Rugarabamu kwa niaba ya Menejimenti ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa akitoa pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya ambaye pia ni Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma kwa ushindi mnono alioupata katika kura za maoni za Chama cha Mapinduzi (CCM) katika kutafuta mgombea wa ubunge Jimbo la Mbinga Magharibi. Eng. Manyanya alishinda kwa kura 13,276 ambapo mshindi wa pili alikua na kura 3,466. Jumla ya wagombea walikua 10 ambapo tisa kati yao walikuwa ni wanaume.
 Awali Jimbo hilo lilikuwa nimeshikiliwa na hayati Capt. John Komba. Kwasasa imebaki hatua ya mwisho ya majina ya wagombea kupitishwa na Uongozi wa juu wa Chama kwa ajili ya kupeperusha bendera ya Chama  cha Mapinduzi majimboni katika uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba mwaka huu 2015. Uongozi na Watumishi wote wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa unamtakia kila la heri Eng. Manyanya katika safari yake hiyo na hatimae aweze kushinda katika Jimbo hilo. 
Akitoa shukurani kwa niaba ya watumishi Katibu Tawala Msaidizi Kitengo cha Serikali za Mitaa Ndugu Albinus Mgonya alimpongeza Mkuu huyo wa Mkoa wa Rukwa kwa msukumo mkubwa wa maendeleo aliouweka katika kipindi cha uongozi wake hususani katika sekta ya elimu ambapo alianzisha Azimio la Kasense kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu mashuleni, Kuboresha afya ya mama wajawazito na watoto wachanga, usafi wa mazingira ambapo alianzisha kampeni ya Sumbawanga Ng'ara iliyozinduliwa na Mhe. Makamu wa Rais, Kampeni ya upandaji miti, kuboresha mazingira ya utalii katika maporomoko ya Mto Kalambo, kuboresha hali ya ulinzi na usalama katika Mkoa, Kuwaunganisha watumishi na viongozi katika kufanya kazi kwa pamoja n.k 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa katika kikao kifupi cha kumpongeza baada ya kushinda katika kura za maoni Jimbo la Nyasa Magharibi kupitia CCM. Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka Viongozi hao pamoja na watumishi kusimamia misingi aliyoiweka ya kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu mkubwa, kufanya kazi kwa pamoja (team work) na kutekeleza majumu yao ya kila siku kwa ufanisi na ubunifu wa hali ya juu. Alisistiza kuwa maendeleo ya taifa la Tanzania hayataletwa tu kwa kutegemea vyama vya siasa bali kwa wananchi na wafanyakazi kutekeleza majukumu na wajibu wao ipasavyo kwa kuweka uzalendo mbele na kufanya kazi kwa bidii na uadilifu uliotukuka.   
 
 Katibu Tawala Msaidizi Kitengo cha Serikali za Mitaa Ndugu Albinus Mgonya akitoa Shukrani na Salamu za pongezi kwa niaba ya watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwa Mkuu wa Mkoa huo Eng. Stella Manyanya kufuatia ushindi alioupata katika kura za maoni kutafuta mgombea wa CCM Jimbo la Mbinga Magharibi. Kwa sasa Mhe. Eng. Manyanya.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa.

WATANZANIA WAMEASWA KUHIFADHI MAZINGIRA.

August 11, 2015

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Sazi Salula akifungua Mkutano wa wadau wa mazingira unaohusu Miradi ya majaribio nchini wa Mkakati wa Kupunguza Uharibifu wa Misitu (MKUHUMI) leo jijini Dar es salaam.
 Kiongozi wa wawezeshaji kutoka Asasi isiyo ya kiserikali ya Niras kutoka Finland inayosimamia Miradi ya majaribio nchini wa Mkakati wa Kupunguza Uharibifu wa Misitu (MKUHUMI) Merja Makela akitoa mada wakati wa mkutano wa wadau wa mazingira kuhusu namna bora ya kuhifadhi mazingira na kuboresha usimamizi wa ardhi na kuongeza mapato kutoka kwenye misitu. Mkutano huo ambao umefanyika leo jijini Dar es salaam umeandaliwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Norway.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Sazi Salula (kushoto) akifuatilia mada wakati wa mkutano wa wadau wa mazingira kuhusu namna bora ya kuhifadhi mazingira na kuboresha usimamizi wa ardhi na kuongeza mapato kutoka kwenye misitu. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Julius Ningu.

KAMATI KUU YAAGIZA KURA ZA MAONI KURUDIWA KATIKA MAJIMBO MATANO

August 11, 2015

Nape Nnauye akizungumza kwenye moja ya mikutano na waandishi wa habari

KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CC) imeagiza kurudiwa kwa uchaguzi   katika majimbo matano  kutokana na dosari mbalimbali zilizojitokeza katika mchakato wa kura ya maoni.
Majimbo hayo ni Makete,Busega,Ukonga,Rufiji na Kilolo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dodoma Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye amesema mchakato  huo utarudiwa siku ya alhamisi Agosti 13.

Amesema baada ya uchaguzi huo matokeo yatapelekwa katika vikao vinavyoendelea kwa ajili ya uamuzi.
Akizungumzia kuhusu vikao vinavyoendelea Ndugu Nape amesema vikao hivyo vinaendelea vizuri ambapo jana kikao cha kamati ya maadili kiliendelea mpaka usiku.
Amesema leo wanatarajia kumaliza  kikao cha CC ambapo kesho na kesho kutwa watamaliza na kikao cha halmashauri kuu ya chama hicho(NEC) kama ilivyopangwa.
chanzo:CCM BLOG

PICHA MATUKIO: LOWASA ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS 2015, SHUHUDIA TUKIO LOTE HAPA

August 11, 2015
MGOMBEA wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa amechukua fomu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ya kuwania nafasi hiyo leo Jumatatu Agosti 10, 2015.
Msafara wa Mgombea huyo ulioanzia kwenye Ofisi za Chama cha Wananchi CUF Buguruni na kuishia kwenye Ofisi za CHADEMA Kinondoni Jijini Dar es salaam na kupelekea msongamano mkubwa wa watu ambao wengi wao ni wafuasi wakuu wa vyama vinavyounda UKAWA, na kufanya shughuli mbali mbali kusimama kwa muda wa takribani saa saba. 

Umati wa watu wakiwemo wafuasi wa vyama vya Siasa vinavyounda UKAWA ukiwa Umefurika kwa wingi kwenye Barabara ya Uhuru, Jijini Dar es salaam kumsindikiza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni, walipokuwa wakielekea Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuchukua Fomu ya kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba 25, mwaka huu. 

Sehemu ya Wapenzi wa vyama vinavyounda UKAWA wakiushangilia Msafara wa MGOMBEA wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa wakati akielekea Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuchukua Fomu ya kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba 25, mwaka huu.













Mh. Freeman Mbowe, Mh. Tundu Lissu na Mh. James Mbatia wakiwa kwenye magari yao wakati wakimsindikiza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni, walipokuwa wakielekea Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuchukua Fomu ya kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba 25, mwaka huu.

Barabara ya Uhuru, Jijini Dar.