TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI

TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI

December 08, 2015
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetuma salamu za rambirambi kwa familia ya marehem Willie Chiwango aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki na mazishi kufanyika eneo la Buguruni jijini Dar e salaam.
Katika salam zake, TFF inawapa pole familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na kusema kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini, wako pamoja katika kipindi hiki cha maombolezo.
Marehemu Willie Chiwango ni miongoni mwa waandishi wa habari wa michezo wakongwe kabisa, aliambatana na timu ya taifa ‘Taifa Stars’ iliyoshiriki michuano ya Mataifa Afrika mwaka 1980 nchini Nigeria.
TFF ilimpa cheti cha heshima marehemu Chiwango katika zoezi la kuwakumbuka na kutambua mchango wa viongozi, wachezaji, waandishi wa habari za michezo waliojitoa katika sekta ya mpira wa miguu nchini.

TUNATOKA MAHAKAMANI KUSIKILIZA PINGAMIZI

December 08, 2015


 Mbunge wa jimbo la Tanga mjini kupiia Chama Cha Wananchi CUF, Mussa Mbarouk wapili kushoto akitoka mahakamani kusikiliza kipingamizi iliyowekwa na aliekuwa mgombea wa jimbo hilo, Omari Nundeu kupinga ushindi wake.



Mfuasi wa CCM, Kassim Omary, akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama kulalamikia wanachama ndani ya chama kukihujumu na kupelekea baadhi ya maeneo kuchukuliwa na wapinzani.
RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MABALOZI WA MALAWI NA SWEDEN IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MABALOZI WA MALAWI NA SWEDEN IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

December 08, 2015


bal1 
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Balozi wa Malawi hapa nchini Mhe. Hawa Ndilowe  Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Desemba 8, 2015
bal2 
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika mazungumzo  na Balozi wa Malawi hapa nchini Mhe. Hawa Ndilowe  Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Desemba 8, 2015
bal5
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipokea barua za salamu toka na Balozi wa Sweden hapa nchini Mhe. Katarina Rangnitt alipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Desemba 8, 2015.
PICHA NA IKULU
U15 YAREJEA DAR

U15 YAREJEA DAR

December 08, 2015

u15camp 
Ziara ya timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U15) iliyoanzia kanda ya ziwa na kanda ya Magharibi kisha kuendelea katika nchi za Rwanda, Uganda na Kenya mwezi huu imesitishwa kutokana na kufungwa akaunti za Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA).
Timu hiyo ya vijana iliondoka wiki iliyopita kuelekea jijin Mwanza, ambapo iliagwa na kukabidhiwa bendera ya Taifa na katibu mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel, ilicheza mchezo mmoja wa kirafiki na timu ya Alliance kabla ya kuelekea mkoani Kigoma.
Ikiwa Kigoma U-15 ilicheza michezo miwili ya kirafiki na timu ya kombaini ya mkoa wa Kigoma U-15, jumapili ikacheza mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya Burundi U-17, na jana asubuhi kuanza safari ya kurejea jijini Dar essalaam.
Awali ziara ya timu hiyo ya U-15 ilikua iendelee katika mji wa Kigali kwa kucheza na U17 ya Rwanda, Kampala kucheza na Uganda U17, jijini Nairobi kwa kucheza na U17 ya Kenya na kumaliza ziara hiyo kwa kuchez ana U15 kombaini ya mkoa wa Arusha Disemba 23, na kurejea jijin Dar es salaam Disemba 24, 2015.
U-15 inajiandaa na michuano ya Viajana U17 kuwania kufuzu kwa Mataifa ya Afrika mwaka 2017 nchini Madagascar itakayoanza kutimua vumbi Juni 2016.
Katibu mtendaji BAKITA amkabidhi kamusi kuu mpya ya kiswahili katibu mkuu wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo.

Katibu mtendaji BAKITA amkabidhi kamusi kuu mpya ya kiswahili katibu mkuu wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo.

December 08, 2015

index 
Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel(kulia) akikabidhiwa kamusi kuu mpya ya Kiswahili kutoka kwa Katibu Mtendaji kutoka baraza la Kiswahili la Taifa(BAKITA) Dkt Selemani Sewangi.Kamusi hiyo mpya ina jumla ya maneno makuu Zaidi ya elfu thelathini na sita(36000) na kurasa 1264.
index2 
Katibu Mtendaji kutoka baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt Selemani Sewangi(kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel kwa baadhi ya maneno ambayo yapo katika kamusi mpya iliyotolewa na Baraza hilo leo jijini Dar es Salaam.
KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA MAGEREZA NCHINI AONGOZA KIKAO MAALUM CHA KUPITIA RASIMU YA MPANGO WA WA JESHI LA MAGEREZA

KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA MAGEREZA NCHINI AONGOZA KIKAO MAALUM CHA KUPITIA RASIMU YA MPANGO WA WA JESHI LA MAGEREZA

December 08, 2015

min1 
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akifungua Kikao Maalum cha Wadau kutoka nje ya Magereza(hawapo pichani) cha kujadili rasimu ya Mpango wa Jeshi la Magereza wa kujitosheleza kwa chakula cha Wafungwa waliopo Magerezani. Kikao hicho kimefanyika leo Desemba 8, 2015 katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam.
min2 
Mshauri Mwelekezi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Beatus Kundy(aliyesimama) akiwasilisha rasimu ya Mpango wa Jeshi la Magereza wa kujitosheleza kwa chakula cha Wafungwa waliopo Magerezani. Jeshi la Magereza limeandaa rasimu hiyo ili kuipunguzia Serikali gharama za kuwalisha wafungwa waliopo magerezani.
min3 
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini uwasilishaji wa Andiko hilo(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Eng. Deonice Chamulesile(wa pili kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa pili kushoto) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga.
min4Mwakilishi kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Hashim Kimmwe akitoa mchango wake wakati wa kujadili rasimu ya Mpango wa Jeshi la Magereza wa kujitosheleza kwa chakula cha Wafungwa waliopo Magerezani.
min5 
Wataalam wa Jeshi la Magereza walioshiriki kikamilifu katika maandalizi ya Andiko la Mpango wa Jeshi la Magereza kujitosheleza kwa chakula kwa kushirikiana na Mshauri Mwelekezi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakifuatilia majadiliano ya rasimu hiyo(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

TGDC NA MKAKATI WA UZALISHAJI WA UMEME KUPITIA JOTOARDHI

December 08, 2015

 Meneja Mkuu Shirika la Uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mhandisi Boniface Njombe (kushoto) pamoja na Mtaalamu Mkuu toka Kampuni ya TOSHIBA Bwana Kentaro Kurahara wakiweka saini Mkataba wa wa Maelewano (MOU) wa kufanya tafiti kwa pamoja zinahusu maeneo yenye viashiria ya upatikanaji wa nishati ya jotoardhi katika Ofisi za TGDC zilizopo Jijini Dar es Salaam.
 Meneja Mkuu Shirika la Uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mhandisi Boniface Njombe (kushoto) pamoja na Mtaalamu Mkuu toka Kampuni ya TOSHIBA Bwana Kentaro Kurahara wakikabidhiana Mkataba wa Maelewano (MOU) wa kufanya tafiti kwa pamoja zinahusu maeneo yenye viashiria ya upatikanaji wa nishati ya jotoardhi katika Ofisi za TGDC zilizopo Jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Paul Masanja (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa ICEIDA, Bwana Engilbert Gudmundsson, wakiweka saini Mkataba wa Makubaliano ya Ushirkiano wa kufanya tafiti kwa pamoja zinahusu maeneo yenye viashiria ya upatikanaji wa nishati ya jotoardhi katika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini zilizopo Jijini Dar es Salaam.

Na Benedict Liwenga-MAELEZO.
KUTOKANA na ongezeko la mahitaji ya nishati ya umeme nchini, nishati itokanayo na jotoardhi (Geothermal Energy) imetajwa kuwa ni muhimu katika kuepukana na hasara kubwa na isiyo ya lazima inayotokana na matumizi ya mitambo ya mafuta katika kuzalisha umeme na kuifanya Tanzania kuondokana na tatizo la umeme usiokuwa na uhakika pamoja na kuleta maendeleo nchini.
Ili kuleta Maendeleo haya katika sekta ya nishati, Tanzania hainabudi kugeukia katika vyanzo vingine vya uzalishaji umeme ikiwemo nishati hiyo ambayo kwa kutumia mvuke wa maji yaliyochemshwa na joto la asili lililopo chini ya ardhi, nishati ya umeme inaweza kuzalishwa na kukidhi mahitaji ya nishati ambayo yatasaidia kuwa kiunganishi cha ukuaji wa uchumi nchini. 
Tanzania iko katika ukanda wa Bonde la Ufa (Rift Valley), hivyo kuna uwezekano mkubwa wa uwepo wa hifadhi kubwa ya nishati itokanayo na jotoardhi ambayo inaweza kutumika katika uzalishaji wa umeme na kuinua uchumi wan chi yetu.
Nishati hii itakuwa mkombozi kwa taifa letu hususani kwa mwananchi wa kipato cha chini kwani tunaamini kuwa matumizi ya nishati hiyo yatapelekea kupungua kwa gharama za manunuzi ya umeme na kutokana na ukweli kwamba nishati hiyo pindi ipatakinapo haitarajiwi kuisha.
Unafuu wa umeme utakaozalishwa na jotoardhi unatokana na ukweli kwamba mitambo inayotumika kuzalisha umeme huo kuendeshwa kwa mvuke ambao unatokana na majimoto toka ardhini tofauti na uzalishaji wa umeme uliokuwa unatumika kwa kutumia mitambo yenye kutumia mafuta ambayo gharama yake ilikuwa juu kwa Serikali.
Hapa nchini, kuna viashiria vingi vinaonyesha uwepo wa jotoardhi hasa kwa maeneo ya vijijini ambako umeme sehemu nyingi haujafika, kutokana na hilo sasa Serikali yetu hainabudi kutupia macho katika nishati hii kwa kuhakikisha kwamba wananchi ambao wnaaishi maeneo ambayo nishati hiyo inapatikana wananufaika na umeme huo.
Jotoardhi ina matumizi mengi kwa jamii yetu, mfano majimoto yatokayo ardhini yanaweza kutumika katika kukaushia mazao mfano matumizi ya Vitalu shamba(Green Houses) badala ya kutegemea jua. Mwananchi wa kipato wa chini anaweza kutumia majimoto kukausha mazao yake kwa mfano mpunga, maharage, mahindi, karanga katika ubora ule ule kama wa jua. 
Matumizi mengine ya majimoto ni katika kupasha nyumba joto hasa katika wananchi wale waishio mikoa yenye baridi kali kwa kujenga mabomba ya kupitisha maji ya moto ndani ya nyumba zao.
Shirika la Uendelezaji Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC) imepewa lengo na Serikali la kuhakikisha kuwa inazalisha umeme wa Megawati 200 na kuuingiza katika gridi ya Taifa kufikia mwaka 2020.
Hivi karibuni, TGDC kwa kushirikiana na Benki ya Dunia (ESMAP) zilifanya warsha ya siku mbili iliyofanyika Jijini Dar es Salaam ambayo iliwakutanisha wadau kutoka Mashirika mbalimbali yanayoshughulikia masuala ya jotoardhi yakiwemo GDC la Kenya, Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), BGR la Ujerumani, ICEIDA la Iceland, Chuo cha Umoja wa Mataifa kinachofundisha nishati ya Jotoardhi (UNU), TNO la Uholanzi pamoja na Shirika la Star Energy la nchini Indonesia ambapo wadau hawa wote wameweza kufanikiwa kuipata nishati hiyo, hivyo watatoa mchango mkubwa kuliwezesha shirika la TGDC kupata mafanikio na hatimaye nishati hiyo kuweza kupatikana.
Katika warsha hiyo, Meneja Mkuu wa Shirika la Uendelezaji nishati ya Jotoardhi (TGDC), Mhandisi Boniface Njombe alisema kuwa warsha hiyo inalenga kujadili kwa kina njia mbalimbali zilizotumiwa na baadhi ya mashirika hayo hadi kufanikiwa kupata nishati hiyo ikiwemo uanishaji wa huduma tofauti zifanywazo na mashirika hayo katika kulisaidia shirika la TGDC. 
“Matokeo ya warsha hii tuliyoifanya tumeweza kuwasiliana na wenzetu wa Benki ya Dunia (ESMAP) kwa kukusanya wataalam toka taasisi mbalimbali pamoja na Mashirika mbalimbali ambayo yamewahi kufanya kazi hii ya utafutaji wa nishati ya jotoardhi na lengo letu ni kutaka kufahamu njia ambazo wenzetu walizitumia mpaka kufanikiwa ili na sisi tupate kujifunza”, alisema Njombe.
Mhandisi Njombe aliongeza kuwa warsha hiyo itawezesha rasilimali chache zilizopo ziweze kutumika ipasavyo katika kuleta matokeo ambayo TGDC inatarajia kuyapata ili kuhakikisha kuwa lengo la upatikanaji wa nishati hiyo linafikiwa.
Sambamba na warsha hiyo, Serikali kupitia TGDC na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la nchini Iceland (ICEIDA), wamesaini Mkataba wa Makubaliano utakaowezesha Tanzania kunufaika na msaada wa kiasi cha Dola za Marekani 1,565,000 kwa ajili ya kupata Mtaalam mwelekezi kufanya tafiti katika maeneo yenye viashiria vya Jotoardhi ikiwemo kuwajengea uwezo Wataalam wetu wa hapa nchini pamoja na kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya utafiti wa nishati hiyo.
Makubaliano hayo yalifikiwa Jijini Dar es Salaam katika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini, kati ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Paul Masanja na Mkurugenzi Mkuu wa ICEIDA, Bwana Engilbert Gudmundsson, huku likishuhudiwa na Meneja Mkuu wa TGDC, Mhandisi Boniface Njombe, Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Uendelezaji wa Nishati Jadidifu, Bwana Edward Ishengoma pamoja na baadhi ya Maafisa kutoka TGDC na Wizara ya Nishati na Madini.
Akizungumza wakati wa utiaji saini wa Mkataba huo, Mhandisi Paul Masanja alisema kuwa, matarajio ya Tanzania ni kuzalisha kiasi cha megawati 200 za umeme unaotokana na nishati ya jotoardhi ifikapo mwaka 2020, ambapo taarifa za awali zinaeleza kuwa, hazina iliyopo kupitia nishati hiyo ina uwezo wa kuzalisha zaidi ya umeme wa megawati 5,000, kutokana na nishati ya jotoardhi toka ardhini.
Mhandisi Masanja aliongeza kuwa, utayari na ushirikiano unaoonyeshwa na nchi ya Iceland kupitia Shirika la ICEIDA itakuwa kichocheo kikubwa kufikia malengo ya Serikali ya kuwa na nishati ya kutosha ya umeme na kuchochea maendeleo nchini.
“Tuna malengo mengi kupitia nishati hii ya jotoardhi, utafiti ndio njia itakayotufanya kufikia malengo haya, ushirikiano huu ni mwanzo mzuri kwa upande wetu sisi Tanzania, na nafahamu kuwa Iceland mlianzia katika hatua za chini kabisa lakini sasa mko mbali, zoefu wenu katika masuala haya ya nishati hii utatuwezesha kuweza kufika mahali tunapotarajia,” alisema Mhandisi Masanja.
Naye, Mkurugenzi wa ICEIDA, Bwana Engilbert Gudmundsson alieleza juu ya umuhimu wa nishati hiyo na unafuu wake wa gharama ikilinganishwa na nishati nyingine na kueleza kuwa, zaidi ya asilimia 25 ya umeme unaozalishwa nchini Iceland unatokana na nishati ya jotoardhi, hivyo Tanzania inaweza kufikia malengo yake ya kupata nishati hiyo kwa kuonyesha juhudi zake ikiwemo kushirikiana na ICEIDA.
“Sisi Ilituchukua kipindi cha miaka 25 kufikia mafanikio tuliyonayo katika nishati ya jotoardhi, hivyo kutokana na uzoefu wetu huu hatunabudi kutoa uzoefu wetu kwa TGDC ili kuhakikisha inafakia malengo,” alisema Gudmundsson.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TGDC, Mhandisi Boniface Njombe alishukuru na kuonyesha hali ya utayari wa ICEIDA katika kuhakikisha kwamba Tanzania inafikia malengo yake ya kuendeleza nishati hiyo, utakaosadia kufanyika kwa tafiti katika maeneo mbalimbali yenye viashiria vya nishati hiyo kama vile maeneo ya Luhoi pamoja na Kibiti Mkoa wa Pwani.
Mhandisi Njombe anabainisha kuwa, kutokana na utafiti utakaofanywa kwa ushirikiano kati ya TGDC na ICEIDA, utawezesha upatikanaji wa takwimu sahihi na halisi ambazo zitafungua njia ya kupata misaada zaidi kutoka katika taasisi na wahisani mbalimbali ambao wamejikita katika masuala nishati hiyo.
Moja ya hatua mbalimbali ambazo zilizofanywa na TGDC mpaka hivi sasa ni kwamba jotoardhi inakuwa chanzo kingine cha uzalishaji umeme nchini na kupitia makubaliano hayo, ICEIDA itawezesha Wataalam wa ndani kutoka TGDC kupata ujuzi na uzoefu utakaowezesha kufanyika kwa tafiti nyingine katika maeneo mengine huko mkoani Mbeya.
Katika hatua nyingine TGDC pamoja na Kampuni ya TOSHIBA ya nchini Japan zimetiliana saini Mkataba wa Maelewano wa kufanya tafiti kwa pamoja zinahusu maeneo yenye viashiria ya upatikanaji wa nishati ya jotoardhi.
Utiaji saini wa mkataba ni hatua nzuri ambayo sasa inaliwezesha Shirika la TGDC kuweza kupata msaada wa kitaalam ambao utaliwezesha shirika hilo kuweza kuchimba ardhini kwa lengo la kupata mvuke utakaoweza kuzalisha umeme.
Akiongea wakati wa tukio la utiaji saini wa Mkataba huo, Meneja Mkuu wa TGDC, Mhandisi Boniface Njombe alisema kuwa kupitia Serikali ya Japan hususani Shirika la Maendeleo Japan (JICA), Kampuni ya TOSHIBA watasaidia kuomba ufadhili wa Serikali yao ili kuweza kuendeleza ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme pamoja na matumizi mengine yanayoendana na nishati hiyo.
“Katika utafiti wa nishati ya jotoardhi tunahitaji watu wenye elimu na uzoefu na ujuzi wa kutosha, miongoni mwa makubaliano ndani ya mkataba huu tuliosaini leo ni wafanyakazi wetu kadhaa kuwapeleka nchini Japan kwenye vyuo vyao ili kuweza kupata mafunzo ya darasani na kutembelea maeneo ambayo Japan wana vituo vya jotoardhi ili wapate ujuzi wa kufanya kazi na Wajapan na kutuletea ujuzi huo hapa nchini”, alisema Njombe.
Kupitia ushirikiano huu unaoonyeshwa na Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania, tuna imani kuwa nchi ya Japan itaendelea kuisadia Tanzania katika kuendeleza nishati ya jotoardhi kwakuwa ni nishati yenye tija katika kutimiza ndoto za Tanzania kwa kuifanya kuwa nchi yenye kipato cha kati kufikia mwaka 2020.
TGDC inatarajia kuanza kuainisha maeneo ya ushirikiano wa pande hizi mbili (TGDC na TOSHIBA) ikiwemo kuyawekea muda wa utekelezaji ambapo mwezi Machi mwakani, Wataalam toka TGDC wataweza kwenda nchini Japan kwa ajili ya kwenda kupata elimu zaidi kuhusu nishati hiyo.
Mtaalamu Mkuu toka Kampuni ya TOSHIBA Bwana Kentaro Kurahara anaeleza kuwa kampuni yao iko tayari kuisaidia Tanzania katika masuala yanayohusu jotoardhi na iko tayari kuomba ufadhili kupitia Serikali ya Japan ikiwemo kuwapa Wataalam wa TGDC elimu ya kutosha inayohusu nishati hiyo ili waweze kuhakikisha kuwa nishati hiyo inapatikana na kuleta maendeleo kwa Tanzania.
“Tunafuraha ya kushirikiana na TGDC katika kufanya tafiti zinazohusu jotoardhi kama mkataba wetu tuliousaini unavyosema, kupitia Serikali ya Japan na Shirika la JICA tutaomba ufadhili kwa ajili ya TGDC ili muweze kuleta wataalam wenu kuja kujifunza Japan pamoja kuwasaidia katika masuala mengine yanayohusu shughuli ya utafutaji wa nishati hii”, alisema Kurahara.
TGDC ikiwa kama Shirika Tanzu lililopo chini ya Kampuni ya Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) limepewa lengo na Serikali la kuharakisha upatikanaji wa nishati ya jotoardhi kufikia Megawati 200 mwaka 2020. Kampuni hiyo imesajiliwa Disemba 19, 2013 na kuanza kufanya kazi Julai 2014 huku ikipewa jukumu la kuharakisha uendelezaji wa nishati ya Jotoardhi nchini ambapo mpaka hivi sasa TGDC imegundua Zaidi ya maeneo yenye viashiria vya jotoardhi ambayo yamegawanyika katika Kanda Nne ambazo ni Kanda kaskazini–Ziwa Manyara, Kreta ya Ngorongoro, Natron na Majimoto Mara, Kanda ya Mashariki–Utete (Pwani), Kisaki (Morogoro), Luhoi (Pwani), Kanda ya Magharibi–Ibadakuli (Shinyanga), Mtagata(Kagera), maeneo mengine ni Dodoma, Singida pamoja na Tanga.

TANZANIA MWENYEJI KWENYE MAFUNZO YA KUKABIRIANA NA MATUKIO YA KINYUKLIA

December 08, 2015


Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Tume  ya Nguvu za Atomiki, Tanzania,  Dr. Mwijarubi Nyaruba aliekaa katikati pamoja na wataalamu wa Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya  namna ya kukabiliana na kuimarisha ulinzi wa matukio ya kinyuklia.

Tume ya Nguvu za Atomiki, Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani wanaendeshesha mafunzo ya namna ya kukabirina na matukio ya mionzi hatari, mafunzo haya yatachukua siku nne na yameanza jana jumatatu tarehe 07 disemba na yatafika ukomo wake tarehe 10 disemba, 2015, mafunzo haya yana jumla ya washiriki 23 kutoka katika nchi sita za ukanda wa Afrika ikiwa ni Uganda, Kenya, Zimbabwe, Botswana, Ethiopia, Namibia na mwenyeji Tanzania mafunzo  yanalenga zaidi kutoa mwongozo jinsi ya kukabiliana na majanga yanayoweza kusababishwa na mionzi hatari ya nyuklia endapo hakutakuwa na uangalizi wa kutosha.

Akifungua mafunzo haya jijini Arusha, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki, Tanzania Dr. Mwijarubi Nyaruba amesema, kutokana na kukua kwa kasi kwa teknolojia duniani ni muhimu sana kwa nchi wanachama wa shirika la nguvu za atomiki duniani kuendelea kutoa mafunzo na kujadiliana jinsi ya kukabiliana na majanga yanayoweza kusababishwa na mionzi  ayonisha.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu Dr. Nyaruba aliendelea kufafanua kuwa kutokana na ongezeko la vitendo vya ugaidi duniani ni lazima kujiimarisha kwa namna yoyote ile ili kuweza kulinda vyanzo vyote vya mionzi vinavyotumika mahospitalini na sehemu zingine za viwanda pamoja na kuvitafuta vyanzo vya mionzi ambavyo vimetekelekezwa au kupotea (Orphan Sources) na kuvihifazi kwa umakini mkubwa vyanzo hivi hatari, visijie kuingia katika mikono ambayo sio salama na kutumika katika matukio ya kigaidi na kuleta athari kubwa kwa wananchi pamoja na mazingira kwa ujumla, hivyo ni jukumu la nchi wanachama kuendelea kubadilishana uzoefu ili kuweza kuzibiti vyanzo hivi.

Naye mshiriki kutoka Kenya , ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha kuzuia majanga, ndugu Pius Masai Mwachi amesema kuwa ni muda muhafaka sasa kwa nchi zote za jumuhiya ya afrika mashariki kukaa pamoja na kutafuta suluhisho la namna ya kukabiliana na majanga yote yanayoweza kusababishwa na mabaki ya mionzi, kwani mionzi ni hatari sana na ni lazima kama nchi wanachama hasa waheshimiwa maraisi wa nchi hizi za jumuhiya ya adfrika mashariki kuweza kuhakikisha wanatoa kipaumbele kikubwa ili kuweza kukabiliana majanga yanayoweza kusababishwa kwa kutumia mabaki ya mionzi.

Mtaalamu mshiriki kutoka Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani IAEA Ndugu John Jones amesema kuwa dunia kwa ujumla inakabiliana na changamoto kubwa juu ya matukio mbalimbali ya kigaidi yanayoendelea duniani, hivyo Nchi zote wanachama ikiwepo Tanzania wana jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa juhudi kubwa zinafanyika ili kuweza kukabiliana na hari yoyote hatarishi pindi matukio na majanga ya kinyuklia yanapoweza kutokea.

Tanzania Kupitia Tume ya Nguvu za Atomiki imejenga jengo maaalumu la kuhifadhia mabaki ya mionzi Central Radioactive Waste Management Facility (CRWMF) ambapo vyanzo vyote vya mionzi vilivyokwisha nguvu kutoka mahospitalini, sehemu za tafiti pamoja na viwandani huchukuliwa na kusafirishwa kwa umakini mkubwa na kuhifadhiwa katika jengo hilo maalumu.

VODACOM FOUNDATION YANOGESHA UZINDUZI WA MAADHIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO LEO

December 08, 2015


 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni A.C.P Camillus Wambura(kushoto)akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia alipowasili ofisini kwake akiwa kama Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto leo katika viwanja vya Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Askari polisi na wanafunzi wa Shule ya Msingi Oysterbay na Mbuyuni wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe maalum wakati wa maandamano ya amani ya uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto leo katika viwanja vya polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo ulidhaminiwa na Vodacom Foundation.
 Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Oysterbay na Mbuyuni wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe maalum wakati wa maandamano ya amani ya uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto leo katika viwanja vya polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo ulidhaminiwa na Vodacom Foundation.
 Askari wa jeshi la polisi kikosi maalum cha Kurasini jijini Dar es Salaam akiongoza maandamano ya amani ya uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto leo katika viwanja vya polisi Oysterbay.Uzinduzi huo ulidhaminiwa na Vodacom Foundation.
  Baadhi ya Askari polisi na wanafunzi wa Shule ya Msingi Oysterbay wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe maalum wakati wa maandamano ya amani ya uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto leo katika viwanja vya polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo ulidhaminiwa na Vodacom Foundation.
 Askari wa jeshi la polisi kikosi maalum cha kutuliza ghasia(FFU)cha jijini Dar es Salaam akiongoza maandamano ya amani ya uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto leo katika viwanja vya polisi Oysterbay.Uzinduzi huo ulidhaminiwa na Vodacom Foundation.
 Kamishina Msaidizi wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni A.C.P Emanuel J. Mley akiongea na wageni waalikwa waliofika katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto leo katika viwanja vya polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam,Kulia kwake ni Mgeni rasmi wa maadhimisho hayo,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia.Uzinduzi huo ulidhaminiwa na Vodacom Foundation.
 Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto,Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia akiongea na wageni waalikwa waliofika katika uzinduzi huo leo katika viwanja vya Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam,Kushoto kwake ni Kamishina Msaidizi wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni A.C.P Emanuel J. Mley.Uzinduzi huo ulidhaminiwa na Vodacom Foundation.
 Mkuu wa Dawati la Jinsia la Polisi Chuo kikuu cha Dar es Salaam,S.P Leah Mbunda(kushoto)akiteta jambo na Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto,Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia(kulia) wakati wa maadhimisho hayo,katika ni Mkaguzi msaidizi wa Polisi anayeshughulikia Dawati la Jinsia katika Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam,A/INSP Prisca Komba.

Kamishina Msaidizi wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni A.C.P Emanuel J. Mley(kulia)akijadiliana jambo na Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto,Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia,Wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika leo katika viwanja vya Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na Vodacom Foundation.

PANAFRICAN ENERGY YATOA YAFADHILI UJENZI WA WODI YA ‘MAMA NGONJEA’ HOSPITALI YA WILAYA KINYONGA KILWA KIVINJE NA KUKARABATI WODI ZA UZAZI NA CHUMBA MAALUM CHA UANGALIZI WA AKINA MAMA

December 08, 2015


Meneja Uwajibikaji kwa jamii kutoka Kampuni ya PanAfrican Energy Andrew  Kangashaki  (kushoto ) na Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa Twalib Mbasha wakikabidhiana mkataba wa miradi  ya ujenzi wa nyumba ya mama ngojea  katika hospital ya Kinyonga  na ukarabati wa wodi  ya uzazi  mara baada ya kumaliza kusaini mikataba hiyo katika hafla fupi iliyofanyika jana Kilwa Kivinje.
Meneja Uwajibikaji kwa jamii kutoka Kampuni ya PanAfrican Energy Andrew  Kangashaki(wa tatu kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa Twalib Mbasha (wa tatu kulia) wakisaini makubaliano ya miradi miwili ya ujenzi wa mama ngojea ‘maternity waiting home’ yaani nyumba maalum kwa kina mama wajawazito watakaokua wakisubiri kujifungua itakayojengwa katika hospitali ya Kinyonga – Kilwa Kivinje na kukarabati wodi ya uzazi na chumba maalum cha uangalizi wa akina mama mara tu baada ya kujifungua katika kituo cha afya cha Kilwa Masoko. 

Huku wakishuhudiwa na Mwanasheria wa Wilaya Mh. Godfrey Makary (wapili kutoka kulia), Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Juma Abdalah Njwayo(wa pili kushoto), Mbunge wa jimbo la Kilwa Kaskazini kupitia chama cha CUF Mh. Vedasto Edgar Ngombale(wakwanza kushoto) pamoja na Mbunge wa Kilwa Kusini kupitia chama cha CUF Selemani Bungawa a.k.a Bwege(wakwanza kulia).

Mbunge wa Kilwa Kusini kupitia chama cha CUF Selemani Bungawa a.k.a Bwege(wapili kulia) akitoa neno la shukrani kwa Kampuni ya PanAfrican Energy kwa niaba ya wananchi wa Kilwa Kusini mara baada ya makabidhiano ya mkataba wa miradi itakayowanufaisha wananchi wa kilwa.
Wafadhili wa mradi wa ujenzi wa wodi ya wazazi Kampuni ya PanAfrican Energy pamoja wakiwaonesha wanahabari chumba cha uzazi katika kituo cha afya cha Kilwa Masoko ambacho kipo katika mradi uliosainiwa kati ya wilaya ya Kilwa na kampuni hiyo. Hii ni katika kuunga jitihada za serikali za kuboresha huduma za afya.
Hali halisi ya mazingira ya wodi ya wagonjwa katika kituo cha afya cha Kilwa Masoko, hii ni wodi ya wanaume. Kiyuo hichi cha afya  kilijengwa mwaka 1952 enzi za ukoloni mpaka sasa hakijawahi kukarabatiwa.
Wakisaini makubaliano ya miradi ya ujenzi wa mama ngojea na ukarabati wa chumba cha uzazi na wodi maalum ya uangalizi wa kina mama mara tu baada ya kujifungua wilayani Kilwa ni Meneja Uwajibikaji kwa jamii kutoka Kampuni ya PanAfrican Energy Andrew Kangashaki(wa pili kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa Twalib Mbasha (wa pili kulia) wanaowashuhudiwa ni Mwanasheria wa Wilaya ya Kilwa Mh. Godfrey Makary ( kulia), Mkuu wa Wilaya ya hiyo Juma Abdalah Njwayo (kushoto) jana katika hafla fupi iliyofanyika jana katika hospitali ya Kinyonga Kilwa Kivinje.

Wanahabari wakihakikisha wanapata habari sahihi kutoka kwa wahusika.

Wauguzi wa Hospitali ya Kinyonga Kilwa Kivinje wakishuhudia makabidhiano ya mkataba wa miradi ya ujenzi wa mama ngojea ‘maternity waiting home’ utakaofanyika katika hospitali yao na mradi mwingine wa ukarabati wa wodi ya uzazi utakaofanyika katika kituo cha afya cha Kilwa Masoko. Hafla hiyo ilifanyika hospitalini hapo jana.PICHA NA MICHUZI  JR-MICHUZI MEDIA GROUP.

=========  =======  ======   ==========
PANAFRICAN ENERGY KUTOA TSH .335,142,142 KUFADHILI UJENZI WA WODI ZA AKINA MAMA WAJAWAZITO WANAOSUBIRI KUJIFUNGUA ‘MAMA NGONJEA’ YAANI MATERNITY WAITIING HOME, HOSPITALI YA  WILAYA ,KINYONGA KILWA KIVINJE NA KUKARABATI WODI ZA UZAZI NA CHUMBA MAALUM CHA UANGALIZI WA AKINA MAMA MARA TU BAADA YA KUJIFUNGUA KITUO CHA AFYA CHA KILWA MASOKO.

Wakazi wa Kilwa wana haki ya kuendelea na kuwa na matumani baada ya kushuhudia makubaliano ya miradi mingine mikubwa  katika eneo lao kati ya Kampuni ya PanAfrican Energy na Wilaya ya Kilwa. Moja ya miradi hiyo ni ujenzi wa wodi ya kupumnzikia wakina mama wakisubiri kujifungua katika Hospitali ya Kinyonga iliyopo Kilwa Kivinje, na mradi mwingine ni ujenzi wa wodi ya wazazi na chumba maalum cha uangalizi wa akina mama mara baada ya kujifungua katika Kituo cha afya cha Kilwa Masoko. 

Katika hospitali ya wilaya , PANAfrican Energy watafadhili ujenzi wa wodi ya kusubiria akina mama, yaani mama ngonjea (maternity waiting home,) ambayo ni sehemu wanaposubiri  akina mama ambao wanaweza kuwa kwenye uzazi hatarishi.  Hii ni njia  kuu ya kuondoa tatizo la umbali mrefu kama kikwazo cha akina mama kujifungua salama ambapo hivi sasa wakina mama hushindwa kufika mapema hospitalini kutokana na kutokuwa na chumba maalum kwa ajili ya kusubiria huduma ya kujifungua. 

Kuwepo kwa wodi ya kupumnzikia akina mama hawa hapa Kinyonga ni manufaa tosha ukiangalia hali halisi ya mazingira na miundombinu ya Kilwa.  Pamoja na  na kupunguza vifo vya akina mama wajawazito kwani watakuwa karibu na hospitali, pia itapunguza gharama  kwani mama huyu anaweza kuchukua usafiri wa kawaida na kwa utaratibu wake na kwenda kusubiria.

Miradi hii miwili inaunga  mkono jitihada za serikali za kuboresha huduma za afya nchini na imekuja muda muafaka ambapo serikali inachukua hatua kupunguza na kutokomeza kabisa vifo vya akina mama wajawazito na matatizo yanayotokana na ujauzito.  Kutokana na utafiti uliofanywa mwaka 2009/10 nchini inaonesha kuwa wanawake 454 hufariki kwa kila 100,000, kila mwaka kutokana na matatizo yanayotokana na ujauzito.

 Vifo vya akina mama wajawazito vinatokana na  kutokwa damu nyingi wakati na baada ya kujifungua, utoaji mimba usio salama, shinikizo la damu, na kukosa uchungu wa kutosha au kukosa kabisa wakati muda wa kujifugua umefika .Uwepo mdogo wa sehemu za dharura na huduma kwa mtoto aliyezaliwa, ukosefu mkubwa wa watoa huduma za afya wenye ujuzi pamoja na mfumo duni wa rufaa, yote haya yanachangia kwa kiasi kikubwa vifo vya kina mama wajawazito.

Akiongea katika hafla ya kusaini makubaliano ya miradi hiyo leo kwa niaba ya Kampuni ya PanAfrican Energy, Meneja Uwajibikaji kwa jamii wa Kampuni ya PanAfrican Energy Bwana Andrew Kangashaki alisema, “Idadi ya vifo vya kina mama wajawazito imekua kubwa ya kutisha na tunataka kuwahakikishia wakazi wa kilwa kwamba ni kupitia miradi kama hii  mabpo tunaweza kuwa sehemu ya kumaliza tatizo hili kwa pamoja.

 Leo tena tunasaini makubaliano mengine na wilaya ya kilwa katika masuala ya afya; Tutafadhili miradi hii miwili yenye gharama ya Tshs 335,142,142. Moja ni nyumba ya kupumzikia kina mama wajawazito wanaosubiri kujifungua katika hospitali ya Kinyonga, Kilwa,  ambayo itagharimu Tsh 220,292,430.00 huku wodi za wazazi katika kituo cha afya cha kilwa masoko kitagharimu Tsh 114,849,636.00. 

Huu ni muendelezo wa kusapoti Nyanja za afya katika wilaya ya kilwa.  Mwanzoni mwa mwaka huu kampuni ya PanAfrican Energy ilikamilisha ujenzi wa nyumba za wauguzi  wa kituo cha affya cha Nangurukuru, ambacho hapo awali walikikarabati.  Nyumba za wauguzi zilikabidhiwa mwezi Juni kwa mkuu wa wilaya ya Kilwa. 

“Lengo letu kuu ni kuchangia mafanikio ya kiuchumi na ya kijamii katika wilaya ambapo Kampuni inafanya kazi, kutambua na kuimarisha uhusiano usiotengeka kati ya ustawi wa biashara na ustawi wa jamii kwa kutimiza mahitaji yao. Tunawasikiliza wananchi wa Kilwa na kuyazingatia mahitaji yao kwa umaakini. “aliongeza, Bw.Andrew.


Naye Mkurugenzi wa wilaya ya kilwa Bw.Twalib Mbasha aliishukuru Kampuni ya PanAfrican Energy kwa jitihada kubwa wanazoendelea kuzifanya katika kuwawezesha wakazi wa kilwa. “Mmetuhakikishia kuwa mpo nasi, nyie ni washirika tunaweza kuwategemea katika Nyanja zinazogusa na kuhusu maisha yetu. 

Tunapenda kuwahakikishia kuwa tutakuwa pamoja katika kukamilisha miradi hii kuanzia mwanzo mpaka mwisho.” Alisema.  Pamoja na wauguzi na wafanyakazi wa sekta ya afya wilaya ya Kilwa, pia walioshuhudia usainishaji wa makubaliano hayo ni Mkuu wa wilaya ya Kilwa, Mhe. Juma Njwayo pamoja na wabunge wa Kilwa Mh.Vedasto Edgar Ngombale and Selemani Bungawa.

MKUTANO WA MWAKA WA WATAALAMU WA MANUNUZI NA UGAVI WAFUNGULIWA JIJINI ARUSHA.

December 08, 2015
Mwenyekiti wa Bodi ya Wataalamu wa Manunuzi na Ugavi nchini(PSPTB)Dk Hellen Bandiho akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Wataalamu unaofanyika kwenye ukumbi wa mikutano ya kimataifa wa AICC jijini Arusha na kusisitiza miiko ya uadilifu katika manunuzi ya umma na sekta binafsi.

Mjumbe wa Bodi ya Wataalamu wa Manunuzi na Ugavi nchini(PSPTB)Ahmed Kilima akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Wataalamu unaofanyika kwenye ukumbi wa mikutano ya kimataifa wa AICC jijini Arusha.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Manunuzi nchini(PSPTB)Dk Clemence  Tesha  akizungumza jambo na wajumbe wa mkutano wa mwaka wa Wataalamu wa taaluma ya Manunuzi na Ugavi unaofanyika kwenye ukumbi wa mikutano ya kimataifa wa AICC jijini Arusha na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka mikoa mbalimbali nchini na wageni kutoka nchi jirani.

Wajumbe wakiwa kwenye ukumbi wa Simba 

Wajumbe wa mkutano ambao ni wana taaluma ya Manunuzi  na Ugavi wakifatilia mada kwenye mkutano huo leo.

Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa Manunuzi  na Ugavi wakifatilia mada kwenye mkutano huo leo.

Wajumbe wa mkutano wa mwaka wa PSPTB

Mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB,Dk Charles Kimei(katikati)akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa fani Manunuzi na Ugavi nchini baada ya kufungua mkutano wa mwaka ambao amesisitiza umuhimu wa kufanya manunuzi sahihi yenye lengo la kuokoa fedha za umma.

MRAGHABISHI MAIMUNA SAIDI AGEUKA SHUJAA WA KIJIJI CHA MWIME KAHAMA

December 08, 2015

Na krantz mwantepele ,       
Ziara niliyofanya katika Kijiji cha Mwime kata ya Mwendakulima  wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga mwishoni wa  mwezi Novemba mwaka huu ,ilinipa mwanga wa jinsi ambavyo wananchi wakiamua kuchukua hatua wanaweza kubadili mfumo mzima na kuweza kujiletea maendeleo katika Nyanja zote za maendeleo .Kijiji cha Mwime ambacho wananchi wengi wanajihusisha na biashara, uchimbaji wa madini na kilimo cha pamba na wapo katika eneo ambalo Barick Buzwagi wanafanya uchimbaji mkubwa wa dhahabu.
Ofisi za   kijiji hicho cha Mwime kilichopo kata ya Mwendakulima wilayani Kahama 
Mgogoro wa Maslahi wa wananchi wanaozunguka mgodi uliokuwa unamilikiwa na Barrick na sasa Accaccia uliopo  wa Buzwagi kwenye wilaya ya Kahama katika kijiji cha Mwime kilichopo kata ya Mwendamkulima  katika wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, Unaibua mashujaa wa kutetea haki na kudai uwajibikaji u wa viongozi katika kuendeleza utawala bora na maendeleo kwa ujumla lakini mwishoni inageuka kuonekana ni maadui wa maendeleo . 
Kwa muda wa miaka zaidi ya mitano  sasa kijiji hiki kimekuwa katika pilikapilika za kuhakikisha wan-aendelea kunufaika na rasilimali yao ya madini ya dhahabu ambayo kwa sasa yanachimbwa na kampuni ya Accacia  katika mgodi wa Buzwagi kupitia Makubaliano ya Nyongeza ya Mkataba yaliyosainiwa mwaka 2007.
Kwa mujibu wa kifungu  1.1 cha Makubaliano ya Nyongeza ya Mkataba baina ya Kampuni ya Madini ya Pangea kwa niaba ya Barrick na kijiji; kampuni itakuwa ikikilipa kijiji kiasi cha Tsh milioni 60/- kila mwaka kwa kipindi cha miaka mitano baada ya uzalishaji kuanza na kisha pande mbili hizi zitakaa pamoja na kupitia kiwango hiki kwa kadri ya uzalishaji utakavyokuwa kwa nia ya kuboresha zaidi. Na uzalishaji wa dhahabu katika mgodi huu ulianza rasmi mwaka 2009.

Nikiwa ziarani  wilaya ya Kahama nilitembelea kijiji hiki ambacho mwanzoni mwa mwaka 2007 wananchi wengi wa kijiji cha Mwime na maeneo ya karibu walijihusisha na uchimbaji wa madini ya dhahabu kabla kampuni ya Pangea kuja kuchukua maeneo hayo kwa kuhodhi mashimo yaliyojulikana kwa majina ya  Zanzibar na majimaji na kuwafanya wakazi hao kuondoka hapo kupisha uchimbaji wa kisasa,
Mategemeo ya wananchi kupata maendeleo makubwa baada ya kampuni ya Pangea kuanza uchimbaji huo wa kisasa yaliendelea kufifia kila uchwao baada ya makubaliano ya kulipwa kiasi cha milioni  60 kila mwaka kwa kipindi cha miaka kipindi cha miaka mitano  cha uchimbaji  wa madini kutotimizwa kwa wakati.Licha ya kutokuwa na uelekezi rasmi wa kiseheria wa makubaliano hayo lakini yaliwafanya  wananchi wa mMwime kuendelea kuishi maisha magumu  licha ya kuwa mgodi wa Buzwagi  kuweza kufanya uchimbaji kwa muda mrefu.
Kuchelewa kwa malipo kama walivyokubaliana kulisababishwa pia na mapungufu ya uongozi wa kijiji kushindwa kufuatilia suala hilo kwa ukaribu.Sababu nyingine inayotajwa ni kwa Wanamwime wenyewe kushindwa kudai na kuwahimiza vi-ongozi wao kuchukua hatua kwa kufuatilia suala hilo.


Bi Maimuna akiwa na  mjukuu wake katika duka lake analouza pembejeo za kilimo kwa wakazi wa kijiji cha Mwime

Mraghabishi na mpambanaji wa haki za binadamu Bi Maimuna Saidi ambaye pia ni mwananchi wa kijiji hicho ambaye yeye na wenzake watano  walichukua hatua ya kuanza kuhimiza ufuatiliaji wa pesa hizo kama walivyokubaliana na baada ya mazungumzo marefu na pia ushirikishaji wa wananchi wote wa kijiji kupitia mikutano ya kijiji waliweza kufanikisha upatikanaji wa  ya million 300/ kama malipo ya mwaka 2009 – 2013 .
Mama maimuma saidi (Mwenye kilembo)akitoa  maelezo jinsi gani walivyofanikisha kupatikana kwa maendeleo katika kijiji cha Mwime kutoka katika mgodi wa Buzwagi  kwa baadhi ya waandishi wa habari na wataalamu wa mitandao ya kijamii  niliombatana nao 

 Hivyo Maimuna Said kupitia ufahamu aliopatiwa alimshawishi Diwani mara kwa mara kuweza kuchukua hatua zaidi, kwa kuwa yeye alikuwa na mamlaka zaidi.Na mwishowe kupitia harakati mbalimbali na ushirikishwaji wa wananchi wenzao walifanikiwa  kupata kiasi hicho cha pesa.
Pesa hizo pia zilitumika kuboresha shughuli mbalimbali za maendeleo na huduma za kijamii  kama ujenzi wa miundombinu ya umeme ,nyumba za manesi, nyumba ya kupumzikia wageni kama kitega uchumi lakini haya yote yalikuwa kama kipaumbele cha wananchi kufaidikapia kiasi kilichobaki kulipa baadhi ya fidia kwa wananchi waliotoa maeneo yao katika upanuzi wa barabara .
Moja ya nyumba zinazojengwa katika kijiji hiki cha Mwime kama moja ya matumizi ya pesa walizopata kutoka katika mgodi wa Buzwagi 

Huu mchakato wote usingeweza kufanikiwa kama Wanamwime wenyewe wasingesimama pamoja na kudai haki yao. Kwa hakika ili tupate tutakachotaka ni lazima tuchukue hatua za dhati pasipo kuchoka wala kukata tamaa huku tukishirikiana na viongozi wetu kwani kuna msemo unasema umoja ni nguvu utengano ni udhaifu kama dhana waliotumia wanaMwime  wakafanikiwa katika harakati zao za kujiletea  maendeleo kijijini hapo.

Imeandaliwa na MWANAHARAKATI MZALENDO BLOG