Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa mjini Mtwara katika mkutano
wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa mjini humo
akihitimisha ziara yake ya siku 16 aliyoifanya katika mikoa ya Lindi na
Mtwara akikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010
inayotekelezwa na serikali kwa kushirikiana na wananchi wenyewe na
kuhimiza uhai wa chama cha Mapinduzi CCM, Katika ziara hiyo Katibu mkuu
huyo aliongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi,
Katika kutano huo Kinana amempa wiki mbili Waziri wa Uchukuzi Dr.
Harrison Mwakyembe kutoa maelezo kwanini bidhaa mbalimbali
hazisafirishwi kwenda nje
kupitia bandari ya
Mtwara, Lakini pia Kinana amewaagiza Waziri wa Nishati na Madini kutoa
maelezo ni kwanini wawekezaji wenye kampuni zinazofanya shughuli zao
mtwara wanalipia kodi zao jijini Dar es salaam badala ya kulipia mkoani
Mtwara ambako wanafanya shughuli zao, Pia waziri wa Ofisi ya Mkamu wa
Rais Mazingira amepewa mwezi mmoja kuhakikisha dampo la taka za sumu
zinazotupwa na wachimbaji wa gesi na viwanda kuacha mara moja kwa sababu
zinahatarisha maisha ya wakazi wa Mtwara, Mwisho akaagiza Ofisi ya
Waziri Mkuu kutoa kibali cha kugawa viwanja katika manispaa ya Mtwara
kwani viwanja vimeshapimwa, Fedha za kulipa fidia zipo ila kibali kutoka
ofisi ya Waziri mkuu ndiyo kimkwama kwa muda wa mwaka mmoja sasa.(PICHA
NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MTWARA)
Kikosi cha zimamoto mkoa wa Tabora kikionesha vifaa vinavyotumika wakati wa uokoaji ajali zinapojitokeza.
Sherehe za wiki ya usalama
barabarani mkoa wa Tabora zilianza kwa maandamano yaliyopita mitaa
mbalimbali hadi viwanja vya mazoezi ya Jeshi la Polisi Tabora ambapo
wananchi walishiriki maandamano hayo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora
kikosi cha usalama barabarani SSP Peter Mnyandwa akitoa taarifa ya
ongezeko la ajali za barabarani mkoani Tabora ambapo zaidi ya watu 150
wamefariki dunia katika ajali 399 huku watu 520 wamejeruhiwa katika
ajali 185.
Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Ludovick
Mwananzila akihutubia katika sherehe hizo za wiki ya nenda kwa usalama
barabarani ambapo mbali ya kusikitishwa na taarifa ya ajali hizo lakini
alisema kuwa asilimia 75 ya ajali hizo zinatokana na makosa ya
kibinadamu na hivyo kuzitaka mamlaka husika kuchukua hatua ya kudhibiti
kupunguza ajali hizo ikiwa ni pamoja na kutotoa leseni kwa madereva
ambao hawajapata mafunzo ya udereva darasani.
Mkuu wa mkoa wa Tabora
Bw.Mwananzila akimpatia cheti cha pongezi Mwenyekiti mstaafu wa Kamati
ya Usalama barabarani mkoa wa Tabora Bw.Moshi Abrahamu maarufu Nkonkota.
Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Ludovick
Mwananzila akikabidhi cheti cha pongezi kwa mmiliki wa kampuni ya
mabasi ya NBS kwa usafirishaji salama bila kusababisha ajali kwa muda wa
zaidi ya mwaka mmoja.