WATOTO 984 WAOZESHWA KWA NGUVU TARIME, 1,628 WAKEKETWA

WATOTO 984 WAOZESHWA KWA NGUVU TARIME, 1,628 WAKEKETWA

August 26, 2014

Baadhi ya washiriki katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara. Uzinduzi huo umefanywa na mjane wa hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust, Bi. Graca Michel leo jijini Dar es Salaam.Baadhi ya washiriki katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara. Uzinduzi huo umefanywa na mjane wa hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust, Bi. Graca Michel leo jijini Dar es Salaam.Mjane wa Hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel (kulia) akishangilia baada ya kutuma ujumbe mfupi kwa njia ya simu za viganjani kwa simu zote zilizosajiliwa nchini Tanzania ikiwa ni ishara ya uzinduzi kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara.Mjane wa Hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel (kulia) akishangilia baada ya kutuma ujumbe mfupi kwa njia ya simu za viganjani kwa simu zote zilizosajiliwa nchini Tanzania ikiwa ni ishara ya uzinduzi kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara.Mjane wa Hayati Nelson Mandela na Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel akimbusu mmoja ya watoto wa kike kutoka Mkoa wa Mara kuonesha ishara ya upendo katika uzinduzi huo. 
Mjane wa Hayati Nelson Mandela na Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel akimbusu mmoja ya watoto wa kike kutoka Mkoa wa Mara kuonesha ishara ya upendo katika uzinduzi huo

RC KILIMANJARO AFUNGUA MKUTANO MKUU WA VIONGOZI TAKUKURU,

August 26, 2014


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU unaofanyika katika ukumbi wa Kuringe.
Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Dk Edward Hosea akizummza wakati wa Mkutano wa mkuu wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU .
Mkurugenzi wa idara ya elimu TAKUKURU ,Marry Mosha akitoa neno la shukurani mara baada ya mgeni rasmi kufungua mkutano huo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama akiteta jambo na Mkurugenzi wa TAKUKURU Dk Edward Hosea.

USAJILI WA COASTAL UNION U -20 JINSI ULIVYOFANYIKA LEO MAKAO MAKUU YA CLUB HIYO BARABARA KUMI NA MOJA JIJINI TANGA

August 26, 2014
  Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Coastal Union ,Salima Bawaziri kushoto ni Meneja wa timu ya U -20 ya Coastal Union wakiendelea na harakati za usajili wa timu hiyo ndogo jana.




Wachezaji wa kikosi cha pili cha U-20 ya Coastal Union ya Tanga wakimsiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Coastal Union Salim Bawaziri ambaye hayupo pichani leo

hapa akisisitiza jambo Bawaziri kulia ni Katibu wa Tawi la Coastal Union Nyumba

Baada ya usajili mazungumzo yakaanza .
RAIS KIKWETE AZINDUA BARABARA YA DUMILA-RUDEWA

RAIS KIKWETE AZINDUA BARABARA YA DUMILA-RUDEWA

August 26, 2014

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe pamoja na Makamu mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa barabara ya Dumila-Rudewa yenye urefu wa Kilomita 45 iliyojengwa kwa kiwango cha lami. 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifungua jiwe la msingi kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Dumila-Rudewa yenye urefu wa Kilomita 45 iliyojengwa kwa kiwango cha lami.
Sehemu ya barabara ya Dumila-Rudewa yenye urefu wa Kilomita 45 iliyojengwa kwa kiwango cha lami.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na baadhi ya Watendaji kutoka Wizara ya Ujenzi ambao walikuwa wakisubiri tukio la ufunguzi wa barabara ya Dumila-Rudewa yenye urefu wa Kilomita 45 uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe kushoto akiwa pamoja na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale wakitazama ramani pamoja na picha mbalimbali za barabara ya Dumila-Rudewa yenye urefu wa Kilomita 45 iliyojengwa kwa kiwango cha lami.
Mc Mavunde kulia akiwatambulisha watendaji mbalimbali kutoka Wizara ya ujenzi kabla ya Ufunguzi rasmi wa barabara ya Dumila-Rudewa
Sehemu ya wakazi wa Dumila waliojitokeza kwa wingi wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete licha ya giza kuingia mjini Dumila.
LIVERPOOL WAJIPANGE UPYA KWA MAN CITY, WAPIGWA 3-1 KAMA WAMESIMAMA …Balloteli ashuhudia kipigo

LIVERPOOL WAJIPANGE UPYA KWA MAN CITY, WAPIGWA 3-1 KAMA WAMESIMAMA …Balloteli ashuhudia kipigo

August 26, 2014
LIVERPOOL WAJIPANGE UPYA KWA MAN CITY, WAPIGWA 3-1 KAMA WAMESIMAMA …Balloteli ashuhudia kipigo

KAMA Liverpool wanadhani wana ubavu wa kupimana nguvu na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya England, Manchester City basi wakajipange upya.
Liverpool inayojinasibu kusaka ubingwa wa Ligi Kuu, imejikuta ikiambulia kipigo cha 3-1 kutoka kwa Manchester City kwenye uwanja wa Etihad Jumatatu usiku.
Ikishuhudiwa na mchezaji wao mpya Mario Balotteli aliyekuwa jukwaani kufuatilia mchezo huo, Liverpool ikakukuruka hadi dakika ya 41 kabla ya kuruhusu bao la kwanza lilifungwa na Stevan Jovetic aliyekuwa nyota wa mchezo.
Watching on: Liverpool missed a striker of Balotelli's class tonight, but his behaviour will have to be managed
Dakika ya 55, kwa mara nyingine tena Jovetic akawafanya Liverpool waende nyavuni kuokota mpira baada ya kufunga tamu lililotokana na pasi 19.
Improved: Jovetic had a tough first season marred by injury, but he has all the attributes to succeed in England
Zilikuwa ni gonga za aina yake ambapo ukingoni mwa gonga hizo Stevan Jovetic alimpa pande Samir Nasir na kukimbia mbele kusubiri arudishiwe mpira na Nasiri na ndivyo ilivyokuwa – akarudishiwa mpira na kumtungua kipa Mignolet, mashabiki wa City wakaingia wazimu.
Sergio Aguero aliyeingia dakika ya 69 kuchukua nafasi  za Dzeko akaipatia City bao tatu sekunde chache tu baada ya kuingia uwanjani.
Liverpool, timu ya pili duniani kwa kumwaga pesa nyingi kwenye usajili msimu huu, ikasubiri hadi dakika ya 83 kupata goli la zawadi kutoka kwa beki wa City, Zabaleta aliyejifunga mwenyewe.

*SERIKA YAPOKEA GARI NA PIKIPIKI KUKABILIANA NA AUGONJWA WA KIFUA KIKUU NA UKOMA NCHINI.

August 26, 2014


 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashidi akiwasha moja ya kati ya magari manne  aliyoyapokea kutoka kwa mwakilishi wa shirika la GLRA la Ujerumani nchini Burchard Rwamtoga leo jijini Dar es salaam.
 01.      Mwakilishi wa shirika la GLRA nchini Burchard Rwamtoga (kushoto) akimkabidhi Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashidi (kulia) ufunguo wa moja kati ya pikipiki 20 zilizotolewa na shirika la hilo leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashidi (kulia) akimkabidhi Mratibu wa huduma za kifua kikuu na ukoma mkoa wa Kigoma Dkt. Deus Leonard (kushoto) moja kati ya magari manne  yaliyokabidhiwa kwa Serikali kutoka kwa  shirika la GLRA la Ujerumani nchini leo jijini Dar es salaam. Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO
********************************
HUYU HAPA DI MARIA AKIWASILI MANCHESTER UNITED …ahadi ya Ed Woodward yatimia

HUYU HAPA DI MARIA AKIWASILI MANCHESTER UNITED …ahadi ya Ed Woodward yatimia

August 26, 2014
On the look out: Di Maria peers out of his United car as he arrives for the completion of his transfer
HATIMAYE yametimia. Wakati mtendaji mkuu wa Manchester United Ed Woodward aliposema kuwa watavunja rekodi ya usajili England msimu huu, ilionekana kama masihara lakini sasa ukweli umedhihirika.
Angel di Maria tayari ametua Manchester United kwaajili ya mazungumzo binafsi pamoja na vipimo vya afya kabla ya kukamilisha usajili wake wa pauni milioni 60 utakaomwingizia mshahara wa pauni 200,000 kwa wiki.
Di Maria ameonekana kwenye gari akiwa ameketi kiti cha nyuma akielekea kwenye uwanja wa mazoezi wa United kwaajili ya kwenda kukamilisha usajili wake.
Spotted: Di Maria is on the left hand side of the back seat on his way into United's training ground
Mshambuliaji huyo atakuwa mchezaji wa pili kwa kulipwa pesa nyingi zaidi Manchester United akitanguliwa na Wayne Rooney na akiwa amemzidi kidogo Robin van Persie.

KINANA AKUTANA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI TANZANIA

August 26, 2014


  
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania ( TUCTA )Nicholaus Mgaya akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipowasili kwenye Makao Makuu ya TUCTA kwa mazungumzo na Viongozi wa vyama vya wafanyakazi.
 
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Wanawake,Jinsia na Watoto (TUCTA) Siham Ahmed kabla ya kuanza kwa mazungumzo baina ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi.
 
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania ( TUCTA )Nicholaus Mgaya akizungumza wakati wa kikao cha Viongozi wa vyama vya Wafanyakazi na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye ukumbi wa mikutano TUCTA.
 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumzwa kwenye kikao na Viongozi wa Vyama Vya Wafanyakazi Tanzania.
 
Sehemu ya Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi Tanzania wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU) Erasto Kihwele akichangia jambo wakati wa kikao hicho.
(Picha na Adam H.Mzee)

*RAIS KIKWETE ATEMBELEA CHUO KIKUU CHA MZUMBE, MJINI MOROGORO

August 26, 2014

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya picha yake ya kuchorwa wakati alipotembelea Chuo Kikuu cha mzumbe ambapo walihutubia wanafunzi, wahadhiri na wananchi katika chuo hicho baada ya kuzindua ukumbi wa mihadhara na jengo la wahadhiri chuoni hapo.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa serikali ya wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Mzumbe mjini Morogoro baada ya kuwahutubia chuoni hapo.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wanafunzi, wahadhiri na wananchi katika Chuo Kikuuu cha Mzumbe Morogoro baada ya kuzindua ukumbi wa mihadhara na jengo la wahadhiri chuoni hapo.
 Meza kuu ikifurahia jambo wakati Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa Mvomero Mhe Amos Makalla akipohutubia wanafunzi, wahadhiri na wananchi katika chuo hicho wakati Rais Kikwete alipotembelea na kuzindua ukumbi wa mihadhara na jengo la wahadhiri chuoni hapo.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea risala toka kwa Rais wa Serikali ya Wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Mzumbe Mhe Boniface Maiga wakati Rais Kikwete alipotembelea na kuzindua ukumbi wa mihadhara na jengo la wahadhiri chuoni hapo.
 Rais wa Serikali ya Wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Mzumbe Mhe Boniface Maiga akisoma risala wakati Rais Kikwete alipotembelea na kuzindua ukumbi wa mihadhara na jengo la wahadhiri chuoni hapo.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua jengo la mihadhara la Chuo Kikuu cha Mzumbe Morogoro akisaidiwa na uongozi wa chuo hicho alipotembelea hapo na kuzindua ukumbi wa huo jengo la wahadhiri chuoni hapo.
 Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Morogoro wakiweka kumbumbuku ujio wa Rais Kikwete alipotembelea hapo na kuzindua ukumbi wa huo jengo la wahadhiri chuoni hapo.
Umati wa wanafunzi, wahadhiri na wananchi wakimsikiliza Rais Kikwete akiwahutubia alipotembelea hapo na kuzindua ukumbi wa huo jengo la wahadhiri chuoni hapo Agosti 25, 2014. PICHA NA IKULU

BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI KUFANYA KIKAO CHAKE CHA BUNGE KARIMJEE DAR ES SALAAM, JK KUUFUNGUA

August 26, 2014

Spika
wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA) Dk. Margaret Nantongo
Zziwa  akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dar es Salaam leo juu ya
mkutano wa kwanza wa Bunge la tatu unaotaraji kuanza jana katika ukumbi
wa Karimjee na kufunguliwa na Rais Jakaya Kikwete kesho kutwa. 
 Spika
wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA) Dk. Margaret Nantongo
Zziwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dar es Salaam jana juu ya
mkutano wa kwanza wa Bunge la tatu unaofanyika ukumbi wa Karimjee.
Wengine kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Amantius Msole, wabunge wa EALA kutoka Tanzania Twaha
Taslima na Shy Rose Banji
Mbunge
wa Bunge la Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Wabunge kutoka Tanzania,
Adam Kimbisa, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika ofisi za
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dar es Salaam jana, juu ya
mkutano wa kwanza wa Bunge la tatu unaofanyika ukumbi wa Karimjee.
Kushoto ni
Spika
wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA) Dk. Margaret Nantongo
Zziwa,wabunge wa EALA kutoka Tanzania, Twaha Taslima na Shy Rose Banji.