RAIS DKT. MAGUFULI AHUTUBIA KATIKA SHEREHE ZA MIAKA 55 YA UHURU WA TANZANIA BARA KATIKA UWANJA WA UHURU JIJINI DAR ES SALAAM

December 09, 2016




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi waliojitokeza katika sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi waliohudhuria sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama wakati wimbo wa Taifa ulipokuwa ukipigwa uwanjani hapo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride katika sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Vikosi mbalimbali vya Majeshi vikipita mbele ya mgeni Rasmi kwa mwendo wa pole na Haraka katika sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha Maadhimisho cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania kikionesha gwaride la kimyakimya mbele ya Amiri Jeshi mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa Uhuru.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mama Fatma Karume mara baada ya kumaliza kuhutubia katika uwanja wa Uhuru.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wananchi katika uwanja wa Uhuru mara baada ya kumalizika kwa sherehe hizo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembea pamoja na Askari Polisi ambao huongoza misafara ya viongozi VIP riders mara baada ya kuwasili Ikulu wakati wakitokea katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi mara baada ya Kuwasili katika uwanja wa Uhuru.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda mara baada ya kuwasili. 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,BungeKazi,Ajira,Vijana na Wenyeulemavu Jenister Muhagama mara alipowasili katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kushiriki nkatika sherehe za Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania bara 


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na  Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman  alipowasili katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kushiriki nkatika sherehe za Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania bara

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam katika sherehe za Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania bara zilizofanyika leo
MKUU WA MKOA AMALIZA MGOGORO WA MAJI – MAKILENGA

MKUU WA MKOA AMALIZA MGOGORO WA MAJI – MAKILENGA

December 09, 2016
nte1
Mkuu Wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (katikati) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Alexander Mnyeti(kushoto0 wakiwalia katika kijiji cha Nkoasenga kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa maji Makilenga.
nte2Mhandi wa Maji Happy Mrisho (aliyesimama) akiwasilisha taarifa ya mradi  kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha(hayupo pichani) wakati wa kikao cha kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa  Maji Makilenga.
nte3Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Makilenga waliohudhuiria kwenye Mkutano wa hadhara.
nte4
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Alaxander Mnyeti akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nkoasenga kwenye Mkutano wa hadara.
nte5Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (aliyesimama mbele) akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nkoasenga kwenye Mkutano wa hadhara
nte6Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Nkoasenga wakifurahia makubaliano yaliyofikiwa katika ya Serikali na kijiji hicho ya kulipa Tsh 1500 kwa huduma ya maji mwezi mzima kwa wanaotumia mabomba ya Kijiji .
……………………………………………………………….
Nteghenjwa Hosseah – Arumeru
Mkuu wa Mkoa wa Arusha  Mhe . Mrisho Mashaka Gambo amemaliza mgogoro wa muda mrefu uliodumu zaidi ya miaka mitatu kati ya Bodi ya Maji ya Makilenga na wananchi wa Kijiji cha Nkoasenga, Kata ya Leburuki Wilayani Arumeru. 
Utatuzi wa mgogoro huo ulifikiwa kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kijiji cha Nkoasenga baada ya Mhe. Gambo kuwashirkisha wananchi wa aneo hilo katika kutatua changamoto hii iliyoathiri wananchi zaidi ya hamsini elfu wa kijiji hiki pamoja na vijiji vingine ishirini na sita vinavyotegemea mradi huo.
Wananchi hawa waliofungiwa maji kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa baada ya kufanya uharibifu wa miundombinu ya Maji pamoja na kuweka kinyesi kwenye mabomba walionyesha kuchoshwa na adha hiyo ya kufuata maji umbali mrefu na kwa gharama kubwa zaidi ilihali maji yanapatikana katika Kijiji chao na walionyesha hali ya kutaka muafaka wa jambo hili ili kuendelea kupata huduma ya maji kama ilivyokuwa hapo awali.
Akiongea katika Mkutano huo baada ya mazungumzo na viongozi wa Kijiji pamoja wananchi Mkuu wa Mkoa Mhe. Mrisho Gambo alisema katika kutoa huduma ya Maji Vijijini tunaongozwa na Sera ya Maji ya mwaka 2002 inayotaka kuchangia hudma za maji na sio kununu Maji hivyo kila kaya inawajibu wa kuchangia kiasi kidogo cha Fedha ili kuwezesha huduma hii iendelee kutolewa siku zote.
“Tunafahamu kwamba maji  haya yanaanzia kwenye Kijiji hiki na wakazi wa Nkoasenga  ndio walinzi wakuu wa mradi huu na wanastahili  kupewa upendeleo wapekee  katika kutumia maji haya ili  wendelee kutunza mradi huu wa Maji,  ni wazi kuwa vijiji vya ukanda wa chini haviwezi kupata Maji endapo tu wana Nkoasenga wataharibu mradi huu wa maji mtiririko”, Alisema Mhe. Gambo.
Aliongeza kuwa umuhimu huu wa nyie kuwa Kijiji mama cha mradi huu hauwapi Kinga ya  kutokuchangia gharama za maji, hivyo nataka mniambia mnaweza kuchangia kiasi gani kadiri ya uwezo wenu na baada ya makubalino haya  mtalipia gharama za maji  kwa mwezi  na sio kwa mwaka tena kama mlivyokuwa mnafanya hapo awali”.
Awali akizungumza katika Mkutano huo Mhandisi wa Maji Bi. Happy Mrisho alisema “mradi wa maji Makilenga uliibuliwa na wananchi wa Kijiji cha Nkoasenga  na baada ya thatmini ya awali ilonekana kuwa mradi ni wa gharama kubwa hivyo usingekidhi vigezo vya kiufadhili kama ungekua mradi wa kijiji kimoja na ili kukidhi vigezo vya kupata fedha toka kwa wafadhili ililazimu kuongeza wanufaika kutoka vijiji 26 na utekelezaji  ukaendelea”.
Aliongeza kuwa baada ya mradi kukamilika iliundwa Kamati tendaji ya Makilema ambayo ndiyo inayosimamia mrdai huu na Madiwani na wenyeviti wote wa vijiji waliingia makubaliano ya  kuchangia  Tsh 10 kwa ndoo lakini baada ya muda mfupi wanakijiji wa Nkoasenga walikiuka makubalino hayo na kudai watalipa Tsh 5000 kwa mwaka na hawewezi kulipa kwa ndoo kwa kuwa maji hayo ni mali  ya Kijiji.
Anderson Sikawa ni Diwani wa Kata ya Leburuki kilipo kijiji cha Nkoasenga alisema hawakatai kuchangia huduma za Maji lakini kutokana na hali duni ya wananchi wa eneo hilo hawawezi kulipa kwa ndoo hivyo wanahitaji kufanya mapitio ya gharama za Maji ili kuendana na hali ya wana Nkoasenga ambayo pia itawaongezea ari wakazi hao kulinda mradi huo kwa manufaa ya vijiji vingine pia alitoa  tuhuma kwa Bodi ya Makilenga kwa matumizi mabaya ya Fedha za maji.
Katika kutoa mapendekezo ya kiasi stahiki cha kuchangia huduma ya Maji  Ndg. Afred Masao ambaye ni mwananchi wa Kijiji cha Nkoasenga aliwakilisha wananchi wote wa Kijiji hicho alisema kuwa  wananchi wako tayari  kuchangia kwa mwezi lakini uwezo wao ni Tsh 1500  na sio Ths 3000 kama ilivyopendekezwa kwenye vikao vya ndani katika ya Mkuu wa Mkoa  na viongozi wa Kijiji.
Rc Gambo alihitimisha Mkutano huo kwa kukubaliana na mapendekezo ya wananchi kuwa watalipia Tsh 1500 kwa mwezi kwa wale wanaotumia mabomba ya Kijiji na kwa wale wenye mabomba nyumbani watalipia kadiri ya  matumizi yao kwa mwezi  na wote watafungiwa Mita za Maji pia  aliwaagiza wananchi hao kulipia gharama hizo Halmashauri na sio kwa Kamati ya Maji Makilenga kama awali.
Mradi wa Maji wa Makilenga ulianza mwaka 2011 kwa lengo la kutoa huduma ya Maji na kuhudmia  Kata nne na vijiji 27; Ulifadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya kwa kutoa kiasi cha Tsh Bil 3.7, OIKOS pamoja na nguvu za wananchi. Mradi huu unaendeshwa na Jumuiya ya watumiaji maji ya Makilenga ambayo ina jukumu na mamlaka ya Kisheria kusimamia mradi huu wa maji.
MAJALIWA:TUMETENGA SH. BILIONI 15 ZA MAFUNZO KWA VIJANA

MAJALIWA:TUMETENGA SH. BILIONI 15 ZA MAFUNZO KWA VIJANA

December 09, 2016
crad
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Frederick Msigara wa CCBRT katika hafla ya utoaji tuzo ya mwajiri bora wa mwaka 2015 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
…………………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Kassim Mjaliwa amesema Serikali imetenga sh. bilioni 15 kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa vijana zaidi 2,500 ili kuwajengea uwezo waweze kushiriki kama nguvu kazi kwenye viwanda vinavyotarajiwa kujengwa nchini.
Alitoa kauli hiyo jana usiku (Alhamis, Desemba 8, 2016) kwenye sherehe za utoaji wa tuzo ya muajiri bora wa mwaka 2016, zilizofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam. Tuzo hizo zimeandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE).
Waziri Mkuu alisema Serikali imeanza kujielekeza katika kutoa mafunzo kwenye sekta za kipaumbele kwa kuzingatia Mpango wa Taifa wa Maendeleo kama kilimo biashara, mafuta, gesi, utalii, usafirishaji, ushonaji na bidhaa za ngozi.
Alisema jitihada zinaendelea kwenye maeneo mengine ili waajiri wawe na wigo mpana wa kuwapata wafanyakazi wenye stadi stahiki kwa kuwa Serikali inatambua umuhimu wa wao kuwa nguvu kazi yenye ujuzi na umahiri mkubwa kwa lengo la kuongeza tija.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alizungumzia changamoto inayolalamikiwa na waajiri ya uwepo wa tozo mbalimbali zinazotolewa na Mamlaka tofauti za Serikali kwa huduma ileile kuwa wanaitambua na tayari mchakato wa kuainisha sheria zote zinazoonekana kukwamisha uwekezaji pamoja na mazingira ya biashara nchini.
“Lengo letu ni kuendelea kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara nchini ili yaweze kuvutia zaidi na mchakato huu unashughulikiwa na Wizara ya Fedha na Mipango. Tunaomba mvumilie na mshirikiane nasi katika kuendelea kuziainisha sheria zinazokwaza biashara ili tuweze kuzijumuisha kwenye mapitio hayo,” alisema.
Hata hivyo, Waziri Mkuu aliwashauri waajiri wote nchini waendelee kufanyakazi zao kwa mujibu wa sheria ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima mahala pa kazi. Pia aliwasihi wafanyakazi wote kufanyakazi kwa bidii na uaminifu mkubwa ili waajiri waweze kupata faida, hivyo kuwaboreshea maslahi yao
Alisema “tunaposema Hapa Kazi Tu, tunamaanisha kazi kwenye sekta zote za uzalishaji na utoaji wa huduma bora nchini, iwe sekta ya binafsi au kwenye utumishi wa umma. Nawasihi ndugu zangu Watanzania, wekeni nadhiri kwamba katika mwaka 2017 mtafanya kazi kwa juhudi na maarifa ili kuongeza tija na ufanisi mahala pa kazi,”.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mheshimiwa Jenista  Mhagama aliwaomba waajiri wawasaidie kuweka msukumo katika juhudi za kutoa mafunzo kwa ajili ya uzoefu na kuongeza ujuzi kwa kutoa nafasi kwa wahitimu kupata uzoefu kwenye maeneo yao ya kazi.
Hata hivyo Mheshimiwa Jenista alisema anatambua umuhimu wa waajiri na wafanyakazi  katika utekelezaji wa sera ya maendendeleo ya nchi hasa kwa kuongeza ajira kupitia sekta ya viwanda kwa asilimia 40 kufikia mwaka 2020, mafanikio ya mpango huo yanategemea mchango wa waajiri kutoka sekta binafsi.
Pia aliwapongeza ATE kwa kutambua umuhimu wa kuwekeza katika rasilimali watu hasa kwa kutoa tuzo katika eneo la kuendeleza vipaji, ambapo aliwaomba tuzo ijayo waongeze kigezo cha kumpata mwajiri aliyetumia rasilimali zake kuongeza ujuzi kwa wafanyakazi wake ambao ndio chanzo cha kuinua tija na ushindani kibiashara.
“Natambua kuwa ATE mnatoa mafunzo katika sheria za kazi na usimamizi wa rasilimali watu ambayo husaidia kupunguza migogoro mahali pa kazi na hivyo kujenga mazingira tulivu maeneo ya kazi. Naomba kutumia wasaa huu kuwakumbusha waajiri kuwawezesha wafanyakazi kwenda kuhudhuria mafunzo mbalimbali ili kuweza kukidhi ushindani katika mazingira ya biashara,” alisema.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Dk. Aggrey Mlimuka alisema lengo la uaandaji wa tuzo hiyo ni kutambua wanachama wenye sera nzuri za usimamizi wa rasilimali watu katika taasisi na makampuni mbalimbali mwanachama hapa nchini.
Alisema kuwa tuzo hizo zinafuata mbinu za Kisayansi na kitaalamu ili kuangalia umuhimu wa Rasilimali watu katika makampuni ya Kibiashara makubwa na madogo na yale ya kati ili kuinua ujuzi wa wafanyakazi wanaofanya kazi kwa kujituma sehemu za kazi.
Dk. Mlimuka alisema kuwa tuzo hio pia ilijikita zaidi katika kuangalia maeneo muhimu ya rasilimali watu, uongozi, utawala, usimamizi wa Rasilimali watu, kusaidia jamii pamoja na kuwajibika katika jamii, ubora na uzalishaji.
NAMNA YA KUSHEREHEKEA MIAKA 55 YA UHURU WA TANZANIA

NAMNA YA KUSHEREHEKEA MIAKA 55 YA UHURU WA TANZANIA

December 09, 2016
Na Jumia Travel Tanzania

Ijumaa hii ya Desemba 9, 2016 Watanzania nchini na duniani kote watakuwa wakiadhimisha miaka 55 ya Uhuru uliopatikana kutoka kwa wakoloni wa Kiingereza mnamo mwaka 1961 chini ya uongozi wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Shamrashamra hizi ambazo zimeambatana na msimu wa sikukuu, Jumia Travel (www.travel.jumia.com) ingependa kukushauri kwamba unaweza kusherehekea kwa namna tofauti kabisa kwa kutembelea na kujivinjari katika hoteli za mikoa ya Dar es Salaam, Zanzibar na Arusha ambapo zimetoa punguzo la zaidi ya 40%.

Zanzibar

Zanzibar ni visiwa mojawapo vilivyobarikiwa kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii barani Afrika ambavyo vinakupa fursa ya kujifunza na kufurahia mengi endapo utatembelea. Kila sehemu ya visiwa hivi ni sehemu ya utalii kuanzia majengo yake, watu wake na tamaduni zao, vyakula pamoja na hoteli nzuri na fukwe safi za kuvutia zilizopo kila kona.

Sehemu kubwa ya watu na watalii wanafurika katika visiwa hivi hususani kuelekea msimu huu wa sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya. Kinachovutia zaidi ni hoteli nyingi kutoa ofa za kipekee kwa wageni ambao watapenda kutembelea huko kama vile malazi ambapo watu wengi hudai kwamba ni ya ghali sana.

Hoteli nyingi zimeshusha bei za malazi kwa kiasi kikubwa mpaka kufikia zaidi ya 40% kwa mfano kama ukitembelea hoteli za Ras Nungwi Beach Resort, Mazsons Hotel, Paradise Beach Resort (https://travel.jumia.com/en-gb/tanzania/o21502/paradise-beach-resort-uroa), Ras Mishamvi Beach Resort na Karamba Zanzibar.

Arusha

Mji wa Arusha uliopo Kaskazini mwa Tanzania umekuwa ni ndoto ya watu na watalii wengi kutembelea katika maisha na hii ni kutokana na hali nzuri ya hewa pamoja na vivutio kadhaa vya kitalii kama vile Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Mlima Meru ambao una asili ya volcano na pia umepakana na njia ya kuelekea ulipo Mlima Kilimanjaro.

Mbali na kuwa na vivutio vya kitalii pia mji huu hupendwa kutumiwa na mashirika pamoja na makampuni mbalimbali nchini na duniani kwa ajili ya vikao mbalimbali kutokana na utulivu ulionao. Kwa mfano Arusha imepewa heshima kubwa ya kuwa na ofisi ya Mahakama ya Umoja wa Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (UN - ICTR).

Kipindi hiki cha kusherehekea miaka 55 ya uhuru ambapo pia ni msimu wa sikukuu unaweza kutembelea na kufurahia vyote hivi huku ukiwa huna wasiwasi wa malazi kutokana na ofa kadha wa kadha zenye punguzo kwa zaidi ya 40% katika hoteli kama vile Ngorongoro Serena Safari Lodge, Arusha Center Inn & Tours, City Link Pentagon Hotel, Lush Garden Hotel (https://travel.jumia.com/en-gb/tanzania/o5079/lush-garden-hotel-arusha) na The Charity Hotel International.  

Dar es Salaam

Mji huu unachukuliwa kama kitovu cha biashara nchini Tanzania kutokana na kuwa na mashirika na makampuni kadhaa ya ndani na nje ya nchi kuwekeza. Wakazi wa Dar es Salaam siku zote wanakuwa wako kwenye pilikapilika za kutafuta riziki ili kuendana na gharama za maisha ambazo kwa kiasi kikubwa ni ghali.

Hali hiyo lakini haizuii kulifanya jiji hili kuwa na sehemu nyingi za kustarehe kwani sio watu wote ambao wanatoka nje ya mkoa huu kipindi hiki cha msimu wa sikukuu.

Kama utabakia jijini Dar likizo hii na hauna mpango wa kusafiri basi ni wakati wako wa kutembelea mtandao wa Jumia Travel na kujionea ofa kamambe za hoteli kama vile; Skippers Haven (https://travel.jumia.com/en-gb/tanzania/o26035/skippers-haven-dar-es-salaam-city-center), Q Bar and Guest House, ShaMool Hotel, Hotel De Mag Deluxe na Ramada Encore ambazo zimetoa punguzo kubwa huku kukiwa na huduma lukuki ndani yake.

Maadhamisho ya miaka 55 ya kusherehekea uhuru ni mingi na inahitaji namna pekee ya kuisherehekea, inawezekana akili na nguvu nyingi za watu zimeelekezwa kwenye sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya lakini siku hii ina umuhimu mkubwa kuienzi.
MWAMUZI JONESIA AZAWADIWA GARI

MWAMUZI JONESIA AZAWADIWA GARI

December 09, 2016
Wadau kadhaa wa mpira wa miguu, wamemzawadia gari Jonesia Rukyaaa mwamuzi mwandamizi wa FIFA ambaye hivi karibuni alichezesha vema michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake iliyofanyika nchini Cameroon.
Jonesia, ambaye amepata pia kuchezesha mchezo wa watani wa jadi katika soka nchini miaka miwili iliyopita, alichezesha mechi ya awali na kuonekana kutokuwa na upungufu kwenye kutafsiri sheria 17 za soka, alipangwa kuchezesha mechi ya mshindi wa tatu kati ya Ghana na Afrika Kusini.
Umahiri wake, umevutia wengi wakiwamo wadau wa mpira wa miguu ambao hawakupenda kutajwa walioamua kumzawadia gari aina Toyota Vits ikiwa ni zawadi na kumbukumbu yake baada ya kuiwakilisha vema nchi.
Kwa upande wa TFF ilimtuza Mwamuzi Jonesia cheti cha kutambua uwezo na kufikia hatua ya kulitangaza shirikisho  na nchi kwa ujumla. Rais wa TFF, Jamal Emil Malinzi ndiye aliyemkabidhi funguo za gari Jonasia.
Rais Malinzi alimsifu Jonesia kwa ujasiri na hatua aliyofikia na kumpa baraka za kumtakia mafanikio zaidi ya hapo ya kusonga mbele baada ya kufanya vema kwenye michuano ya Afrika Mashariki ya wanawake (CECAFA challange) na hiyo ya Wanawake Afrika.
“Ni Mtihani mkubwa to officiate (kuchezesha) mechi kubwa kama hiyo. Maana kila kosa linaweza kukuondoa na mafanikio ya kupata medali ya dhahabu kati ya waamuzi wanne ni hatua kubwa inayopaswa kutuzwa. Siwasemi FIFA, lakini itoshe kusema kuwa Jonasia unaweza kufika hatua ya kuchezesha fainali za kombe la dunia,” alisema Malinzi.
Rais Malinzi alipigia upatu kwa waamuzi wanaume nao kuandaliwa vema na kuchezesha michezo mikubwa ikiwamo ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwani kinachohitajika ni mikakati tu na kuitekeleza.
“Kamati ya waamuzi nawaachia kazi hii. Maana kazi kubwa ya uamuzi ni kusoma na mazoezi,” alisema Malinzi mbele ya baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Waamuzi akiwamo Mwenyekiti wake, Saloum Chama.
Jonesia ambaye wakati wote alikuwa na faraja, alimshukuru Mungu kwa mafanikio aliyofikia pia wadau wote wakiwamo wazazi wake na bibi yake aliyemlea baada ya kufariki mama yake mzazi na viongozi mbalimbali ambao aliwaelezea kumtia moyo.

MSD WAASWA KUBORESHA UPATIKANAJI DAWA NCHINI

December 09, 2016


 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mpoki Ulisubisya (kushoto), akihutubia wakati akizindua Baraza la tatu la Wafanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD), Dar es Salaam leo.
 Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi MSD, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo.
 Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakielezwa na viongozi wao katika mkutano huo.
 Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wakiwa kwenye
mkutano huo.

Na Dotto Mwaibale

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mpoki Ulisubisya amewaasa watumishi wa Bohari ya Dawa (MSD) kuhakikisha kuwa wanatekeleza majukumu yao ipasavyo ili kupunguza malalamiko ya wananchi juu ya ukosefu wa dawa.

Katibu Mkuu huyo ameyasema hayo Dar es Salaam leo wakati akizindua Baraza la tatu la Wafanyakazi la Bohari ya Dawa (MSD) ambapo pia amesisitiza kuwa Baraza hilo libuni mbinu na mikakati mbadala za kuboresha utendaji bila kusahau kutii miiko ya utumishi wa umma. 

Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi MSD, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu amemweleza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya kuwa tayari MSD imeanza kununua dawa na vifaa tiba kutoka kwa wazalishaji, ambapo hadi sasa wanawazalishaji 20 ambao wanamikataba, na wazabuni wengine 76 wadawana 79 wa vifaa tiba zabuni zao zinaandaliwa.

Mkutano huo umehudhuriwa na wajumbe kutoka Makao Makuu ya MSD na Kanda zote nane za MSD ambao ni pamoja na Mwenyeviti wa Tughe na matawi pamoja wawakilishi wa wafanyakazi.


WAMACHINGA JIJINI DAR ES SALAAM WAMPONGEZA RAIS DK.JOHN MAGUFULI KWA KUWARUHUSU KUFANYABIASHARA BILA KUBUGUDHIWA

December 09, 2016
 Mchuuzi wa urembo katika Soko la Tandika 
Kamtanda Hamisi akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi 
wakati akitoa maoni yake baada ya Rais Dk.John Magufuli kuwaruhusu wafanyabiashara kufanya biashara zao pasipo kubugudhiwa. Habari na maelezo ya wafanyabiashara wengine soma habari hapo chini.
 Muuza mitumba Hassan Bakar.
 Mfanyabiashara Juma Abdul 
 Mfanyabiashara wa viatu Evord Lyimo.
 Mfanyabiashara wa matunda Salum Ramadhan.
Mfanyabiashara wa mitumba Salum Mwinyimkuu
Wauza mitumba katika Soko la Tandika wakiwa wamepozi kwa furaha baada ya Rais Dk.John Magufuli kuwaruhusu kufanya biashara zao pasipo kubugudhiwa.

Na Dotto Mwaibale

WAFANYABIASHARA ndogo ndogo wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam wamempongeza Rais Dk.John Magufuli kwa kuwaruhusu kuendelea kufanyabiashara zao bila ya kubugudhiwa na kumtaja kuwa ni kiongozi wa wanyonge na watu wa chini.

Kauli hiyo wameitoa leo asubuhi wakati wakitoa maoni yao baada ya Rais kutoa tamko hilo Dar es Salaam jana.

Mchuuzi wa urembo katika Soko la Tandika Kamtanda Hamisi alimshukuru rais kwa kuwaruhusu na kuwajali watu wa chini.

"Nawaomba wafanyabiashara wenzangu ruhusa ya rais isiwe kibali cha sisi kuanza kupanga biashara zetu barabarani tufuate sheria" alisema Hamisi.

Muuza mitumba Hassan Bakar alisema Rais Magufuli yupo vizuri tunakila sababu ya kumpongeza katika jambo hilo la kuwatetea wanyonge yupo katika mstari ulionyooka na tumeteseka kwa miaka mingi.

Juma Abdul alisema anafuraha kwa uamuzi huo wa rais kwani ametimiza ahadi yake aliyoitoa wakati wa uchaguzi mkuu.

"Tulitukanwa sana na kunyang'anywa bidhaa zetu sasa baba yetu Magufuli ametuona na kutuondoa kwenye mateso hayo" alisema Abdul.

Mfanyabiashara wa viatu Evord Lyimo alisema walikuwa wakiishi kama digidigi na kupoteza bidhaa zao baada ya kuchukuliwa na mgambo sasa vitendo hivyo vimekoma kupitia kwa rais wetu tunampongeza kwa hatua hiyo.

Salum Mwinyimkuu alisema Rais yupo sahihi kwa hatua hiyo,  kazi hii tunayoifanya ndio ajira yetu inayotuwezesha kuishi na familia zetu.

Mfanyabiashara wa matunda Salum Ramadhan alisema wanamshukuru rais kwa ruhusa hiyo hivyo akatoa mwito kwa wenzake kuzingatia sheria ya kutofanya biashara barabarani na kuzuia vyombo vya moto visipite.