MIDO’ MZIMBABWE AWASILI YANGA SC TAYARI KUSAINI MIAKA MIWILI

August 05, 2015


Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
NAHODHA wa FC Platinum ya Zimbabwe kiungo, Thabani Kamusoko (pichani) amewasili Dar es Salaam jioni hii kwa ajili ya kusaini Mkataba wa kujiunga na Yanga SC.
Kamusoko amepokewa na Meneja wa Yanga SC, Hafidh Saleh jioni hii Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam na moja kwa moja kupelekwa kwenye kikao na viongozi.
Kamusako aliyewahi pia kuchezea Dyanamos FC ya Zimbabwe anatarajiwa kusaini Mkataba wa miwili Yanga SC.
Rasta huyo aliyeivutia Yanga SC ilipokutana na klabu yake, FC Platinum katika Kombe la Shirikisho mwanzoni mwa mwaka huu, anatarajiwa kuchukua nafasi ya Kpah Sherman aliyeuzwa Mpumalanga Black Aces ya Afrika Kusini.
Lakini pia, Yanga SC inafikiria kuwaacha wachezaji wake wengine wawili wa kigeni, beki Mghana Joseph Tetteh Zutah na kiungo Mbrazil, Andrey Coutinho.
Dirisha la usajili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara linatarajiwa kufungwa Saa 6:00 usiku wa kesho na kutakuwa na nafasi ya kusajili wa wachezaji huru tu kwa wiki moja ya mwisho kabla ya kuanza msimu mpya. 
Thabani Kamukoso (kushoto) akiwa na Meneja wa Yanga SC, Hafidh Saleh baada ya kuwasili JNIA

Baada ya Yanga SC kutolewa katika Robo Fainali michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame imekitathmini kikosi chake na kugundua Zuttah na Coutinho hawana faida.
Coutinho alijiunga na Yanga SC msimu uliopita akiletwa na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Mbrazil mwenzake, Marcio Maximo na hadi sasa ameichezea timu hiyo mechi 33 na kuifungia mabao sita.
Mbrazil huyo alikuwa ana wakati mzuri chini ya kocha Maximo, lakini tangu ujio wa Mholanzi, Hans van der Pluijm amepoteza nafasi katika kikosi cha kwanza.
Zuttah amesajiliwa Juni mwaka huu kufuatia kupendekezwa na kocha Pluijm, lakini baada ya wiki mbili za Kombe la Kagame, uongozi umeona hana umuhimu.
Mbali na Sherman, Coutinho na Zuttah wachezaji wengine wa kigeni Yanga SC ni Mkongo, Mbuyu Twite, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima, Mrundi Amissi Tambwe na Mzimbabwe Donald Ngoma.
Yanga SC ilifungwa kwa penalti 5-3 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 katika Robo Fainali ya Kagame dhidi ya Azam FC wiki iliyopita na tathmini ya baada ya mashindano, inaonyesha timu inahitaji marekebisho madogo. 
Na kwa kuona uimara wa Azam FC iliyotwaa Kombe la Kagame mwishoni mwa wiki na namna wapinzani, Simba SC wanavyojiimarisha, Yanga SC imeona kuna umuhimu wa kuleta wachezaji wengine bora zaidi kuchukua nafasi za Coutinho na Zuttah.
Tayari wakala Mganda, Gibby Kalule aliyewahi kuwauzia Yanga SC Sherman amependekeza beki wa kimataifa wa Togo, Vincent Bossou mwenye umri wa miaka 29 anayechezea Goyang Hi FC ya Korea Kusini
CCM WAANZA KUTUPA MAKOMBORA KWA LOWASSA

CCM WAANZA KUTUPA MAKOMBORA KWA LOWASSA

August 05, 2015


Mgombea wa urais kupitia CCM, John Pombe Magufuli pamoja na Mwenyekiti wa CCM taifa, Rais Jakaya Kikwete wakionesha fomu za kugombea nafasi hiyo alizochukua leo katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini(NEC).

Mgombea wa urais kupitia CCM, John Pombe Magufuli pamoja na mgombea mwenza, Samia Suluhu wakionesha fomu za kugombea nafasi hiyo walizochukua leo katika ofisi za Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC).




Wanachama wa CCM wakiwa makao makuu ya ofisi za CCM Dar es Salaam katika hafla ya mgombea wa CCM nafasi ya uraisi kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo alizochukua leo katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini(NEC).




Wanachama wa CCM wakiwa makao makuu ya ofisi za CCM Dar es Salaam katika hafla ya mgombea wa CCM nafasi ya uraisi kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo alizochukua leo katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini(NEC).


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Nape Nnauye akisalimia wanaCCM.


Mwenyekiti wa CCM taifa, Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM makao makuu ya CCM Dar es Salaam katika hafla ya mgombea wa CCM nafasi ya uraisi kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo alizochukua leo katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini(NEC).


Mgombea wa urais kupitia CCM, John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM makao makuu ya CCM Dar es Salaam.


Mwenyekiti wa CCM taifa, Rais Jakaya Kikwete akiimba wimbo na wananchi na wanachama wa CCM makao makuu ya CCM Dar es Salaam katika hafla ya mgombea wa CCM nafasi ya uraisi kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo alizochukua leo katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini(NEC).



Mwenyekiti wa CCM taifa, Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM makao makuu ya CCM Dar es Salaam katika hafla ya mgombea wa CCM nafasi ya uraisi kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo alizochukua leo katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini(NEC).CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kinakwenda kuingia kwenye Uchaguzi Mkuu kwa kushindana na wagombea ambao ni makapi yake ambao ni viongozi waliotoka chama tawala. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahaman Kinana alipokuwa akizungumza kwenye hafla ya mapokezi ya Mgombea Urais wa CCM, John Pombe Magufuli na mgombea mwenza, Samia Suluhu walipokuwa wakipokelewa baada ya kuchukua fomu ya kugombea urais toka Tume ya Uchaguzi nchini (NEC).
Kinana alisema CCM haina hofu na uchaguzi maana inakwenda kushindana na makapi yake ambao ni watu walioshindwa uchaguzi ndani ya chama na kukimbilia vyama vingine. “…Tunaenda kushindana na makapi yetu ni lazima kushinda, kwasababu tunashindana na makapi,” alisema Katibu Mkuu huyo wa chama tawala.
Magufuli na mgombea mwenza, Bi. Suluhu wamechukua fomu rasmi za kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo majira ya saa sita mchana katika msafara mkumbwa ukiongozwa na umati mkubwa wa wanaCCM waliojitokeza kwa wingi kumsindikiza mgombea wao hadi ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi na baadaye shughuli hiyo kupokelewa yalipo makao makuu ya ofisi za CCM mtaa wa Rumumba jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafka hivyo, Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete ambaye pia ni Rais wa Tanzania alisema chama hicho kina kila sababu ya kujidai kwani kimefanya maendeleo makubwa katika uongozi wake kikiwa madarakani mambo ambayo hata jumuiya za kimataifa zinayatambua. Alisema CCM inasifa na uzoefu mkubwa wa kuendesha dola hivyo inakila sababu ya kushinda Uchaguzi Mkuu na itawashinda wapinzania wake kama wamesimama.
“…Yaani kama ni mpira wa miguu tutafunga magoli wao wakiwa wamesimama…Tumejiandaa vya kutosha kushinda na kushinda tutashinda, tunao uzoefu, tunayo maarifa na uwezo wa kushinda tunao,” alisema huku akishangiliwa na wanaCCM.
Hata hivyo aliwataka wanaCCM wasimdharau adiu kwani aduni ni adui hata akiwa mdogo, hivyo kuwataka kushirikiana katika kuelekea uchaguzi kuhakikisha chama kinapata kura za kutosha. Aliongeza kuwa CCM imejipanga kwa hoja na ina mengi ya kuzungumzia uzuri wa chama hicho. “…Nchi ni tulivu, maendeleo yanaonekana na dunia nzima inajua tumepata mafanikio sasa kwanini CCM isishinde,” alihoji Rais Kikwete na kuendelea kuwa nchi ina demokrasia na utawala bora pamoja na uhuru wa vyombo vya habari.
Akizungumza katika hadhara hiyo Dk. Magufuli aliwashukuru umati wa watu na wanaCCM waliojitokeza kumsindikiza kuchukua fomu na kuwaahidi amejiandaa kuwatumikia bila kujadi itikadi zao, alisema yeye pamoja na mgombea mwenza anautambua ushirikiano huo. Alikishukuru chama cha CCM kwa kumuamini na kumteuwa kupeperusha bendera ya chama hicho.
Alisema mkusanyiko wa watu waliojitokeza kwenye hafla hiyo na msafara mzima ni ushahidi tosha kuwa chama hicho kitaendelea kuwa madarakani. Leo ilikuwa ni siku ya kuchukuwa fomu na nyinyi mmeshuhudia tumechukuwa na tutaizungusha kupata wadhamini kama ilivyo elekeza,”
Alisema shida za watanzania anazijua na matatizo ya Watanzania anayajua hivyo haita kuwa ngumu kufanya kazi yake na ukizingatia msingi mzuri uliowekwa na chama chake hivyo ni dhahiri CCM ina kila sababu ya kuendelea kuwa madarakani. Aliongeza kuwa anamengi ya kusema kwa wananchi lakini wakati wa kampeni bado hivyo wakati ukifika atazungumza.
CCM inatarajia kuzinduwa kampeni zake Agosti 22 jijini Dar es Salaam na tayari kuanza kazi ya kuinadi ilani ya chama na wagombea wake.

MTOTO WA LOWASSA, UMESHAMUONA AMEVAA GWANDA.... NIMEKUWEKEA HAPA AKIWA NA MH.SUGU

August 05, 2015


 
Mtoto wa Mh Edward Lowassa, Fred Lowassa akiwa na Mh. Joseph Mbilinyi Sugu

William Rutto – Hongera Rais Kikwete kwa kukuza tasnia ya filamu Nchini Tanzania

August 05, 2015
Makamu wa Rais Wa Kenya, Mh William Rutto akifungua maonyesho ya pili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Utamaduni Festival yajulikanayo kama JAMAFEST kwa kuwakaribisha washiriki kutoka nchi zote za Afrika Mashariki katika ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa Kenyatta uliopo jijini Nairobi, Nchini Kenya. Makamu wa Rais wa Kenya, Mh William Rutto akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Kenyatta kabla ya ufunguzi wa maonyesho ya JAMAFEST 2015
 Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini tawi la Makumira wakitoa burudani ya ngoma wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya pili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Utamadanu Festival yajulikanayo kama JAMAFEST katika ukumbi wa mikutano wa kimtaifa wa Kenyatta.
 Baadhi ya washiriki wa maonyesho ya JAMAFEST 2015 kutoka nchini Burundi wakiwa katika viwanja vya KICC Nairobi Kenya
Na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
Makamu wa Rais wa Kenya, Mh William Rutto amempongeza rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuweza kukuza tasnia ya filamu nchini Tanzania na kupelekea Wananchi wa Kenya na Jumuiya ya Afrika Mashariki kupenda zaidi filamu za Kitanzania ambazo zimekuwa na soko kubwa sana katika nchi za Jumuiya ya Mashariki.
Akizungumza hayo wakati wa uzinduzi wa tamasha la Jumuiya ya Afrika Mashariki Utamaduni lijulikanalo kama JAMAFEST 2015 linalofanyika katika viwanja vya ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Kenyatta uliopo katika Jiji la Nairobi Nchini Kenya, Makamu wa Rais wa Kenya, Mh Rutto pia aliwapongeza marais wa nchi za Jumuiya Ya Afrika Mashariki kwa juhudi zao katika Shughuli mbalimbali za kijamii, uchumi, utamadanu na Michezo.
Mh Rutto alitoa pongezi kwa Rais Wa Rwanda, Mh Paul Kagame kwa kutoa mchango mkubwa sana katika Michezo kwa kudhamini Michuano ya Kombe la Kagame ambapo mwaka Huu Timu ya Azam FC kutoka Nchini Tanzania iliweza kuibuka mshindi kwa kuifunga Timu yao ya Kenya Gor Mahia kwa mabao Mawili kwa sifuri. Vilevile Mh Rutto aliipongeza timu ya Azam kwa kuweza kuwa mabingwa wa Kombe la Kagame kwa kuweza kuifunga timu yao ya Kenya ya Gor Mahia na kuweza kuibuka washindi wa Kombe la Kagame linalodhaminiwa na rais wa Rwanda Nh Paul Kagame. Mbali na Kumpongeza rais wa Rwanda na Tanzania pia Makamu wa Rais wa Kenya, Mh William Rutto aliwapongeza pia rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa kuwa mstari wa mbele katika Kukuza utamaduni wa Nchi yake huku Rais wa Burundi akipongezwa Kwa Kuweza kusakata kabumbu na kusema kuwa anatamani awe rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA).
Maonyesho ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Utamaduni (JAMAFEST) yameshirikisha nchini zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo Kila Nchi mwanachama wameweza kuonyesha Bidhaa zao pamoja na utamaduni wao. Maonyesho haya ya JAMFEST hufanyika kila baada ya Miaka Miwili ambapo mwaka 2013 Maonyesho haya yalifanyika nchini Rwanda na mwaka huu yanaendelea kufanyika Nchini Kenya huku mwaka 2017 maonyesho haya yanatarijiwa Kufanyika Nchini Tanzania.
NCHI WAHISANI WATOA DOLA ZA MAREKANI MILIONI 802.15 KUKABILI MABADILIKO YA TABIA NCHI

NCHI WAHISANI WATOA DOLA ZA MAREKANI MILIONI 802.15 KUKABILI MABADILIKO YA TABIA NCHI

August 05, 2015
IMG_1116
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akimkaribisha ofisini kwake Mwakilishi wa mtandao wa FANPRAN, Sithembile Ndema kwa ajili ya kusaini kitabu cha wageni kabla ya kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Na Mwandishi wetu
JUMLA ya dola za Marekani milioni 802.15 zimetolewa na nchi wahisani katika kusaidia mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi katika kipindi cha miaka miaka mine iliyopita.
Hayo yalielezwa na Mkurugenzi wa Kituo cha Mabadiliko ya tabia nchi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Profesa Pius Yanda wakati alipokuwa akitoa mada kuhusu utafiti alioufanya yeye na wenzake kuhusu mchango wa uwezeshaji mapambano hayo kutoka nchi marafiki.
Alisema kiasi hicho cha fedha ni sawa na wastani wa dola milioni 200 kila mwaka zilizokuwa zikipelekwa katika sekta mbalimbali nchini.
Alisema utafiti walioufanya ambao ulilenga kuona kiasi cha fedha zilizotoka kwa wafadhili kwa ajili ya miradi mbalimbali ni awamu ya pili ya utafiti ambao awali ulijikita kuona bajeti ya taifa inavyotumika kukabili mabadiliko ya tabia nchi.
Profesa Yanda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere cha Mazingira amesema kwamba sehemu kubwa ya fedha ipo katika miradi ya maendeleo ambayo utekelezaji wake pamoja na kutosema kwamba unakabili mabadiliko ya tabia nchi, matokeo yake ndiyo yanayobainisha.
IMG_1128
Mkurugenzi wa Kituo cha Mabadiliko ya tabia nchi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Profesa Pius Yanda (kushoto) akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (wa pili kushoto) huku wengine wakishuhudia zoezi hilo, Kulia ni Mwakilishi wa FANPRAN, Sithembile Ndema na wa pili kulia Mtafiti msaidizi kutoka ESRF, Ian Shanghvi.
Alitolea mfano kuwa miradi ya kusambaza umeme vijijini ( REA) nchini ambayo ilipata fedha nyingi katika miaka ya 2011 na 2012 ni miradi ya maendeleo lakini hatima yake ni kuzuia ukataji hovyo wa miti kwa ajili ya nishati.
Akifafanua fedha hizo zaidi alisema kwamba Tanzania mwaka 2010 jumuiya ya kimataifa zilitoa dola za Marekani milioni 171.93, mwaka 2011 dola za Marekani milioni 225.35, mwaka 2012 dola za Marekani milioni 229.74 na mwaka 2013 Tanzania ilipata dola za Marekani milioni 175.14.
Utafiti huo ambao uligharamiwa na COMESA, EAC na SADC umewasilishwa katika mkutano wa kitaifa wa uwezeshaji wa miradi ya kukabili tabia nchi kwa mfumo wa ndani ambapo pia Mwakilishi wa mtandao wa FANRPAN, Sithembile Ndema alikuwepo kuelezea maana ya mikutano ya kisera katika nchi zinazounda mtandao huo.
Mtandao huo ambao ulianzishwa mwaka 1994 baada ya mkutano wa mawaziri wa kilimo wa nchi za SADC, EAC na COMESSA na makao makuu yake kuwa nchini Zimbabwe ulianza kazi mwaka 1997 na sasa makao makuu yapo nchini Afrika Kusini.
Mtandao huo umelenga kuwezesha mataifa ya Afrika kuendesha kilimo na ufugaji unaozingatia mabadiliko ya tabia nchi na hivyo kutunza mazingira na kuongeza tija.
Mikutano ya aina hiyo pia inafanyika Uganda, Ethiopia, Kenya na Zambia.
Profesa Yanda alisema kwamba pamoja na fedha hizo kuonekana nyingi kiukweli ni haba kutokana na hali halisi ilivyo sasa na hasa ikizingatiwa kwamba kunatakiwa pia fedha za mabadiliko tabia nchi yenyewe badala ya kutumia miradi ya maendeleo ambao matokeo ni kukabili mabadiliko ya tabia nchi.
IMG_1149
Mshehereshaji Hanif Tuwa kutoka ESRF, akitoa mwongozo wa yatakayojiri kwenye mkutano wa kitaifa wa kujadili sera ya uwezeshaji kifedha mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za ESRF.
Alisema takwimu walizopata kuhusu fedha zilizofika nchini kutoka katika jumuiya ya kimataifa zililingana na taarifa zilizopo Hazina na kuonesha kwamba fedha hizo zilienda kutumika katika makadirio yaliyokusudiwa.
“tofauti iliyopo ni tafsiri ya miradi ya mabadiliko ya tabianchi. Miradi ya maendeleo, inatamkwa kama miradi ya maendeleo lakini ukiangalia mwishoni ni miradi hiyo kusaidia katika kukabili mabadiliko ya tabia nchi” alisema katika mahojiano baadae na na waandishi wa habari.
Alisema kama Mkurugenzi wa Kituo cha mabadiliko ya tabia nchi anashauri serikali kuhimiza wananchi wake kuendelea kusimamia mazingira vyema huku wakulima na wafugaji wakisikiliza maofisa ugani kwa ajili ya kuwa na kilimo na ufugaji bora usioharibu mazingira..
Alisema tafiti mbalimbali zinaonesha kuwepo kwa athari kubwa ya mabadiliko ya tabia nchi ambapo sasa hata sehemu za baridi za nyanda za juu zimeanza kuwa na magonjwa ya Malaria huku wakulima wakiwa hawajui muda wa kupanda kutokana na mabadiliko ya joto na pia unyeshaji wa mvua.
Alisema pia nyanda za juu sasa zinakabiliwa na wadudu waharibifu wa mazao vitu ambavyo awali havikuwepo.
Alisema kwamba bado taifa linahitaji kufanya tafiti nyingi zaidi na kuzitumia kuelimisha umma kuhusu nini kinatokea na nini kinastahili kufanywa kukabili mabadiliko hayo.
IMG_1174
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akihutubia mkutano wa kitaifa wa kujadili sera ya uwezeshaji kifedha mabadiliko ya tabia nchi. Mkutano huo umefanyika jana jijini Dar es salaam katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za ESRF na kujadili taarifa ya utafiti uliofanywa kwa miaka minne kuhusiana na uwezeshaji.
Mkutano huo wa kitaifa ulifunguliwa na Mkurugenzi wa Taasisi huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) Dk. Tausi Kida ambaye alisema lengo la mkutano huo ni kuchambua utafiti uliofanywa na kuja na maazimio yatakayosaidia kuboresha kilimo na kuhifadhi mazingira katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.
Aliwaambia washiriki kuiangalia kwa makini tafiti ya Profesa Pius Yanda na kuhakikisha kwamba wanakuwa na uelewa wa maudhui na kuwezesha kutoa dira ya utekelezaji katika siku za usoni.
Alisema wakati taifa linajipanga kutekeleza mpango wake wa maendeleo wa kuelekea katika uchumi wa viwanda suala la mabadiliko tabia nchi haliwezi kuachwa na hivyo wajumbe wa mkutano walitakiwa kuangalia na kuja na mapendekezo yao.
Mapendekezo hayo ni pamoja na kuwa na kilimo na ufugaji wenye tija unazoingatia ufanisi katika hifadhi ya mazingira na namna uwezeshaji wa ndani unavyoweza kuendeleza mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.
Alisema ni muhimu kilimo kuwa ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
ESRF ni taasisi yinayojishughulisha na tafiti mbalimbali za jiuchumi na kijamii zinazotoa mwelekeo wa utekelezaji wa sera na kanuni mbalimbali za maendeleo na ustawi wa jamii.
Pmaoja na kuratibu mkutano huo pia ilitoa nafasi ya ukumbi wake kutumika na kutoa mwelekeo wa mkutano na umuhimu wake katika mpango wa pili wa maendeleo wa taifa ambao unatakiwa uzingatie mabadiliko ya tabia nchi.
IMG_1161
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akisoma hotuba na kuwakaribisha washiriki wa mkutano wa kitaifa wa kujadili sera ya uwezeshaji kifedha mabadiliko ya tabia nchi. Kulia ni Mwakilishi wa FANPRAN, Sithembile Ndema na kushoto ni Mkurugenzi wa Kituo cha Mabadiliko ya tabia nchi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Profesa Pius Yanda.
IMG_1203
Mwakilishi wa FANPRAN, Sithembile Ndema akielezea mradi wa COMESA wa uwezashaji wa ndani wa fedha kwa ajili ya mabadiliko ya tabia nchi katika mkutano huo.
IMG_1249
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (katikati) na Mkurugenzi wa Kituo cha Mabadiliko ya tabia nchi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Profesa Pius Yanda (kulia) wakifuatilia ka umakini 'presentation' ya Mwakilishi wa FANPRAN, Sithembile Ndema (hayupo pichani).
IMG_1318
Mkurugenzi wa Kituo cha Mabadiliko ya tabia nchi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), Prof. Pius Yanda, akitoa mada ya ufadhili wa kimataifa wa uwezeshaji wa kifedha wa mabadiliko ya tabianchi Tanzania katika mkutano huo.
IMG_1370
Pichani juu na chini washiriki wakichangia mawazo yao kuhusu namna sera ya uwezeshaji kifedha mabadiliko ya tabia nchi inavyopaswa kuwa katika mkutano huo.
IMG_1343
IMG_1150
Pichani juu na chini ni washiriki kutoka taasisi mbalimbali za serikali na zisizo za serikali, watafiti, na wadau wa maendeleo waliohudhuria mkutano wa kitaifa wa kujadili sera ya uwezeshaji kifedha mabadiliko ya tabia nchi.
IMG_1155
IMG_1231 IMG_1260
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa kitaifa wa kujadili sera ya uwezeshaji kifedha mabadiliko ya tabianchi.
IMG_1256
Picha ya pamoja ya washiriki.

WASHIRIKI WA SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2015 WAWASILISHA MIRADI YAO YA KILIMO NA MAZINGIRA KWA WANAKIJIJI WA KISANGA WILAYANI KISARAWE PWANI

August 05, 2015


 Washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015 wakiwa katika Bwawa la Lamboni wakipata maelezo kutoka kwa wanakijiji hii ikiwa ni moja ya sehemu ya ziara yao jana .
 Wenyeji pamoja na  Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula wakielekea Mabondeni..Ilikuwa ni nafasi yao ya kufahamu maeneo mbalimbali Kijijini hapo...
 Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa chakula wakioneshwa Madhari ya shule ya Msingi ya Kisanga na mmoja wa wanakijiji aliyesimama Mbele Kulia.
 Hapa washiriki wa Shindano la Mama Shijaa wa chakula 2o15 linalo andaliwa na Oxfam kupitia kampeni yao ya Grow , kipindi kinachoruka kila siku ITV kuanzia Saa Kumi na mbili  Jioni na Kurudiwa saa Tano na nusu asubuhi  wakiwa katika ofisi ya Kusindika zao la Mihogo
 Hapa washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 msimu wa nne wakiwa katika moja ya kisima ambacho maji yake yananukia Mafuta, maji haya yanatumika zaidi katika shughuli za Kufulia Nguo.
 Mwakilishi kutoka Oxfam Eluka Kibona aliyesimama (Kulia) akizungumza na Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula Pamoja na wanakijiji katika Kijiji Cha Kisanga jana.
 Kundi la kwanza la Washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015 wakiwasilisha Mradi wao wa Mazingira..
 Wanakijiji na Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 wakiwasikiliza jinsi Miradi inavyo wasilishwa.
 Kundi la pili la washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 wakiwasilisha Mradi wao wa Kilimo Bora.

 Kundi la Tatu la washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 wakiwasilisha Mradi wao wa Kilimo Bora cha Mboga Mboga na Hihogo.
********
Ni siku nyingine tena katika kijiji cha Kisanga, jua la saa nne asubuhi ni kali huku  mti huu mkubwa wa mkorosho uliopo eneo la makutano unatusitiri. Washiriki wa shindano la Mama shujaa wa Chakula Shindano lililiondaliwa na Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow, walikuwa wamesimama vikundi vikundi, bila shaka walikuwa wanahadithiana chakula walichowapikia wenyeji wao jana. 

Siku ya ilikuwa  inaanza kwa waandaaji wa shindano kutengeneza makundi matatu ya kina Mama Shujaa wa Chakula watano watano. 

Kwa muda watakaokaa hapa kijijini Kisanga, kila kundi linatakiwa kutengeneza mradi wa maendeleo endelevu kwa manufaa ya kijiji cha Kisanga. Ili kufahamu fursa na changamoto zilizopo, uongozi wa kijiji unawatembeza sehemu nne. 

Upatikanaji wa maji ya uhakika kijijini hapa ni changamoto. Kina Mama Shujaa wa Chakula wanaletwa sehemu hii yenye bwawa, wenyeji wanaiita lamboni. Inasadikika kuwa zamani kulikuwa na kisima, ila kwa sasa kimefunikwa na wingi wa maji. Pia kuna viumbe wakali kama vile chatu. 

Elimu ya msingi katika kijijini Napo inatolewa katika shule ya msingi Kisanga. Wakina Mama Shujaa wa Chakula wanaoneshwa mandhari ya shule na mwenyeji. 

Wakazi wa kijiji cha Kisanga wanapata maji ya kunywa na kupikia katika visima vilivyopo eneo hili linaloitwa Mfuru. Kufuatia msimu wa mvua ulioisha, visima vyote vinne vina maji ya kutosha, japo kisima kimoja maji yake hayatumiwi kwa kunywa kwani yana harufu inayosadikika kuwa ni ya mafuta. Hata hivyo, wakati wa kiangazi kina mama (wenyeji) wanalazimika kuamka saa tisa alfajiri kutokana na uhaba wa maji, na kibaya zaidi usalama wao wakiwa njiani ni wa mashaka kwani hawapewi msaada na waume zao (kwa walioolewa). 

YST YAENDESHA MAONYESHO YA 5 YA SAYANSI, JIJINI DAR

August 05, 2015

Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi Mwenza wa taasisi ya Young Scientists Tanzania (YST), Dk. Gosbert Kamugisha, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo hii wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya siku tatu ya miradi na ubunifu wa kisayansi uliofanywa na wanafunzi kutoka shule 120 nchini. Maonyesho hayo yatafikia kilele Ijumaa Agosti 7, 2015. (Picha zote na Daniel Mbega wa www.brotherdanny.com).

Mwanzilishi Mwenza wa YST, Joseph Clowry, akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo hii. 
Makamu wa Rais wa kampuni ya kuchakata mafuta na gesi ya BG Tanzania, John Ulanga, akizungumzia udhamini wao katika maonyesho hayo ya YST. Kampuni hiyo imetoa kiasi cha Dola 200,000 kudhamini maonyesho ya mwaka huu. 
Naibu Balozi wa Ireland nchini, Brian Noran, akizungumzia maendeleo ya tafiti za kisayansi kwa taifa lolote duniani. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi Mwenza wa YST, Dk. Gosbert Kamugisha.
Mkutano ukiwaunaendelea. 
Wanahabari wakiwa kazini. 
Wanahabari wakifuatilia kwa makini. 
Mwalimu Geofrey Ndunguru (kulia) na mwanafunzi Yussuph Mwenda kutoka Shule ya Sekonari ya Wavulana Songea nao wanashiriki maonyesho hayo kuzungumzia Uchambuzi wa Mtazamo wa Wanafunzi Wasioona kuhusiana na Sayansi. 
Mwanafunzi Gladness Mpelemba (kulia) wa kidato cha tatu kutoka Shule ya Sekondari Sumaye mjini Morogoro akielezea kuhusu utafiti wao wa 'Kutumia Njia za Asili za Kupanga Uzazi Kupunguza Madhara kwa Wanawake'. Kushoto ni mwenzake Glory Crispine. 
Wanafunzi wakiendelea kuonyesha tafiti zao. 
Mojawapo ya utafiti uliofanywa na wanafunzi Saada Abeid na Zaina Maliki wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Mtwara. 
Majaji wakiwa kazini leo hii ili kuwapata washindi watakaotunukiwa zawadi mbalimbali hapo kesho ambapo Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, ndiye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Na Daniel Mbega
MAONYESHO ya Tano ya Sayansi kwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini yamefunguliwa rasmi jijini Dar es Salaam leo yakiwa yanaendeshwa na kuratibiwa na taasisi ya Young Scientists Tanzania (YST).Maonyesho hayo ambayo yanafanyika kwenye Ukumbi wa iamond Jubilee yanashirikisha jumla ya wanafunzi 240na walimu 120 kutoka shule 120 nchini yanatarajiwa kufikia kilele keshokutwa Ijumaa ingawa kesho Alhamisi zawadi mbalimbali zitatolewa kwa washindi zikiwemo fedha taslimu, medali, vikombe, vifaa vya maabara pamoja na maktaba.
Dk. Gosbert Kamugisha, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi Mwenza wa YST, amesema mgeni rasmi atakayetoa zawadi kwa washindi hapo kesho atakuwa Rais mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi.
“Maonyesho haya ni kwa ajili ya kuonyesha ubunifu na utafiti wa kisayansi uliofanywa na wanafunzi wa sekondari na katika kipindi cha siku tatu kuanzia leo wanafunzi hao wataonyesha miradi mbalimbali katika maeneo tofauti ya kisayansi kama kemikali, fizikia na sayansi ya hisabati, sayansi ya kibaolojia na kiikolojia, sayansi ya kijamii na kitabia, na teknolojia,” alisema Dk. Kamugisha.
Aliongeza kwamba, kama njia ya kutambua kazi iliyofanywa na wanafunzi hao, ndiyo maana wameandaa zawadi mbalimbali kuwamotisha ambapo mbali ya zawadi zilizotajwa, pia wanafunzi sita wanaweza kupata udhamini (scholarship) kwa ajili ya masomo ya chuo kikuu kwa fani mbalimbali za sayansi na teknolojia, udhamini ambao hutolewa na taasisi binafsi ya Karimjee Jivanjee Foundation ya jijini Dar es Salaam.
“Maonyesho ya mwaka 2015 ya YST yanalenga kuonyesha vipaji na ubunifu wa wanafunzi wa sekondari, lakini pia ushuhuda wa umahiri wa mbinu za ufundishaji kwa walimu ambao ndio wanaowaongoza wanafunzi hao yakiwa ni matunda ya mafunzo yanayotolewa na YST kwa walimu wa sayansi katika kipindi cha miaka minne iliyopita,” aliongeza Dk. Kamugisha.
Amewataja wadhamini wakubwa wa maonyesho ya mwaka huu kuwa ni kampuni ya BG Tanzania inayojihusisha na masuala ya utafiti wa mafuta na gesi asilia pamojana Shirika la Kimataifa la Misaada la Ireland (Irish Aid).
Akizungumzia mafanikio ya maonyesho hayo, Dk. Kamugisha alisema mwitikio umekuwa mkubwa zaidi tofauti na walipoanza maonyesho hayo mwaka 2011.
“Wakati tulipoanza mwaka 2011 walishiriki wanafunzi nane tu, mwaka 2012 wakawa 300 kwani zilikuwepo shule 100, mwaka 2013 walishiriki wanafunzi 200, mwaka 2014 pia walikuwepo wanafunzi 200 lakini mwaka huu wamekuwa 240 kwani hata shule zimeongezeka kutoka 100 hadi 120.
“Tulipokea maombi ya shule 400 nchi nzima, lakini tukaamua kuzichagua hizi 120. Tulizitembelea shule zote 400 mara tatu kwa mwaka, ndipo hatimaye tukaziteua hizi zinazoshiriki ingawa tunaamini kwamba shule nyingi sasa zimehamasika na watoto wanapenda sayansi,” alisema.
Akizungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari, Mwanzilishi Mwenza wa YST Joseph Clowry, alisema kwamba kuna dalili za mafanikio tangu walipopata wazo la kuanzisha taasisi hiyo mwaka 2009, kwani mwitikio umeonekana kuwa mkubwa kadiri miaka inavyokwenda.
Alisema, ili taifa lolote liendelee, ni vyema kuwekeza zaidi katika tafiti za kisayansi kwa kuanzia kwenye ngazi za chini kabisa kama wao wananvyofanya.
“Ireland ilikuwa nyuma kimaendeleo kama zilivyokuwa nchi nyingi ulimwenguni, lakini walipoamua kuwekeza kwenye sayansi hali imebailika hivi sasa ambapo wapo wanasayansi mahiri kabisa na vijana nao wanapenda kujifunza masomo ya sayansi,” alisema Clowry.
Kwa upande wake, Makamu Rais wa BG Tanzania anayeshughulikia Sera na Masuala ya Uhusiano, John Ulanga, alisema wameamua kujitolea kudhamini YST kwa sababu wanatambua kwamba Tanzania inahitaji kuwa na wanasayansi wengi hasa tunapozungumzia suala la mafuta na gesi ambayo yakitafitiwa yakapatikana na kuchakatwa yanaweza kuinua uchumi wa taifa kwa kiwango kikubwa.
“Tunahitaji wanasayansi wa kutosha katika sekta hii adhimu ya mafuta na gesi, tukiwa nao wazalendo itakuwa ni bora zaidi, hivyo ni lazima tuwadhamini watu kama YST ambao wanajenga msingi imara katika kuwapata wataalamu wa kesho,” alisema Ulanga.
Ulanga alisema kwamba, kwa mwaka huu kampuni yake imetoa Dola 200,000 (takriban Shs. 450 milioni) kwa ajili ya udhamini wa maonyesho hayo na akaahidi kwamba wataendelea kudhamini kwa kadiri ya mahitaji na hali itakavyoruhusu.
Naye Brian Noran, Naibu Balozi wa Ireland nchini, amesema ni jambo la busara kwa serikali na jamii kuwekeza katika utafiti wa kisayansi kama kweli taifa linataka maendeleo, lakini akaahidi kwamba serikali yake itaendelea kusaidia kwani inatambua umuhimu wa kuwa na wanasayansi wabunifu.
Aliwapongeza YST kwa hatua waliyoifikia mwaka huu na kuwahamasisha waongeze bidii zaidi ili kujenga taifa la wanasayansi kwa kuanzia ngazi ya chini.
“Sayansi ndiyo inayoweza kuleta mabadiliko na maendeleo, hivyo ni muhimu kuendelea kuwazalisha wanasayansi ambao watakuja kuwa wabunifu wazuri hasa katika karne hii ya sayansi na teknolojia,” alisema Noran.
(IMEANDALIWA NA www.brotherdanny.com. Simu 0656-331974)