DAVID MWAMWAJA: LENGO LETU MSIMU UJAO NI KUIRUDISHA JUU PRISONS
Kocha mkuu wa Prisons, David Mwamwaja ( wa kwanza kulia)
Na
Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
David
Mwamaja hajafanya usajili mkubwa licha ya kikosi chake kupambana hadi dakika ya
mwisho msimu uliopita ili kusalia katika ligi kuu.
Baada
ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ashanti United, 24 April, Tanzania Prisons
ilifanikiwa kubaki katika ligi kuu Bara. Wengi walitaraji timu hiyo ingefanya
usajili mkubwa wakati wa dirisha la usajili kwa kuamini kuwa timu hiyo
inahitaji mabadiliko makubwa.
Haijawa hivyo na Mwamaja ameweza kuhakikisha
mchezaji wa timu ya Taifa ya Zanzibar, Amir Omary anatua katika kikosi chake
kwa lengo la kuongeza makali katika safu ya mashambulizi ambayo ilibebwa zaidi
na mshambulizi, Peter Michael na Richard Peter msimu uliopita.
“
Ligi itakuwa ngumu msimu ujao, lakini tunataka kuirudisha juu Tanzania Prisons
kama ilivyokuwa enzi za kina Osward Morris.Nimeongezwa katika timu hii kwa
lengo la kusaidiana na wachezaji waliopo ili kuifanya Prisons kuwa timu bora
msimu ujao.. Tangu nimefika hapa nimepata vitu vingi vipya ndani na nje ya
uwanja. Upendo, ushirikiano na umoja ni mambo yaliyotawala hapa” anasema
mshambulizi, Amir Omary ambaye amesajiliwa akitokea klabu iliyoshuka daraja ya
JKT Oljoro.
Michael
alifunga mabao 12 msimu uliopita, Richard alifunga mabao manne na Amir alifunga
mabao sita katika kikosi cha Oljoro msimu uliopita na mchexzaji huyo wa
Zanzibar Heroes anaamini kuwa umoja wao utawasumbua walinzi wengi msimu wa
2014/15.
“
Ni safu kali ya mashambulizi, kila timu imejiandaa msimu ujao lakini nachoweza
kusema tumejipanga kuhakikisha Prisons inafanya vizuri msimu ujao. Mwalimu yoko
poa na kila mmoja kikosini anafahamu ni kitu gani ambacho kinatakiwa”
RAIS KIKWETE AKUTANA NA BIBI YAKE RAIS OBAMA WA MAREKANI,JIJINI NAIROBI LEO
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Bibi yake Rais wa Marekani,Mh. Barack
Obama,Mama Sarah Obama walipokutana Leo kwenye hoteli ya Villa Rosa
Kempiski jijini Nairobi, Kenya, wakati Rais Kikwete akijiandaa kurejea
nchini.Mama Sarah Obama anatarajia kuzindua taasisi ya kusaidia elimu
kijijini Kogelo nchini Kenya,alikozaliwa Baba yake na Rais Obama wa
Marekani itakayofahamika kama (Sarah Obama foundation) ambapo atajenga
shule kuanzia za awali mpaka sekondari. Rais kikwete sasa hivi yuko
mjini Kondoa kuendelea na ziara yake ya Mkoa wa Dodoma.PICHA NA IKULU
Rais Dk.Shein na Marais mbali mbali katika uzinduzi wa Mpamgo wa WIOCC SAMOA.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,akisalimiana na Waziri wa Mambo ya nje ya nchi wa Seychels
Jeun-Paul Adam baada ya Waziri huyo kutoa hotuba yake katika Uzinduzi wa
Mpango wa Magharibi ya Bahari ya Hindi ya Changamoto za Ukanda wa Pwani
namabadiliko tabianchi jana katika Orator Hotel,Apia Samoa[Picha na
Ramadhan Othman,Samoa.]
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,akitoa hutuba yake katika Uzinduzi wa Mpango wa Magharibi ya
Bahari ya Hindi ya Changamoto za Ukanda wa Pwani na mabadiliko tabianchi
jana katika Orator Hotel,Apia Samoa ambapo Mkutano wa Tatu wa Kimataifa wa Nchi za Visiwa unaendelea.[Picha na Ramadhan Othman,Samoa.],[Picha na Ramadhan Othman,Samoa.]
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,(katikati) Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Bibi
Fatma Abdulhabib Fereji,pamoja na viongozi wengine wakiwa katika
Uzinduzi wa Mpango wa Magharibi ya Bahari ya Hindi ya Changamoto za
Ukanda wa Pwani na mabadiliko tabianchi jana katika Orator Hotel,Apia
Samoa ambapo Mkutano wa Tatu wa Kimataifa wa Nchi za Visiwa
unaendelea.[Picha na Ramadhan Othman,Samoa.]
Baadhi ya washiriki katika uzinduzi wa Mpango
wa Magharibi ya Bahari ya Hindi ya Changamoto za Ukanda wa Pwani na
mabadiliko tabianchi jana katika Orator Hotel,Apia Samoa ambapo Mkutano
wa Tatu wa Kimataifa wa Nchi za Visiwa unaendelea wakifuatilia kwa
makini hutuba mbali mbali zilizotolea na Viongozi kutoka Nchi
tofauti,(kushoto) Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimaifa
Mahadhi Juma Maalim.[Picha na Ramadhan Othman,Samoa.]
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,(katikati)akiteta na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa
Rais Bibi Fatma Abdulhabib Fereji, katika Uzinduzi wa Mpango wa
Magharibi ya Bahari ya Hindi ya Changamoto za Ukanda wa Pwani na
mabadiliko tabianchi jana katika Orator Hotel,Apia Samoa ambapo Mkutano
wa Tatu wa Kimataifa wa Nchi za Visiwa unaendelea katika nchi
hiyo.[Picha na Ramadhan Othman,Samoa.]
MKURUGENZI NHC ATEMBELEA ENEO LA MRADI WA NYUMBA ZA WATUMISHI HALMASHAURI YA BUSOKELO MBEYA
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw.Nehemia Kyando Mchechu wa kwanza kulia mbele akitembelea
eneo la ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zitakazojengwa katika
Halmashauri ya Busekelo Mkoani Mbeya alipotembelea Halmashauri hiyo
Septemba 3 mwaka huu .Picha na Saguya wa NHC.
|
Shirika la Nyumba la Taifa lakabidhi mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana Arusha
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Nyirembe Munasa, Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa Bi.Rachel Kassanda wakiwa tayari kutoa hundi kwa mmoja wa kiongozi wa vikundi vya vijana baada ya kupokea hundi. (Picha zote kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Jamii)
Kiongozi wa mbio za mwenge Rachel Kassanda akikagua matofali na nyuma yake ni mkuu wa wilaya ya Arumeru Nyerembe Munasa.
Maafisa toka NHC Amoni Mazanda na Gibson Mwaigomole wakiangalia baadhi ya mambo yaliyoratibiwa na wenyeji wao H ya Meru
Maafisa wa shirika wa mauzo na miliki Amoni Mazanda wakiwa na maafisa maendeleo wa Halmashauri ya wilaya ya Arusha Mwatumu Dossi na wa Halamashauri ya Meru Bwana Mrema
Jiwe la Msingi
Nyumba za gharama nafuu zilizopo Longido kama zinavyoonekana pichani
Wageni wakiwasili eneo la nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa Longido
Mbunge wa Longido Lekule Laizer akiwa na Mkuu wa wilaya ya Longido James Olle Millya wakiangalia jiwe la msingi la mradi wa nyumba za gharama nafuu Longido.
Maelezo kwa kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa wakati wa makabidhiano ya mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana
KUANZA MCHUJO WA WAGOMBEA WAKE LEO
Mkurugenzi wa Organizesheni, Mafunzo na Uratibu wa Kanda wa Chama cha
demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Singo Kigaila Benson akizungumza na waandishi
wa habari Dar es Salaam jana wakati akitamngaza majina ya wagombea
mbalimbali katika chaguzi za chama hicho.
Mkurugenzi wa Organizesheni, Mafunzo na Uratibu wa Kanda wa Chama cha
demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Singo Kigaila Benson akizungumza na waandishi
wa habari Dar es Salaam jana wakati akitamngaza majina ya wagombea
mbalimbali katika chaguzi za chama hicho.Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Habari CHADEMA, Tumaini Makene.
OKWI.BANDA WASAJILIWA TIMU MBILI-TFF
Na Fadha Kidevu Blog
SHIRIKISHO la soka Tanzania TFF,limetoa
majina ya wachezaji waliosajiliwa na timu 14 ambazo zinashiriki Ligi Kuu ya
Tanzania bara huku majina ya wachezaji Emmanuel Okwi na Abdi Banda yakitokea
kwenye timu mbili.
Jina la Okwi linatokea kwenye
usajili wa timu za Simba na Yanga ilhali jina la beki wa kushoto
Banda,limetokea kwenye usajili wa Coastal Union na Simba .
Fadha Kidevu ilijaribu kuwatafuta
viongozi wa TFF,wanaoshuhulika na maswala ya usajili ili kutaka kujua sakata
hilo na vipi litaamuliwa lakini viongozi hao hawakuweza kupatikana.
Suala hilo linatarajiwa kutolewa
uwamuzi baada ya kumalizika kipindi cha mapingamizi ambayo itakuwa ni Septemba
6 kabla ya Kamati ya Maadili na hadhi za wachezaji itakapokutana na kutoa
suluhisho la tatizo hilo.
Subscribe to:
Posts (Atom)