DIANA THEO JACKSON NDIO NICE&LOVELY MISS TANGA 2014

June 22, 2014
  Nice&Lovely Miss Tanga 2014,Diana  Theo Jackson akiwa kwenye kiti na taji la Miss Tanga mara baada ya kuibuka mshindi kwenye shindano ambalo lilifanyika juzi kwenye ukumbi wa Hotel ya Mkonge kushoto ni mshindi namba mbili Noon Juma na mshindi wa tatu Vannessa Charles


PINDA AMPOKEA MAKAMU WA RAIS WA CHINA ARUSHA

PINDA AMPOKEA MAKAMU WA RAIS WA CHINA ARUSHA

June 22, 2014

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda  akiongozana na Makamu wa rais wa  Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao baada ya mgeni huyo kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Arusha  Juni  21, 2014 kwa ziara ya kikazi nchini. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) PG4A3097 
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda  akiongozana na Makamu wa rais wa  Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao baada ya mgeni huyo kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Arusha  Juni  21, 2014 kwa ziara ya kikazi nchini. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya  Rais, Utawala Bora, Capt.George Mkuchika.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) PG4A3170 
Waziri Mkuu, Mizego Pinda  akizungumza na Makamu wa Rais wa China , Li Yuanchao baada ya mgeni huyo kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Arusha  Juni 21, 2014 kwa ziara ya kikazi nchini. (Picha na Ofisi   ya Waziri Mkuu) PG4A3185 
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda  akizungumza na Makamu wa Rais wa  Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao baada ya mgeni huyo kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Arusha  Juni  21, 2014 kwa ziara ya kikazi nchini.  Kulia ni Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Rais, Utawala Bora, Capt. George Mkuchika. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAGENI KUTOKA CHINA NA OMAN LEO

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAGENI KUTOKA CHINA NA OMAN LEO

June 22, 2014

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Dkt Anne Suk-Ching, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Chama Tawala cha Jamhuri ya Watu wa China aliyemtembelea  Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2014 c3 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Dkt Anne Suk-Ching, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Chama Tawala cha Jamhuri ya Watu wa China baada ya kukutana naye  Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2014 o1 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mhe Saoud Ali Mohamed Al Ruqaishi, Balozi wa Oman hapa nchini na Mjumbe Maalum wa Sultan Qaboos Bin Said wa Oman ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2014
o2 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ujumbe kutoka kwa  Mhe Saoud Ali Mohamed Al Ruqaishi, Balozi wa Oman gapa nchini na Mjumbe Maalum wa Sultan Qaboos Bin Said wa Oman ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2014
Kampeni ya Diwani Bonnah Kaluwa wa Kipawa ya kuchangia damu yafikia kilele leo

Kampeni ya Diwani Bonnah Kaluwa wa Kipawa ya kuchangia damu yafikia kilele leo

June 22, 2014

Meya wa Ilala, Jerry Silaa akifungua rasmi tamasha la kuchangia damu katika viwanja vya Stakishari, Majumbasita, Dar es Salaam leo. Kampeni hiyo ya siku 10 iliratibiwa na Diwani wa Kipawa Bonnah Kaluwa (CCM). 02 
Meya Silaa akipata maelezo kutoka kwa maofisa wa Damu Salama kabla ya kuchangia damu ili kuwaokoa wagonjwa wakiwemo wakina mama wajawazito katika viwanja vya Sitakishari Majumbasita, Dar es Salaam. 03 
Meya Silaa na Diwani Bonnah wakiendelea kusikiliza maelezo kutoka kwa maofisa wa damu salama kabla ya kuchangia damu ili kuwaokoa wagonjwa wanaoteseka mahospitali kwa kukosa damu. Meya wa Ilala, Jerry Silaa akiugulia maumivu ya sindano wakati akitoa damu ili kuwaokoa wagonjwa wanaohitaji damu katika hospitali mbalimbali wakiwemo wajawazito bila kuwasahau madereva na abiria wa bodaboda wanaoandamwa na ajali. 05 
Diwani wa Kipawa, Bonnah Kaluwa naye akidhihirisha azma yake ya kuchangia damu kwa vitendo katika kilele cha kampeni yake ya kuchangia damu jana katika viwanja vya Sitakishari, Majumbasita ambapo mamia ya wakazi wa Dar es Salaam walijitokeza. 06 
Mwakilishi wa Chuo cha Diplomasia, Kennedy Ndosi (katikati)  aliyewahamasisha wanafunzi wa Chuo hicho waliofika kuchangia damu akiwasikiliza Meya Silaa na Diwani Bonnah wakati wa tamasha hilo. 07 
Meya Silaa na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Dk Willy Sangu (kulia) wakiondoka baada ya kumaliza zoezi la kuchangia damu katika tamasha lililoandaliwa na Diwani wa Kipawa, Bonnah Kaluwa katika Viwanja vya Sitakishari leo.
KAMANDA KOVA AZINDUA PIKIPIKI YA HERO DAWN 125 CC

KAMANDA KOVA AZINDUA PIKIPIKI YA HERO DAWN 125 CC

June 22, 2014

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova
(katikati), na  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya  Astarc Motors
Tanzania Ltd, Sameer Musale (kushoto), akifungua kitmbaa kuashiria
uzinduzi wa pikipiki mpya aina ya Hero Dawn 125cc katika hafla
yailiyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
01 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova
akijaribu moja ya pikipiki mpya aina ya Hero Dawn 125cc katika hafla
ya uzinduzi wa pikipiki hiyo jijini Dar es Salaam jana. Wa tatu
kushoto ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya  Astarc Motors Tanzania
Ltd, Sameer Musale na wawakilishi kutoka Astarc.
02 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova
(kulia), akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya  Astarc
Motors Tanzania Ltd, Sameer Musale (kushoto) katka hafla hiyo.
03 
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda ya Dar es Salaam
Kamishna Msaidizi wa Polisi, Amiri Konja (kulia) akitoa rai kwa
waendesha bodaboda kutii sheria za barabarani ili klupunguza ajali
ambazo tawimu zinaonyesha kuongezeka. Kulia kwake ni  Kamanda wa
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova (katikati), na
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya  Astarc Motors Tanzania Ltd, Sameer
Musale.
04Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Roma Mkatoliki akitoa burudani

katika hafla ua uzinduzi wa pikipiki aina ya Hero Dawn 125cc jijini
Dar es Salaam jana.

HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA KUTUMIA KIASI CHA SH.BILIONI 6.1 KWA MWEZI KWA AJILI YA KULIPIA STARTIMES.

June 22, 2014
NA OSCAR ASSENGA,TANGA.

HALMASHAURI ya Jiji la Tanga inatarajia kutumia kiasi cha Sh.bilioni 6.1 kila mwezi kwa ajili ya kuilipa kampuni ya Star Times ili kuiwezesha Televisoni ya Tanga TV kurusha matangazo yao kwenye maeneo mbalimbali mkoani Tanga.


Hayo yameelezwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Omari Guledi wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mkoani hapa kuhusu kurudi hewani kituo hicho cha Halmashauri ya Jiji la Tanga katika mfumo wa digitali.