BARAZA LA WAKULIMA LALAMIKIA BAJETI

June 20, 2013

Na Oscar Assenga,Tanga.
Baraza la Wakulima Tanzania limeeleza kusikitishwa kwake nas namna ambavyo Bajetion ya serikali iliyosomwa hivi karibuni ilivyoendnelea kuwapuuza wakulima pamoja na Baraza hilo kupeleka mapendnekezo yao kwa serikali.

Mwenyekiti wa Baraza hilo, Salum Shamte akitoa maoni ya Baraza katika mahojiano  na vyombo vya Habari alisema kuwa Bajeti ya mwaka huu, pamoja kutangaza neema kwa kuanza kwa Benki ya Wakulima ambayo ilikuwa kilio kikubwa cha wakulima, bado haijagusa masuala nyeti kwa wakulima kama vile suala la muda mrefu la kupunguza mzigo wa kodi kwa nia ya kuwawezesha wakulima kuongeza tija, uwekezaji, mapato na hatimaye kuondo umaskini.

“Kodi hizo maranykingine zinaongezwa kineyemela na kimya kimya bila serikali kufanya majadiliano na wadau,” alilalamika Mwenyekiti huyo.

Alisema kuwa kama Tanzania inataka kuleta mapinduzi ya kijani katika kilimo lazima iwe makini katika suala la kuondoa kero ya kodi nyingi kwa wakulima na wazalishaji wengine.

Shamte alitoa mfano wa ushuru wa mazao unatozwa na halamshauri za serikali za mitaa ambao alisema wakuilma wamalazimika kulipa ushuru wa asilimia 5 ambao ni mara 17 zaidi ya wenye viwanda ambao hulipa ushuru wa huduma wa aslimia 0.3. “Hii haieleweki, haielezeki na haikubaliki,” alisema Mwenyekiti huyo.

Alibainisha kuwa Baraza limefanya utafiti kuta kujua kama mapato hayo yanayopkusanya na Halmshauri yanafika katika hazina za halmashauri hizo. “NI asilimia 67 tu ya makusanyo hayo ya ushuru ambayo yanafika halmashauri na fedha nyingine zinayeyuka kastika mifuk ya wajanja,’ alieleza.

Alisema serikali lazima isikie kilio cha wakulima na kuchukua hatua kuhus kodi hiyo kwa mujibui w a maepndekezo ili kuleta tija wa wakulima.

Shamte pia alieleza kuhusu kupanda kwa kiasi kikubwa kwa kodi ya aardhi mwaka jana mwezi Agosti ambapo kodi hiyo imepnda kwa asilimia 500 kutoka Sh. 200 kwa hekta hadi Sh. 1,000 ka hekta kwa walioko maeneo ya vijijini na Sh. 10,000 kwa hekta kwa mashamba ambayo yako maeneo yaliyoko chini ya mamlaka za miji kwa wale ambao wana hati.

Alisema kuwa kodi hiyo hailipiki kwa sababu kama wakulima watalipa kodi hiyo na nyingine zinazowakabili basi watafunga shughuli zao. Alitoa mfano wa Ranchi ya Ruvu ambayo alisema hivi sasa inatakiwa kulipa Sh. milioni 107  kwa mwaka hata kabla hawajaanza kuuza ndama.

Akizungumzia mkonge, Shamte ambaye pia ni Mkrugenzai Mtendaji wa Kampuni ya Mkonge wa Katani Limited ya Tanga, alisema kuwa sekta ya mkonge italazimika kulipa jumla ya Sh.Bilioni 1.18 kwa mwaka kama kodi ya ardhi kutoka Sh. Milioni 87 iliyokuwa ikilipa awali.

Pia alizungumzia ongezeko la kutisha la kodi ya OSHA ambayo imepandishwa kutoka Sh. 5,000 kwa mfanyakaazi hadi Sh. 40,000 kwa mfanyakazi kwa mwaka jambo ambalo kwa mfano katika sekta ya mkonge itaifanya ilazimike kulipa jumla ya Sh. Bilioni 14 kwa mwaka kwa ajili ya kodi hiyo tu.

Alitaja pia kodi ya huduma za zimamoto ambayo imepanda kutoka Sh. 200,000 kwa mwaka hadi kufikia Sh. milioni 2 kwa mwaka . alisema kuwa kdo hiyo kwa mashamba mengi haina maana sana kwa sababu yako mabli sana na huduma hiyo.

Shamte pia alilalamikia ongezeko la mamfuta ya diseli ambayo amesema kuwa ndio roho kwa kwa sababu hahwatumii mafuta hayo kwa usairishaji tu bali katika utayaruishaji wa mashamba, jambao ambalo litaongeza gharama za uendeshaji wa mazao na kuua faida kwa wakulima pamoja na kushindwa katika  ushindani na bidhaa kama hizo katika soko la kimataifa.

Alisema kuwa katika nchi nyingine kilimo kinapewa upendeleo fulani kwa kuondoa kodi kanma hizo ili kuongoeza tija.

Mwenyekiti huyo, wakati huo aliitaka serikali kuhakikisha kuwa inapopunguza kodi jambo hilo linatekelzw ipasavyo. Alitoa mfano kuwa nmawka jana serikali ilipunguza kodi kwa vipuri lakini hadi  hivi kodi hiyo inaendele kutozwa.

MWISHO

MKURUGENZI wa Jiji aifunda timu ya Umitashumta Tanga

June 20, 2013
 Na Oscar Assenga,Tanga.
MKURUGENZI wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, Juliana Malange ameitaka timu ya Mkoa wa Tanga ya Umitashumta kuhakikisha inauwakilisha vema mkoa katika mashindano ya kanda na kuweza kurudi na kombe la michuano hiyo.

Malange alitoa wito huo mwishoni mwa wiki wakati wa ufungaji wa mashindano hayo ngazi ya mkoa ambayo yalifanyika katika viwanja vya shule ya ufundi ya Tanga School na kuhudhuriwa na wanamichezo 900 ambao walishiriki michezo mbalimbali.

Mkurugenzi huyo alisema michezo inafaida nyingi sana katika maisha ya kila siku ikiwemo kuwaepusha vijana kujiepusha na vitendo vyote vinavyoweza kuwaingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya na ulevi wa aina yoyote na ngono zembe kwa kuwa mambo hayo huaribu kabisa ndoto ambazo wamejiwekea maishani na kudhoofisha nguvu kazi ya taifa.

Aidha alisema anaimani kubwa na wanamichezo 122 ambao wamechaguliwa kuuwakilisha mkoa kwenye mashindano ya Umitashumta ngazi ya Kanda watafanya vizuri na kuwataka kupambana vilivyo ili kuuwakilisha vema mkoa wa Tanga ambapo kati yao wavulana 71 na wasichana 51.

“Ninaimani kuwa timu iliyochaguliwa kuuwakilisha mkoa kwenye mashindano ngazi ya kanda itakuwa ni nzuri, napenda kuwatakia kila heri lakini mfahamu kuwa mmepewa dhamana kubwa ya kuuwakilisha mkoa hivyo hakikisheni mnawapa raha wakazi wa mkoa huu “Alisema Malange.

Pia aliwataka walimu wanaosimamia wachezaji hao katika michezo mbalimbali wahakikishe wanaongeza juhudi kwenye kila mchezo ili kuweza kuchukua ushindi wa jumla kwenye mashindano hayo.

Mkurugenzi huyo alimshukuru na kumpongeza rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Jakaya Mrisho Kikwete kwa hatua yake ya kurudisha michezo mashuleni na hivyo kuwafanya wanafunzi wa shule mbalimbali hapa nchini kushiriki michezo kupitia mashindano hayo.Hata hivyo aliwataka walimu hao kuwa karibu na wachezaji wao ili waweze kufahamu changamoto zinazowakabili na kuweza kuzifanyia kazi kwa wakati ikiwemo kuwapa hamasa kufanya vizuri.

Lakipi pia aliwataka wachezaji hao kuzingatia kauli mbiu ya mashindano ya umitashumta 2013 isemayo “Michezo na utulivu kwa maendeleo ya Taifa”huku akiwasisitiza walimu na viongozi kuhakikisha wanakuwa karibu na wachezaji wakati wote ili kujua matatizo yao na kuyatafutia ufumbuzi mapema.


Mashindano hayo msimu huu yalishirikisha michezo ya mpira wa miguu,mpira wa mikono kwa wasichana na wavulana,mpira wa pete wa wasichana,mpira wa wavu wavulana na wasichana na michezo yote ya riadha.

Mwisho.

“African Sports kuchagua viongozi wake Agosti 15 mwaka huu”.

June 20, 2013

Na Oscar Assenga, Tanga.
MABINGWA wa Ligi kuu Tanzania Bara mwaka 1988 African Sports “Wanakimanumanu” inatarajiwa kufanya mkutano mkuu wa uchaguzi Agosti 15 mwaka huu baada ya uongozi wa muda uliopo madarakani kumaliza wakati wake.

Akizungumza na blog hii, Katibu Mkuu wa Klabu hiyo, Khatibu Enzi alisema uchaguzi huo unafanyika kutokana na kuongozwa na viongozi wa muda hivyo wakapendekeza kuitishwa mkutano huo ambao utatoa mwelekeo wa kuwapata watendaji wapya ambao watakuwa na jukumu la kuingoza klabu hiyo.

Enzi alisema fomu za kuwania nafasi katika uchaguzi huo zitaanza kutolewa kuanzia Julai 2 mwaka huu kwenye makao makuu ya klabu hiyo zilizopo barabara 12 jijini Tanga baada ya kikao cha kamati ya utendaji wanachama wao.

Katibu huyo alizitaja nafasi ambazo zitagombewa katika uchaguzi huo kuwa ni nafasi ya mwenyekiti, makamu mwenyekiti, katibu mkuu, katibu msaidizi, mweka hazina na msaidizi wake huku nafasi kumi za wajumbe watakaounda kamati ya utendaji wa klabu hiyo nazo zikiwaniwa.

Aidha katibu huyo alisema kuelekea uchaguzi huo wanatarajiwa kutoa fomu mpya za uanachama kwa wanachama wapya ambao wanataka kujiunga na klabu hiyo ambazo zitatoka kuanzia June 22 mpaka Julai 30 mwaka huu.

Mwisho.

RAIS Kikwete kuwasili mkoani Tanga kesho.

June 20, 2013

Na Oscar Assenga,Tanga.

RAIS wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Jakaya Mrisho anatarajiwa kuwasili mkoani Tanga kesho kwa lengo la kuzindua mradi wa kanda maalumu ya uwekezaji katika eneo la viwanda Pongwe  wenye ukubwa wa eneo la mradi ni hekta 67.7 kwa viwanda na hekta 4.3 kwa eneo la makazi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana,Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu,Chiku Gallawa alisema mradi huo wa kanda maalumu ya uwekezaji ni mradi ulioanzishwa na Tanga Economic Corridor Limited(Industrial Park Developer)ambayo ni kampuni inayoundwa kwa ubia kati ya halmashauri ya jiji la Tanga yenye hisa 48 asilimia na (Good PM group LTD through Africa Future)yenye hisa 51 asilimia) ambayo ni taasisi isiyo ya kiserikali inayowezesha uendelezaji wa miundo mbinu africa.

Alisema makubaliano yaliyopo ni halmashauri ya Jiji la Tanga kuchangia eneo na Good PM Group Limited kuwekeza katika miundo mbinu ambapo mradi mzima unatarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi za kimarekeni milioni 277 kati ya hizo shilingi za kimarekani milioni 40 zitatumika kwa kuendeleza miundo mbinu na shilingi  za kimarekani milioni 237 zitatumika kwa uwekezaji wa moja kwa moja kutoka kwa viwanda vyote.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema baada ya mradi huo kukamilika unatarajiwa kutoa fuksa za ajira kwa vijana zaidi ya 2,000 katika viwanda 17 vinavyotarajiwa kujengwa mkoani hapa ili kuweza kuleta maendeleo kwa wakazi wa mkoa na wilaya zake.

Aidha mkuu wa mkoa wa Tanga aliwataka wananchi wote kujitokeza kwa wingi kumlaki mheshimiwa Rais katika uwanja wa ndege tanga kuanzia saa 4.00 asubuhi na kushiriki katika uzinduzi wa mradi huo utakaofanyika kata Pongwe katika halmashauri ya Jiji la Tanga.

Mwisho.

UHURU seleman arudi Nyumbani”

June 20, 2013

Na Oscar Assenga, Tanga.

UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga “Wagosi wa Kaya” umeingia mkataba wa mwaka mmoja na kiungo mshambuliaji Azam Fc  ,Uhuru Selemani kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo msimu ujao.

Athibitisha habari hizi,Mwenyekiti wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga, Hemed Aurora “Mpiganaji”ni kweli wamefanya hivyo na kueleza ujio wa mchezaji huyo utaleta chachu na ushindani katika kikosi hicho ambacho kinatarajiwa kuwa tishio katika medani ya soka hapa nchini.

Aurora alisema makubaliano ya mkataba huo yaliafikiwa jana na kukubaliana na mchezaji huyo ili aweze kuitumikia timu hiyo katika msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara ambapo alieleza wao kama uongozi wa klabu hiyo wamefarijika sana na ujio wake.

Alisema Uhuru ni miongoni mwa wachezaji wapya waliosajiliwa na klabu hiyo msimu huu wengine ambayo tayari wameshasaini kuichezea klabu hiyo ni Haruna Moshi “Boban” na Juma Nyoso ambayo ni wachezaji wenye uzoefu mkubwa ambao wataweza kuwa kuleta upinzani mkubwa.

Aidha Aurora alisema klabu hiyo itaendelea kuwa na msimamo wake wa kuwasajili wachezaji ambao hawana majina ili waweze kushirikiana na wachezaji wachache ambao wamewasajili wenye majina makubwa na uzoefu wa kisoka hapa nchini.

Aliongeza kuwa hivi sasa nguvu zao wanazielekeza kwa wachezaji wachanga ambao hawana majina makubwa kwenye medani ya soka kwani wanaamini wachezaji wachanga wanauwezo mkubwa wa kuifanya timu hiyo ipate mafanikio.

Akizungumzia tetesi zilizozagaa kuwa wana mpango wa kumchukua mlinda mlango Juma Kaseja ,Aurora alisema mpango huo kwa sasa hawana kutokana na kuwa na makipa wazuri watatu ambao wataitumia klabu hiyo msimu ujao.

Aliwataja makipa hao kuwa ni Mlinda mlango nambari moja Shabani Kado, Said Rubawa ambaye alikuwa mlinda mlango wa JKT Oljoro ya Arusha na Ally Mansour ambaye aliidakia timu hiyo katika mechi za uhai Cup akiwa na kikosi cha pili cha timu hiyo chini ya umri wa miaka 20.

Mwisho

“Zawadi za mshindi wa shindano la Redd’s Miss Tanga 2013 zawekwa hadharani

June 20, 2013

Na Oscar Assenga, Tanga.  

ZAWADI kwa mshindi wa Redd’s Miss Tanga 2013 anatarajiwa kuondoka na kitita cha sh.laki tano 500,000 huku msanii wa muziki wa kizazi kipya, Tunda Man, akiongoza kwa upande wa Burudani, katika shindano litakalofanyika Jumamosi katika uwanja wa Mkwakwani.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa Mkurugenzi wa Kampuni ya DATK Intertainment Asha Kigundula,alisema kuwa maandalizi ya shindano hayo yapo vizuri ambapo zawadi kwa mshindi wa pili atajinyakulia kitita cha shilingi  300,000.

Kigundula alisema katika shindano hilo mshindi wa tatu atazawadiwa kitita cha shilingi  250, 000 wakati mshindi wa nne na tano wakipata sh.200, 000 kila mmoja na warembo wengine watakaosalia watapata kitita cha sh.laki moja moja kila mmoja 100,000 kama kifuta jasho pamoja na zawadi kwa mrembo mwenye nidhamu ili kuweza kuboresha shindano hilo.

Alisema kuwa hata hivyo kutakuwa na zawadi kwa washindi watatu watakaoibuka katika shindano la vipaji (talent), ambapo mshindi wa kwanza atainyakuliwa kitita cha shilingi 100,000 na mshindi wa pili na watatu kila mmoja atajinyakulia shilingi 50,000.

Kwa upande wa Burudani msanii wa kizazi kipya, Tunda Man, ataongoza safu ya burudani, ambapo itakuwa na wasanii mbalimbali wakiwemo Dr John, Nabisha kutoka kundi la THT, Fady Dady na wasanii chipukizi kutoka mkoani hapa.

Kigundula alisema shindano hilo linatarajiwa kuanza majira ya saa mbili usiku na kushirikisha warembo 12 ambao watachuana ili kuweza kumpata malkia wa mkoa huu ambaye atauwakilisha mkoa katika mashindano hayo ngazi ya kanda.

Warembo hao ni Hawa Ramadhani (18),Hazina Mbaga (19)Like Abdulraman (19), Irene Thomas(20), Tatu Athumani (19), Winfrida Gutram (21)Lulu Mbonela (19) ,Hazina Daniel (19),Lulu Matawalo(22),Judithi Moleli (21),Neema Jonas na Hawa Twaybu(21)

Wakati huo huo Warembo hao wanaowania Taji la Mlimbwende wameiomba Halmashuri ya Jiji la Tanga kuifanyia marekebisho barabara inayokwenda katika mapango ya Amboni ili iweza kuwa nzuri na ipitike kirahisi nyakati zote.

Ombi hilo lilitolewa na warembo hao mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea mapango hayo ambapo walikwenda kujifunza histori yake pamoja na kuingia mapangoni lengo likiwa ni kujifunza utalii wa ndani ili kuweza kuuutangaza kwa wageni na jamii nzima.

Akizungumza mmoja wa warembo hao, Asia Rashid alisema mapango hayo ni mzuri na endapo yatafanyiwa maboresho ikiwemo kufanyiwa ukarabati barabara inayoelekea katika kivutio hicho itarahisisha usafiri na kupitika bila shida nyakati zote.

Asia alisema wao kama washiriki wa shindano la Redd’s Miss Tanga 2013 wamefarijika sana kupata nafasi ya kutembelea mapango hayo na kuwataka wananchi wa mkoa wa Tanga na wageni wanaoingia mkoani hapa kuwa na utaratibu wa kutembelea vivutio hivyo na kujifunza mambo mwengi ya kale.

Kwa upande wake, Hawa Ramadhani aliwashauri watanzani kujenga utamaduni kutembelea vivutio vya utalii hapa nchini ikiwemo kutunza misitu yetu ili nchi yetu ipendeze na kuwavutia wageni wanaoingia hapa nchini kutoka mataifa mbalimbali.

Hawa alisema wao wamejipanga vema kuhakikisha wanafanya vizuri katika fainali ya shindano hilo ambalo litafanyika June 22 mwaka huu kwenye uwanja wa mkwakwani mkoani Tanga na kushirikisha warembo.
 
Mwisho.
CCM Tanga wajiimarisha zaidi kuweza kurudisha kata tisa”

CCM Tanga wajiimarisha zaidi kuweza kurudisha kata tisa”

June 20, 2013
Na Oscar Assenga,Tanga.
KATIBU wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga (CCM),Gustav Mubba amesema chama hicho kimejiwekea mikakati kabambe ya kuhakikisha wanarudisha kata tisa zilizochukuliwa na vyama vya upinzani katika uchaguzi mkuu ujao 2015.

Pamoja na kata hizo lakini pia watahakikisha vijiji vyote vilivyochukuliwa na vyama vya upinzani vinarudi kwenye chama hicho kwani hilo linawezekana kutokana na uimara wa chama hicho.

Mubba alitoa kauli juzi wakati wa sherehe za kuwapongeza madiwani wapya wa CCM waliochaguliwa katika uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata za Genge na Tingeni wilayani Muheza na kueleza ushindi huo unaonyesha ni jinsi gani wananchi walivyokuwa na imani na mapenzi mema na chama hicho.

Alisema urudishwaji wa kata hizo katika chama hicho unawezakana kutokana na sera makini zinazotekelezeka pamoja na kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika uchaguzi uliopitia ambapo anaamini hilo litaweza kuwapa mafanikio ya kutimiza matarajio yao.

Aidha alielezea kufurahishwa na ushindi walioupata katika uchaguzi huo mdogo kutokana na upinzani uliokuwa ukionyeshwa na vyama vya upinzani ambavyo vilikuwa zikiwania nafasi hiyo.

Katibu huyo aliwataka makatibu wa wilaya katika chama hicho kuhakikisha wanawasimamia kikamilifu madiwani kufanya ziara za kukagua miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao ikiwemo kufanya mikutano ya hadhara. 

Aliwataka madiwani wa chama hicho kuhakikisha wanasimamia vyema ilani za chama hicho lakini pia aliwapongeza viongozi hao kwa kupata ushindi katika uchaguzi huo.

Katika uchaguzi huo, Asha Mohamed alichaguliwa kuchukua nafasi ya udiwani kupitia chama hicho kwenye kata ya Tingeni na Mlaguzi Steven akichaguliwa kuchukua nafasi hiyo kupitia kata ya Genge iliyopo wilayani Muheza.

Akizungumza katika sherehe hizo, Diwani wa Kata ya Tingeni Asha Mohamed alisema atahakikisha anashirikiana bega kwa bega na wananchi wa kata hiyo ili kuweza kuwapatia maendeleo pamoja na kuhamasisha vikundi vya ufugaji wa kuku ili wananchi wake waweze kujiajiri wenyewe.

Kwa upande wake, Mlaguzi Steven ambaye ni diwani wa kata ya Genge alisema atahakikisha anajipanga vilivyo na viongozi wengine kwenye kata hiyo ili kuwapa maendeleo wananchi wake.

Lakini pia Katibu Mubba alimtaka diwani wa kata ya Genge Mlaguzi Steven kuwa posho za baraza la madiwani zisimfanye amtekeleze mkewe wake.
  
   “Madiwani wakiwa wanagombea wanabembeleza sana, wakishinda hawatelezi ahadi zao,  watu wakishapata madaraka wanadharau wananchi wao sio tabia nzuri hivyo nawaasa mhakikishe mnawanyenyekea wananchi wenu na kuwa nao karibu “Alisema Mubba.

Mwisho.

Redd's Miss Tanga 2013 watembelea TBL Tanga.

June 20, 2013
MWENYE Fulana ya Njano ni Bahati Mbise Mwalikishi wa Mauzo TBL mkoa wa Tanga,akitoa maelezo lwa warembo wanaoshiriki Redd's Miss Tanga 2013,shindano ambalo lifanyika Jumamosi hii kwenye uwanja wa mkwakwani,Picha kwa hisani ya Bin Zuberi.