MHE MWANJELWA AWATAKA WATUMISHI WA TAASISI YA UTAFITI (TPRI) MJINI ARUSHA KUWA WAZALENDO NA KUFANYA KAZI KWA WELEDI

December 16, 2017
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akipokelewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (TPRI) Dkt Margaret Mollel wakati alipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Tropiki (Tropical Pesticides Research Institute-TPRI) katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha, Leo 16 Disemba 2017. Picha Zote Na Mathias Canal
 Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa (Katikati) akisikiliza  maelezo ya namna ya ufanyaji kazi mara baada ya kutembelea Kitengo cha Unyunyuziaji wa Viuatilifu alipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Tropiki (Tropical Pesticides Research Institute-TPRI) katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha, Leo 16 Disemba 2017. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (TPRI) Dkt Margaret Mollel.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa (Kushoto) akitembelea baadhi ya maeneo ya Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Tropiki (Tropical Pesticides Research Institute-TPRI) katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha, Leo 16 Disemba 2017.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa  akitumia mashine ya Kunyunyizia viuatilifu wakati alipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Tropiki (Tropical Pesticides Research Institute-TPRI) katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha, Leo 16 Disemba 2017.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisikiliza kwa makini maelezo ya namna maabara ya kupima masalia ya Viuatilifu inavyofanya kazi wakati alipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Tropiki (Tropical Pesticides Research Institute-TPRI) katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha, Leo 16 Disemba 2017.

Na Mathias Canal, Arusha

Watumishi wa serikali wanaofanya kazi katika Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Tropiki (Tropical Pesticides Research Institute-TPRI) wametakiwa kuwa wazalendo na kufanya kazi kwa Weledi, Bidii na Nidhamu.

Kauli hiyo imetolewa Leo 16 Disemba 2017 na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa alipokuwa akizungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Taasisi hiyo wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha.

Mhe Mwanjelwa aliwataka watumishi hao kufanya kazi kwa bidii, Juhudi, Maarifa na Ubunifu kwani kufanya hivyo kutathibitisha matokeo chanya katika utendaji wao huku akiwapongeza kwa kufanya kazi kwa moyo na uvumilivu mkubwa pamoja na kuwepo kwa kadhia ya upungufu wa watumishi.

Sambamba na Taasisi hiyo kuwa na jukumu la kufanya utafiti, kutoa huduma za usajili na udhibiti wa viuatilifu, Mafunzo kuhusu visumbufu na kufanya hifadhi ya Bioanwai husika ili kuchangia uhakika wa chakula lakini pia ina jukumu la kuendelea na kudumisha mashamba darasa kwa ajili ya Utafiti na mafunzo kwa wadau hususani katika matumizi sahihi na salama ya Viuatilifu.

Aidha, Alimpongeza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (TPRI) Dkt Margaret Mollel kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya ya kusimamia Taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na umakini wa Taasisi katika kufanya kazi zake katika kipindi cha miaka 10 ya utekelezaji wa muundo mkakati wa TPRI (2005-2015).

Alimsihi Mkurugenzi huyo anayesimamia Taasisi hiyo ya (TPRI) iliyotungiwa sheria na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (The TPRI Act No 18 of 1979) ikisimamiwa na Wizara ya Kilimo, kuongeza ufanisi zaidi katika usimamizi wa kazi kwa mujibu wa sheria na Taratibu za nchi.

WAZIRI MWIJAGE AZINDUA BODI MPYA YA KAMPUNI YA MBOLEA YA TAIFA (TFC), AITAKA KUTOINGIA MIKATABA YA HASARA

December 16, 2017
 Waziri wa Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage, akizungumza na wajumbe wa bodi mpya ya Kampuni ya Mbolea ya Taifa (TFC), (hawapo pichani), wakati akiizindua bodi hiyo jijini Dar es Salaam jana.
 Wajumbe wa bodi hiyo wakiwa katika hafla ya uzinduzi.
 Mwenyekiti wa bodi hiyo, Profesa, Egid Mbofu, akizungumza katika uzinduzi huo. Kulia ni Meneja Mkuu wa TFC, Salum Mkumba.
 Wajumbe wa bodi hiyo wakiwa bize kuchukua maagizo ya Waziri Mwijage.
 Waziri Mwijage akisisitiza jambo katika uzinduzi huo.



 Hapa ni kalamu zikizungumza katika uzinduzi huo wakati Waziri Mwijage alipokuwa akiipa majukumu bodi hiyo mpya ya TFC.
 Uzinduzi ukiendelea.
Waziri Mwijage akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi hiyo.

Na Dotto Mwaibale

WAZIRI wa Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage, ameitaka Kampuni ya Mbolea ya Taifa (TFC) kubadilisha mfumo wa utendaji ikiwa ni pamoja na kutoingia mikataba inayoweza kuisababishia serikali hasara, badala yake kuangalia wabia wanaoweza kuisaidia kujipanua na kupata faida kubwa zaidi.

Waziri Mwijage, aliyasema hayo juzi wakati akiizindua bodi mpya ya Wakurugenzi ya TFC, na kuongeza kwamba serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk John Pombe Magufuli, haiko tayari kuona taasisi zake za umma zikiingizwa katika mikataba mibovu na isiyokuwa na tija.

Pia aliagiza kwamba, baada ya kuizindua bodi hiyo, Mwenyekiti wa Bodi hiyo,  Profesa Egid Mbofu na wajumbe wake, waanze kazi mara moja na moja ya majukumu yao ya awali ni kuangalia ama kuipitia upya miokataba ambayo awalo iliingiwa na TFC.

Alisema TFC ikifanya kazi kwa uadilifu mkubwa na kujielekeza kwenye kazi zenye faida kubwa, itaweza kusaidia kasi ya kuendeleza sekta ya kilimo nchini, na kufikia malengo ya serikali ya awamu ya tano ya Taifa la uchumi wa kati na wa Viwanda.

"Tunatambua sekta ya kilimo ni nguzo muhimu kwa ajili ya uchumi wa TANZANIA, lakini haiwezi kuleta mafanikio makubwa kwa jamii, ikiwa TFC haitaweza kupewa uwezo na kuwafikia wakulima wengi zaidi", alisema Waziri Mwijage.

Aliongeza kusema kwamba, mazingira ya sasa ya kilimo kwa Tanzania, yanahitaji umakini katika uagizaji wa mbolea zinazotumiwa na wakulima wengi ambao malengo yao ni kupata faida, lakini wamekuwa wakiangushwa na baadhi ya wafanyaviashara wanaoagiza mbolea feki.

TFC ni mtoto wa serikal, hivyo nimeagizwa na mheshimiwa Rais, kuwaonoa hofu na kwamba tunahitaji kuiongezea uwezo ili Taifa liweze kufikia malengo ya uzalishaji mkubwa wa chakula pamoja na mazao mengine yanayohitajika kama malghafi katika viwanda.

Kwa upande wake Profesa Mbofu, alimshukuru Waziri Mwijage na kumuahidi kwamba, wako tayari kwa kazi hiyo lakini pia akasema wamfikishie Rais shukrani zao kwa uaminifu wake kwao.

"Ninaomba kwa niaba ya wajumbe wa bodi hii, menejimenti ya TFC kukushukuru kwa kazi hii nzuri na maagizo yako yote kwetu, tunakuahidi kuifanya kazi hii kwa uaminifu na uadilofu mkubwa na tutaendelea kuomba ushauri wako kila tunapohitaji kufanya hivyo kama njia ya kupata miongozo zaidi," alisema Profesa Mbofu.

Meneja Mkuu (GM),  Salum Mkumba, alimhakikishia Waziri Mwijage, kwamba TFC iko tayari kwa mabadiliko ya aina yeyote na wafanyakazi wako tayari kwa kusimamia maagizo kwa ajili ya kuendana na Tanzania ya Viwanda kulingana na sera na miongozo ya serikali ya awamu ya tano.


Pia GM Mkumba, alisema TFC ni miongoni mwa taasisi za umma zilizo chini ya wizara ya Viwabda na Uwekezaji, ambazo tayari zilianzisha mabaraza ya wafanyakazi kwa ajili ya kuwashirikisha wafanyakazi na kuwajengea uwezo wa kushauri kasi ya maendeleo kwenye kampuni hiyo ya umma.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)

NGORONGORO WAZINDUA KAMPENI YA KUPINGA UKEKETAJI

NGORONGORO WAZINDUA KAMPENI YA KUPINGA UKEKETAJI

December 16, 2017
Wanaharakati wa kupinga ukeketaji wakisikiliza kwa makini mafunzo kabla ya kuanza kampeni ya mwezi mmoja ya kupinga ukeketaji wilayani Ngorongoro. Mafunzo hayo yaliratibiwa na Shrika la UNESCO. Kampeni hiyo inafanywa kwa ushirikiano wa UNESCO, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro na Baraza la Wazee wa Mila wa Kimaasai (Laigwanan). Kampeni hiyo imeanza Tarehe 5/12/2017 na itaendelea kwa mwezi mzima. Afisa wa UNESCO anayewakilisha miradi ya Ololoswakan Wilayani Ngorongoro Bwana Hamidun Kweka akiwafundisha wanafunzi wa Shule ya Msingi Oloirien wilayani Ngorongoro madhara ya ukeketaji katika uzinduzi wa kampeni ya kupinga ukeketaji wilayani humo. Kampeni hizo zilizinduliwa rasmi Tarehe 5 na zitadumu kwa mwezi mmoja. Ngariba mstaafu akiimba na watoto nyimbo za kupinga ukeketaji baada ya mafunzo ya kuwaelimisha madhara ya ukeketaji katika shule ya msingi Oloirine wilayani Ngorongoro mnamo Tarehe 7, 2017. Wafanyakazi wa UNESCO na Walimu wa Shule ya Msingi Oloirien wakiwa pamoja baada ya uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Ukeketaji wilayani Ngorongoro.

NATIONAL STAKEHOLDERS DIALOGUE ON EARLY AND UNINTENDED PREGNANCY AND ESA COMMITMENT JOINT PLANNING MEETING

December 16, 2017

BAGAMOYO 18 – 23 DECEMBER 2017
UNESCO, in close collaboration with Tanzania Commission for AIDS (TACAIDS) will hold a national stakeholders dialogue as part of a broader situational analysis aimed at determining the status of early and unintended pregnancy (EUP), and how it impacts girl’s education in ten ESA countries. Findings of the situation analysis will inform the development and implementation of a region wide campaign aimed at reducing EUP. The campaign seeks to reduce EUP through increasing awareness on the consequences of EUP, improving delivery of comprehensive sexuality education, promoting consistent condom use and increasing access and use of effective contraception for sexuality active young people in the East and Southern African Region.
The objectives of the National Stakeholder dialogues are:
-To understand the national policy and programmatic response to EUP in the country.
-To understand the education sector response to EUP (including provision of quality CSE and implementation of re-entry policies.
-To understand linkages (referral system) between schools and health services in enhancing adolescent access to health and education services.
-To understand the forms and impact of stigma and discrimination on pregnant and childbearing girls in schools and communities.
Early and unintended pregnancy (EUP) jeopardises educational attainment for girls. Preventing EUP is therefore an important component of a wider response to provision of rights based, quality education, and emphasises the connections between girls’ access to school, comprehensive sexuality education, child marriage, access to health services and school related gender based violence. Preventing and managing EUPs require an effective response from education and health sectors, in collaboration with other sectors.

MHE MWANJELWA AAGIZA BODI YA KAHAWA KUTOCHELEWESHA MALIPO KWA WAKULIMA

December 16, 2017
 Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikaanga kahawa mara baada ya kutembelea Kitengo cha kukaanga Kahawa katika Ofisi za Bodi ya Kahawa akiwa ziarani Mkoani kilimanjaro, Jana 16 Disemba 2017. Picha Zote na Mathias Canal
 Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua namna kahawa zinazohifadhiwa mara baada ya kutembelea Maabara ya kuandaa kahawa kwa ajili ya wanunuzi katika Ofisi za Bodi ya Kahawa akiwa ziarani Mkoani kilimanjaro, Jana 16 Disemba 2017
  Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisikiliza maelezo kuhusu uendeshaji wa mnada wa kahawa kwa mfumo wa kisasa Kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa Ndg Primus Kimaryo alipotembelea Ofisi za Bodi ya Kahawa akiwa ziarani Mkoani kilimanjaro, Jana 16 Disemba 2017
 Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akiwasili katika chuo cha mafunzo ya Kilimo Kilimajaro (KATC) wakati wa ziara ya kikazi Mkoani humo, Jana 16 Disemba 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua miongoni mwa mashamba ya kufundishia kilimo cha mpunga mara baada ya kikao na watumishi wa chuo cha mafunzo ya Kilimo Kilimajaro (KATC) wakati wa ziara ya kikazi Mkoani humo, Jana 16 Disemba 2017

Na Mathias Canal, Kilimanjaro

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya serikali iliyopewa jukumu la Kusimamia sekta ya Kahawa nchini Ndg Primus Kimaryo ameagizwa kusimamia na kuwalipa haraka wakulima malipo mara baada ya kukusanya mazao yao kwani kufanya hivyo kutawezesha mazingira mazuri ya biashara na kuwanufaisha wakulima kutokana na kilimo hicho.

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa ametoa agizo hilo jana Disemba 16, 2017 alipotembelea Ofisi za Bodi ya Kahawa akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Kilimanjaro.

Mhe Mwanjelwa alisema kuwa pamoja na wakulima kuuza kahawa kwa bei ya shilingi 5000 kwa kilo katika msimu wa mwaka 2016/2017 lakini bado changamoto ni kubwa ya ucheleweshaji wa malipo kwa wananchi jambo ambalo linarudisha nyuma ufanisi wa zao.

Alisema miongoni mwa kazi kubwa ya Bodi ya Kahawa nchini ni pamoja na kulinda maslahi ya wakulima dhidi ya makundi mbalimbali yanayofanya biashara ya zao la kahawa hivyo kucheleweshwa kulipwa malipo yao ni ishara ya Bodi hiyo kutotekeleza majukumu yake ipasavyo.

Aidha, Kaimu Mkurugenzi huyo wa Bodi ya Kahawa ametakiwa kuwa na mikakati imara na yenye tija itakayolifanya zao la kahawa kuwa na ubora zaidi Duniani kwa kwa kuliongezea thamani.

Katika ziara hiyo pia Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa alitembelea chuo cha mafunzo ya Kilimo Cha Kilimajanro (KATC-Kilimanjaro Agricultural Training College) ambapo ameupongeza uongozi wa Chuo hicho kwa kuwawezesha zaidi ya wakulima 7000 katika skimu zaidi ya 100 kuboresha kilimo cha mpunga na mazao mengine hivyo kupata ongezeko kubwa la mazao.

Sambamba na pongezi hizo pia amewataka kuongeza ufanisi katika utendaji ili kuunga mkono kwa vitendo serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kufanya kazi kwa bidii, ufanisi, na ubunifu.

Aliwasisitiza wananchi hao kutofanya kazi kwa mazoea badala yake kuwa wabunifu katika kazi ikiwa ni pamoja na kuzikabili changamoto na kuzigeuza kuwa fursa.