Story ya michezo ya kubahatisha ya Biko

April 10, 2017
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MCHEZO wa bahati nasibu unaoendeshwa na Biko, unaotambulika kama Ijue nguvu ya Buku unatarajiwa kuchezesha droo yake ya kwanza ya kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 10, Jumapili hii.
Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, James Mbalwe (wapili kushoto), akimkabidhi Leseni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya BIKO Charles Mgeta kwa ajili ya kufanya shughuli za mchezo wa kubahatisha nchini. Hafla hiyo ilifanyika Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja wa Udhibiti wa Bodi hiyo Sadick Elimusu na Kulia ni Meneja Masoko wa BIKO Goodhop Heaven. Picha zote na Mpigapicha Wetu.
Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, James Mbalwe akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya BIKO Charles Mgeta mara baada ya kupeana leseni ya kufanya shughuli za mchezo wa kubahatisha nchini unaoitwa kama Nguvu ya Buku. Hafla hiyo ilifanyika Dar es Salaam jana. Picha zote na Mpiga Picha Wetu.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Biko, Charles Mgeta, alipofanya mazungumzo na waandishi wa Habari, jijini Dar es Salaam leo na kuhudhuriwa na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya viongozi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania.

Akizungumza katika mazungumzo hayo, Mkurugenzi Mkuu Mgeta, alisema droo yao itakuwa ya kwanza tangu walipoanzisha mchezo huo wenye zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5000, 10000, 20000, 50,000, 200,000 na sh Milioni moja, huku zawadi ya Sh Milioni 10 ikipatikana kila mwisho wa wiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Biko, Charles Mgeta wa pili kutoka kulia akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea leseni ya uendeshaji wa michezo ya kubahatisha kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, James Mbalwe wa pili kushoto. Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Udhibiti wa Bodi hiyo Sadick Elimusu na Kulia ni Meneja Masoko wa BIKO Goodhop Heaven.
Charles Mgeta akizungumza leo jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari juu ya kampuni yao ya Biko kuendesha michezo ya kubahatisha, ambapo Jumapili hii watachezesha droo ya kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 10.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, James Mbalwe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo baada ya kuipa leseni kampuni ya Biko inayondesha mchezo wa kubahatisha unaojulikana kama Nguvu ya Buku.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Biko, Goodhope Heaven, kulia akizungumza na waandishi juu ya mchezo wao wa kubahatisha unaojulikana kama Nguvu ya Buku, ambapo mwishoni mwa wiki hii watachezesha droo ya kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 10.

“Leo pamoja na kutangaza juu ya kumpata mshindi wa Sh Milioni 10 Jumapili, bali pia tumekabidhiwa rasmi cheti cha utendaji wa kazi zetu kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, ambapo tunaamini safari yetu itakuwa ya mafanikio zaidi kwa Watanzania.

“Taratibu zetu ni rahisi kwa sababu washiriki wetu wanatakiwa kufanya miamala ya simu za MPESA, TIGO PESA na Airtel Money kwa kuingiza namba ya kampuni yetu ambayo ni 505050, huku pia akipaswa kuingiza namba ya kumbukumbuku ambayo ni 2456 ambapo kila ujumbe mmoja wa simu atatozwa kwa sh 1000, huku kiasi hicho cha pesa kikiwa na nafasi mbili ikiwa ni zawadi za papo kwa hapo pamoja na nafasi ya kumuingiza kwenye droo ya wiki ya kujishindia Sh Milioni 10,” Alisema.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, James Mbalwe, aliwapongeza BIKO kwa kuingia katika mchezo huo kama sehemu ya kuwapatia maisha bora Watanzania kwa kupitia sekta ya michezo ya kubahatisha.

“Naomba kuwatangazia Watanzania kwamba BIKO wamesajiliwa rasmi katika kuchezesha michezo hii na tunawaambia kwamba wapo salama hivyo kila Mtanzania apaswa kucheza ili aweze kujiwekea mazingira mazuri ya ushindi wa zawadi mbalimbali,” Alisema Mbalwe.

Biko wameanza kuchezesha mchezo huo wa bahati nasibu huku wakiwa wamejiwekea malengo makubwa ya kuhakikisha kwamba kila Mtanzania anajiwekea fursa ya kuibuka na ushindi wa zawadi mbalimbali kwa kupitia sekta ya michezo ya kubahatisha kutoka kwenye kampuni yao.
Benki ya NMB yadhamini mkutano wa mwaka wa TEF

Benki ya NMB yadhamini mkutano wa mwaka wa TEF

April 10, 2017
Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa na Serikali wa NMB –Richard Makungwa (kulia) akimpongeza mwenyekiti wa jukwaa la wahariri TEF- Teophil Makungwa mara baada ya kupokea mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni ishirini kutoka benki ya NMB. NMB imetoa kiasi cha fedha hiyo kama sehemu ya ufadhili wa mkutano wa mwaka wa jukwaa la wahariri ambao umefanyika mkoa wa Kilimanjaro. Wengine katika picha ni maofisa wa benki wakishuhudia tukio hililililofanyika mwishoni mwa wiki hapa Kilimanjaro. 
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) wakizungumza katika mkutano huo uliofanyika Mkoa wa Kilimanjaro. Wengine katika picha ni maofisa wa benki wakishuhudia tukio hililililofanyika mwishoni mwa wiki hapa Kilimanjaro. Benki ya NMB imetoa kiasi cha sh 20,000 kama sehemu ya ufadhili wa mkutano huo. 
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) wakizungumza katika mkutano huo uliofanyika Mkoa wa Kilimanjaro. Wengine katika picha ni maofisa wa benki wakishuhudia tukio hililililofanyika mwishoni mwa wiki hapa Kilimanjaro. Benki ya NMB imetoa kiasi cha sh 20,000 kama sehemu ya ufadhili wa mkutano huo.

 BENKI ya NMB imedhamini mkutano mkuu wa mwaka wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliofanyika kwa siku moja ya Aprili 4, 2017 mkoani Kilimanjaro na kuhudhuriwa na wahariri wa vyombo mbalimbali nchini ambao ni wanachama wa TEF. 

Akizungumza katika uzinduzi wa mkutano huo, Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali, Richard Makungwa alisema NMB inathamini mchango wa waandishi wa habari nchini na imekuwa ikishikiana nao kwa muda mrefu hivyo kudhamini mkutano huo ni sehemu ya kuendeleza ushirikiano ulipo baina ya NMB na waandishi wa habari. 

“Kwa niaba ya uongozi wa Benki ya NMB, napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza kwa dhati kabisa kwa kutambua kuwa NMB ni benki iliyo karibu na jamii yote ya Watanzania na kugusa mahitaji ya kila jamii ya watanzania wa kila kada.

 “Waandishi wa habari kwa NMB ni wadau muhimu sana kwani mafanikio ya NMB mpaka kufikia hapa kwa kiasi kikubwa yamechangiwa na vyombo vya habari. Hivyo tunafarijika na sisi kushikiriana nanyi kwenye shughuli zinazowagusa ninyi moja kwa moja,” alisema Makungwa na kuongeza. 

“Kwa NMB, huu ni mkutano muhimu sana na maazimio mtakayoyafikia, yatakuwa yenye tija huku mkiweka mbele uzalendo wan chi yetu. Mkiwa mnaendelea na mkutano huu, tambueni kuwa tunawathamini sana na kazi zenu tunazithamini sana.”

 Udhamini wa NMB kwa mkutano mkuu wa mwaka wa TEF una thamani ya milioni 20 na hiyo siyo mara ya kwanza kwani hata mwaka jana ilidhamini mkutano wa TEF, mkutano mkuu wa mwaka wa TBN, mkutano wa TAJATI na pia NMB kuwezesha kutolewa kwa tuzo za uandishi mahiri kwa kushirikiana na MCT.

DC KASESELA MAZOEZI LAZIMA IRINGA ILI KUJENGA UCHUMI

April 10, 2017
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa kwenye mazoezi na wananchi wa kijiji cha Tosamaganga pamoja na mwanachama wa club ya Tosamaganga sports club 
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akicheza Mpira wa kikapu kuashiria kuwa anapenda Mpira wa kikapu

Na Fredy Mgunda,Iringa


Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela aliwaomba wananchi kuendelea kufanya mazoezi kwa ajili ya kuimalisha afya zao pamoja kuujenga uchumi wa nchi hii.

Tukiendelea kufanya mazoezi tutapunguza sana kupata magonjwa mbalimbali kwa kuwa tuna kuwa tunaimalisha afya na kujenga miili yetu lakini hii itasababisa wananchi kujituma kufanya kazi kwa nguvu na morali mpya kila mwanzo mwa wiki kwa kuwa wanakuwa na nguv,stamina na akili Mpya kutokana mazoezi ya mwisho mwa Juma.

"Kwa mfano mimi saizi nipo sawa kiakili kutokana na haya mazoezi maana bila haya mazoezi nisinge kuwa vizuri kiaafya,saizi naweza kufanya kazi kwa masaa mengi kutokana na hili zoezi la Leo sasa nawaomba wananchi na viongozi mbalimbali kufanya mazoezi ili kuongeza ufanisi kazini"alisema Kasesela

Aidha Kasesela aliwashukuru wananchi wa Tosamaganga sports club kwa kuanziasha club ya Tosamaganga ambayo inamichezo mingi kama mpira wa miguu,mpira wa pete,riadha,na mpira wa kikapu hivyo naomba wananchi wengine waanzishe vitu kama hivi ili Wilaya nzima iwe inafanya mazoezi kwa kuimalisha Afya.

Kasesela amewataka viongozi wa kata,kijiji,mtaa,na tarafa kuanzisha mazoezi huku waliko ili kupanua wigo wa eneo kubwa la watu kufanya mazoezi ili kuimalisha afya zao na kupunguza kunyemelewa na magonjwa mbalimbali ambayo yamekuwa yanapunguza nguvu kazi za taifa katika kujenga uchumi wa taifa.

"Hii ni moja ya club ambayo nimeizindua ambayo itatuongezea wigo wa sehemu za kufanyia mazoezi ya kuimalisha afya zetu na kuipa moyo serikali kupanua wigo wa maeneo ya kuafanyia mazoezi" alisema Kasesela

Nao baadhi ya viongozi wa club ya Tosamaganga sports club walimushukuru mkuu wa Wilaya kwa kukuza Michezo katika Wilaya ya Iringa na kuongeza ufanisi wa kazi hasa makazini kwa kuwa ndio jadi ya kukuza uchumi katika mkoa wa Iringa.

MBUNGE RITTA AKABIDHI SARUJI KWA AJILI YA UKARABATI WA SHULE

April 10, 2017
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akikabidhiwa msaada wa mifuko ya saruji kwa ajili ya ukarabati wa shule ya msingi Kigonzile na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la bima (NIC)  Tanzania Samwel Kamanga
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la bima (NIC)  Tanzania Samwel Kamanga akimkakabidhi kiasi cha Pesa mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati zilizochangwa na baadhi ya wadau walijitokeza kwenye ukarabati wa shule ya msingi Kigonzile
Baada ya kufanikiwa kukarabati shule ya msingi Azimio iliyopo Kata ya Mshindo Mbunge wa Viti Maalum kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati ameanza kukabati shule ya msingi Kigonzile iliyopo Kata ya Nduli kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwapo shirika la bima Tanzania (NIC)ambao walijitokeza kusaidia ukarabati wa shule hiyo ya Kigonzile.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa vitakavyo tumika katika kukarabati shule hiyo Kabati alisema kuwa amuamua kufanya shughuri za kijamii ili kuifanya jamii ya watu wa Iringa kuwa na Elimu iliyobora na kuweza kuwa na kizazi ambacho kitakuwa cha kimaendeleo.

"Mimi sipendi kuona watoto wa Iringa wanakuwa wafanyakazi wa kazi za ndani kwa watu kwenye Pesa au wafanyakazi wengi najiuliza tu kwanini ile Iringa ndio chimbuko la wafanyakazi wa kazi za ndani,nitapambana kuhakikisha Iringa inakuwa na wasomi wengi ili kupunguza utegemezi"alisema kabati

Kabati alisema kuwa kuna shule nyingi zimehalibika hapa Manispaa ya Iringa hivyonitakikisha natafuta wafadhili mbalimbali kila kona hapa nchini na nje ya nchi ili kuhakikisha tunazikarabati shule zote ambazo chakavu.

"Hii ni moja ya shule ambazo tayari nimeanza kuitafutia wafadhili hivyo hata shule nyingine nitahakikiaha nafanya kazi na serikali yangu ya chama cha mapinduzi (CCM) chini ya Rais wetu mpendwa Dr John Pombe Magufuli ambaye anaongoza vizuri sana " alisema Kabati

Aidha Kabati aliomba wananchi kufanya kazi kwa kushirikiana na viongozi kuleta maendeleo kwa kuwa wakiitegemeea serikali tu hawawezi kupiga hatua ya kimaendeleo kutoka hapa walipo na kuweza kufikia malengo ya juu kimaisha.

Lakini Kabati aliwaomba viongozi na serikali kutafuta wahisani mbalimbali kila mahali ili kuweza kufanikisha kufikia malengo ya kimaendeleo na kuacha kuwa tegemezi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la bima (NIC)  Tanzania Samwel Kamanga alisema kuwa ameguswa sana na uchakavu wa shule ya msingi Kigonzile kwa hali iliyonayo hivyo licha ya kuwa amechangi zaidi ya 160 ya mifuko ya saruji kwa ajili ya ukarabati.

"Mimi nimesoma kwenye shule kama hii na ndio sababu Leo hii nipo hapa kama Mkurugenzi hivyo Leo nimeguswa sana hii shule imeharibiaka sana na inahitaji Pesa nyingi hivyo tumetoa kiasi kidogo sana narudi makao makuu ya shirika letu nitatoa jibu kwa namna gani nitasaidia kuiboresha na kuwa kama shule nyingine za watu binafsi"alisema Kamanga

Aidha Kamanga aliwaomba wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya taifa ili kuepukana na kupunguza gharama wakati wa majanga kwa kuwa hujui lini utakumbana na matatizo ni vyema wananchi wakajua umuhimu wa bima ya afya ya taifa inamsaidia kimaisha.

Nae Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alimshukuru mbunge wa viti maalum Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kwa jitihada zake za kuleta maendeleo katika Mkoa wa iringa kwa kufanya kazi nyingi za kijamii tofauti na wanasiasa wengine.

"Tukiwa na wabunge kama Hawa basi nchi itapiga hatua kubwa ya kimaendeleo kwa kuwa watakuwa wachapakazi na sio waroho wa madaraka wala sio wapenda Pesa basi tutatoka hapa tulipo na kufika kule tunako staili" alisema Kasesela

Ila Kasesela aliwaomba viongozi wa serikali na wananchi kutumia bima ya taifa ya Tanzania NIC kwa kuwa imekuwa inafanya kazi zake vizuri kuliko bima nyingine hivyo ni lazama kuitambua bima hiyo kwa kuwa ni ya uhakika tofauti na bima nyingine zilizopo hapa nchini.

Nao baadhi ya wananchi wa Kata ya nduli mtaa wa Kigonzile waliwashuku viongozi wa serikali, shirika la bima ya taifa,diwani pamoja na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati kwa Juhudi kubwa za kukarabati shule hiyo ya Kigonzile kwa kuwa ilikuwa katika wakati mgumu sana.

HAPPY BITHDAY TO ME ... BLOGGER CATHBERT ANGELO KAJUNA

April 10, 2017
Leo Aprili 10 ni siku ya kuzaliwa kwangu Blogger Cathbert Angelo Kajuna mmiliki wa Kajunason Blog (www.kajunason.com), Namshukru sana mwenyezi Mungu kwa kunilinda mpaka kufika hapa nilipo na kunipa nguvu, ujasili wa kupambana na misukosuko ya hapa na pale, hakika yeye ndiye muweza wa kila jambo.
Natoa shukrani kubwa kwa familia yangu, ndugu, jamaa na marafiki wote ikiwa na member wa TBN members na wote waliweza kuwa nami katika safari yangu ya maisha mpaka hii leo namuomba Mwenyezi Mungu aniongezee uhai na uzima ...