VODACOM YAJIPANGA KUZUIA MIMBA MASHULENI

October 19, 2015
Mgeni rasmi katika mahafali ya 13 ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Shimbwe iliyopo Uru Moshi vijijini,Ofisa Mkuu wa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Mawasiliano ya simu za Mkononi,Georgia Mutagahywa (mwenye suti nyeusi) akizungumza jambo mara baada ya kutembelea darasa la Kompyuta shuleni hapo juzi.
Mgeni rasmi katika mahafali ya 13 ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Shimbwe iliyopo Uru Moshi vijijini,Ofisa Mkuu wa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Mawasiliano ya simu za Mkononi,Georgia Mutagahywa akiongozana na mkuu wa shule hiyo Jacob Costantine wakielekea eneo la mahafali.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Hassan Majaar Trust ,Balozi Mwananidi Sinare Majaar (kushoto) pia alikuwa ni miongoni mwa wageni waliofika shuleni hapo kwa ajili ya mahafali ya 13 ya kidato cha nne.
Wananfunzi wakionesha umahiri wa kucheza parade wakati wa kuwakaribisha wageni waalikwa.
Wahitimu wakiwa wima kwa ajili ya wimbo wa taifa.
Mgeni rasmi pamoja na meza kuu wakiwa wima kwa ajili ya kuimba wimbo wa taifa.
Baadhi ya wazazi wenye watoto wanaohitimu kidato cha nne katika shule ya sekondari Shimbwe wakifuatilia mahafali hayo.
Mkuu wa shule ya sekondari ya Shimbwe ,Jacob Costantine akizungumza wakati wa mahafalai ya 13 ya kidato cha nne yaliofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo.
Mwenyekiti wa Bodi ya shule ya sekondari ya Shimbwe ,Batromeo Temba akizungumza wakati wa mahafalai ya 13 ya kidato cha nne yaliofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo,Geogia Mutagahywa alishindwa kujizuia wakati wanafunzi wa shule hiyo wakitoa burudani kwa wageni waalikwa.
Balozi Mwanaid Majaar pia aliamua kuonesha umahiri wake katika kucheza kwaito.
Baadhi ya wanafunzi wanao hitimu kidato cha nne katika shule ya sekondari Shimbwe.
Wanafunzi Daudi Silayo na Rehema Kira wanaohitimu kidato cha nne katika shule ya sekondari Shimbwe wakisoma risala mbele ya mgeni rasmi.
Mgeni rasmi akiwapongeza wanafunzi waliosoma risala.
Balozi Mwananidi Majaar akizungumza wakati wa mahafali ya 13 ya shule ya sekondari ya Shimbwe alipohudhuria kama mgeni mualikwa.
Mwakilishi wa wazazi wa watoto wanaomaliza elimu yao ya kidato cha nne shuleni hapo Eliaringa Owoya akizungumza kwa niaba ya wazazi wenzake.
Mgeni rasmi katika mahafali ya 13 ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Shimbwe iliyopo Uru Moshi vijijini,Ofisa Mkuu wa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Mawasiliano ya simu za Mkononi,Georgia Mutagahywa akitoa hotuba yake kwa wazazi na wanafunzi waliofika kwa ajaili ya shughuli ya mahafali hayo.
Mgei rasmi akitunuku vyeti kwa wanafunzi waliohitimu kidato cha nne.
Mgeni rasmi pia alitunuku vyeti kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao na uongozi shuleni hapo.
Baadhi ya ndugu waliofika katika mahafali hayo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
KAMATI YA TAIFA STARS YATAMBULISHWA RASMI

KAMATI YA TAIFA STARS YATAMBULISHWA RASMI

October 19, 2015
Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa Stars iliyoteuliwa hivi karibuni na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Bwana Farough Baghozah leo hii amekutana na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam na kuitambulisha rasmi kamati hiyo.
Katika kamati hiyo ya Taifa ya Stars wapo Michael Wambura – Makamu Mwenyekiti, Bi Teddy Mapunda – Katibu, Wakili Imani Madega – Mweka Hazina, na wajumbe wengine ni Juma Pinto, Isaac Chanji, Salum Abdalla na Moses Katabaro.
Pia Mwenyekiti amechukua fursa hiyo kutangaza kamati ndogondogo na wajumbe wake kama ifuatavyo:
 1. Maandalizi ya timu, zikiwemo huduma kwa timu ya Taifa stars
 Mwenyekiti – Imani Madega
 Wajumbe – Msafiri Mgoyi,Teddy Mapunda.
2. Uhamasishaji wa mchezo (Michezo ijayo) na Masoko
 Mwenyekiti – Juma Pinto
 Wajumbe – Baraka Kizuguto, Mlamu Ng’ambi, Charles Hamka, Hashim  Lundenga, Maulid Kitenge, Shaffih Dauda, Salehe Ally, Peter Simon,  Edo Kumwembe na Mahmoud Zubeiry.
 3. Kamati ya Fedha
Mwenyekiti – Farough Baghozah
Wajumbe – Teddy Mapunda, Michael Wambura, Imani Madega,          Juma Pinto,        Isaac Chanji, Moses Katabaro na Edgar Masoud.
4. Mikakati ya ushindi – itakuwa na kamati ndogondogo na zitakuwa na wajumbe mbalimbali wakiwemo Mwenyekiti Farough Baghozah, Teddy Mapunda, Mohamed Nassoro, Philemon Ntahilaja, Isaac Kasanga, Cresencius Magori.
Pia kamati imetangaza kauli mbiu ya ushindi inayosema “NCHI YETU, TIMU YETU, TAIFA LETU, USHINDI WETU” itakayoanza kutumika kuanzia leo hii.  Pia Kamati imemteua Bi Teddy Mapunda kuwa msemaji mkuu wa kamati hiyo.
Timu inatarajia kuweka kambi Nje ya Nchi kwa takribani siku 12 ili kujiandaa na mechi dhidi ya Algeria Novemba 14 Dar es salaam, na Novemba 17 nchini Algeria.
Aidha Mwenyekiti alitumia nafasi hiyo kuwaomba Watanzania wote warudishe imani kwa timu yao, wajitokeze kwa wingi kwenye mechi ijayo tarehe 14 November dhidi ya Algeria hapa nyumbani.  Pia akatoa wito kwa Watanzania Wote kuchangia timu kwa hali na mali (Madawa, Maji, vifaa vya michezo na kadhalika)…aliongeza ‘Mwenyekiti wa Kamati Bwana Farough Baghouzah.
UNDP YASISITIZA VITA YA UMASKINI KWA KUTUMIA MAZINGIRA

UNDP YASISITIZA VITA YA UMASKINI KWA KUTUMIA MAZINGIRA

October 19, 2015
IMG_6436
Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) Tanzania, (Ushauri na Miradi), Amon Manyama akitoa maelezo kuhusu mradi wa PEI na salamu kutoka UNDP kwa washiriki wa mafunzo hayo hivi karibuni jijini Mwanza.
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
MKURUGENZI Msaidizi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Amon Manyama, alisema vita dhidi ya umaskini inakuwa na maana kubwa kama inalinganishwa na mazingira.
Alisema kwamba umaskini wa kipato ambao umekuwa ukipiganwa sana kwa sasa unastahili kupiganwa kwa kuangalia umaskini kutokana na ukweli kuwa kuboreshwa kwa mazingira ndio hatua kubwa ya kupigana na umaskini katika sura zote zilizobaki.
Mkurugenzi msaidizi huyo alisema hayo hivi karibuni mjini Mwanza wakati akielezea mradi wa mtaji na elimu wa UNDP ambao umefanyiwa kazi kwa pamoja kati ya shirika hilo, Tume ya Mipango, Hazina na Ofisi ya Makamu wa Rais, katika mafunzo ya siku moja ya Uimarishaji wa Ushirika wa Akiba na Mikopo, yaliyofanyika Mwanza.
Mradi huo umelenga kuwezesha ushirika wa akiba na mikopo katika wilaya sita nchini kuwezesha wananchi kushiriki katika kukabili umaskini unaosababishwa na mazingira.
Akifafanua alisema kwamba inawezekana muda wa kusubiri kuvuna samaki ziwani umekwisha kwa hiyo kinachotakiwa kufanyika ni kupanda samaki ndani au nje ya ziwa na watu waweze kutumia nafasi hiyo kuboresha maisha yao.
IMG_6389
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida akitoa maelezo ya utangulizi juu ya madhumuni ya mafunzo hayo kwa washiriki kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua rasmi.
Alisema hali hiyo pia ipo katika misitu. Wakati watu wanakata misitu unawapa elimu na mtaji wa kupanda misitu mingine na hivyo mazingira yakaendelea kubaki na kuwa mtaji wa kukabili umaskini.
Mradi huo ambao upo katika wilaya sita kwa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2021 na ifikapo muda huo utakuwaupo wilaya 21 na kutumika kama kichochea cha utekelezaji wa malengo 17 ya maendeleo endelevu yenye nia ya kupiga vita umaskini, kuondoa ubaguzi na njaa.
Alisema mafunzo yaliyotolewa katika kongamano la viongozi mbalimbali wa vyama vya ushirika vya aina mbalimbali mjini Mwanza kwa msaada wa UNDP na kutekelezwa na Taasisi ya utafiti wa masuala ya kiuchumi na kijamii (ESRF) yamelenga kuwezesha SACCOS kutambua fursa hizo za mazingira kukabili umaskini.
Alisema katika mazingira ya sasa wanawake ndio wanaathirika zaidi katika umaskini kutokana na wao kuwa wazazlishaji na wahudumiaji wa kaya na kwamba kama kutakuwepo na mabadiliko na mazingira yakatengeneza fursa ya kupiga vita umasikini wanawake wataendelea kustawi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya utafiti wa masuala ya kiuchumi na kijamii (ESRF) ESRF Dk. Tausi Kida alisema lengo la mafunzo hayo ni kuimarisha ushirika wa akiba na mikopo mkoani Mwanza.
Akizungumzia historia ya mradi alisema wao kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) pamoja Tume ya mipango, walianza kutekeleza mradi wa kukuza uchumi, kuleta maendeleo endelevu kupitia utunzaji mazingira, usawa wa kijinsia na kupunguza na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi yaani (PEI) toka mwaka 2014.
IMG_6182
Pichani juu na chini ni baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Ushirika (SACCOS na VICOBA) na Maafisa Ushirika wa kutoka Wilaya za Bunda, Bukoba na Sengerema wakifuatilia kwa umakini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa.
Alisema tafiti mbili chini ya mradi wa PEI zilizofanyika katika wilaya za Bunda, Ileje, Sengerema, Bukoba vijijini, Ikungi na Nyasa kubaini changamoto na fursa zinazopatikana katika wilaya hizo.
Alisema matokeo ya tafiti yalionyesha umuhimu wa kuzipa uwezo taasisi za kifedha kama SACCOSS, VICOBA na vikundi mbalimbali vya kifedha kwa kuzijengea uwezo wa kitaaluma na kifedha.
Alisema hata hivyo pamoja na matokeo hayo Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ilitenga na kutoa fungu la fedha na kuipatia benki ya Twiga ili kukopesha kwa riba nafuu kwenye taasisi kama SACCOSS na VICOBA kwa lengo kuu kuweza kuwafikia wananchi wengi zaidi ili waweze kupata fursa ya kukuza mitaji yao na kuwafanya muweze kutekeleza fursa hizi katika maeneo yao.

DKT. SHEIN AENDELEA KUUNGURUMA MKUTANO WA CCM JIMBO LA MPENDAE UNGUJA

October 19, 2015
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na wanaCCM na Wananchi wa Jimbo la Mpendae katika mkutano wa hadhara wa Kampeni za CCM uliofanyika leo katika uwanja wa Binti Amran Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
UN, SMZ KUSHIRIKIANA KUKOMESHA UDHALILISHAJI WA KIJINSIA

UN, SMZ KUSHIRIKIANA KUKOMESHA UDHALILISHAJI WA KIJINSIA

October 19, 2015
IMG_9939
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Dawati la Jinsia na Watoto, Mkoa wa Kaskazini Unguja katika Kijiji cha Mahonda wakati wa ziara fupi ya kukagua miradi inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa visiwani humo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja huo tangu kuanzishwa.
Na Mwandishi wetu, Zanzibar.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez amesema Umoja huo utaendelea kushirikiana na Serikali ya mapinduzi Zanzibar (SMZ) katika kukomesha vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia.
Akizungumza katika ziara ya kutembelea Dawati la jinsia la Wanawake na Watoto, Mkoa wa Kaskazini Unguja katika Kijiji cha Mahonda alisema umoja huo umelenga kusaidia uwepo wa utawala wa sheria na wenye kujali haki na utu wa binadamu kupitia mpango mkakati wake uliomo katika malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kuanzia mwaka 2016 utakosaidia kuondoa vitendo hivyo.
Alieleza kuwa tatizo la udhalilishaji wa kijinsia sio kwa Zanzibar pekee bali ni la kidunia, hivyo umoja wa mataifa(UN) unawajibu kusaidia juhudi za serikali kupambana na tatizo hilo.
“Tushirikiane kwa kila hatua ili kuondosha vitendo hivi kwani ni tatizo na kero kwa jamii ya Zanzibar pia ni miongoni mwa ishara tosha zinazoashiria uvunjifu wa haki za binadamu.”, alisema Rodriguez na kusisitiza kuwa ili kukomesha vitendo hivyo ni kuwepo na utawala wa kisheria utakaotenda haki kwa wale wanaoozalilishwa utu wao.
IMG_9951
Aidha Bw. Rodriguez aliyataka madawati ya jinsia kutumia vyombo vya habari kuwaelimisha wananchi kupambana na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia ili kuhakikisha vinapungua ama kuisha kabisa kwa lengo la kujenga jamii yenye uadilifu.
Naye Mtendaji wa Dawati hilo, kutoka Jeshi la Polisi Koplo, Fatma Juma alifafanua kuwa kesi za ubakaji kwa wanawake na watoto zimepungua ikilinganishwa na miaka iliyopita.
Alisema kwa sasa kuna changamoto ya utoroshwaji na utelekezaji wa watoto kesi ambazo kwa sasa ni nyingi lakini wanaendelea kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu ili kuhakikisha zinapungua.
Akizitaja changamoto zilizopo katika dawati hilo kuwa ni pamoja na kukosekana kwa ushahidi wa kina kwa baadhi ya kesi hivyo kupelekea kuharibu mwenendo mzima wa kesi kutokana na kukosekana uthibitisho.
IMG_9928
Mtendaji wa Dawati la Jinsia na Watoto, Mkoa wa Kaskazini Unguja katika Kijiji cha Mahonda, kutoka Jeshi la Polisi Koplo, Fatma Juma akitoa taarifa fupi ya maendeleo ya kituo hicho tangu kufunguliwa ikiwa ni mwaka mmoja sasa kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (hayupo pichani) ikiwa ni awamu yake ya pili kutembelea Dawati hilo. Kulia ni Mtaalamu wa masuala ya ulinzi kwa watoto wa UNICEF Zanzibar, Bw. Ahmed Ali.
Alifahamisha kuwa changamoto nyingine ni jamii ya wazanzibar kuwa na tabia ya mukhari (kuoneana haya) hivyo kumaliza kesi kwa njia ya kifamilia bila ya kufuata utaratibu wa kisheria, hali inayokuwa kikwazo cha kuwafikisha katika vyombo vya kisheria wahalifu wa kesi za ubakaji.
“Bado nasisitiza ni lazima Wazanzibar tubadilike na kuondokana na masuala ya muhari kwani unawaumiza watoto wetu na tujenge utamaduni wa kujiamini kwa kutoa ushahidi ili tutokomeze janga hili.,” alisisitiza Fatma.
Pamoja na hayo alishukru msaada unaoendelea kutolewa na Umoja wa mataifa (UN) kwa kuunga mkono juhudi za serikali katika kuwawezesha katika mambo mbali mbali kwa lengo la kupunguza vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia.
Mwakilishi huyo Mkazi katika ziara hiyo alitembelea miradi mbali mbali ya umoja huo ikiwa ni moja ya sherehe za kutimiza miaka 70 ya kuanzishwa kwa umoja huo.
IMG_9935
Baadhi ya waandishi wa habari wa visiwani Zanzibar na maofisa wa Umoja wa Mataifa waliombatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (hayupo pichani) katika ziara ya kukagua miradi inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa visiwani humo.
IMG_9969
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akipitia kitabu cha orodha za kesi katika Dawati la Jinsia na Watoto, Mkoa wa Kaskazini Unguja katika Kijiji cha Mahonda. Kulia ni Mtendaji wa Dawati hilo, kutoka Jeshi la Polisi Koplo, Fatma Juma na kushoto ni Mtaalamu wa masuala ya ulinzi kwa watoto wa UNICEF Zanzibar, Bw. Ahmed Ali.
IMG_9963
IMG_9983
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiwa ndani ya chumba cha dawati la Jinsia.
IMG_0009  
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiagana na Mkuu wa Upelelezi wa Dawati la Jinsia na Watoto, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Kombo Khamis Kombo (kulia) alipofanya ziara ya kutembelea Dawati la Jinsia na Watoto, Mkoa wa Kaskazini Unguja katika Kijiji cha Mahonda ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa. Kushoto ni Mtaalamu wa masuala ya ulinzi kwa watoto wa UNICEF Zanzibar, Bw. Ahmed Ali.
IMG_9904
Mradi huu ulifadhiliwa kwa pamoja kati ya Jumuiya ya Ulaya (EU) na Shirika linalohudumia watoto duniani, UNICEF.
IMG_0023
Muonekano wa jengo la Dawati la Jinsia na Watoto mkoa wa Kaskazini Unguja.