PUMA YAZINDUA MPANGO WA MAFUNZO YA USALAMA BARABARANI KWA WANAFUNZI

April 24, 2018













Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mbande, Dar es Salaam, Nasri Mustafa akumuonesha Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti (kulia) picha aliyoichora na kushinda tuzo ya usalama barabarani 2017, wakati wa uzinduzi wa mpango wa Puma wa mafunzo ya ya usalama barabarani kwa wanafunzi, jana katika Makao Makuu ya Puma, Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Matibu Mbunja aliyemwakilisha Kamanda wa Kikosi cha Poilisi cha Usalama Barabarani Tanzania.Wa pili kushoto ni SajentiHussein Ramadhan Mwalimu wa Trafiki Makao Makao Makuu ya Usalama Barabarani.Imeandaliwa na Richard Mwaikenda.


Na Mwandishi Wetu


KAMPUNI ya Puma Energy Tanzania imezindua kampeni maalumu ya mafunzo ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi kwa lengo la kueneza elimu hiyo kuanzia ngazi ya chini.

Kampeni hiyo inayokwenda sambamba na mashindano ya uchoraji michoro ya usalama barabarani imezinduliwa Dar es Salaam jana na ofisa wa Polisi, ASP Mbuya Matibu, kutoka Makao Makuu ya Kikosi cha Usala,ma Barabarani.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo, ASP Matibu, alisema Puma Energy Tanzania, wana mchango mkubwa katika utoaji elimu ya usalama barabarani, hivyo kuwataka wadau wengine kuiga mfano huo.

Pia, aliwataka madereva nchini wasiendeshe magari kwa kukariri sheria, bali wazitambue ili waweze kuzitumia vizuri kupunguza ajali.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti, alisema elimu ya usalama kwa wanafunzi ni muhimu, kwani inawapa uelewa wa matumizi ya barabara kwa usalama.

Tunawaangalia sana watoto wa shule za msingi kwani wao wanakabiliwa na hatari nyingi za barabarani," alisema Corsaletti na kuongeza;

"Hivyo kwa kuwafundisha usalama barabarani tunawapa ufahamu wa kuwajenga katika matumizi salama ya barabara...hiki ndicho kipaumbele chetu."

Alifafanua kwamba baada ya mafunzo wanafunzi wanapewa nafasi ya kuchora michoro ya usalama barabarani na mshindi pamoja na shule anayotoka wanazawadiwa.

Corsaletti alisema kampuni hiyo ilianzisha mafunzo hayo mwaka 2013 na imeendelea kufanya hivyo hadi sasa kwa kufikia shule 47 na kuwafundisha wanafunzi 60,000 kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro na Geita.


Aliongeza kuwa uchunguzi uliofanywa umeonesha kuwa kiwango cha ajali katika shule zilizopatiwa mafunzo kimepungua

Corsaletti, alisema kampuni hiyo itaendelea na kampeni ya usalama barabarani na kuahidi kufanyakazi pamoja na Kikosi cha Usalama Barabarani, maofisa kutoka manispaa au wilaya zinatoka shule zilizochaguliwa ili kuhakikisha lengo linatimia.
Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti (kulia), akimshukuru Mbunja kwa kuzindua mpango huo.
Matibu Mbunja aliyemwakilisha Kamanda wa Kikosi cha Poilisi cha Usalama Barabarani Tanzania, akihutubia wakati wa uzinduzi wa mpango huo.



















Meneja Rasilimali Watu wa Puma Tanzania Bi Loveness Hoyange akiiweka sawa picha iliyochorwa na Mwanafunzi Nasri Mustafa na kushinda tuzo ya Usalama barabarani 2027

Shemu ya wadau wa usalama barabarani
Baadhi ya walimu na wanafunzi waliohudhuria uzinduzi huo
Wanahabari wakiwa kazini
Sehemu ya wadau wa usalama barabarani
Mwanafunzi Nasri Mustafa akionesha picha aliyoichora ya usalama barabarani. Picha hiyo ilishinda tuzo ya kwanza 2017

Wadau wa usalama barabrani wakisikiliza kwa makini wakati wa uzinduzi a mpango huo
 
Mgeni rasmi, Mbunja na Meneja Mkuu wa Puma,Corsaletti wakiwa na furaha
Meneja Mkuu wa Puma,Corsaletti, Akisalimiana na wadau baada ya uzinduzi
Wakiwa katika picha ya pamoja


WAZIRI WA AFYA AZINDUA UGAWAJI WA VYANDARUA VYENYE DAWA YA MUDA MREFU KIGOMA

April 24, 2018
*Vyandarua Bure kwa Wajawazito na Watoto,atakaeuza kukiona

WAZIRI Wa Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameagiza Waganga Wakuu Wa Mikoa,Wa Wilaya na Waganga Wafawidhi kuweka Matangazo katika Vituo vya Afya, Zahanati na Hospitali kwamba huduma za upimaji na Matibu ya Malaria ni bure na Wananchi hawatakiwi kulipia kwakuwa kuna wafadhili wanao gharamia gharama hizo.

Maagizo hayo aliyatoa jana Mkoani Kigoma katika Zahanati ya Mwandiga Wakati akizindua ugawaji wa Vyandarua endelevu vyenye dawa ya Muda mrefu ,kwa Wakina Mama wajawazito na Watoto wenye umri wa Mwaka Moja wa ushirikiano wa Serikili ya Tanzania kupitia wizara ya afya kitengo cha kudhiti malaria na Shirika la misaada la marekani (USAID) ambapo alipokea Malalamiko kutoka kwa Wananchi wakidai kutozwa fedha kwaajili ya Matibabu na Wakati serikali imeagiza Zoezi hilo ni bure.

Waziri Mwalimu alisema Ugawaji endelevu wa Vyandarua ni mradi unaoendeshwa kwa pamoja na shirika la JohnsHopkins Center for Communication na Vectorworks kwa ufadhili wa shirika la misaada la Marekani (USAID) kupitia mfuko wa Rais wa Marekani wa Kudhibiti malaria Na kuratibiwa na Serikali kupitia Mradi wa Kupambana na Malaria NMCP kwa hiyo vyandarua hivyo ni bure na Wananchi wanatakaiwa wasilipie.

Aidha alisema ofisi ya takwimu (NBS) katika kaya mwaka 2017 zilionyesha kupungua kwa kiwango cha Maambukizi ya Malaria hadi chini ya asilimia 10% kutokana na Mikakati iliyowekwa na Wizara kuhakikisha wanatokomeza ugonjwa wa Malaria.

Alisema mikakati ya Serikali ni kuongeza kasi ya upimaji wa Malaria kwa kutumia kipimo cha (mRDT) Hadubini na Kutumia dawa za mseto pindi wanapothibitika kuwa na Vimelea vya malaria , kuwapatia Wajawazito Vyandarua vyenye viuatilifu ili kujikinga kuumwa na Mbu pia kuwapatia dawa za Sp kwa kipindi maalumu wakati wa ujauzito ilikuwakinga na madhara yatokanayo na Malaria.

"Niendelee Kusisitiza dawa za malaria na Matibabu ni bure Wananchi hawatakii kulipia, wafadhiri wetu wanajitoa sana kuhakikisha Suala la Malaria liishe , Waganga wafawidhi wanatuangusha sana niombe muweke matangazo na namba za simu kwenye vituo vya Afya iliwananchi watakao lipishwa watoe Malalamiko yao ilikuweza kuondokana na changamoto ya Ugonjwa wa Malaria", alisema Mwalimu.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Vijijini , Elisha Robarti alisema zahanati hiyo inakabiliwa na upungufu wa Watumishi wahitaji ni watumishi 15 na waliopo ni watumishi saba hali inayopelekea Watumishi kulemewa.

Wakitoa Malalamiko yao Wananchi waliofika kupata huduma Katika Zahanati hiyo mbele ya Mh Waziri, Lydia Leonard alisema Wamekuwa wakitozwa shilingi 2500/= kwaajili ya Kipimo cha Malaria na kulipa dawa wanapofika kwaajili ya Matibabu .

Alisema pamoja na kuwa na Kadi ya bima ya Afya lakini bado wanaendelea kutozwa fedha na wanamuomba Waziri kusimamia suala hilo iliwaweze kupata Matibabu bure kama serikali inavyo elekeza.

Hata hivyo Wananchi hao Shukuru Issa aliomba Serikali kuwajengea Kituo cha Afya Kata ya Mwandiga pamoja na kuboreshewa huduma Za Maji kwani maji wanayo yatumia sio salama na Wanalazimika kutumia Kilomita 13 kufuata huduma na Waziri alitoa maelekezo kwa halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Vijijini kuanza ujenzi wa kituo hicho kwakuwa kata hiyo inawatu wengi na inahitajika kupata kituo cha Afya.

WAZIRI Wa Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ''Vyandarua bure kwa Wajawazito na Watoto,atakaeuza kukiona''.Waziri Ummy akizungumza leo kwenye ugawaaji wa Vyandarua katika Zahanati ya Mwandiga mapema leo,mkoani Kigoma

WAZIRI Wa Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimkabidhi chandarua chenye dawa ya muda mrefu Mwantum Mohammed baada ya kuzindua kuzindua ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu kwa akinamama wajawazito na watoto wenye umri wa mwaka mmoja, mpango ambao unaendeshwa na shirika la Johns Hopkins kupitia mradi wa Vectors Work chini ya ufadhili wa USAID kupitia mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na Malaria. Kulia ni mwakilishi wa USAID Tanzania Andy Karas.
Mwakilishi wa USAID Tanzania Andy Karas akimkabidhi chandarua chenye dawa ya muda mrefu Asha Juma baada ya uzinduzi wa ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu kwa akinamama wajawazito na watoto wenye umri wa mwaka mmoja, mpango ambao unaendeshwa na shirika la Johns Hopkins kupitia mradi wa Vectors Work chini ya ufadhili wa USAID kupitia mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na Malaria.

WAZIRI Wa Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwasikiliza akinamama wanaudhuria kliniki kwenye Zahanati ya Mwandinga Wilaya ya Kigoma Vijijini baada ya kuzindua ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu kwa akinamama wajawazito na watoto wenye umri ya mwaka mmoja mpango ambao unaendesha na shirika la Johns Hopkins kupitia mradi wa Vectors Work chini ya ufadhili wa USAID kupitia mfuko wa Raisi wa Marekani wa kupambana na Malaria.
WAZIRI Wa Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwasikiliza akinamama wanaudhuria kliniki kwenye Zahanati ya Mwandinga Wilaya ya Kigoma Vijijini baada ya kuzindua kuzindua ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu kwa akinamama wajawazito na watoto wenye umri ya mwaka mmoja mpango ambao unaendeshwa na shirika la Johns Hopkins kupitia mradi wa Vectors Work chini ya ufadhili wa USAID kupitia mfuko wa Raisi wa Marekani wa kupambana na Malaria.
WAZIRI Wa Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimkabidhi chandarua chenye dawa ya muda mrefu Mwantum Mohammed baada ya kuzindua kuzindua ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu kwa akinamama wajawazito na watoto wenye umri ya mwaka mmoja mpango ambao unaendesha na shirika la Johns Hopkins kupitia mradi wa Vectors Work chini ya ufadhili wa USAID kupitia mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na Malaria.

-- Ahmad Issa Michuzi Editorial Director P.O BOX 9033, DAR ES SALAAM. issamichuzi.blogspot.com www.michuzijr.blogspot.com othmanmichuzi.blogspot.com Phone:0713 422 313/ 0783 422 313 Tanzania- East Africa.

TAARIFA KUTOKA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI TFF LEO

April 24, 2018
NGORONGORO HEROES YAREJEA,WAPEWA MAPUMZIKO SIKU TATU

Timu ya Taifa ya Vijana U20 (Ngorongoro Heroes) imerejea nchini Leo ikitokea nchini DR Congo kwenye mchezo wake wa marudiano wa kufuzu fainali za Africa za Vijana U20 dhidi ya DR Congo.

Wachezaji wa Ngorongoro ambao wamefanikiwa kuivusha timu hiyo kwenda raundi ya pili wamepewa mapumziko ya siku tatu kwa mujibu wa program ya Kocha Mkuu Ammy Ninje.

Katika raundi ya pili Ngorongoro Heroes watacheza dhidi ya Mali mwezi ujao mchezo wa kwanza wakianzia nyumbani.

SERENGETI BOYS KUPIGA NUSU FAINALI KESHO

TIMU YA Taifa ya Vijana U17 (Serengeti Boys) kesho inatupa karata yake muhimu kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Kenya.

Mchezo huo utachezwa saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Muyinga nchini Burundi.

Kufuzu hatua ya nusu fainali Serengeti Boys walitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Uganda kwenye mchezo wa kwanza kabla ya kuifunga Sudan kwa magoli 6-0 kwenye mchezo wa mwisho wa kundi B.

Tunaitakia kila la kheri Serengeti Boys iweze kufanya vizuri kwenye mchezo huo wa nusu fainali.

Mungu Ibariki Tanzania,Mungu Ibariki Serengeti Boys.



MECHI YA SIMBA NA YANGA MAGETI KUFUNGULIWA MAPEMA,JESHI LA POLISI LAWEKA ULINZI MKALI

Mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara utakaowakutanisha Simba na Yanga Jumapili Aprili 29,2018 uliopangwa kuchezwa saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Taifa Tiketi zinaendelea kuuzwa kupitia Selcom.

Yeyote anayetaka kununua tiketi hizo kupitia Selcom anachotakiwa kufanya ni kujaza pesa kwenye kadi yake ya Selcom ambayo inamuwezesha kuweza kununua tiketi hizo kupitia simu ya mkononi.

Mageti yanatarajia kufunguliwa mapema kuanzia saa 2 asubuhi ambapo vyakula na vinywaji vitapatikana ndani.

Jeshi la Polisi limehakikisha ulinzi utakua wa hali ya juu na kuwatahadharisha wale wote wenye nia ya kufanya vitendo vya uovu.

Mamlaka ya Uwanja imethibitisha kuongezeka kwa camera za Uwanjani ambapo sasa zimefikia 109 ambazo zitakuwa zinafuatilia matukio yote

MILANZI AFAGILIA JESHI LA WANANCHI KWA MCHANGO WAKE KATIKA UHIFADHI NA ULINZI WA MALIASILI NCHINI

April 24, 2018

Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi akizungumza na wanajeshi wa nchi mbalimbali za Afrika ambao wapo nchini kujifunza mambo mbalimbali ya sekta ya utalii nchini na mchango wake kwenye uchumi na namna ambavyo jeshi linashiriki kwenye ukuaji wake.

Na Mwandishi Maalum-Dar es Salaam
...................................................................................
JESHI la Wananchi licha ya kuwa na majukumu yake ya msingi ya ulinzi, limetajwa kuwa na mchango mkubwa kwenye utunzaji wa maliasili za nchi na uhifadhi kwa ujumla.

Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi, alipokuwa akizungumza na wanajeshi wa nchi mbalimbali Afrika, ambao wanasoma kwenye chuo cha ukamanda na unadhimu cha nchini Ghana.

Wanajeshi hao, ambao wapo nchini kwa siku saba kwa ziara ya mafunzo, walikutana na Meja Jenerali Milanzi, ili kufahamu juu ya masuala mbalimbali ya sekta ya utalii nchini na mchango wake kwenye uchumi na namna ambavyo jeshi linashiriki kwenye ukuaji wake.

Akizungumza kwenye hotuba yake, Milanzi alisema sekta ya utalii pamoja na faida zake lukuki kwenye taifa lolote ikiwemo Tanzania, ina changamoto nyingi ambazo kwa namna moja au nyingine utatuzi wake unaweza kufikiwa haraka kama jeshi litashirikishwa.

"Sekta ya utalii ina changamoto kadhaa ikiwemo suala la ujangili, ambayo kwa Tanzania tumejitahidi kupambana nayo kwa msaada wa majeshi yetu ambapo kwa kufanya hivyo tumefanikiwa pakubwa," alisema.

Alitumia nafasi hiyo kuwataka wanajeshi hao kutumia ziara hiyo ya kimafunzo, kujifunza namna ya kusaidia ukuaji wa sekta ya utalii nchini mwao na Afrika kwa ujumla huku pia akiwashauri wajifunze kuhusu utangamano wa bara la Afrika.

"Nchi za Afrika ni ndugu, nimewaambia waendelee kujifunza vitu vingi kuhusu utalii wa nchi mbalimbali hasa ikizingatiwa wanyamapori hawana mipaka, kwa hivyo kama udhibiti wa ujangili utafanyika sehemu moja na nyingine pakawa hapana chochote, tatizo litaendelea kuwepo," alifafanua.

Wakitoa shukrani kwa Wizara ya maliasili na utalii, askari hao kwa nyakati tofauti walisema wamejifunza mengi kutokana na uwasilishaji wa Katibu Mkuu Milanzi na kwamba itawasaidia kwenye kukamilisha mafunzo yao mara watakaporudi chuoni.

Kwa mujibu wa Kanali Hamza Mzee, ambaye ni mwenyeji wa ugeni huo, msafara wa askari hao unahusisha watu 16 na kwamba ni ziara ya kawaida ya mafunzo kwa askari kama wanavyofanya askari wa JWTZ, wanaosoma chuo cha ukamanda na unadhimu Duluti, Arusha.