NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, JAPHET HASUNGA AFUNGUA KITUO CHA MAFUNZO YA MISITU NA UCHAKATAJI WA MAGOGO MKOANI IRINGA

December 01, 2017
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) na Balozi wa Finland nchini, Mhe. Peka Huka wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Kituo cha Mafunzo ya Misitu na Uchakataji wa Magogo kilichoanzishwa mwezi  Desemba, 2016 katika mji wa Mafinga, Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa chini ya ufadhili wa Serikali ya Finland katika hafla iliyofanyika jana mkoani humo.

Na Hamza Temba-WMU-Iringa
........................................................................
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga amefungua Kituo cha Mafunzo ya Misitu na Uchakataji wa Magogo ambacho kimeanzishwa katika Mji wa Mafinga, Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa chini ya ufadhili wa Serikali ya Finland kupitia mradi wa Panda Miti Kibiashara.

Akizungumza kwenye hotuba yake ya ufunguzi wa kituo hicho jana mjini hapa, Naibu Waziri Hasunga ameishukuru Serikali ya Finland kwa msaada huo na misaada mingine ambayo imekuwa ikiitoa katika kuimarisha sekta ya Misitu nchini toka miaka ya 1970s.  

Alisema lengo la kituo hicho ni kusaidia kutoa elimu kwa vitendo na ujuzi kwa makundi mbalimbali ambayo yapo katika mnyororo wa kuongeza thamani ya mazao ya misitu ikiwemo watu binafsi, viwanda vya misitu na taasisi za Serikali kuanzia hatua za mwanzo za upandaji wa miche ya miti hadi kwenye hatua za mwisho za uchakataji wa magogo.

Aidha, kutokana na kituo hicho kuwa chini ya mradi huo, Naibu Waziri Hasunga amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Meja Jenerali Gaudence Milanzi kuangalia uwezekano wa kukiweka kituo hicho chini ya Wizara yake ili mafunzo yanayotolewa yawe endelevu hata kama mradi husika utafikia ukiongoni.

Pia, ameagiza mitaala ya kituo hicho ipitiwe na isajiliwe kupitia Mfumo wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi– VETA ili yaweze kutambulika na wahitimu wapewe vyeti kulingana na mahitaji ya soko katika sekta ya viwanda vya misitu nchini.

Katika hatua nyingine amemuagiza Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara hiyo, Dk. Ezekiel Mwakalukwa kukagua viwanda vyote vya misitu nchini kwa ajili ya kujiridhisha kama vinakidhi vigezo vilivyowekwa na wizara ikiwemo kuwa na wafanyakazi wenye ujuzi unaostahili.

Alisema uwepo wa kituo hicho cha mafunzo utawezesha viwanda hivyo kuwapatia mafunzo kwa vitendo wafanyakazi wake ambao hawana vigezo ili waweze kukidhi vigezo na ujuzi stahiki ikiwemo kuwa na Fundi Misumeno, Fundi Mwendesha Mashine ya Kuchakata Magogo na Fundi Mitambo.

Alitoa wito kwa wananchi wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini pamoja na maeneo mengine nchini kujiunga na kituo hicho waweze kupata mafunzo ya kitaalamu na ujuzi wa kuotesha miti kwa njia za kisasa iweze kuzalisha mbao na samani zenye ubora zaidi.

Kwa upande wa Balozi wa Finland, Mhe. Peka Huka amesema nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuboresha sekta ya misitu nchini iweze kutoa mchango chanya kwa jamii na taifa ujumla.

Naye Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi amesema kituo hicho kitatoa fursa pana ya mafunzo kwa makundi mbalimbali katika sekta ya misitu nchini tofauti na vituo vingine ambavyo huitaji vigezo mbalimbali vya kitaaluma kujiunga. Alisema maelekezo yote yaliyotolewa na Naibu Waziri Hasunga yatafanyiwa kazi ili kuimarisha sekta hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alisema Serikali ya Mkoa wake imefurahishwa kwa kuanzishwa kwa kituo hicho cha mafunzo katika mkoa wake na kuahidi kushirikiana na mamlaka zingine kukilinda na kukiendeleza. Alisema katika maeneo aliyopanga kumpeleka Mhe. Rais kwenye ziara zake mkoani humo ya kwanza itakuwa katika kituo hicho.

Toka kuanzishwa kwake mwezi Desemba mwaka jana, 2016 mpaka sasa kituo hicho cha mafunzo kimeshaandaa na kuendesha zaidi ya kozi 20 kwa ajili ya usimamizi wa misitu, afya na usalama kazini, huduma ya kwanza, ujasiriamali na ufundishaji. Wastani wa muda wa mafunzo yanayotolewa kituoni hapo ni siku nne ambapo jumla ya washiriki 400 wameshapatiwa mafunzo hayo huku wanawake ikiwa ni asilimia 35.

Aidha kwa sasa jumla ya wanafunzi 40 kutoka Chuo cha Misitu Olmotonyi na Chuo cha Viwanda vya Misitu Moshi wanapatiwa mafunzo kwa vitendo katika kituo hicho.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akipanda mti wa kumbukumbu muda mfupi baada ya kufungua rasmi Kituo cha Mafunzo ya Misitu na Uchakataji wa Magogo kilichoanzishwa katika mji wa Mafinga, Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa chini ya ufadhili wa Serikali ya Finland. Kutoka kushoto wa tatu ni Balozi wa Finland nchini, Mhe. Peka Huka, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza. 
Balozi wa Finland nchini Tanzania, Mhe. Peka Huka akipanda mti wa kumbukumbu muda mfupi baada ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) kufungua rasmi Kituo cha Mafunzo ya Misitu na Uchakataji wa Magogo kilichoanzishwa mwezi Desemba, 2016 katika mji wa Mafinga, Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa chini ya ufadhili wa Serikali ya Finland. Kutoka kulia wa tatu ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Christina Mndeme na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi jana muda mfupi baada ya kufungua rasmi Kituo cha Mafunzo ya Misitu na Uchakataji wa Magogo kilichoanzishwa mwezi  Desemba, 2016 katika mji wa Mafinga, Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa chini ya ufadhili wa Serikali ya Finland. Wengine pichani ni Balozi wa Finland nchini, Mhe. Peka Huka (wa pili kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Christina Mndeme. 

SBL YAZINDUA KAMPENI YA KUHIMIZA UNYWAJI KISTAARABU MSIMU WA SIKUKUU I

December 01, 2017
Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Helene Weesie akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya kuhimiza unywaji kistaarabu katika msimu huu wa sikukuu pembeni yake kutoka kulia ni Meneja Masoko wa SBL ,Anitha Rwehumbiza na kushoto kwake ni  Ofisa  Mnadhimu wa Kikosi cha Usalama Barabarani ACP Theopista Mallya na mwishoni ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wilfred Kidau mapema jana katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam.
Meneja Masoko wa SBL Anitha Rwehumbiza akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya unywaji kistaarabu ambayo imeshirikisha timu ya Taifa mapema jana katika hoteli ya hyatt Regency jijni Dar es salaam.

SHIRIKA LA AGPAHI LIKISHIRIKIANA NA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA WAENDESHA ZOEZI LA UPIMAJI WA VVU KATIKA VITUO VYA AFYA JIJINI TANGA

December 01, 2017
 Kushoto ni Muuguzi wa kituo cha Afya Ngamiani Lea Kakunya akichukua maelezo ya mkazi wa Jiji la Tanga ambaye alijitokeza kupima VVU wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani.
 Wakazi wa Jiji la Tanga wakiingia kwenye viwanja vya Kituo cha Afya Ngamiani kwa ajili ya kupima VVU katika zoezi ambalo liliendeshwa na Shirika la AGPAHI katika vituo vya Afya vya Makorora,Ngamiani ,Pongwe na Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo ambapo zaidi ya wananchi 1900 walijtokeza kupima.
 Kushoto ni Ochieng Makaranga ambaye ni Mratibu wa Huduma na Tiba kwa watu wenye VVU Kituo cha Afya Ngamiani Jijini Tanga akichukua maelezo ya mkazi wa Jiji hilo wakati wa zoezi la Upimaji wa VVU  jana Desemba Mosi
 Baadhi ya wakazi wa Jiji la Tanga wakiwa kwenye kituo cha Afya Makorora wakisubiri huduma ya kupima VVU.
 Afisa Tabibu kutoka kituo cha Afya Makorora Jijini Tanga,Silvesta Leonard kulia akichukua maelezo kwa mmoja kati ya wananchi wa Jiji hilo ambaye alijitokeza kupima VVU Jana Desemba 1,2017
 Muuguzi wa Afya katika Kituo cha Afya Makorora Jijini Tanga,Salima Athumani akimpima virusi vya Ukimwi VVU mkazi wa Jiji hilo wakati wa upimaji huo uliokuwa ukiendeshwa na Shirika la AGPHA
 Baadhi ya wakazi wa Jiji la Tanga waliojitokeza kupima VVU katika kituo cha Afya cha Makorora Jijini Tanga.
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Tanga waliojitokeza kupima VVU katika kituo cha Afya cha Makorora Jijini Tanga.

Shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS Health Care Initiative (AGPAHI) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Tanga wameendesha zoezi la upimaji vya virusi vya Ukimwi kwa wakazi wa Jiji hilo huku zaidi ya wakazi 1900 wakijitokeza kupima  na kupatiwa ushauri wa namna ya kuweza kujikinga na maambukizi ya VVU .

Upimaji huo ulifanyika kwenye vituo vya Afya Makorora, Ngamiani, Pongwe na Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo ikiwa ni kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani inayoadhimishwa kila mwaka hapa nchini. Zoezi hili la upimaji lililenga wanafamilia wa watu wanaoishi na VVU katika jiji la Tanga. Upimaji huo ulianza siku ya Jumatano hadi Ijumaa (29 Novemba – 01 Disemba) ambayo ndiyo siku ya Ukimwi duniani.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya kupima afya zao mkazi mmoja wa Donge Jijini Tanga, Zilipa Elangwe alisema zoezi hilo limekuwa ni zuri kwa sababu linasaidia watu kuweza kujua afya zao na namna ya kujikinga.

Alisema wanapokuwa wakijua afya zao inawasaidia kuweza kujiepusha na vitendo ambavyo vinaweza kupelekea kuingia kwenye maambukizi ikiwemo kujiepusha na ngono zembe.

Aidha alisema huduma hiyo ya upimaji wa VVU ambayo imetolewa na Shirika la AGPAHI likishirikiana na halmashauri ya jiji la Tanga imewasaidia kujua afya zao kutokana na baadhi ya familia kutokuwa na uwezo wa kifedha kwenda kupima mara kwa mara hivyo ni jambo nzuri.

“Kwa kweli tunalishukuru sana Shirika la AGPAHI kwa kutuletea huduma hii ya upimaji wa VVU maana imetusaidia kujua afya zetu lakini pia kuchukua tahadhari ya kuhakikisha tunaepukana na maambukizi mapya “Alisema.

Naye  Saidi Sharifu mwenye miaka 72 aliliomba Shirika hilo kuendelea kutoa huduma za upimaji huo kila wakati ili kuweza kuwasaidia wananchi wanaokumbana na maambukizi waweze kujitambua na kuanza kutumia dawa.

Alisema ni ukweli usiopingika wapo watu wanaweza kukumbana na maambukizi kutokana na kushiriki tendo la ndoa bila kujijua hali zao hivyo kunapokuwa na huduma hiyo ya uhamasishaji upimaji wa VVU inasaidia kubaini hali yao ya kiafya na kuanza kuchukua hatua.

Naye Tabu Khamisi ambaye ni mkazi wa Makorora Jijini Tanga, alisisitiza kuwepo na uhamasishaji wa upimaji wa VVU wa mara kwa mara ili jamii iweze kupata fursa ya upimaji VVU na familia zao. Pia alisema upimaji huo umekuwa chachu ya wananchi kuweza kujitokeza kwa wingi kujua hali zao na namna nzuri ya kujikinga na maambukizi hususani wazazi waliojitokeza kwa wingi na watoto wao.
Naye Mratibu wa Ukimwi wa jiji la Tanga, Dr. Hamisi Mvugalo alisema juhudi ambazo zinafanywa na shirika la AGPAHI zinapaswa kuungwa mkono na kuwa endelevu kwani zina manufaa kwa jamii inayotuzunguka.

WIZARA YA AFYA YATOLEA UFAFANUZI KUHUSIANA NA UZINDUZI WA MKAKATI WA KONDOM

December 01, 2017
Kumekuwa na taarifa mbalimbali, hamaki na kejeli zinazoenea katika mitandao ya kijamii kuhusiana na taarifa iliyotolewa tarehe 27 Novemba 2017, Mnazi Mmoja kwenye uzinduzi wa Mkakati wa Taifa wa Kondom kuhusu mpango wa Serikali kununua na kusambaza kondom 500,000,000 katika kipindi cha miaka mitatu 2018 hadi 2020.

Tunapenda kuukumbusha umma wa Watanzania kwamba maambukizi ya VVU na UKIMWI bado ni tatizo katika nchi yetu. Takriban watu 1,400,000 wanakadiriwa kuwa na VVU. Hivyo katika mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI Serikali inaendeleza afua mbalimbali ili kuzuia maambukizi mapya. 
Asilimia 40% ya maambukizi mapya yanatokea miongoni mwa vijana wenye umiri wa miaka 15-24. Aidha makundi maalum kama vile wanaojidunga madawa ya kulevya, wanaofanya biashara ya ngono na wale wanaoamiiana wa jinsia moja wako katika hatari kubwa ya kupata maambukizi.  Makundi mengine ya walio katika hatari ni waendesha magari ya masafa marefu, wavuvi na wananchi wa kwenye migodi.

Wizara inatekeleza afua mbalimbali ikiwa ni pamoja na ushauri nasaha na kupima uwepo wa VVU, na kisha kuanza tiba na matunzo, pamoja na kutoa dawa za kufubaza kwa watakao kuwa na maambuzi ya VVU. Kuna afua pia za kuzuia maambukizi ya mama kwenda kwa mtoto, kutoa elimu ya VVU/UKIMWI na afya uzazi kwa vijana, elimu kuhusu VVU/UKIMWI kwa jamii na tohara kwa wanaume. 
Matumizi ya kondom ni moja wapo ya afua katika kuzuia maambukizi mapya. Hata hivyo utafiti wa viashiria vya Malaria na UKIMWI wa mwaka 2011/12 umebaini kuwa kuna matumizi duni ya kondom, kwani ni asilimia 27 tu ya watu wenye wenza zaidi ya mmoja waliokiri kutumia kondom mara ya mwisho walipofanya ngono. Hivyo Serikali itaendelea kununua na kusambaza kondom kwa lengo la kuzuia maambukizi ya VVU, magonjwa ya ngono na mimba zisizo tarajiwa ikiwa ni mojawapo ya afua hizo za kudhibiti maambukizi ya VVU.

MHE MWANJELWA AIPONGEZA NFRA KUANZISHA MRADI WA KUONGEZA UWEZO WA KUHIFADHI MAZAO KUPITIA UJENZI WA VIHENGE NA MAGHALA NCHINI

December 01, 2017
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo mara baada ya kutembelea Ghala la Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Makambako, Mkoani Njombe wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja, Leo Novemba 1, 2017. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza na Wakulima wa Mji wa Makambako, Mkoani Njombe katika ukumbi wa Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Makambako, Mkoani Njombe wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja, Leo Novemba 1, 2017.
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua mahindi yaliyohifadhiwa kwenye Ghala la Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Makambako, Mkoani Njombe wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja, Leo Novemba 1, 2017.
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Wa (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba ya namna ya ununuzi na uhifadhi wa mahindi kwenye Ghala la Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Makambako, Mkoani Njombe wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja, Leo Novemba 1, 2017.

Na Mathias Canal, Njombe

Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa amesifu juhudi za uongozi Wa Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kwa utendaji kazi kwa ubunifu kwa kuanzisha Mradi Wa kuongeza uwezo Wa kuhifadhi Mazao.

Mradi huo utahusisha ujenzi Wa Vihenge vya kisasa, Mghala ya kisasa pamoja na ukarabati Wa Ofisi ambapo baada ya mradi huo kukamilika wakala utakuwa umeongeza uwezo Wa kuhifadhi Shehena ya mahindi ya uzito Wa zaidi ya Tani 250,000 ambapo Vihenge vya kisasa ni 190,000 MT na Maghala 60,000 MT.

EfG YAZINDUA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA JIJINI DAR ES SALAAM

December 01, 2017
 Mkurugenzi wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita akihutubia katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika Dar es Salaam jana Soko la Tabata Muslim.
 Mratibu wa Mradi wa Mpe Riziki Si Matusi, Susan Sita akimpatia fulana Mwakilishi wa Mbunge wa Segerea, Bonah Kaluwa aliyefika kwaniaba yake kama mgeni rasmi, Shanisudin Ahmed wakati wa uzinduzi huo.
  Mkurugenzi wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita, akimkaribisha mgeni rasmi katika uzinduzi.
 Mwenyekiti wa Soko la Tabata Muslim, Haji Mohamed akihutubia.
 Mratibu wa Mradi wa Mpe Riziki Si Matusi, Susan Sita, akihutubia.
 Wawezeshaji wa kisheria wa EfG wakiwa na furaha katika uzinduzi huo.
 Burudani ikitolewa.
 Burudani ikiendelea.


 Mkurugenzi wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita akihutubia
 mgeni rasmi, Shanisudin Ahmed, akihutubia wakati wa uzinduzi huo.
 uzinduzi ukiendelea.
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo
 Mkurugenzi wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita akiteta jambo na mgeni rasmi.
Mgeni rasmi akijumuika na wadau mbalimbali na wawezeshaji sheria wa shirika hilo.

Na Dotto Mwaibale

SHIRIKA la Equality for Growth (EfG) lenye makao makuu yake jijini Dar es Salaam, jana limezindua siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kama taifa na kuungana na mataifa mengine duniani katika maadhimisho hayo.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika Soko la Tabata Muslim Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa shirika hilo, Jane Magigita amesema kwa sasa EfG inaendesha mradi unaoitwa "MPE RIZIKI SI MATUSI" ambao umeongeza wigo wa mapambano ya ukatili wa kijinsia  katika Wilaya ya Ilala na Temeke katika masoko sita.

Ameyataja masoko hayo kuwa ni Mchikichini, Kisutu,Tabata Muslim, Feri, Gezaulole na Temeke Stereo.

Magigita aliongeza kuwa, lengo la mradi huo ni kuona wanawake wafanyabiashara wa Manispaa ya Ilala na Temeke wanafanyabiashara katika mazingira huru dhidi ya ukatili wa kingono, kimwili, matusi na kisiasa, vilevile kuona wanawake wakipewa heshima kama binadamu wengine ili waweze kujipatia kipato chao bila vikwazo.

SAVE THE CHILDREN YATOA MSAADA WA GARI,PIKIPIKI KUENDELEZA MAPAMBANO DHIDI YA UKATILI WA WATOTO SHINYANGA

December 01, 2017
Shirika la Kimataifa la Save The Children limetoa msaada wa gari aina ya Toyota Landcruiser katika Halmashauri ya Mji Kahama mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kusaidia ufuatiliaji wa matukio ya ukatili na unyanyasaji wa watoto. 

HOSPITALI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA PANGANI YAFANYA VIZURI KATIKA MPANGO WA MATOKEO MAKUBWA (B.R.N)

December 01, 2017
Hospitali ya Halmashauri ya wilaya ya Pangani imefanya vizuri katika mpango wa  matokeo makubwa sasa (B.R.N)kwa Kanda ya Kaskazini kutokana na utendaji kazi mzuri wa hospitali hiyo

Akizungumza leo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya Pangani Dokta Kombo Mhina amesema kuwa  hivi karibuni wametembelewa na wasimamizi kutoka Wizara ya Afya ambao hukagua utendaji kazi wa hospitali mbali  mbali nchini ambapo kwa hospitali hiyo wamepata nyota tatu na alama 72.

“Katika hili tumejitahidi  vyakutosha  tunamshukuru  mungu hospitali yetu imepata  nyota  tatu na alama 72 na kwa mwaka jana tulipata nyota  tatu pia  lakini ilikuwa  na alama 67 kwa hiyo tumebakiza point chache tufikie alama za juu zaidi” alisema dokta kombo
Katika hatua nyingine  dokta Kombo amesema pia wametembelewa na usimamizi wa Safe Carekutoka Wizara ya Afya na mara baada ya kufanya ukaguzi wao waliona kuwa wamefanya vizuri na kuwakabidhi zawadi ya ngao.

“Na katika safe care baada ya ufanisi nakuonekana tunafanya tulipewa  zawadi ya ngao na wawakilishi kutoka wizara ya afya”alisema dokta kombo

Wasimamizi hao kutoka Wizara ya Afya huwa wanapita katika hospitali mbali mbali nchini Tanzania ili kuona utendaji kazi wa watumishi wa Idara ya Afya katika kutoa huduma kwa wananchi na kuangalia namna wahudumu  wa afya wanavyojilinda na kuwalinda wagonjwa  wasiweze kupata maambukizi yoyote.

MAMLAKA YA MAJI PANGANI MJINI( PAWASA) INAWAOMBA RADHI WATEJA WAKE

December 01, 2017
Na Kelvin Mpinga,Pangani

MAMLAKA ya maji Pangani mjini( PAWASA) inawaomba radhi wateja wake kwa usumbufu kutokana na tatizo la kuharibika kwa mashine ya kupandishia maji iliyopo kijiji cha Boza wilayani humo.

Akizungumza na Mwandishi wa Habari wa Blog hii,Kaimu Meneja Mamlaka ya Maji Pangani mjini John Kisiwa (Pichani) amesema kuwa kwa kipindi kifupi kutakuwa na upatikanaji mdogo wa maji kutokana na hitilafu iliyojitokeza kwenye mashine inayotegemewa.

“Napenda kuuatarifu  umma kuwa tumepata  hitilafu katika  mashine yetu kubwa ambayo tunaitegemea ya uzalishaji  maji pale  boza  lakini  jitihada kubwa  zinafanyika  ili huduma hii iweze kurejea katika hali  ya kawaida hivyo  tutakuwa  na changamoto  ya upatikanaji wa  maji kwa  vipindi hivyo tunaomba radhi sana kwa wateja wetu”Alisema bwana kisiwa.

Kisiwa ameongeza kuwa kwa sasa mashine tayari iko kwa fundi kwaajili ya matengenezo  na kusisitiza kuwa  tatizo hilo litaisha kwa muda mfupi pale matengenezo yatakapo kamilika.
 
“Kwasasa  tumefanikiwa  kuitoa  ile mashine na tayari ipo kwa  mtaalamu ambaye anaendelea kuishughulikia sasa kiukweli  hilo linategemea sana na mtaalamu lini atatupa  majibu tayari amefanikisha lakini  tunaamini ndani ya kipindi kifupi tayari itakamilika  na imeshasukwa imekaa vizuri na huduma"

SHIRIKA LA UZIKWASA KURATIBU SHINDANO LA KAMATI BORA YA KUDHIBITI UKIMWI YA KIJIJI (VMAC),MWANAMKE BORA WA MFANO NA KIJANA BORA WA MFANO

December 01, 2017
SHIRIKA la Uzikwasa limesema bado linaendeleo na utaratibu wake wakuratibu mashindano makuu matatu ambayo ni kamati bora za kudhibiti ukimwi za vijiji,mwanamke bora wa mfano wa kuigwa  na kijana bora wa mfano wa kuigwa.

Hayo yamesemwa na  mratibu wa masula ya jinsia na uongozi wa shirika hilo Salvata Kalanga  wakati akiwa katika kipindi cha asubuhi ya leo kinachorushwa na kituo hiki ambapo amevitaja baadhi ya  vigezo vya shindano la mwanamke bora .

“kigezo cha kwanza tunamuangali mwanamke mwenye ujasiri na udhubutu wa kuhoji na kuchangia shughuli zakimaendeleo,mwanamke mwenye uwezo wakufichua kutoa taarifa na kufuatilia matukio ya kikatili  na unyanyasaji wa kijinsia unaofanyika katika jamii,mwanamke mwenye kujishughulisha na shughuli mbalimbali za kimaendeleo zinazonekana na kutambulika si mwanamke anaekaa  nyumbani tu na kusubiri kupewa’’ aliendelea kutaja vigezo nyengine ambavyo ni 

‘‘mwanamke mwenye udhubutu na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi pindi zinapotokea ,na mwanamke anaetetea haki za wanawake na za jamii kwa ujumla’’ alisisitiza Salvata

Kwa upande wa shindano la kijana bora amevitaja vigezo  na miongoni mwa vigezo hivyo ni umri kati ya miaka 18 hadi 35 ambapo akivitaja vigezo hivyo

‘‘Awe kijana anaeshawishi vijana wenzake katika sughuli za kimaendeleo,awe jasiri na kushiriki katika nafasi mbalimbali za kiungozi,kijana asiye na makundi na anae nyumbulika,na kwendana na wakati wa sasa katika kufichua na kufuatilia matukio ya kikatili’’ aliendele kusisi tiza bi salvata kuwa  

ALLY AIBUKA MWENYEKITI WA UCHUKUZI SC

December 01, 2017
Bw. Hassan Ahmad (kulia) aliyesimama akiomba kura kwa wapigakura wa klabu ya michezo ya Uchukuzi, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la Kwanza la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TB1).
Katibu aliyemaliza muda wake Bw. Alex Temba akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali mbele ya wapigakura wa klabu ya Uchukuzi kabla ya kufanyika uchaguzi kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la Kwanza la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TB1). Aliyeshika chupa ya maji mbele ni Kocha Kenneth Mwaisabula ‘Mzazi’ akimsikiliza kwa makini
Bw. Mbura Tenga (mbele aliyesimama) akimwaga sera zake kwa wapigakura wa klabu ya Uchukuzi uliofanyika kwenye ukumbi wa Jengo la Kwanza la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBI).
Wachezaji wa timu ya Uchukuzi wakihesabu kura za Katibu Mkuu mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi uliofanyika kwenye ukumbi wa Jengo la Kwanza la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.

      

                       Na Mwandishi Wetu
MWENYEKITI aliyemaliza muda wake wa Klabu ya michezo ya Sekta ya Uchukuzi ,  Mohamed Ally ameshinda kwa kishindo kwa kutetea nafasi yake katika  uchaguzi wa klabu hiyo uliofanyika kwenye ukumbi wa Transit wa Jengo la Kwanza la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa (JNIA-TBI) kwa kupata kura 113.
Hatahivyo, Ally pamoja na kupigiwa kura nane (8) za hapana na sita (6) zikiharibika hakuwa na mpinzani baada ya aliyejitokeza awali Bw.Emmanuel  Tumaini kujitoa dakika chache kabla ya kuingia kwenye ukumbi wa mkutano wa uchaguzi.
Bw. Hassan Ahmad ameshinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti kwa kupata kura 71 akiwashinda Hamis Mussa (57) na Neema Makassy (8); huku Katibu Mkuu akichaguliwa Mbura Tenga (73) aliyewashinda Katibu aliyemaliza muda wake Alex Temba (46), Ramadhani Kalima (5) na Leonard (2).
Bw. Mrisho Harambe ameweka rekodi kwa kushinda kwa kura 124 katika nafasi ya Katibu Msaidizi ambapo zikiwa ni kura nyingi zaidi walizopata wagombea wengine wa nafasi mbalimbali; na alimshinda Saidi Marusu aliyepata kura nane (8).
Mweka Hazina alichaguliwa Bw. Benjamin Bikulamti (87) aliyemshinda Wilson Magesa (42); huku wajumbe watano waliochaguliwa kutoka katika 14 walioomba kura ni Hilda Mwakatobe (75), Kurwa Sanga (72), Burton Willy (71), Evarist Mmanda (56) na Siraji Silimu (53).