January 24, 2014

*RAIS KIKWETE AONGOZA WANANCHI WA MIONO JANA KATIKA MAZIKO YA ALIYEKUWA MBUNGE WA CHALINZE, RAMADHAN BWANAMDOGO.

 Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (kushoto) na Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, wakati wakiwa katika maziko ya aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki dunia juzi.
Rais Jakaya Kikwete, akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, kwa tiketi ya CCM, Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki dunia juzi. Maziko ya marehemu Bwanamdogo, yamefanyika kijijini kwake Chalinze Miono, Wilaya ya Bagamoyo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, kwa tiketi ya CCM, Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki dunia juzi. Maziko ya marehemu Bwanamdogo, yamefanyika kijijini kwake Chalinze Miono, Wilaya ya Bagamoyo.
 Rais Jakaya Kikwete, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, kwa tiketi ya CCM, Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki dunia juzi. Maziko ya marehemu Bwanamdogo, yamefanyika kijijini kwake Chalinze Miono, Wilaya ya Bagamoyo.
January 24, 2014

MSIMU WA PILI SOKOINE MARATHON KUFANYIKA APRILI 12, 2014, WILAYANI MONDULI

Mwaka huu Tanzania inaadhimisha miaka 30 tangu kifo cha aliyekuwa waziri mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. Jakaya Kikwete atakuwa mgeni rasmi katika dhifa hiyo itakayofanyika kitaifa Monduli mahali alipozaliwa kiongozi huyo shupavu.

Madhumuni ya kuandaa mbio hizo ni kuthamini bidii,  uzalendo na ujasiri aliotuonyesha wakati wa uhai wake.

Watanzania wote wanaojali utu, haki, amani na Utaifa Kwanza mnakaribishwa katika kumbu kumbu hiyo. ‘Tujikumbushe baadhi ya nukuu zake akiwa waziri mkuu’
 
“Ole wake kiongozi mzembe na asiye na nidhamu nitakayemkuta: Kiongozi wa siasa hana usalama wa aina yoyote. Usalama wake ni kudra ya Mungu na Wananchi peke yake. Viongozi wazembe na wabadhirifu wahesabu siku zao. Labda tusiwajue. Hawa hatuna sababu ya kuwapa imani, kuwa tutawalinda kama vitendo vyao viovu” - Edward Moringe Sokoine, 26 Machi 1983.

“Katika nchi inayojali haki na usawa, majeshi hayana budi yawe ni chombo cha kulinda haki na maslahi ya walio wengi. Na kamwe hayaruhusiwi kuwa ni chombo cha wachache wenye kujali nafsi zao na kusahau maslahi ya walio wengi” - Edward Moringe Sokoine, 1 Februari 1977.