MBUNGE MGIMWA AMEKABIDHI MIFUKO 400 YA SARUJI NA BATI 150 KWA AJILI YA UJENZI NA UKARABATI WA MAJENGO YA SHULE NA ZAHATI ZA KATA YA MAPANDA

December 29, 2017
Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mahamoud Mgimwa akiwa na diwani wa kata ya Mapanda Obed Kalenga na mwenyekiti wa kijijicha Ihimbo wakati wa kueleza vitu gani ambavyo amevifanya kwenye kata hii kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa kata ya Mapanda
Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mahamoud Mgimwa akiwa kwenye moja ya darasa ambalo litakarabatiwa kutumia mfuko wake wa jimbo ili liwe kwenye kiwango kinachotakiwa
Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mahamoud Mgimwa  akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua majengo ya shule na kuangalia majengo yapi yanastahili kukarabatiwa
 Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mahamoud Mgimwa akiwa kwenye moja ya zahati ambayo inatakiwa kufanyiwa ukarabati ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa kata ya Mapanda

 Na Fredy Mgunda,Mufindi.

Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mahamoud Mgimwa   amekabidhi  jumla ya mifuko ya saruji 400 na bati 150 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa madarasa ya shule za msingi pamoja na zahati za Kata ya Mapanda kwa lengo la kuboresha maendeleo ya wananchi wa jimbo hilo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, alisema kuwa niliomba kuwa mbunge kwa lengo la kuwatumikia wananchi hivyo najitahidi huku na kule kuhakikisha natimiza azma yangu ya kuleta maendeleo kwa wananchi wa jimbo la Mufindi Kaskazini.

“Nimetoa jumla ya mifuko ya saruji 400 na bati 150 kwa ajili ya kuhamasisha ujenzi na ukarabati wa madarasa katika shule na zahati za kata hii ikiwa ni mwamzo tu nitaendelea kutoa saruji nyingine na bati hata vitu vingine ili kulifanya jimbo la Mufindi Kaskazini kupata maendeleo kwa kasi” alisema Mgimwa

Mgimwa alisema kuwa halmashauri ya Mufindi imeshaanda mpango kabambe ambao utakuwa msaada mkubwa kuchochoe maendeleo kwa kasi huku serikali ikiendelea kufanya jitihada za kuhakikisha wananchi wanapata maji ya kutosha na kuitumia vizuri ardhi ya halmashauri hiyo kwa kufanya maendeleo.

“mimi lengo langu inapofika kipindi cha uchaguzi ninakuwa nimetatua kero zote za wananchi na kujihakikishia napewa ridha ya kuongoza kipindi kingine kwa maendeleo ya wananchi wa jimbo la mufindi kaskazini na kuongeza kuwa hatakusikia kuwa kuna kitu kinasababisha migogoro ya kugombea ardhi katika jimbo hili la Mufindi Kaskazini” alisema Mgimwa

Aidha Mgimwa alisema kuwa shule na zahanati zilizopata saruji na mabati ni shule za kijiji cha Mapanda,shule ya kijiji cha Uhafiwa,Ukama,Ihimbo na Chogo lengo ni kuchochoe kuleta maendeleo kwa wananchi.

Mgimwa amewapongeza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo katika kata na ametoa ahadi ya kuendelea kushirikiana kwa kuchangia ujenzi wa shule zote za jimbo la Mufindi Kaskazini na kutatua kero nyingine za wananchi wa jimbo hilo.

Obedi Madembo, Peter Kaguo, Kristopher Ngunda,Thobias Luvinga na Fransisco Mfaume ni wenyeviti wa vijiji vya kata ya Mapanda walimpongeza mbunge huyo kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwatafutia wananchi mandeleo kwa kutumia nguvu zake zote.

“Hata ukiangalia mwandishi utagundua gharama alizozitumia mbunge zimewaondolea wananchi kuchangia kabisa hivyo bila mbunge huyu mzigo wote huu ulikuwa unawaangukia wananchi wa vijiji vyote vya kata ya Mapanda” walisema wenyeviti wa vijiji vya kata ya Mapanda

Kwa upande wake diwani kata ya Mapanda Obed Kalenga alimshukuru kwa kazi kubwa aliyoifanya na kuwataka wananchi kuendelea kumuunga mkono mbunge huyo ili andelee kufanya kazi ya kuwatafutia maendeleo wananchi wa kata ya Mapanda na jimbo la Mufindi Kaskazini kwa ujumla.

“Wananchi kweli wananjitoa sana kufanya kazi za kuleta mandeleo hiyo wanapoona kuwa mbunge naye anatumia nguvu kubwa kufanya maendeleo kutaongeza chachu ya kufanya kazi kwa kujitolea kwenye shughuli za kimaendeleo hata mchakato ulivyokuwa hadi kupelekea kushirikiana na wananchi kuanzisha ujenzi na ukarabati wa shule na zahati ili kuendelea kutoa elimu bora kwa wanafunzi wa kata hiyo na kupatikana kwa huduma za afya bora kwa wananchi wote” alisema Kalenga

MWANJELWA ATOA SIKU MOJA KWA WAFANYABIASHARA WALIOFUNGA MAGHALA YA MBOLEA LA SIVYO KUNYANG'ANYWA LESENI

December 29, 2017
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa (Katikati) akikagua mbegu zilizohifadhiwa ghalani kabla ya kuanza kusambazwa alipotembelea Wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seeds Agency-ASA) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro, Leo 29 Disemba 2017. Wengine ni Kaimu Mkurugenzi Wakala wa Mbegu Dkt Sophia Kashenge Kilenge (Kulia) na Meneja uzalishaji Wakala wa Mbegu Ndg Charles Levi (Kushoto). Picha Zote Na Mathias Canal 
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana na Mkurugenzi Wakala wa Mbegu Dkt Sophia Kashenge Kilenge alipotembelea Wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seeds Agency-ASA) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro, Leo 29 Disemba 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo baada ya kukagua baadhi ya mashine za mbegu alipotembelea Wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seeds Agency-ASA) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro, Leo 29 Disemba 2017. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua namna mbegu za mazao mbalimbali zilivyohifadhiwa alipotembelea Wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seeds Agency-ASA) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro, Leo 29 Disemba 2017. 

Na Mathias Canal, Morogoro

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa leo Disemba 29, 2017 amewaagiza wafanyabiashara wa mbolea kote nchini walioweka mgomo wa kupeleka mbolea kwa wakulima kufikia 30 Disemba 2017 wawe wamefungua maghala yao kwa ajili ya kuwauzia mbolea wakulima.

Alisema endapo wafanyabiashara hao wasipofanya hivyo serikali itawanyang'anya leseni zao haraka iwezekanavyo ili kuruhusu wafanyabiashara wenye uwezo wa kufanya jukumu hilo pasina kuwaumiza wakulima kutokana na bei ghali ya mbolea.

Mhe Mwanjelwa ametoa agizo hilo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro alipotembelea Wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seeds Agency-ASA) Mara Baada ya kubaini kuwa kuna wafanyabiashara ambao wameanza kufunga maghala kwa madai ya kupanda kwa mbolea katika soko la Dunia.

Alisema kuwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria na kuijaribu serikali kwani malalamiko yao ya kupanda kwa bei katika soko la Dunia hayana tija kwani mbolea zote zilipo nchini tayari wakishanunua kipindi soko likiwa kwenye unafuu mkubwa.

Alisema kuwa serikali ilitoa bei elekezi katika mbolea ya kukuzia na kupandia ikifahamu fikra kuwa kupitia gharama hiyo wakulima watanufaika lakini pia wafanyabiashara watanufaika kutokana na faida wanayoipata lakini wameamua kubadili utaratibu wa kutaka kupata faida kubwa zaidi pasina kujali wakulima wataumizwa na bei hiyo kwa kiasi gani.

Mhe Mwanjelwa ameitaka kampuni ya Premium ambayo ni moja ya kampuni zilizogoma kufungua maghala na kupeleka mbolea kwa wakulima kwa bei elekezi iliyotolewa na serikali.

Alisema kuwa wafanyabiashara hao kwa makusudi wameamua kufifisha juhudi za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli ya kuwakomboa wakulima kupitia gharama nafuu ya mbolea hivyo kufikia kesho wasipofungua maghala hayo watanyang'anywa leseni zao ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa sheria.

DC, MBUNGE MUHEZA WASHIRIKIANA NA WANANCHI KUANZA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA HIYO

December 29, 2017
 Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo akichimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya wilaya hiyo itakayojengwa eneo la Kijiji cha Lusanga wilayani humo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo Like Gugu wakishuhudia tukio hilo
 Mbunge wa Jimbo la Muheza,Balozi Adadi Rajabu akichimba mtaro kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo eneo la Lusanga wilayani humo kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo,Like Gugu
 Sehemu ya wananchi wakishiriki katika uchumbaji wa msingi kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Muheza Mkoani Tanga
 Mbunge wa Jimbo la Muheza,Balozi Adadi Rajabu akishiriki kubeba tofali kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali itakayojengwa eneo la Kijiji cha Lusanga wilayani Muheza

 Sehemu ya wadau wa maendeleo wilayani Muheza wakishiriki kwenye zoezi la ubebaji wa matofali wilayani humo
 Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa tatu kutoka kulia akiwa na Mbunge wa Jimbo la Muheza Balozi Adadi Rajabu wa pili kutoka kulia wakipokea mifuko 600 ya saruji kutoka kwa kampuni ya Lucky Cement ya Kisarawe Mkoani Pwani kwa ajili ya kuanza ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza kushoto  ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza,Like Gugu
 Sehemu ya shehena ya saruji ambayo ilishushwa kwa ajili ya kuanza ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza
 Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kupokea saruji hiyo ambapo aliishurku kampuni hiyo huku akiyataka makampuni mengine yaliyopo mkoani hapa kuunga mkono jitihada hizo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Muheza,Balozi Adadi Rajabu kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza,Like Gugu
 Mbunge wa Jimbo la Muheza,Balozi Adadi Rajabu akizungumza katika halfa hiyo ambapo aliishukuru kampuni hiyo kwa kuamua kuwasaidia ujenzi huo huku akiyataka makampuni mengine kuiga mfano huo
Meneja Masoko wa Kampuni ya Lucky Cement iliyopo Kisarawe,Emanuel Muya akizungumza na waandishi wa habari kuhusu azma yao ya kusaidia mifuko ya saruji 600 kwa ajili ya ujenzi wa Hospital ya wilaya ya Muheza kushoto ni Mkuu wa wilaya hiyo,Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Muheza,Balozi Adadi Rajabu na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza,Like Gugu 
 
MKUU wa wilaya ya Muheza, Mhandisi Mwanasha Tumbo,Mbunge wa Jimbo hilo,Balozi Adadi Rajab na wakazi wa wilaya hiyo  wakishirikiana kwa pamoja wameanza kuchimba msingi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya katika Kijiji cha Lusanga Kata ya Lusanga ambayo itasaidia kuondoa changamoto ya kutokuwepo kwa kipindi cha miaka 37.
Hatua ya viongozi hao ina lengo la kuandika historia tokea wilaya hiyo ilipoanzishwa mwaka 1974 ambapo wananchi walikuwa wakitegemea kupata huduma za matibabu kwenye hospitali ya Teule Muheza kutoka maeneo mbalimbali kabla ya kufikiria kuanzishwa kwa hospitali hiyo ambayo itakayogharimu zaidi ya bilioni 11.
Akizungumza wakati akishiriki zoezi la uchimbaji wa mtaro wa Hospitali hiyo na kupokea mifuko ya saruji 600 ya Lucky kutoka kwa Kampuni ya kuzalisha Saruji ya Kisarawe, Mhandisi Mwanasha alisema waliamua kufanya hivyo kutokana na kuwepo kwa changamoto ya huduma ya afya ambayo ilimlazimu wakati ameteuliwa kuiongozi wilaya hiyo kukutana na wadau kuweza kuona namna ya kuweka mikakati ya kupatikana kwake.
Aidha kutokana na kuwepo kwa hospitali ya wilaya walikuwa wakilazimika kutimia hospitali ya teule Muheza tokea ilipoanzishwa lakini imeonekana kuzidiwa na watu wanaohitaji huduma hasa ukizingatia pia zahanati na vituo vya afya vipo vichache huku wananchi wakiongezeka.
“Nilibaini changamoto ya hospitali ya wilaya wakati nilipokuwa nikifanya vikao kwa kuzunguka kata zote nikaona tatizo la huduma ya afya ni kubwa sana na hivyo kuonekana kuna haja ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza lakini hata kwenye baraza la madiwani suala hilo lilizungumzwa”Alisema
Mkuu huyo wa wilaya alisema baada ya kufikiria wazo hilo la ujenzi wa hospitali hiyo waliona wafanya mazungumzo na Agro Tan ambao wanamiliki Shamba la Muheza Estate ambao walikubali kutoa eneo lao la ekari 100 kwa ajili ya ujenzi huo.
Awali akizungumza katika eneo hilo,Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu alisema juzi ilikuwa  ni siku muhimu sana kwao kutokana na wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye msaragambo kwa nia ya kujengwa hospitali ya wilaya ambacho kilikuwa kilio chao kwa muda mrefu.
 Alisema waliamua kuanzisha mchakato wa ujenzi wa hospitali hiyo baada ya kuona huduma ambazo zilikuwa zikitolewa katika hospitali ya Teule Muheza kuelemewa kutokana na watu kuongezeka huku maradhi yakiwa mengi kila wakati na ndio walipoamua kuchukua uamuzi huo.
Mbunge huyo alisema wananchi wa wilaya hiyo waliposikia mipango ya kuwepo kwa ujenzi huo walianza kujitolea fedha kiasi cha elfu mbili ikiwemo kushiriki kwenye uchimbaji wa msingi wa ujenzi wa hospitali hiyo tokea alfajiri wakiunga mkono juhudi za serikali.
“Lakini pia nisema tunawashukuru kampuni ya Lucky Cement kwa kutukabidhi mifuko 600 ya saruji na tunategemea pia kuvitumia viwanda vilivyopo mkoani Tanga kwa lengo la kuongeza nguvu katika ujenzi wa hospitali ya wilaya yetu tunavifaa vya kutosha vya kuanzia tutaanza na baadae wataingiza kwenye bajeti kuiomba serikali iwasaidie”Alisema Mbunge huyo
Kwa upande wake,Meneja Masoko wa Kampuni ya Lucky Cement iliyopo Kisarawe,Emanuel Muya  alisema wao kama wadau wa maendeleo waliguswa na kuamua kuchangia ujenzi wa hospitali hiyo ili kuwasaidia wananchi kuondokana na changamoto za huduma ya afya katika wilaya hiyo.
Alisema kwa kutambua thamani ya maendeleo katika nchi ndio sababu kubwa iliyowasukuma kuamua kusaidia saruji hiyo kwa ajili ya kuanza mchakato wa ujenzi wa hospitali hiyo ambapo itakapokamilika itawasaidia kuwaondolea changamoto wananchi.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KUHUSU VITALU VYA UWINDAJI WA KITALII

December 29, 2017

MAVUNDE AZITAKA TAASISI BINAFSI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WATU WENYE ULEMAVU

MAVUNDE AZITAKA TAASISI BINAFSI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WATU WENYE ULEMAVU

December 29, 2017
IMG-20171229-WA0037
Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Anthony Mavunde akizungumza wakati wa kukabidhi fimbo kwa ajili ya watu wasioona mjini Dodoma,kushoto kwake ni mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dodoma Neema Majule na kulia kwake ni meneja wa Next Generation Microfinance Sospeter Kansapa.
IMG-20171229-WA0035
Naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu kazi,vijana na ajira Anthony Mavunde akimkabidhi fimbo mwenyekiti wa chama cha wasioona mkoa wa Dodoma Omari Lubuva ikiwa ni msaada uliotolewa na Next Generation Microfinance.
IMG-20171229-WA0032
Naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu kazi,vijana na ajira Anthony Mavunde akiwa na baadhi ya viongozi wa chama cha wasioona mkoa wa Dodoma na meneja wa Next Generation Microfinance wakijaribu kutumia fimbo zilizotolewa na taasisi hiyo kwa ajili ya watu wasioona mkoa wa Dodoma.
IMG-20171229-WA0029
Katibu wa chama cha wasioona(TLB)mkoa wa Dodoma Enock Mbawa akizungumza wakati wa kupokea msaada wa fimbo kwa ajili ya watu wasioona,kushoto kwake ni meneja wa Next Generation Microfinance Sospeter Kansapa na kulia kwake ni mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Dodoma Bill Chidabwa.
IMG-20171229-WA0030
Meneja wa Next Generation Microfinance Sospeter Kansapa akizungumza wakati wa kukabidhi fimbo kwa ajili ya watu wasioona mkoa wa Dodoma.
IMG-20171229-WA0027
Naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu kazi,vijana na ajira Anthony Mavunde akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa jumuiya za CCM mkoa wa Dodoma na wafanyakazi wa Next Generation Microfinance baada ya kukabidhi fimbo kwa ajili ya watu wasioona wa mkoa wa Dodoma.
……………..
NAIBU waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde leo amekabidhi msaada wa fimbo za kisasa thelathini (30)kwa ajili ya watu wasioona wa mkoa wa Dodoma huku akitoa rai kwa taasisi binafsi na jamii kuweka utaratibu wa kusaidia makundi yenye mahitaji.
Msaada huo umetolewa na taasisi inayojishughulisha na kutoa huduma ya mikopo(NEXT GENERATION MICROFINANCE).
Akikabidhi msaada huo Mavunde ambaye ni mbunge wa Dodoma mjini ameipongeza taasisi hiyo kwa kutumia faida waliyoipata kusaidia watu wenye mahitaji maalum jambo ambalo linapaswa kuwa chachu kwa taasisi nyingine pia.
“Ndugu zanguni mlichokifanya leo kina maana kubwa sio duniani tu bali hata mbinguni,mmeona ni busara kutumia faida mliyoipata kwa ajili ya kusaidia wenzetu wenye mahitaji badala ya kutumia kufanya party,naomba utaratibu huu usiishie leo tu bali muendelee kugusa na makundi mengine yenye uhitaji,”alisema Mavunde.
Katika kusaidia makundi hayo ameiomba pia taasisi hiyo kusaidia chama cha waandishi wa habari wa mkoa wa Dodoma ili waweze kuwa na ofisi yao inayoendana na hadhi ya makao makuu.
Ametoa rai pia kwa viongozi wa chama cha wasioona mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanagawa fimbo hizo kwa walengwa bila ya upendeleo wowote.
Akitoa neno la shukrani baada ya kupokea msaada huo katibu wa chama cha wasioona(TLB)mkoa wa Dodoma Enock Mbawa ameishukuru taasisi hiyo kwa kusaidia serikali kupunguza changamoto walizonazo na kuahidi  kuhakikisha fimbo hizo zinafika kwa walengwa waliokusudiwa.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi meneja wa Next Generation Microfinance Sospeter Kansapa amesema wameamua kuitikia wito wa rais John Magufuli wa kuwataka wadau wa maendeleo kote nchini kujitokeza kutoa mchango katika ustawi wa Taifa wakiamini kuwa fimbo hizo zitakuwa chachu katika kuleta maendeleo ya Taifa.
WAZIRI JAFO AVITAKA VITUO VYOTE VYA AFYA KUTENGENEZA BUSTANI ZA KUPUMZIKIA!

WAZIRI JAFO AVITAKA VITUO VYOTE VYA AFYA KUTENGENEZA BUSTANI ZA KUPUMZIKIA!

December 29, 2017
1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo(katikati) akikagua ujenzi wa miundombinu ya Afya katika Kituo cha Afya Makole kilichopo katika Manispaa ya Dodoma.
2
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo(Kushoto) akimsikiliza Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Makole kuhusiana na maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Afya.
3
Jengo la Maabara  kama linavyoonekana likiwa katika hatua ya Lenta.
4
Jengo la Wodi ya Kinamama kama linavyoonekana likiwa linefikia katika hatua ya Lenta.
5
Jengo la Chumba cha Upasuaji kama linavyoonekana likiwa katika hatua ya Lenta.
6JPG
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo(kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi(katikati) baada ya ukaguzi wa ujenzi wa miundombinu ya Afya Katika Kituo cha Afya Makole.
7
Ujenzi wa Chumba cha Kuhifadhia Maiti ukiwa katika hatua ya Lenta.
……………..
Nteghenjwa Hosseah, TAMISEMI.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amevitaka vituo vyote vya Afya Nchini sambamba na hospital za Wilaya kutengeneza bustani ya kupumzikia kwa wagonjwa wanaosubiria matibabu katika maeneo hayo.
Waziri jafo ameyasema hayo wakati akikagua Ujenzi wa miundombinu ya Afya katika Kituo cha Afya Makole kilichopo Manispaa ya Dodoma na kuutaka uongozi wa Kituo hicho kutenegenza bustani ya kisasa pamoja na kupanda miti ya kutosha ili kutunza matunzingira lakini kupendezesha eneo la hospital.
“Hili Agizo liende kwa Vituo vyote Nchini pamoja na Hospital za Wilaya zilizoko chini ya TAMISEMI kuhakikisha wanaekeleza maelekezo haya katika ameneo yote nataka hospital iwe sehemu ya kupa faraja mgonjwa kwa kupata huduma nzuri lakini pia kusubiria huduma hiyo katika maeneo yanayovutia wakati wote” Alisema Waziri Jafo.
Akikagua majengo matano yanayojengwa katika Kituo hicho cha Afya na kusimamiwa na TAMISEMI Waziri Jafo amesema ameridhishwa na Ujenzi wa miundombinu hiyo ya Afya katika Hospital ya Makole  kwani umefuata ramani zilizotolewa na Wizara, unajengwa kwa ubora na uko ndani ya muda wa Utekelezaji.
“Hivi ndio ninavyotaka wataalamu wangu kujiongeza katika baadhi ya maeneo mfano hapa Mmejenga Mabara kubwa kulingana na wingi wa wagonjwa mnaowahudumia kwa siku sasa sio kwa sababu ramani imeonyesha maabara ndogo basi kila mtu anafuata hivyo hivyo ni lazima tujiongeze kulingana na mahitaji ya ameneo yetu ya huduma” Alisema Waziri Jafo.
Akizungumzia maendeleo ya mradi Mganga Mfawidhi wa  Kituo cha  Afya Makole  amesema Ujenzi huu umesema ujenzi wa Maabara, chumba cha Upasuaji, Wodi ya Kina Mama, Nyumba ya Mganga pamoja na Ukarabati wa Kichomea Taka utakamilika mapema mwezi February 2017 na Fedha zilizopokelewa kwa ajili ya ujenzi huo zitatosha na kukamilisha ujenzi wa miundombinu yote.
Kituo cha Afya Makole ni miongoni mwa vituo 211 Nchini vilivyopokea/vitakavyopokea  Fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya Afya lengo ikiwa ni kuboresha Miundombinu ya Afya ili kuweza kutoa huduma bora kwa watanzania.
TAMISEMI YA WANANCHI.