RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA RASMI BARABARA YA BARIADI-LAMADI KM 71.8 BARIADI NA KUWAHUTUBIA WANANCH WA MKOA WA SIMIYU

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA RASMI BARABARA YA BARIADI-LAMADI KM 71.8 BARIADI NA KUWAHUTUBIA WANANCH WA MKOA WA SIMIYU

January 11, 2017
bari
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwe la ufunguzi wa barabara ya Bariadi-Lamadi yenye kilometa 71.8 wengine katika picha ni  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Luhaga Mpina, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, Mwenyekiti wa CCM Simiyu Titus Kamani na Mbunge wa Bariadi Andrew Chenge.
keti
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe  na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka pamoja na Waziri wa Ujenzi Profesa Makame Mbarawa kuashiria ufunguzi wa barabara ya Barabara ya Bariadi-Lamadi yenye kilometa 71.8.
pogia
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa Bariadi mara baada ya kumaliza kufungua barabara ya Bariadi-Lamadi yenye urefu wa kilometa 71.8.
hutu
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Bariadi kabla ya kufungua rasmi barabara ya Bariadi-Lamadi, katika mkoa wa Simiyu. PICHA NA IKULU

MUFTI AWATAKA WAISLAMU KUOMBA NCHI IPATE MVUA IONDOKANE NA UKAME NA BAA LA NJAA

January 11, 2017
 Msemaji wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania, Sheikh Khamis Said Mataka (katikati), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kwa niaba ya Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Bin Zubeir Bin Ali, kuhusu waislamu kote nchini kuiombea nchi ipate mvua na iondokane na ukame na baa la njaa. Kulia ni Katibu Mkuu wa Bakwata aliyemaliza muda wake, Suleiman Lolila na kushoto ni Mshauri Mkuu wa Mufti, Sheikh Abubakar Ali.
 Mshauri Mkuu wa Mufti, Sheikh Abubakar Ali (katikati), akizungumza katika mkutano huo.
 Katibu Mkuu wa Bakwata aliyemaliza muda wake, Suleiman Lolila (kushoto), akitangaza rasmi kustaafu wadhifa huo.
 Mkurugenzi wa Daa'wa na Tabligh Bakwata Makao Makuu Sheikh Hassan Said Chizenga (wa pili kushoto), akiongoza dua maalumu katika mkutano huo.
 Dua likifanyika.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
 Wanahabari wakiwa kazini.
Wapiga picha wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale

WAISLAM nchini wametakiwa kuomba nchi ipate mvua ili kuondokana na ukame na kuepusha baa la njaa.

Mwito huo umetolewa na Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Bin Zubeir Bin Ali wakati ukitolewa kwa niaba yake na Msemaji wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania, Sheikh Khamis Said Mataka wakati akizungumza na wanahabari Dar es Salaam leo.

"Taarifa mbalimbali zinaashiria nchi kukabiliwa na ukame kwa kukosa mvua za msimu zilizotarajiwa kutokana na hali hiyo Mufti anawaomba Masheikh, Maimamu na Waislamu wote kwa ujumla kuleta toba,kumuomba msamaha Mwenyezi Mungu ili 
aijaalie nchi yetu na nchi jirani zetu kupata mvua za kheri zitakazotusaidia kutuepushia ukame na madhara yake ikiwemo baa la njaa" alisema Sheikh Mataka.

Katika hatua nyingine Mufti wa Tanzania  amewateua Mwenyekiti wa Halmshauri Kuu Bakwata Taifa, Sheikh Khamis Said Mataka na Mkurugenzi wa Daa'wa na Tabligh Bakwata Makao Makuu Sheikh Hassan Said Chizenga kuwa wasemaji rasmi wa Baraza
Kuu la Waislamu wa Tanzania (Bakwata) uteuzi ambao umeaanza mara moja.

Akizungumzia matumizi ya wadhifa wa Sheikh Mkuu alisema kumekuwa na matumizi yasiyosahihi kwa baadhi ya masheikh wa mikoa na wilaya kujiita masheikh wakuu wa maeneo hayo.

Alisema wadhifa wa Sheikh Mkuu ni Mufti pekee na si vinginevyo na akasisitiza kuwa masheikh wa mikoa na wilaya na mitaa wanakumbushwa kutumia nyadhifa zao kama ilivyoainishwa katika katika ya Bakwata.

Katika mkutano huo aliyekuwa Katibu Mkuu wa Bakwata Sheikh Suleiman Lolila alitumia fursa hiyo kutangaza rasmi kustaafu kutokana na kutumikia nafasi hiyo kwa muda mrefu na kuwa na umri mkubwa.

Nafasi hiyo hivi sasa itashikiliwa kwa muda na Ustadhi Salm Ahmed.


KAMANDA WA POLISI KILIMANJARO,SACP MUTAFUNGWA AKAGUA UJENZI WA KITUO CHA POLISI URU

January 11, 2017
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,SACP,Wilbroad Mutafungwa (kushoto mwenye fimbo) akizungumza jambo wakati akikagua maenedeleo ya ujenzi wa kituo cha Polisi cha Kimanganoni Uru wilaya ya Moshi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro akikagua ujenzi wa kituo cha polisi kinachojengwa kwa nguvu za wananchi eneo la Uru Kimanganoni kati. Kushoto ni askari mstaafu,mkazi eneo hilo Philipo mushi akimpokea Mutafungwa .

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

Sabodo: Ukaribu wangu na Mwl. Nyerere uliokoa Taifa

January 11, 2017
 Mfanyabiashara maarufu, Mustafa Jaffar Sabodo
 Baba wa Taifa, Hayati Julius Kambarage Nyerere
Aliyekuwa Kiongozi wa Taifa la Iran, Ayatolah Khomein 

Mwandishi Wetu
HAKIKA ukitaja jina la Mustafa Jaffer Sabodo, siyo geni masikioni mwa Watazania wengi.

Hii ni kutokana na mchango wake kwa jamii katika kuliondoa taifa kutoka sehemu moja ya chini kwenda juu, yaani maendeleo.

Sabodo mfanyabiashara maarufu ambaye ni Mtanzania mwenye asili ya Asia amekuwa akitoa mchango kwa maendeleo ya Taifa katika nyanja mbalimbali kuanzia za uchumi, siasa, elimu, afya na maji.

Mfanyabiashara huyo ambaye ni mzaliwa wa mkoani Lindi takriban miaka 73 iliyopita amejitolea kujenga shule mbalimbali nchini, hospitali, visima vya maji hata kufadhili shughuli za kisiasa na kiuchumi.

Michango yake hiyo kwa jamii ya Watanzania, imefanya jina lake kuandikwa katika mioyo ya wananchi wengi kwani alidhirisha tabia yake isiyojificha ya uzalendo kwa Taifa lake Tanzania.

Sabodo anatajwa kuwahi kuvifadhili vyama vya siasa vya CCM na Chadema kwa nyakati tofauti.

Pia anatajwa kwamba alikuwa rafiki wa karibu wa Mwalimu Julius Nyerere na wanasiasa mbalimbali nchini hata kuwahi kutumwa kwenda nchini Iran kukutana na kuomba mafuta kwa aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo la Kiislamu, Ayatolah Khomein katika miaka ya 1970 baada ya taifa kukumbwa na uhaba wa mafuta uliochagizwa na sababu mbalimbali ikiwamo ukosefu wa fedha za kigeni.

Hali hiyo ilitokea kipindi hicho wakati dunia ilikuwa bado ikishuhudia mgawanyiko kwa baadhi ya nchi kuegemea Marekani kisiasa na kimfumo, nyingine zikifuata mfumo wa iliyokuwa Muungano wa nchi za Kisovieti za Urusi (USSR).

Si hivyo tu kwa kusoma alama za nyakati, baadhi ya nchi zilikaa kando na utengano huo na kuanzisha Jumuia ya Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote.

Miungoni mwa mataifa yaliyofuata siasa za kutofungamana na upande wowote, Tanzania wakati huo chini ya uongozi wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ilikuwa mojawapo.

Tofauti hizo za kisiasa hata kidini kati ya mataifa zilisababisha athari zilizozaa tofauti ya hali hasa kiuchumi na kisiasa hata baadhi ya nchi kuingia kwenye mahangaiko ikiwamo Tanzania iliyokumbwa na uhaba wa mafuta ya Petroli na fedha za kigeni.

Sabodo anasimulia kwamba kufuatia hali hiyo iliyoilazimu Serikali kuzuia magari yake kutembea Jumapili huku Jumamosi yakitembea hadi saa nane mchana, alipata nafasi ya kukutana na Rais Nyerere.

Anasimulia kwamba katika mazungumzo hayo alimwabia Rais Nyerere haja yake ya kutaka kwenda Iran kuomba mafuta.

“Nikamwambia wacha niende Iran. Nilifanya hivyo nikiamini Khomein atanisikiliza. Nakumbuka nilikwenda na Chifu Adam Sapi Mkwawa,” anasema.

Anasimulia: “Mimi ni Khoja, Mwislamu wa dhehebu la Shia na Khomein pia, nilipokutana naye, nikamwambia wanaoteseka Tanzania kwa shida ya mafuta wamo piaWaislamu wa Shia wengi tu.”

“Nilimwambia Tanzania ni nchi nzuri haina ubaguzi na Rais Nyerere ni mtu mwema, hata Waziri Mkuu wake ni Rashid Kawawa na Waziri wa Madini na Mafuta ni Anoor Kassam, nikamwangukia miguuni nikiliaa kuomba aipe nchi yetu mafuta, akakubali” anakumbuka Sabodo.

Hata hivyo, anasema licha ya kukubali, Khomein  akasema hawezi kumpa mafuta yeye Sabodo hadi watu wa Serikali ya Tanzania watakapofika Iran kuthibitisha ombi hilo.

“Nikarudi Tanzania na kumpa taarifa baba wa Taifa naye alimwambia Kawawa na John Malicela ikakubalika tukaenda tena Iran safari hii nikiwa na mawaziri wa Fedha, Cleopa Msuya, Anoor Kassam wa Mafuta na Usafirishaji pia alikuwepo Peter Noni kwa niaba ya Benki Kuu na Adam Sapi Mkwawa,” anasema.

Sabodo anakumbuka kuwa safari hiyo ilizaa matunda kwani Khomein aliipa Tanzania mafuta yenye thamani ya Dola za Kimarekani 80,000.

“Nakumbuka hapo urafiki wangu na Nyerere uliniwezesha kuliokoa Taifa kwa kupata mafuta baada ya kunituma kwenda Iran nilipomshauri,” anasema Sabodo ambaye wazazi wake alizaliwa Lindi.

Anakumbuka kuwa pia katika safari hiyo alimshauri Khomein kufungua ofisi ya Ubalozi wa Iran nchini naye alikubali na alifanya hiyo pia kwa Zambia, Tanzania nayo ikafungua ubalozi Iran.


Don’t forget to read my book; CORRUPTION IS CRUCIFICATION OF TANZANIA, which is in process

MWIMBAJI MPYA WA INJILI KANDA YA ZIWA, JIMMY GOSPO, AACHIWA WIMBO WAKE RASMI

January 11, 2017

Na George Binagi @BMG
Jimmy Gospo (pichani) ni mwanamziki mpya kwenye muziki wa injili nchini Tanzania. Kabla ya mwaka 2014 alikuwa akifanya muziki wa Bongo Fleva, akiwakilisha mkoa wa Geita na Kanda ya Ziwa kwa ujumla.

Baada ya mwaka 2014, Jimmy Gospo aliamua kugeuza uelekeo na kuanza kuimba nyimbo za injili kwenye matamasha mbalimbali ya injili hususani Kanda ya Ziwa. Baada ya hapo alianza kurekodi albamu yake ambayo hadi sasa jina liko kampuni.

Mwaka huu 2017 ameanza kuachia rasmi baadhi ya nyimbo zilizo kwenye albamu hiyo. Ameanza na wimbo uitwao "Nakujua Bwana" ambao hakika ni wimbo bora kusikiliza na hata mafundisho yake.

"Ni nyimbo nzuri kwa watu wengi hasa wale ambao tunatamani kuisikia faraja ya Bwana ikitenda na sisi. Niwakaribisheni watanzania wote tuisikilize Ninakujua Bwana, ni nyimbo nzuri na natumaini utaifurahia na kuipenda". Amesisitiza Jimmy.
Mwimbaji wa muziki wa injili, Jimmy Gospo (kulia), akizungumza na George Binagi-GB Pazzo wa BMG (kushoto), kuhusiana na ujio wake kwenye muziki huo, baada ya kuachana na muziki wa kidunia.
Sikiliza Mahojiano Hapa kusikiliza mahojiano.

MKURUGENZI TAASISI YA ILTC YA JIJINI MWANZA AOMBA SERIKALI KUZISAIDIA TAASISI BINAFSI ELIMU.

January 11, 2017
Na George Binagi-GB Pazzo
Taasisi ya lugha ya International Language Traing Centre iliyopo Isamilo Jijini Mwanza, imeiomba serikali kuzisaidia taasisi binafsi za kelimu nchini ili kutimiza vyema wajibu wake.

Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Mwalimu Charles Mombeki (pichani), ameyasema hayo wakati akizungumza na Lake Fm ya Mwanza na kuomgeza kwamba ikiwa serikali itafanya hiyo, itazisaidia taasisi hizo kutekeleza vyema wajibu wa kutoa elimu bora kwa wananchi.

Amesema si vyema serikali kuzifungia taasisi binafsi za kielimu ikiwemo shule na vyuo pindi zinapokabiriwa na changamoto za kielimu badala yake inaweza kuzisaidia katika kuondokana na changamoto hizo.

Taasisi ya International Language Training Centre inajihusisha na uendelezaji wa lugha mbalimbali ikiwemo lugha za asili, Kiswahili, kiingereza, kifaransa na nyinginezo.
Bonyeza hapa kusoma zaidi