SHEREHE MURWA YA JAMBO LEO YA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA 2016

January 16, 2016
 Baadhi ya wafanyakazi wa  Gazeti la Jambo Leo na familia zao, wakigongeana glasi zenye vinywaji ikiwa ni ishara ya kutakiana heri wakati wa hafla ya kuuaga mwaka 2015 na kuukaribisha ya Mwaka Mpya 2016, katika Mgahawa wa City Sports Lounge, Dar es Salaam
 Wafanyakazi wa Jambo Leo na familia zao pamoja na wageni waalikwa wakiburudika kwa muziki uliokuwa ukiporomoshwa wakati wa hafla hiyo iliyofanyika kwenye Mgahawa wa kisasa wa City Sports Lounge, katikati ya Jiji la Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA
 Mhariri wa Michezo na Burudani wa Gazeti la Staa Spoti ambalo ni gazeti dada la  Jambo Leo, Zahoro Mlanzi akigawa 'champagne' kwa wafanyakazi wenzake wakati wa hafla hiyo.
 Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Richard Mwaikenda (wa pili kulia), akijadiliana jambo na wakurugenzi wa Kampuni za Jambo Concerpts Tanzania Limited na Jambo Communication, Theophil Makunga (kushoto), Benny Kisaka (wa pili kushoto) na Juma Pinto wakati wa hafla hiyo.
 Baadhi ya wafanyakazi wa gazeti la Jambo Leo, wakiwa na furaha wakati wa hafla hiyo ya kuuaga mwaka 2015 na kuukaribisha Mwaka Mpya 2016, Dar es Salaam juzi. Kutoka Kushoto ni Stellah Kessy,  Magendela Hamis, Salha Mohamed, Celina Mathew, Suleiman Msuya na Edith Msuya.



 Wakipata mlo wa usiku




 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concepts, Juma Pinto  (kushoto), akimuelezea Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Richard Mwaikenda kuwa wakati gazeti la Jambo Leo lilipoanzishwa 2009, alikuwa mfanyakazi wa kwanza kujiunga na gazeti hilo akitokea Kampuni ya Business Times.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concepts, Juma Pinto  (kushoto), akimuelezea Mhariri wa Habari wa Gazeti la Jambo Leo, Said Mwishehe kuwa wakati gazeti la Jambo Leo lilipoanzishwa 2009, alikuwa miongoni mwa wafanyakazi wa kwanza kujiunga na gazeti hilo akitokea Kampuni ya Business Times.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concepts, Juma Pinto  (kushoto), akimuelezea Mwandishi Mwandamizi wa Michezo na Burudani, Asha Kigundula  kuwa wakati gazeti la Jambo Leo lilipoanzishwa 2009, alikuwa miongoni mwa wafanyakazi wa mwanzo  kujiunga na gazeti hilo akitokea Kampuni ya Business Times.
 Mpigapicha Mkuu wa Jambo Leo na magazeti mengine ya Staa Spoti na Jambo Brand Tanzania, Richard Mwaikenda, akitoa shukrani wakati wa hafla hiyo/
 Mfanyakazi Moi Dodo akiwa na wife wake
 Champagne zikifunguliwa
 Asha Kigundula akiwamiminia champagne wanahafla
 Mwishehe na Kigundula wakikumbatiana kwa furaha

 Sasa ni wakati wa kusakata muziki


 Ni furaha tele



MGODI WA BUZWAGI WAPONGEZWA KWA KUZINGATIA SHERIA ZA MAZINGIRA

January 16, 2016
Meneja wa kinu cha kuchenjua dhahabu wa Mgodi wa Buzwagi Festo Shayo (wa kwanza kulia) akitoa maelezo kwa Naibu waziri ofisi ya makamu wa rais anaeshughulikia mazingira na Muungano, Luhaga Mpina namna mgodi wake unavyohifadhi maji yaliyotumika kusafishia dhahabu.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira na Muungano Luaga Mpina (wa kwanza kushoto), akisikiliza maelezo ya Afisa Mazingira wa Mgodi wa Buzwagi bwana Frank Ngoroma (wa kwanza mkono wa kulia), aliyesimama katikati ni meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo.
Mh Luhaga Mpina akisisitiza jambo wakati wa ziara hiyo katika eneo la kituo cha Uthibiti wa taka mbalimbali mgodini hapo.

Naibu Waziri pamoja na wataalamu wake wakikagua moja ya maeneo ambayo NEMC yalitoa ushauri kuwa yafanyiwe kazi katika ziara zao, ambapo wakati wa ziara hii utekelezwaji wake ulikutwa umeisha kamilika kama walivyokuwa wameelekezwa.
Mmoja wa maafisa wa mazingira aliyekuwa ameandamana na naibu Waziri akiuliza jambo wakati wa ziara hiyo.

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo akifafanua jambo wakati wa ugeni wa naibu Waziri wa mazingira.
Baadhi ya maofisa wa Mgodi wa Buzwagi wakitoa maelezo mbele ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira na Muungano Luaga Mpina
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Shinyanga.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Luhaga Mpina, ameupongeza Uongozi na wafanyakazi wa Mgodi wa Buzwagi kwa kuzingatia sheria za mazingira Mgodini hapo.

Pongezi hizo alizitoa wakati alipofanya ziara ya kushitukiza katika Mgodi huo kwa lengo la kujionea namna mwekezaji huyo anavyozingatia maelekezo ya wataalamu wa wizara yake juu ya utunzaji wa mazingira.

Akiwa katika ziara hiyo Naibu Waziri huyo alitembelea bwawa maalumu kwa ajili ya kuhifadhia maji yalitumika kuchenjulia dhahabu na kujionea namna ambavyo mgodi huo unavyochukua tahadhari ya hali ya juu katika kuhakikisha maji yanayohifadhiwa ndani ya bwawa hilo hayawezi kuwa na madhara kwa Jamii, pia naibu Waziri huyo alitembelea  kituo cha udhibiti taka, Uwanda wa kuvuna maji ya mvua mgodini hapo pamoja na karakana ya mgodi huo.

“Bwawa hili kama unavyoliona usanifu wake, umezingatia tahadhari zote kuhakikisha hakuna maji yoyote yanatoka nje na hasa ukizingatia maji yanayopatikana hapa ni yenye mchanganyiko wa madawa yanayotumika kuchenjua dhahabu” Alisema Meneja wa Kituo cha Uchenjuaji dhahabu bwana Festo Shayo, wakati alipokuwa akitoa maelezo juu bwawa hilo.

Kwa upande wake naibu Waziri Mpina amesema licha ya kufanya ziara katika Migodi mingi bwawa la kuhifadhia maji yanayotoka katika kinu cha kuchenjulia dhahabu la Buzwagi ni la kiwango cha juu na ameitaka Migodi mingine pia kutembelea kwa lengo la kujifunza usanifu wake.

“Ni seme tumepita maeneo mengi ila hapa mmejitahidi kuhakikisha wananchi wanaowazunguka wako salama, nafikiri kuna haja ya migodi mingine kuja kujifunza hapa, karakana yenu pia ni nzuri na inazingatia utunzaji wa mazingira. Alisema mh Mpina.

Aidha akiwa katika kituo maalumu cha udhibiti taka Mgodini hapo Naibu Waziri huyo ameutaka uongozi kujenga paa kwenye eneo la udhibiti wa taka za vyuma ili kuzuia maji ya mvua kugusa taka hizo.

“Mmejitahidi kuhakikisha taka zinawekwa katika utaratibu mzuri, ila kukosekana kwa paa hapa ni tatizo, hivyo nawaagiza ndani ya siku therathini eneo hili liwe na paa” alisema Naibu Waziri Mpina.

Awali akiukaribisha ugeni wa naibu Waziri huyo Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo alimueleza naibu Waziri huyo kuwa sekta ya madini kwa sasa duniani imekumbwa na changamoto ya kuporomoka kwa bei ya dhahabu, hali ambayo imepelekea wawekezaji wengi kujikuta wakijiendesha kwa hasara.

“Mheshimiwa naibu Waziri, Mgodi wa Buzwagi toka uanze shughuli zake umekuwa ukishirikiana na Jamii katika kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo na tunaendelea kufanya hivyo, Hata hivyo changamoto ni kubwa kwani kila siku bei ya dhahabu inashuka na hii inatufanya tushindwe kujiendesha kwa faida”alisema Mwaipopo.

“Tumeanza mchakato wa maandalizi ya kusitisha shughuli za uchimbali maana gharama zinazidi kuwa kubwa hata hivyo kama bei ya soko itabadilika tutafikiria vinginevyo” aliongeza Mwaipopo.

Akizungumzia hatua ya mgodi huo kutaka kusitisha shughuli za uchimbaji naibu Waziri Waziri ofisi ya makamu wa rais anaeshughulikia mazingira na muungano Luaga Mpina, amewaomba wawekezaji hao kuangalia namna ingine itakayowawezesha kuchimba kwa gharama ndogo inayoendana na bei ya dhahabu.

“kwa kweli serikali inawahitaji sana wawekezaji na tunaposikia mnaondoka kwetu sisi ni hasara kwa sababu kodi mbalimbali ambazo mmekuwa mkilipa kwa halmashauri ya mji wa Kahama hazitakuwepo tena na hii itafanya miradi mingi ya Maendeleo isitekelezeke baada ya ninyi kuondoka, tunawaombea bei ya dhahabu ipande ili muendelee kuwepo” Alisema Mpina.

Ziara hiyo ya kushitukiza ili lenga kujionea namna ambavyo mgodi wa Buzwagi unazingatia maelekezo mbalimbali ya wataalamu wa wizara yake.

JE WEWE NI MSANII NA UNAKAZI YAKO UNAHITAJI KUUZA???

January 16, 2016
Je wewe ni msanii na unakazi yako unahitaji kuuza??? ClickPay Africa tunahusika na uuzaji wa vitu mbalimbali ikiwemo Audio, Video, Movies, Photos, Live concerts, PDF, E-books, Documentaries, articles, etc. Kwa msanii yoyote mwenye kazi yake na anahitaji kuuza kwa njia ya mtandao anakaribishwa. Mawasiliano. Email : info@clickpayafrica.co.tz Website : www.clickpayafrica.com Mobile : 0719280280 / 0655353535 ---- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.blogspot.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''