Tupo makini kukusikiliza Mkuu

May 23, 2013
WANANCHI wa kata ya Bungu wilaya ya Korogwe Vijijini wakimsiliza MJUMBE wa Halmashauri Kuu  CCM Taifa kupitia wilaya ya Korogwe Vijijini,Dr.Edmund Mndolwa akipokuwa akiwahutubia wananchi wa kati hiyo juu ya umuhimu wa kilimo cha  Alizeti,Picha na Oscar Assenga,Korogwe.







MNDOLWA:Awahimiza wakinamama kulima zao la Alizeti.

May 23, 2013
Na Oscar Assenga, Korogwe.
MJUMBE wa Halmashauri Kuu  CCM Taifa kupitia wilaya ya Korogwe Vijijini,Dr.Edmund Mndolwa amesema atahakikisha anawahamasha wakina mama wilayani hapa kutumia kilimo cha alizeti kwa sababu ni mkombozi wa maendele na wakulima wa zao hilo mara nyingi wanakuwa na fedha zao mikononi .

Dr.Mndolwa alitoa kauli hiyo wakati akitoa mada katika semina ya wakina mama wajasiriamali iliyokua ikielezea kuhusu umuhimu kilimo cha zao la alizeti na kushirikisha wajumbe wa baraza la Umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) wilaya ya Korogwe vijijini iliyofanyika katika ukumbi wa CCM wilaya ya Korogwe .

Alisema kuwa ubora na umuhimu wa zao hilo ni mkubwa kutokana na kuwa ni miongoni mwa mazao ambayo hayahitaja mvua nyingi ili kuweza kustawi na huwa hayaingiliani na kilimo cha mahindi ambapo aliwataka wakinamama hao kuhakikisha wanakuwa mabalozi wazuri katika jamii zao kupanda zao hilo ambalo soko lake kupatikana ni rahisi pamoja na mkulima kuweza kujikomboa kimaisha.

Mndolwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wazazi (CCM)mkoa wa Tanga alisema katika kitu cha kwanza wakulima wa zao hilo wakae kwenye vikundi ili kuweza kuangalina mamna ambavyo wanaweza kulima zao hilo kwa kushirikiana kwa pamoja ili kuweza kuendesha maisha yao kupitia kilimo.

“Ajira kubwa inapatikana kupitia kilimo na kuwashauri wakinamama wahakikishe wanalima alizeti kwa sababu hakiingiliani na mazao mengine ikiwemo mahindi na wala hakiitaji mvua nyingi hivyo wakipanda zao hilo wataona faida zake kwa kipindi kifupi “Alisema Dr.Mndolwa.

Aidha alisema atahakikisha anapita kila tarafa kuhamasisha  wananchi kulima zao hilo ambapo uhamasishaji huo utakwenda sambamba na kuwashawishi watu wenye uwezo mkubwa kuweka mashine za kukamulia alizeti katika maeneo mbalimbali wilayani humo nia ikiwa ni kuwapa dona wakavue samaki.

Mndolwa aliwataka wakina mama waunde vikundi kila kata ili kuweza kufanya mpango wa kutoa shamba kwa vijana hekta tano ili kuweza kuwainua vijana kiuchumi na kuwaepusha na kuendelea kukaa vijiweni ikiwemo kujihusisha na vitendo viovu visivyotakiwa katika jamii zao.

Alieleza kuwa endapo malengo hayo yatafanikiwa itasaidia kuwaondoa vijana kwenye vijiwe ambavyo wanakuwa wakitumia muda mwingi kutumia madawa ya kulevya pamoja na kujadili jinsi gani ya kupata pesa kwa njia zisizo za halali hali ambayo sio nzuri kwa maisha yao ya baadae.

Kwa upande wake,Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Korogwe Vijijini,Nassoro Hemed Nassoro “Mali Ngumu”alisifu jitihada zinazofanywa na Dr.Mndolwa kwa kuona umuhimu kuwaandalia semina wakinamama hao na kuleza kuwa  itawasaidia kuweza kujiajiri wenyewe kuliko kuendelea kuwa tegemezi katika jamii zao.
   
        Mwisho.











DC Mgaza akitoa hotuba yake kwenye uzinduzi wa uandikishaji wanachama NSSF

May 23, 2013
MKUU wa wilaya ya Mkinga,Mboni Mgaza akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Kichalikani Kata ya Kwale leo mara baada ya wanachama wapya wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF kukabidhiwa kadi zao ambapo jumla ya wanachama wapatao 500 walikabidhiwa kadi,kushoto ni Mkurugenzi uendeshaji mfuko huo Crescentius Magori na kulia kwake ni Meneja wa Mfuko huo mkoa wa Tanga,Frank Maduga.

Wanachama wapya wakionyesha kadi zao Mpya walizokabidhiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF leo

May 23, 2013
WANACHAMA wapya waliojiunga na mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) leo wilayani Mkinga wakionyesha kadi zao baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa wilaya ya Mkinga,Mboni Mgaza.Picha na Mwandishi Wetu.

DC Mgaza akigawa kadi kwa wanachama wapya wa NSSF Kichalikana leo

May 23, 2013
MKUU wa wilaya ya Mkinga akimkabidhi kadi ya uanachama wa mfuko wa hifadhi ya Jamii NSSF Mkazi wa Kijiji cha Kichalikani Kata ya Kwale,kulia ni Mkurugenzi uendeshaji mfuko huo ,Crescentius Magori na kushoto ni Meneja wa Mfuko huo mkoa wa Tanga,Frank Maduga,Picha na kulia kwa Mkurugenzi aliyevaa miwani ni Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Huduma kwa wateja NSSF Eunice Chiume,Picha na Mwandishi wetu

NSSF wakabidhi kadi 500 kwa wanachama wapya wa mfuko huo Mkinga

May 23, 2013
MKURUGENZI wa Uendeshaji Mfuko wa Hifadhi ya Jamii nchini (NSSF),Crescentius Magori akisalimiana na mkazi wa kijiji cha Kichalikani Kata ya Kwale tarafa ya Mkinga leo mara baada ya kukabidhiwa kadi ya uanachama wa mfuko huo na mkuu wa wilaya ya Mkinga,Mboni Mgaza katika halfa iliyofanyika kijiji hapo ambapo jumla ya wanachama 500 walikabidhiwa kadi zao.