BALOZI WA PSPF MWANAMITINDO WA KIMATAIFA FLAVIANA MATATA AKABIDHI MABEGI NA MADAFTARI KWA SHULE ZA MSINGI DODOMA NA SINGIDA

October 07, 2015

Balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Flaviana Matata, akikabidhi begi kwa mwanafunzi wa Shule ya Msingi, Nyerere iliyoko Manispaa ya Singida, Oktoba 7, 2015. PSPF kupitia Sera yake ya kusaidia jamii imetoa msaada wa mabegi na madaftari kwa shule hiyo na ile ya Chididimo iliyoko nje kidogo ya Manispaa ya Dodoma
NA K-VIS MEDIA, DODOMA NA SINGIDA
BALOZI wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Flaviana Matata, ametoa wito kwa wanafunzi wa shule za msingi Chididimo iliyoko Manispaa ya mji wa Dodoma na ile ya Nyerere iliyoko mkoani Singida kuwahimiza wazazi wao kujiunga na Mfuko huo.
Balozi huyo ambaye pia ni Mwanamitindo wa Kimataifa anayefanyia kazi zake nchini Marekani, ameyasema hayo kwa nyakati tofauti, wakati akikabidhi vifaa vya shule kwa wanafunzi hao Oktoba 7, 2015.
“Mimi kama Balozi wa PSPF, ninatoa wito kwa wanafunzi mliopo hapa, kufikisha ujumbe huu kwa wazazi wenu, kwani kujiunga na PSPF kuna faida nyingi katika maisha ya sasa na ya baadae.” Alisema
Alisema, PSPF inatoa mikopo mbalimbali kwa wanachama wake kama vile ya viwanja, mkopo wa elimu, na mkopo wa kuanzisha maisha.
Lakini pia PSPF inatoa mafao mbalimbali kwa wanachama wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, yaani (PSS), ikiwemo, Fao la Uzazi, Fao la Uzeeni, Fao la Elimu, Fao la Ulemavu na Fao la Ujasiriamali.
“Wazazi wenu wawe wakulima, wafanyakazi walioajiriwa au kujiajiri wanaweza kujiunga na PSPF kupitia mpango wa Uchangiaji wa Hiari.” Alifafanua Balozi huyo.
Naye Afisa Masoko Mwandamizi wa PSPF, Rahma Jemina Ngassa, alisema moja ya Sera za Mfuko huo ni kuchangia sekta ya Elimu na msaada huo ni utekelezaji wa Sera wa kusaidia jamii.
“PSPF inaamini vifaa hivyo vitapunguza kwa kiasi Fulani changamoto zilizokuwa zinawakabili wanafunzi hao na hivyo watakuwa kwenye nafasi nzuri ya ushiriki wa masomo kikamilifu.” Alisema.
Kwa upande wake, Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Dodoma, Christopher Ligonda, ameupongeza Mfuko huo kwa kuwajali wanafunzi ambao wazazi wao kwa namna moja au nyingine ni wanachama au wanachama watarajiwa na hata wanafunzi wenyewe.
Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nyerere iliyoko mkoani Singida, Yesaya Ramadhani, ameushukuru uongozi wa PSPF kwa kuwafikiria wanafunzi wa shule hiyo katika kuwasaidia vifaa hivyo ambavyo ni mabegi na madaftari kuwa ni kitendo cha kweli katika kusaidia jamii ambayo inakabiliwa na changamoto mbalimbali.

JIMBO LA SHINYANGA MJINI WASTUKA

October 07, 2015

Ray Kigosi akimwaga sera zake.naye ni mmoja kati ya wasanii wanaoendesha kampeni za Nimes’tuka,

Mchekeshaji Mboto, naye ni mmoja kati ya wasanii wanaoendesha kampeni za Nimes’tuka,
MEFMI YAFANYA MAJADILIANO NA MAGAVANA WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KUSINI.

MEFMI YAFANYA MAJADILIANO NA MAGAVANA WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KUSINI.

October 07, 2015

unnamedbb 
Dr. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali wa kwanza kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Magavana wa Mashariki na Kusini mwa Afrika baada ya mkutano wa MEFMI .
……………………………………………………………………………………
Na Ingiahedi Mduma -Msemaji Mkuu Wizara ya Fedha Lima – Peru
Katika kipindi hiki cha mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa, kumekuwa na mikutano mbalimbali inaendelea hapa nchini Peru. Mikutano hiyo inaendeshwa na Taasisi mbalimbali zenye utaalamu wa kiuchumi na kifedha. Akizungumza na waandishi wa habari, katibu Mkuu Wizara ya fedha Dr. Servacius Likwelile alisema “MEFMI ni chombo kikubwa kwa Afrika Mashariki na Kusini katika kutoa mafunzo ya usimamizi wa mambo ya uchumi kwa watendaji wa nchi wanachama.” Aliendelea kusema kuwa katika siku hizi mbili wamekutana na chombo hicho kwa madhumuni ya kuzungumzia maendeleo ambayo yanatokana na rasilimali kama vile gesi na madinii na kutoa mapendekezo ya namna gani Afrika inaweza kusimamia rasilimali hizo. Akitoa ufafanuzi katika majadiliano hayo Dr. Likwelile alisema”Tanzania kuna rasilimali nyingi kama vile gesi ambayo imegunduliwa Mtwara na kusisitiza kuwa kuna nchi mbalimbali barani Afrika ambazo zina dhahabu ya kutosha ambayo inaweza kuinua uchumi wa Afrika kama kutakuwa na utaratibu mzuri wa kuzitumia. “Lengo kuu la mkutano wa MEMFI ni kuzungumzia shughuli zinazofanywa na MEMFI ili kuwezesha kupanga namna ya kuboresha uwezo na kuendesha shughuli zetu katika kuinua uchumi wa Afrika kwani tutahitaji fedha nyingi kwa ajili ya kuwekeza kwenye miundombinu lakini lazima tuhakikishe kwamba tunafanya hivyo ili kuhakikisha uchumi wetu unakuwa imara na kunakuwa na utaratibu wa kuweka akiba kwa ajili ya vizazi vijavyo, hili ni suala la msingi sana” alisistiza Likwelile. Likwelile aliongeza kuwa “Vizazi vingi vinatumia rasilimali zote bila kuangalia utaratibu wawakati ujao kuwa utakuwaje, hivyo katika kikao hiki tumekubaliana kuanzisha mfuko ambo ni kwa ajili ya kuwekeza kwa ajili ya matumizi ya baadae (Sovereign Wealth Fund). Masharti ya mfuko huoyatakuwa ni kama ifuatavyo: (i) Mfuko huo lazima uweze kuzalisha ajira, (ii)Mfuko huo lazima uwe na misingi imara ya kusimamia uendeshaji wa shughuli zake,(iii) Mfuko lazima uwe na chombo imara kinacho kisimamia mfuko huo. (iv) Lazima kuwe na utaratibu ambao unasema mfuko huu utafanya nini na hautafanya nini.
La msingi kuwe na mfumo wa kisheria lakini tuangalie rasilimali watu ili kuweza kuhifadhi mfuko huo. Na namna gani miundombinu itawezakusaidia kuimarisha uchumi ili uweze kutambuliwa.” Naye Gavana wa Benki kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu alisema kuwa,ni muhimu kujua mapato yetu yatokanayo na upatikanaji wa madini kwani tunaweza kuyatumia vizuri katika kuhakikisha tunatengeneza miundombinu, kuongeza uwezo wa kuzalisha na baada ya hapo nchi iweze kuendelea kupiga hatua hata kama madini yatakuwa yamekwisha. Waziri wa Fedha ni Gavana katika mikutano hii, akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile ambaye ni Gavana msaidizi kwa upande wa Benki ya Dunia (WB), aidha Gavana wa Benki kuu Prof. Benno Ndulu ni Gavana msaidizi kwa upande wa Shirika la Fedha la Kimataifa(IMF). Hali ya hewa mjini hapa ni baridi, rasharasha na manyunyu ya hapa na pale hasa nyakati za asubuhi.
Imetolewa na: Ingiahedi Mduma Msemaji Mkuu Wizara ya Fedha Lima – Peru 7/10/2015

MAMA SALMA KIKWETE AHUDHURIA MAZISHI YA NHAYATI SIMON KAMILLIUS MEMBE.

October 07, 2015

Baadhi ya waombolezaji wakishiriki kwenye ibada ya mazishi ya Marehemu Simon Kamillius Membe iliyofanyika katika kijiji cha Rondo huko Lindi Vijijini tarehe 7.10.2015.
Mheshimiwa Benard Membe akitoa heshima za mwisho wakati wa kuuaga mwili wa marehemu kaka yake Ndugu Simon Camillius Membe mara baada ya kufanyika ibada ya mazishi huko Kijijini Rondo tarehe 7.10.2015.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwapa pole wana familia ya Marehemu Simon Kamillius Membe mara baada ya kuhudhuria ibada ya mazishi iliyofanyika huko Rondi, Lindi Vijijini tarehe 7.10.2015.
Baadhi ya waombolezaji wakipita mbele ya jeneza ulimolazwa  mwili wa Marehemu Simon Membe aliyefariki dunia huko India tarehe 3.10.2013,
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Benard Kamillius Membe akitoa neo la shukrani kwa viongozi wa serikali, Chama Cha Mapinduzi na wananchi waliojitoa kwa hali na mali katika kufanikisha mazishi ya marehemu kaka yake Bwana Simon Kamillius Membe aliyefariki dunia huko India tarehe 3.10.2015.
Maandamano ya kwenda kuulaza mwili wa Marehemu Simon Membe kwenye nyumba yake ya milele huko kijijini Rondo katika wilaya ya Lindi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la Marehemu Simon Membe wakati mwa mazishi katika Kijiji Rondo huko Lindi .
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Benard Membe akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu mdogo wake ndugu Simon Membe wakati wa mazishi yake huko Rondo TAREHE 7.10.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiweka shada la maua kwenye kaburi la Marehemu Simon Kamillius Membe aliyefariki dunia huko India tarehe 3.10.2015.
PICHA NA JOHN LUKUWI.

MAGUFULI AZIDI KUIBOMOA CHADEMA KILIMANJARO,AWATOLEA UVIVU WATENDAJI WA SHIRIKA LA UMEME NCHINI

October 07, 2015
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Moshi mjini Ndugu Davis Mosha kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa,mkoani Kilimanjaro jioni ya leo.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-KILIMANJARO.
 Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli na mgombea ubunge wa jimbo la Moshi mjini Ndugu Davis Mosha wakimsikiliza Bw. Lema aliyekuwa Katibu wa Chadema wilaya ya Hai wakati alipojiunga na CCM katika mkutano huo.

 Mgombea Urais wa CCM Dkt Jonh Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa CCM ndani ya jimbo la Arumeru Mashariki,ndugu John Daniel Pallangyo,kweye mkutano wa kwampeni uliofanyika katika uwanja wa Ngareselo (USA River),jijini Arusha.

 Mmoja wa wajumbe wa timu ya ushindi ya kampeni za CCM,Dkt Emmanuel Nchimbi akimnadi Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,kweye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa CCM,Sanya Juu,mkoani Kilimanjaro.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Siha,Ndugu Aggrey Mwanri mbele ya wakazi wa Siha (hawapo pichani),waliokuwa wamekusanyika katika uwanja wa CCM kwenye mkutano wa kampeni

Sehemu ya Umati wa Wananchi wa mji wa moshi waliofika katika viwanja vya mashujaa wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,leo jioni kwenye mkutano wa kampeni,mkoani Kilimanjaro.
Magufulika Style  inavyozidi kushika kasi,Davis Mosha mgombea ubunge jimbo la Moshi mjini na madiwani wa Moshi mjini wakimagufulika jukwaani kuonyesha ukakamavu wao.
 Sehemu ya Umati wa Wananchi wa mji wa moshi waliofika katika viwanja vya mashujaa wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,leo jioni kwenye mkutano wa kampeni,mkoani Kilimanjaro.

Katika mkutano wake wa Moshi mjini Dkt. Magufuli amewaonya watendaji wa Shirika la Umeme nchini TANESCO na kuwaambia kama wanazima umeme makusudi ili kuwafanya wananchi waichukie serikali wanafanya makosa na ole wao kwa vitendo hivyo visivyo vya kistaarabu, Amewaambia kwamba bado siku 17 za kampeni akichaguliwa na wananchi na kuapishwa kuwa Rais atawashughulikia ipasavyo kwani  wanajulikana.  “Katika siku hizi zilizobaki watubu wafanye kazi usiku na mchana ili umeme upatikane bila kukatika na kuleta adha kwa wananchi vinginevyo akiingia Ikulu atalala nao mbele”,alisema Dkt Magufuli huku uwaja mzima ukilipukwa kwa mayowe.
 Sehemu ya Umati wa Wananchi wa mji wa moshi waliofika katika viwanja vya mashujaa wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,leo jioni kwenye mkutano wa kampeni,mkoani Kilimanjaro.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akisisitiza jambo alipokuwa akihutubia umati wa Wananchi wa mji wa moshi waliofika katika viwanja vya mashujaa Kumsikiliza alipokuwa akijinadi na kuwaga sera zake katika kuomba kura za kuwania nafasi ya Urais kwa kipindi cha awamu ya tano,kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
 Sehemu ya Umati wa Wananchi wa mji wa moshi waliofika katika viwanja vya mashujaa wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,leo jioni kwenye mkutano wa kampeni,mkoani Kilimanjaro alipokuwa akijinadi na kuomba kura za kutosha ili aibuke kuwa Rais wa Tanzania wa awamu ya tano,katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akihutubia umati wa Wananchi wa mji wa moshi waliofika katika viwanja vya mashujaa Kumsikiliza alipokuwa akijinadi na kuwaga sera zake katika kuomba kura za kuwania nafasi ya Urais kwa kipindi cha awamu ya tano,kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
 Mgombe Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akisoma mabango aliyokuwa yamebebwa na baadhi ya wafuasi wa chama cha CCM,wakati akiwasili kwenye uwanja wa mkutano wa kampeni ndani ya jimbo la Arumeru Mashariki (Usa river),uliofanyika katika uwanja wa Ngareselo mkoani Arusha.
Baadhi ya wakazi wa USA River wakiwa wamekusanyika kwenye uwanja wa mkutano wa kampeni ndani ya jimbo la Arumeru Mashariki,katika uwanja wa Ngareselo,kumsikiliza  Mgombe Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi sera zake 
 Kiongozi wa Msafara wa Kampeni za Mgombea Urais wa CCM,Ndugu Abdallah Bulembo akisalimiana na kada wa CCM,aliyekuwa mkuu wa kwanza wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jenerali Mirisho Sarakikya huku Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufulia akishuhudia tukio hilo
 Baadhi ya wakazi wa USA River wakiwa wamekusanyika kwenye uwanja wa mkutano wa kampeni ndani ya jimbo la Arumeru Mashariki,katika uwanja wa Ngareselo,kumsikiliza  Mgombe Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi sera zake za kuomba kuwania nafasi ya Urais.
  Baadhi ya wakazi wa USA River wakishangilia jambo kwenye uwanja wa mkutano wa kampeni ndani ya jimbo la Arumeru Mashariki,katika uwanja wa Ngareselo,wakati Mgombe Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi sera zake na kuomba kuwania nafasi ya Urais.
 Wananchi wa wilaya ya Siha wakimsikiliza Mmoja wa wajumbe wa timu ya ushindi ya kampeni za CCM,Dkt Emmanuel Nchimbi alipokuwa akimnadi Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,kweye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa CCM,Sanya Juu,mkoani Kilimanjaro.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,akijinadi mbele ya wakazi wa wilaya ya Hai,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye stendi ya Malori ndani ya mji wa Boma ng'ombe,mkoani Kilimanjaro
 Mgombea Urais wa CCM Dkt Jonh Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo Moshi Vijijini Dkt Cyril Chami pamoja na madiwani ndani ya mji wa Uru Shimbwe,kwenye mkutano wa kampeni
-- Ahmad Issa Michuzi Editorial Director P.O BOX 9033, DAR ES SALAAM. issamichuzi.blogspot.com www.michuzijr.blogspot.com othmanmichuzi.blogspot.com Phone:0713 422 313/ 0783 422 313 Tanzania- East Africa.

LOWASSA AWATAKA WATANZANIA KUCHANGAMKIA FURSA ZA AJIRA ZITOLEWAZO NA AFRIKA MASHARIKI

October 07, 2015

WATANZANIA wametakiwa kujifunza kuchangamkia fursa za ajira zinazotolewa na Afrika Mashariki kama ilivyo kwa nchi nyingine.

Kauli hiyo ilitolewa jana na mgombea wa Urais kupitia Chadema, Edward Lowassa alipokuwa kwenye kampeni zake zilizofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Namanga.
Lowassa alisema iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, atahakikisha kuwa watanzania wanachangamkia fursa za Afrika Mashariki kama ilivyo kwa Kenya.
“Napenda mahusiano ya Afrika Mashariki yawe ya kweli na siyo upande mmoja unafaidi na mwingine haufaidi,”alisema na kuongeza kuwa:
“Watanzania wakiwa wanapita kwenye mpaka wa Namanga wasisumbuliwe wapite bila shida.”
Sehemu ya wananchi wa eneo la Kisongo, Jijini Arusha wakiwa wamefunga barabara kuzuia msafara wa Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, ili waweze kumsalimia na kumsikiliza, wakati alipokuwa njiani kuelekea eneo la Ngaramtoni mpaka Namanga, kwenye Mkutano wa Kampeni, leo Oktoba 7, 2015.
PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI, ARUSHA.
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa kwa vijana wa eneo la Kisongo, walipokuwa wakimsindikiza mpendwa wao.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwasili kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Mringa, Jimbo la Arumeru Magharibi, Jijini Arusha leo Oktoba 7, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni zake.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwapungia wananchi wa Jimbo la Arumeru Magharibi waliohudhulia Mkutano wa Kampeni zake, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Mringa, Jimbo la Arumeru Magharibi, Jijini Arusha leo Oktoba 7, 2015.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Jimbo la Arumeru Magharibi katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Mringa, Jimbo la Arumeru Magharibi, Jijini Arusha leo Oktoba 7, 2015.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwapungia wananchi wa Jimbo la Longido waliohudhulia Mkutano wa Kampeni zake, uliofanyika kwenye Uwanja wa Namanga, Jijini Arusha leo Oktoba 7, 2015.

Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwasalimia watoto walikuwepo kwenye Mkutano huo.
Lowasaaaaa……   Mabadilikoooooooo……
Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye akiwasalimia wananchi wa Mji wa Namanga, katika Jimbo la Longido, wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Namanga, Jijini Arusha leo Oktoba 7, 2015.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Namanga, Jimbo la Longido, wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Namanga, Jijini Arusha leo Oktoba 7, 2015. 
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Longido kupitia Chadema, Onesmo Ole Nangole, wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Namanga, Jijini Arusha leo Oktoba 7, 2015. 
Zawadi: Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye akionyesha kwa wananchi zawadi iliyotolewa na Vijana wa Mji wa Namanga kwa Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa.
Burudani ya Asili ya Kimaasai.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiteta jambo na aliewahi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani katika Serikali ya Kenya, Mzee John Keen, aliefika eneo la Namanga kuhudhulia Mkutano wa Kampeni zake, leo Oktoba 7, 2015.