WANANCHI WATAKIWA KUTUNZA MAZINGIRA ILI YAWALETEE KIPATO ENDELEVU

WANANCHI WATAKIWA KUTUNZA MAZINGIRA ILI YAWALETEE KIPATO ENDELEVU

October 15, 2017
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Profesa Faustine Kamuzola ameitaka jamii kujenga tabia ya kutunza mazingira katika maeneo yao kwa faida ya vizazi vya sasa na vizazi vijavyo. Katibu mkuu Profesa Kamuzola ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akifunga mafunzo ya mradi wa uchumi wa kijani chini ya Jangwa la Sahara, yaliofanyika jijini Tanga. Alisema kuwa ni vyema wananchi wakajua umuhimu halisi wa kutunza mazingira na kuyatumia katika kujiongezea kipato. Mradi wa uchumi wa kijani chini ya Jangwa la Sahara ulikuwa ukifadhiliwa na taasisi ya Korea ya ushirikiano wa kimtaifa KOICA chini ya Programu ya UNESCO. Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Profesa Faustine Kamuzola akiongea na washiriki wa mradi wa Uchumi wa Kijani ndani ya Hifadhi ya Hai (GEBR) wakati akifungua mkutano wa majadiliano wa kufunga mradi huo uliokuwa ukifadhiliwa na taasisi ya Korea ya Ushirikiano wa Kimataifa (KOICA) chini ya Programu ya UNESCO iliyofanyika mjini Tanga. Lengo la mradi huo ilikuwa ni kupunguza umaskini, kuhifadhi bioanuwai na maendeleo endelevu katika nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara - Usambara ya Mashariki, Tanzania. Picha zote na KAJUNASON/MMG-TANGA. 
Kwa upande wake Katibu tawala wa mkoa wa Tanga, Mhandisi Zena Saidi ameisisitiza jamii kupokea vizuri miradi wanayokuwa wakiletewa na wafadhili ili iwaongezee kipata na elimu zaidi katika utunzaji wa mazingira. "Wananchi ni vyema mkabadirika na kuacha kuishi bila kutambua kuwa mazingira ukiyatunza yanakuletea kipato cha juu kabisa, ukiangalia unaona unaweza kutengeneza mkaa kwa kutumia magunz ya mahindi baada ya kuwa umeshavuna hiyo ni faida tosha kabisa," alisema Mhandishi Zena Saidi. Naye Mhifadhi wa Mazingira ya asili ya Amani, Bi. Mwanaidi Kijazi aliwashukuru sana wafadhili wa mradi huo kwa kuweza kutoa elimu kwa wananchi ... elimu ambayo imekuwa endelevu na kuwazalishia kipato cha hali ya juu. Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi Zena Saidi ambaye alimwakilisha mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigella akifungua rasmi na kumkaribisha mkutano wa majadiliano wa kufunga mradi huo uliokuwa ukifadhiliwa na taasisi ya Korea ya Ushirikiano wa Kimataifa (KOICA) chini ya Programu ya UNESCO. 
 Bi. Mwanaidi alisema kuwa wananchi baaada ya kupewa elimu wameweza kujiendeleza katika miradi mbali mbali ikiwemo kutengeneza mkaa kwa kutumia majani ya mimea/magunzi, ufugaji wa vipepeo ambao wamekuwa wakiwazalisha kwa kutengeneza mapambo, kilimo cha uyoga, kilimo cha asali. Hifadhi ya mazingira ya amani inaendeleza ikolojia na bioanuwai ambazo ni adimu duniani na zinapatikana katika milima ya usambara mashariki, na ina jumla ya vijiji 72. Kaimu Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Axel Plathe akizungumza wakati akifungua mkutano wa majadiliano wa kufunga mradi huo uliokuwa ukifadhiliwa na taasisi ya Korea ya Ushirikiano wa Kimataifa (KOICA) chini ya Programu ya UNESCO iliyofanyika mjini Tanga. Meza Kuu. Mhifadhi wa Mazingira ya asili ya Amani, Bi. Mwanaidi Kijazi. Picha juu na chini ni washiriki wa mradi huo wakiuliza maswali... Pichani juu na chini washiriki wakifuatilia kwa makini. Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.

HABARI NA PICHA OPARESHENI MAALUM YA MIFUGO MWANGA

October 15, 2017




Katika picha kikosi kazi maalum cha oparesheni ya angani ya ukaguzi wa uvamizi wa mifugo katika Wilaya ya Mwanga inayotokea katika nchi jirani ya Kenya , mbele ni rubani wa ndege hiyo maalum ya TANAPA Bw. Mark Athumani akiongoza ujumbe huo kupanda ndege katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Kilimanjaro (KIA).



Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akiongea na kikosi kazi maalum kikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt Maria Mashingo na Rubani wa ndege hiyo  maalum ya TANAPA Bw. Mark Athumani walipokuwa wakijiandaa kwenda kwenye oparesheni maalum ya angani ya ukaguzi wa uvamizi wa mifugo katika wilaya ya Mwanga wanaotokea katika Nchi jirani ya Kenya.


Waziri Mpina akimpungia mkono Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvivi Dkt Maria Mashingo akiwa na baadhi ya wajumbe wakiingia  kupanda ndege maalum kuanza oparesheni ya ukaguzi wa uvamizi wa mifugo katika Wilaya ya Mwanga wakitokea Kenya.


NA MWANDISHI  MAALUM – KILIMANJARO
Serikali haitaweza kuwavumilia watendaji wazembe katika suala zima la uvamizi wa mifugo hususan ng’ombe kutoka katika nchi jirani ya Kenya.
Hayo yamebainishwa wilayani Mwanga na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina alipozindua rasmi oparesheni maalum ya uvamizi  na utambuzi wa mifugo hiyo tokea angani.
Mpina alisema kuwa uvamizi wa mifugo hiyo tokea nchi jirani ya Kenya unaleta changamoto kubwa ya malisho ya mifugo ya ndani ya nchi unaopelekea migogoro ya mara kwa mara kati ya wakulima na wafugaji na husababisha mmomonyoko wa udongo  na uharibifu wa mazingira.
Baada ya kupokea taarifa ya timu ya wataalam iliyoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara Mifugo na Uvuvi Dkt Maria Mashingo, iliyofanya oparesheni hiyo  maalum kwa kutumia  ndege ya shirika la taifa la hifadhi ya wanyamapori, (TANAPA) taarifa iliyobaini kuwepo kwa makundi makubwa ya ng’ombe waliokuwa wakihama kutoka sehemu moja kwenda nyingine na kuwepo kwa idadi kubwa ya Maboma, Waziri Mpina alisema ,
“ Haiwezekani ng’ombe wanaingia kwa makundi makubwa hivi nchini na watendaji wa serikali wapo, lazima kutakuwa na shida katika utendaji, Oparesheni hii itakuwa ni ya mwisho, kwa ng’ombe watakaoingia tena watendaji watatolewa sadaka.” Alibainisha Mpina.
“Yawezekana ng’ombe wote 4000 ambao inasemekana walitoroshwa hapo awali wapo, hivyo Oparesheni ianze rasmi tuwakamate ng’ombe wote, tuheshimu sana sheria, na nchi jirani tushirikiane katika mambo tuliyokubaliana kisheria na lolote litakalotokea katika suala hili la uvamizi wa mifugo sheria itachukua mkondo wake na tusilaumiane” Alisisitiza Mpina.
Awali wataalam waliyokuwepo katika oparesheni hiyo maalum waliezeza kuwa mifugo mingi iliyoonekana kutokea angani ilikuwa zaidi katika maeneo ya malisho na maji ya vijiji vya kiti cha Mungu,njiapanda,kirya na kitongoi cha Mangulai.
Timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilya ya Mwanga imeingia kazini tayari kwa kuanza oparesheni hiyo maalum.