“HITILAFU YA UMEME YAUNGUZA BAADHI YA VIFAA OFISI YA ELIMU SEKONDARI JIJI LA TANGA”

December 08, 2017
Kaimu Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji mkoa
wa Tanga,Inspekta Kumenya Bakari akizungmza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Jiji wakitoa
vitu nje kwenye ofisi ya Elimu Sekondari ya Jiji hilo baada ya kuungua kutokana na hitilafu ya umeme .

HITILAFU ya Umeme iliyotokana na mgandamo wa hewa imesababisha ofisi ya Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Jiji la Tanga kuungua moto ikiwemo baadhi ya vitu vilivyo kuwemo ndani kabla kuzimwa ili usiweze kusambaa kwenye maeneo mengine ndani ya Halmashauri ambao ungeweza
kuleta athari kubwa.

Jitihada za kuufanya moto huo usiweze kusambaa kwenye maeneo mengineulifanywa na watumishi wa halmashauri hiyo  ambao walitumia vifaa vya kuzimia moto huo baada ya kupatiwa elimu ya kupambana na majanga ya
moto.

Akizungumza jana,Kaimu Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Tanga,Inspekta Kumenya Bakari alithibitisha kuungua kwa ofisi hiyo ambapo alisema tukio hilo lilitokea  Desemba  8 asubuhi  saa tano asubuhi baada ya kupata taarifa kutoka kwa kijana wa boda boda na ndipo walipoamua
kutoka na magari yao.

Alisema pamoja na kupewa taariufa hizo wakiwa wanajiandaa kufika eneo la tukio wakasikia alamu iliyopo ofisini iliwaonyesha kuna moto unawaka eneo la ofisi ya halmashauri na ndipo vijana wakatoka kwa haraka sana pamoja na askari waende kuona na kuchukua hatua ya kuuzima.

Aidha alisema ushupavu wa watumishi hao kuwahi na kuuzima moto huo kwa kuanzia na uzimaji wa swichi kubwa ya umeme inatokana na elimu ambayo walikwisha kuwapatia namna ya kukabiliana na majanga ya namna hiyo pindi yanapotokea kwenye maeneo yao na hivyo kuweza kuuzima mapema.

Naye kwa upande wake,Msaidizi wa Afisa Habari wa Kikosi hicho mkoani Tanga,Sajenti Mussa Msengi alisema baadhi ya vitu ambavyo vimeungua niSimu moja,pazia, Fax  Mashine,Printer,Meza ,Rimu na Nyaraka mbalimbali
zilizokuwemo ndani ya ofisi hiyo.

Akizungumzia tukio hilo, Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga, Alhaj
Mustapha Selebosi alisema baada ya kutokea tukio hilo watakachokifanya hivi sasa ni kurekebisha kutokana na kuwepo kwa vitu vingi ambavyo vimejaa hivyo kunaweza kupelekea matukio ya namna hiyo.

Alisema iwapo wasingekuwa na mitambo yao ya kuzimia moto inaweza kupelekea hasara kubwa kwa kuungua jengo lote.

“Kwanza nishukuru kuwepo kwa mitambo yetu wenyewe ya kuzimia moto hasa yanapojitokeza majanga ya moto ni moja kati ya vitu muhimu vilivyosaidia kukabiliana na janga hili “Alisema.

MBUNGE WA TANGA ASHIRIKI KUUZIMA MOTO.

Awali akizungumza na gazeti hili,Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) AlhajiMussa Mbaruku  alikuwa ni miongoni mwa  watu walioshiriki kwenye zoezi la kuuzima moto huo ili usiweze kuleta madhara katika maeneo megine.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa tukio hilo,Mbunge Mussa alisema ipo haja halmashauri kuongezwe vifaa vya kuzimia moto lakini pia kuwepo na alama ambazo zitakuwa zikitoa ishara wakati yanapojitokeza mambo ya namna hiyo.

"Kwa kweli hali ilikuwa mbaya sana wakati wa tukio hili linatokea kwa sababu na mimi nilikuwepo na nimeshuhudia lakini niseme upo umuhimu mkubwa kuwepo kwa vifaa vya kutosha vya kuzimia moto katika maeneo mbalimbali ya majengo ya serikali kuweza kunusuru na hasara zinazoweza kutokea kama ilivyokuwa leo(jana) tulivyoweza kupambana na moto na
kuuzima "Alisema.

DKT SHEIN AWASILI MKOANI DODOMA KUHUDHURIA SHEREHE ZA UHURU WA TANZANIA BARA KESHO

DKT SHEIN AWASILI MKOANI DODOMA KUHUDHURIA SHEREHE ZA UHURU WA TANZANIA BARA KESHO

December 08, 2017
DSC_6783
RaIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma na kusalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe Sezaria Makota, kwa ajili ya kuhudhuria Sherehe za Miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara zitakazofanyika katika uwanja wa Jamuhuri leo
DSC_6787
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Katibu Mkuu wa UVCCM  Shaka Hamdu Shaka alipowasili Uwanja wa Ndege wa Dodoma kuhudhuria sherehe za Uhuru wa Tanzania Bara zinazofanyika katika Uwanja wa Jamuhuri
DSC_6796
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Mkoani Dodoma alipowasili katika uwanja wa ndege kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za Uhuru wa Tanzania Bara kesho katika viwanja vya Jamuhuri Dodoma.
Picha na Othman Maulid

SERIKALI YATANGAZA KAMATI YA KITAIFA YA KUANDAA URITHI WA TANZANIA

December 08, 2017
Serikali kupitia Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamisi Kigwangalla ameunda Kamati ya Kitaifa ya kuandaa mwezi maalum wa maadhimisho ya urithi wa Tanzania ambapo kamati hiyo itajumuisha viongozi mbalimbali waandamizi wakiwemo wakuu wa Mikoa, Mawaziri, Wakurugenzi na wakuu wengine wa Idara za Serikali na mashirika binafsi.

Naibu Waziri Nditiye atoa siku 14 kwa Tipper kuunganisha bomba kwa TPA

December 08, 2017
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Ashasta Nditye, ametoa siku 14 kuhakikisha bomba la mafuta la Kimataifa linalosambaza mafuta (TIPPER), liwe limeunganishwa kwenye mfumo unaodhibitiwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ili serikali iweze kupata mapato sahihi.

Kutokana na bomba la tipper kuunganishwa katika bandari kumesababisha serikali kupata mapato kwa kampuni hiyo kujisimamia yenyewe.

Akizungumza katika ziara ya kikazi aliyoifanya bandarini hapo jana,  Nditye amesema, TPA kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na EWURA wafanye uchunguzi wa haraka kufahamu upotevu wa mapato ya serikali yaliyotokana na Tipper kujiunganishia mafuta kutoka kwenye meli bila kupitia katika kituo cha Kurasini Oil Jet (KOJ).

Amesema Tipper  wamekiuka maagizo ya Waziri Mkuu, Kassim Majaaliwa yaliyolewa Februari mwaka jana  ya kutaka waunganishe bomba lao katika mfumo wa TPA ili kufahamu kiwango cha mafuta wanayoyachukua.

" Wizi wa waziwazi  tangu Februari mwaka jana alipoagiza Waziri  Mkuu  hadi leo TIPPER mmeshindwa kuunganisha bomba lenu hali inayochangia mapato ya Serikali kuzidi kupotea," alisema Nditye.

Amesema TIPPER waliagizwa na waziri ndani ya mwezi.mmoja wawe wamejiunga katika.mfumo huo lakini cha ajabu maaagizo yamekiukwa hali inayoashiria bado kuna ujanja unaendelea.

Amesema haiwezekani TIPPER wakajiunganisha wenyewe halafu wakajisimamia wao.kufahamu kiwango cha mafuta ya dizeli na ya kula wanayotumia.

Aliagiza pia TPA iimarishe ulinzi kwa mtoa taarifa za upotevu wa mafuta hayo na endapo atapata madhara Serikali.itachukua hatua.

Awali Meneja Mafuta wa Bandari ya Dar es Salaam, Kapteni Paul Paul alisema TIPPER wamekiuka.agizo la waziri Majaliwa ambapo hadi sasa hawajajiunganisha katika mfumo wa bomba linalodhibitiwa na TPA.

Amesema hadi sasa makampuni yaliyounganishwa katika mfumo wa TPA ili kuangalia kiasi cha mafuta kinachotumika ni pamoja na Lake Oil,  Moil, Hass pamoja na World Oli/Sahara/Kobil.

Paul alisema kitendo cha mita za mafuta ya TIPPER kudhibitiwa na wenyewe linatakiwa liangaliwe kwani lina athari.

 Mkurugenzi Msaidizi wa TIPPER, Paul Mzava alisema, walipokea.maelekezo kutoka kwa Msajili wa hazina kusitisha kuhamishwa kwa bomba hilo mara baada ya waziri Majaaliwa kutoa agizo. Alisema taarifa hizo walizipeleka kwa uongozi wa TPA kwa maandishi.

Mzava alisema kuhamishwa kwa bomba linalomilikiwa na TIPPER kulipeleka kwenye mfumo wa TPA kuna umbali wa mita 400 hivyo waliona ni gharama kulihamisha. Alisema pia waliona katika kituo kile cha KOJ kitahamishwa muda wowote hali itakayochangia hasara.

Akijibu hoja hizo, Mhandisi Deusdetit Kakoko alisema alichokuwa anafahamu ni kuwa tayari TIPPER wamejiunga na mfumo wao.

 "Binafsi nilipewa taarifa kuwa tayari TIPPER wamejiunga katika mfumo wetu kinyume na hapo sina taarifa nyingine,"alisema Kakoko.

Alisema kutokana na hali hiyo atahakikisha anafuatilia undani jambo hilo pamoja na.kuwawajibisha watendaji waliokwenda.kinyume na agizo hilo.
 Naibu  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi  Ashasta Nditye akizungumza na Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) katika ziara yake alipotembelea mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini  (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko  akitoa taarifa za utendaji wa mamlaka hiyo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi  Ashasta Nditiye (Kushoto) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea mamlaka ya Bandari jijini Dar es Salaam.
 Naibu  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi  Ashasta Nditiye akizungumza katika ujenzi wa scanner ya ukaguzi katika bandari ya Dar es Salaam.
Naibu  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano ,Mhandisi  Ashasta Nditiye akifanya majumuisho baada ya kufanya ziara katika bandari ya Dar es Salaam.

WAZIRI KIGWANGALLA ATANGAZA KAMATI YA SHEREHE ZA MWEZI WA URITHI WA TANZANIA

December 08, 2017
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamisi Kigwangalla  mapema leo Desemba 8,2017 Mjini Dodoma, ameunda kamati ya kuongoza maandalizi ya namna watanzania na wageni wa Tanzania watakavyosherehekea Utanzania wao  kwenye mwezi maalum utakaojulikana kama ‘TANZANIA HERITAGE MONTH’.
Akielezea wakati wa kutangaza kamati hiyo iliyojumlisha wadau mbalimbali wakiwemo wanahabari, wanamichezo na wadau wengine mbalimbali na wafanyabishara, amesema:
“Kwenye mwezi huu kila kitu kitakuwa cha kitanzania na tutataka kwenye kila ofisi ya umma, ofisi binafsi, shule, chuo, hotel, balozi zetu n.k mtu akifika tu, ‘utanzania’ wetu uonekane!” alieleza Dk.Kigwangalla.
Utanzania huo ambapo kila mwezi huo utakapofika ambapo moja ya mambo hayo ni pamoja na aina ya mavazi maalum, vyakula,  na mambo mengine yanayobeba na kujumuisha Utanzania.

VPL: MUDATHIR YAHAYA MCHEZAJI BORA NOVEMBA

December 08, 2017

Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.
Mchezaji wa timu ya Singida United ya Singida, Mudathir Yahaya amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi Novemba, 2017 wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) Tanzania Bara msimu wa 2017/2018.
Mudathir alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, Beki Asante Kwasi wa Lipuli ya Iringa na Mshambuliaji Danny Usengimana pia wa Singida United, alioingia nao fainali ya kuwania nafasi hiyo.
Katika uchambuzi uliofanywa Dar es Salaam wiki hii kwenye kikao cha Kamati ya Tuzo za VPL zinazotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutokana na mapendekezo kutoka kwa makocha waliopo viwanja mbalimbali ambavyo ligi hiyo inachezwa msimu huu.
Mchezaji huyo alitoa mchango mkubwa kwa Singida United mwezi huo ikipata pointi saba katika michezo mitatu iliyocheza na kupanda katika msimamo wa ligi kutoka nafasi ya sita iliyokuwepo mwezi Oktoba hadi ya nne.
Singida United ilitoka 0-0 na Yanga, iliifunga Mbeya City mabao 2-1 na pia iliifunga Lipuli bao 1-0, ambapo Mudathir anayecheza nafasi ya kiungo alicheza dakika zote 270 sawa na michezo mitatu na hakuwa na kadi yoyote.
Alitajwa mchezaji bora wa mchezo wa Singida United na Yanga uliofanyika Uwanja wa Namfua, Singida, alicheza kwa kiwango cha juu wakati Singida United ilipochuana na Lipuli, pia alisaidia kutengeneza nafasi ambazo zilitumiwa vyema na wenzake katika kupata ushindi dhidi ya Mbeya City, huku yeye akihusika kwa kwa kiasi kikubwa kupambania ushindi huo.
Mafanikio yake kwa mwezi huo yalisaidia kumrudisha katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na kile cha Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’, ambacho kinashiriki michuano ya Chalenji inayoendelea nchini Kenya.
Kampuni ya Vodacom, ambao ndiyo wadhamini wa ligi hiyo ina utaratibu wa kuwazadiwa wachezaji bora wa kila mwezi, huku pia mwisho wa msimu kukiwa na tuzo mbalimbali zinazohusu ligi hiyo, ambapo msimu wa mwaka 2016/2017 kulikuwa tuzo 16 zilitolewa kwa washindi wa kada mbalimbali.
Mudathir atazawadiwa Sh milioni moja kutoka Vodacom pamoja na kisimbusi (decoder) cha Azam kwa kuibuka Mchezaji Bora wa mwezi.
YONDANI KUIKOSA RWANDA, MBARAKA NAFUU

YONDANI KUIKOSA RWANDA, MBARAKA NAFUU

December 08, 2017
Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.
Beki wa timu ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ Kelvin Yondani ataukosa mchezo dhidi ya Rwanda utakaofanyika kesho Jumamosi Desemba 9, 2017 kwenye Uwanja wa Kenyatta, Machakos Kenya.
Yondani amepewa mapumziko ya siku tatu baada ya kupata majeraha ya kifundo cha mguu kwenye mchezo wa jana dhidi ya Zanzibar.
Hivyo atakosa mchezo huo wa kesho ukiwa ni miongoni mwa mechi mechi za michuano ya kuwania Kombe la Afrika Mashariki maarufu kama Cecafa Senior Challenge inayofanyika hapa Kenya.
Jopo la Madaktari wa Kilimanjaro Stars linaloundwa na Dk. Richard Yomba na Dk Gilbert Kigadye limethibitisha kuwa majeraha aliyoyapata Yondani sio makubwa na yanahitaji apumzike kwa saa 72 ambazo ni sawa na siku tatu.
Vipimo vilivyochukuliwa vinaonesha kuwa hakuna mfupa wowote ulioathirika zaidi ya kupata mshtuko kiasi kwa hiyo wamempa siku tatu za mapumziko wakiendelea kumtazama maendeleo yake kwa ukaribu.
Kwa upande wa Mbaraka Yusuph ambaye alipata majeraha ya misuli kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Libya, amepona na anatarajia kuingia kwenye program ya utimamu wa mwili.
Hata hivyo Mbaraka hataweza kucheza kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Rwanda.

Wakati huo huo, leo kikosi cha Kilimanjaro Stars kimefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Machakos Academy licha ya mvua zinazoendelea kunyesha hapa County ya Machakos.
Kilimanjaro inajiandaa na mchezo wa kesho dhidi ya Rwanda utakaochezwa saa 8 mchana kwenye Uwanja wa Kenyatta, Machakos.
Mchezo huo wa kundi A una umuhimu mkubwa kwa Kilimanjaro Stars katika harakati zake za  kuitafuta tiketi ya kucheza hatua ya nusu fainali.
Kilimanjaro Stars ina pointi moja mpaka sasa baada ya kutoka sare na Libya kwenye mchezo wa kwanza kabla ya kufungwa na Zanzibar kwenye mchezo wake wa pili.
Kundi A linaongozwa na  Zanzibar wenye pointi sita (6) wakifuatiwa na Uganda wenye pointi (4) wakati Libya yenyewe ina pointi (3) ikikamata nafasi ya tatu ikifuatiwa na Kilimanjaro Stars na Rwanda wenye pointi (1) kila mmoja.

WATENDAJI NA WATAALAMU WA WILAYA YA HANDENI WATAKIWA KUSIMAMIA SUALA LA ELIMU YA MADHARA YA UKEKETAJI

December 08, 2017
Watendaji na wataalamu wa Wilaya ya Handeni wametakiwa kusimamia na kuweka suala la elimu ya madhara ya ukeketaji kuwa ajenda rasmi kwenye vikao vyao ngazi ya Kata na Tarafa ili kukomesha kabisa vitendo vya ukeketaji kwa watoto wa kike wa jamii ya wafugaji hususani pindi mradi wa “KIJANA WA LEO” unaofadhiliwa na shirika la Amref kukoma.

.Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe ametoa rai hiyo leo alipohudhuria sherehe za uvushwaji rika wa wasichana 170 wa jamii ya wafugaji(Ndito) zilizofanyika Kata ya Malezi katika mtaa wa Kwamadule.

Mh. Gondwe alisema kuwa ni haki ya binti anapokuwa mtu mzima na kuvushwa rika asiweze kunyanyaswa kijinsia, kwasababu athari za ukeketaji zinafahamika ikiwa ni pamoja na kuwa ni kitendo ambacho ni kinyume na maagizo ya Mungu lakini pia uvunjwaji wa haki za binadamu..

Ameongeza kuwa jamii ya wafugaji inatamaduni zilizoshiba na wanachangia kwa kiasi kikubwa kuingizia pato na fedha za kigeni Taifa, ni utamaduni bora unaotambulisha Tanzania kwa zaidi ya makabila 120.Watu wanapenda tamaduni za kimasai na jamii za wafugaji wengine lakini mila ambazo ni potofu zinazoleta maumivu katika jamii zitokomezwe.

“ sherehe na kila kitu kifanyike, watoto wafundishwe lakini ukeketaji hapana ili tumuokoe binti huyu na maumivu makali kwa sababu morani wamekubali kuoa wananwake ambao hawajakeketwa na kwasasa wanaoa hata jamii zingine ambazo wanawake hawajakeketwa” alisema Mkuu wa Wilaya.

Aidha aliwataka wataalamu wote ngazi ya Tarafa Hadi vitongoji ikiwa ni pamoja na idara zote hususani Elimu na Mendeleo ya jamii kuendelea kutoa elimu na kubaini wale ambao bado wanaendeleza vitendo vya ukeketaji kwa siri ili kuchukua hatua za kisheria kwasababu wanakwenda kinyume na haki za binadamu na kisheria hairuhusiwi.

Wakati huohuo alizitaka jamii za kifugaji kuweka kipaumbele suala la elimu kwa watoto kwasababu ni haki yao ya msingi na kwamba hakuna gharama yoyote mzazi ataipata kwa kumuelimisha mtoto ili jamii yote ielimike.

Kwaupande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Handeni Bw.Kenneth Haule alisema kuwa huu sio wakati wa kutegemea mifugo na ardhi katika kuendesha maisha pekee, kwa sababu dunia na jamii kwa ujumla inabadilika, lazima wafugaji wabadilike ili kuendana na hali ya mazingira kwa kuwasomesha watoto wao ili waje kuelimisha jamii zao na kupinga ukeketaji.

Meneja mradi wa Amref Health Africa Dk.Aisha Byanaku amesema kuwa lengo kuu la mradi ni kuborehsa afya ya uzazi kwa vijana ambao wako katika umri wa miaka 10-24 ambapo hadi sasa elimu kwa jamii ya wafugaji imetolewa ikiwa ni pamoja na mangariba, watoa huduma za afya na viongozi wa kimila.

Mradi wa “KIJANA WA LEO”ulizinduliwa na Amref Health Africa Wilayani Handeni Octoba 2015 ukifadhiliwa na Allen&Overy na big Lottery fund ambapo hadi sasa jumla ya wasichana 830 wamefanyiwa sherehe za kimila (kuvushwa rika) bila kukeketwa kwa Kata za Malezi,Msomera na Kwamagome za Wilaya ya Handeni.

Sherehe za uvushwaji rika zimehudhuriwa na wakurugenzi wa Handeni na wataalamu mbalimbali wa Halmashauri ya Mji na Wilaya ya Handeni.

Imetolewa na:

Kitengo cha Teknolojia, Habari na Mawasiliano
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe akikaribishwa kwenye sherehe za uvushaji rika.
 Morani na Ndito wakiwa wamejipanga na kucheza wakati wa sherehe za uvushaji rika.
 mangariba wakionesha namna ambavyo  huwakamata wasichana (ndito) wa kimasai kuwapeleka kwenye chumba cha ukeketaji.
  Mkuu wa Wilaya ya Handeni akizungumza na Mangariba na kuwapongeza kuelimika kuacha vitendo vya ukeketaji kwa watoto wa kike.
  ​mmoja wa wazee wa kimila akishukuru nAmref kwa alimu waliyopewa juu ya uvuhsaji rika wasichana kwa kufanya sherehe na mila zao bila kukeketa.​
​Mratibu wa mradi  kutoka Amref Health Africa Dk.Aisha Byanaku akitoa maelezo na malengo makuu ya mradi wa KIJANA WA LEO,​
​ mmoja wa wsichana waliovushwa rika bila kukeketwa akipokea cheti cha kufuzu mafunzo ya kuzuia ukeketaji na mafunzo ya afya ya uzazi​.

WATAKAOKUTWA NA BIDHAA ZA MAGENDO MUHEZA KUSHTAKIWA KWA UHUJUMU UCHUMI

December 08, 2017

MKUU wa wilaya ya Muheza mkoani Tanga, Mhandisi Mwanasha Tumbo amesema wananchi watakaokutwa na bidhaa za magendo kwenye nyumba zao watakamatwa na kupelekwa kwenye vyombo vya sheria wakishtakiwa kwa kosa la kuhujumu uchumi wa nchi.

Hatua hiyo ina lengo la kuhakikisha biashara za magendo ambazo zimekuwa zikiingizwa wilayani humo kupitia bandari bubu ya Kigombe zinakoma ikiwa ni mkakati wa kukabiliana kwa vitendo ili kukomesha shughuli hizo ambazo zinaisababishia serikali kukosa mapato.

Aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kigombe kata ya Kigombe wilayanu humo katika mkutano wa hadhara uliofanyika  kuhusiana na operesheni zinazoendesha na Jeshi la Polisi mkoa wa Tanga kudhibiti biashara hizo ambazo zimekuwa kikwazo cha kukusanya mapato.

Alisema biashara za magendo vimekuwa na athari kubwa kwa ukuaji wa uchumi wanchi kutokana na kukosa mapato ambayo yangeweza kuwasaidia katika harakati mbalimbali za kimaendeleo kwa wananchi kwenye maeneo mbalimbali nchini.

“Niwaambie tu tukija nyumbani kwako tukikuta dawa za kuleva na bidhaa za magendo tutawachukua watu wote watakaokutwa na kuwashtaki kwa kosa la uhujumu uchumi lakini hata wale watakaokuwa na dawa za kulevya watakamatwa “Alisema.

“Lakini pia niwatake wananchi mtoa ushirikiano kwa operesheni
inayoendelea kwenye eneo hili kwa kutoa taarifa ambazo zinaweza kusaidia kufanikisha suala la biashara za magendo na dawa za kulevya linatoweka kwenye maeneo yenu “Alisema.

Akizungumza katika mkutano huo mmoja wa wananchi wa kijiji hicho, Mohamed Khatibu alilalamikia kitendo cha askari kupekua nyumba zao kwa madai ya kusaka bidhaa za magendo kitendo ambacho sio kizuri.

“Kwa kweli kitendo cha askari kuja nyumbani kwetu na kuanza kutupekua tena bila kibali sio cha kiungwana hivyo tunaomba suala hilo lifanyiwe kazi na mamlaka zinazohusika “Alisema.
MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM ) RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO WA TISA WA UMOJA WA WANAWAKE TANZANIA (UWT) MJINI DODOMA

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM ) RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO WA TISA WA UMOJA WA WANAWAKE TANZANIA (UWT) MJINI DODOMA

December 08, 2017

1
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM , Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wajumbe wa mkutano  Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kabla ya kufungua mkutano wao wa Tisa uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma.
4..
Wajumbe wa mkutano wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wakishangilia kabla ya ufunguzi wa  mkutano huo wa tisa wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma.
5
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akivalishwa Kitambaa kichwani mara baada ya kutangaza kuhamia Chama cha Mapinduzi CCM katika Mkutano wa tisa wa (UWT) uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma.
6
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira mara baada ya kuhamia rasmi katika Chama cha Mapinduzi CCM katika mkutano wa wa tisa wa UWT uliofanyika mjini Dodoma.
7
Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira mara baada ya kutangaza kuhamia Chama cha Mapinduzi CCM katika mkutano wa tisa wa UWT uliofanyika mjini Dodoma.
8
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiimba  nyimbo za CCM pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan wa pili kutoka (kushoto), Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wa pili kutoka (kulia), Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wakwanza kulia mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa tisa wa UWT uliofanyika mjini Dodoma.
9
Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson akishangilia katika mkutano huo wa tisa wa UWT uliofanyika mjini Dodoma.
10
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo mara baada ya kufungua mkutano huo wa tisa wa (UWT) mjini Dodoma.
11.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasalimia wajumbe wa Mkutano wa Tisa wa UWT mjini Dodoma.
12
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimsalimia Mama Maria Nyerere ambaye pia alihudhuria katika mkutano huo wa wa Tisa wa UWT uliofanyika mjini Dodoma.
13
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akizungumza katika mkutano huo wa UWT uliofanyika mjini Dodoma.
14
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa CCM, Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma pamoja na bendi ya Tanzania One Theater TOT wakati ikitumbuiza katika mkutano huo wa tisa wa UWT uliofanyika mjini Dodoma.
15
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akicheza pamoja na wajumbe wengine wa UWT mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo wa tisa wa UWT uliofanyika mjini Dodoma.
18
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akizungumza jambo na Mama Maria Nyerere mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT uliofanyika mjini Dodoma.
PICHA NA IKULU

Tigo Yatoa Mamilioni kwa Washindi wa Promosheni ya Msimu wa Sikukuu

December 08, 2017
Afisa Vigezo wa Tigo, Abdallah Nguba (kushoto) pamoja na Meneja wa Wateja wa Tigo Mary Rutta (kati) wakifanya droo ya kuwapata washindi wa promosheni inayoendelea ya 'Tumia Tigo Pesa na ushinde,' ambapo wateja wa Tigo wanapata fursa ya kushinda hadi milioni 15 kila wanapotumia Tigo Pesa. Jumla ya wateja 20 walijishindia kati ya shilingi laki tano na milioni moja leo. Kulia ni Afisa wa Bodi ya Michezo ya Bahati na Sibu Tanzania, Jehud Ngolo. 

Meneja wa Wateja wa Tigo Mary Rutta (kulia) akiwatangaza washindi wa  wa promosheni inayoendelea ya 'Tumia Tigo Pesa na ushinde,' ambapo wateja wa Tigo wanapata fursa ya kushinda hadi milioni 15 kila wanapotumia Tigo Pesa. Jumla ya wateja 20 walijishindia kati ya shilingi laki tano na milioni moja leo. Kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael

Mojawapo ya washindi wa promosheni inayoendelea ya 'Tumia Tigo Pesa na ushinde,', Saidi Khatib Kiko, mkaazi wa Kimara akionesha sura ya furaha ya ushindi wakati wa hafla ya kukabidhiwa zawadi iliyofanyika katika ofisi za Tigo jijini Dar es salaam leo. Saidi alikuwa mojawapo ya washindi 20 waliojinyakulia kati ya shilingi laki tano na shilingi milioni moja katika promosheni hiyo ambapo wateja wa Tigo Pesa wana nafasi ya kujishindia hadi shilingi milioni 15.   
Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kushoto) akiwatangaza washindi wa  wa promosheni inayoendelea ya 'Tumia Tigo Pesa na ushinde,' ambapo wateja wa Tigo wanapata fursa ya kushinda hadi milioni 15 kila wanapotumia Tigo Pesa. Jumla ya wateja 20 walijishindia kati ya shilingi laki tano na milioni moja leo. Kulia ni Meneja wa Wateja wa Tigo, Mary Rutta.




  • Wateja 20 wapokea zawadi kemkem za pesa kwa kufanya miamala kupitia Tigo Pesa


Dar es Salaam, 8 Novemba, 2017- Huduma ya kutuma na kupokea fedha inayoongoza nchini Tanzania, Tigo Pesa leo imewatangaza na kuwazawadia washindi 20 wa promosheni yake ya ‘Tumia Tigo Pesa na Ushinde,’ inayoendelea katika msimu huu wa Krismasi na Mwaka mpya ambapo wateja wanajishindia mamilioni ya pesa.


Washindi wanne (4) wamepata bahatiya kushinda zawadi za kila siku za shilingi milioni moja kila mmoja, huku wengine 16 wakijaza mifuko yao na donge nono la shilingi laki tano (TZS 500,000) kila mmoja.  each. Jumla ya shilingi milioni 12 zimetolewa kama zawadi kwa wiki  hii.


Washindi wa zawadi za TZS 1 milioni ni wafanyabiashara Neema Fredrick Mosha, Fredrick Joseli Mponzi , Sefu Athumani Sefu na Hadija Mohamed Lukulumbale ambaye ni mama nitilie.


Washindi  wa zawadi za TZS 500,000 ni Michael Joseph Moshi, Moses Muhonga Amuli, Saidi Khatib Kiko, Sylvester Michael Madaga, Aziza Ramadhani Ngozi, Evelyne Gwamaka Mwakyembe, Tumsifu Harold Temu na Sikudhani Constantine Mwenda. Wengine walioshinda TZS 500,000 ni Queentina Msafiri Mbwambo, Hilary Andrew Massawe, Ashura Ally Salim, Halima Saidi Shaabani, Fatuma Ally Makumbo, Halima Saidi Sangiwa, Jenifer Samuel Apolinale na James John Mkanula.


‘Tunatarajia kupata jumla ya washindi 153 katika kipindi cha mwezi mmoja wa promosheni hii. Bado tuna zawadi za thamani ya TZS 108 milioni kutoa kwa washindi 133,’ Meneja wa Wateja wa Tigo, Mary Rutta alisema wakati akikabidi zawadi kwa washindi Dar es Salaam leo.


Alibainisha kuwa pamoja na zawadi za kila siku, promosheni hiyo ya ‘Tumia Tigo Pesa na Ushinde,’  itakuwa na zawadi kubwa za mwezi  TZS 15 milioni, TZS 10 milioni na TZS 5 milioni.


‘Kushiriki katika promosheni hii ni rahisi na ni wazi kwa wateja wote wa Tigo Pesa ambao wanahitaji kutumia huduma ya Tigo Pesa kwenye simu zao ili kupata nafasi ya kushinda. Kadri unavyotumia huduma ya Tigo Pesa ndivyo unavyojiongezea nafasi ya kushinda,’ alisema.


Tigo Pesa inajivunia kufanya miamala ya zaidi ya TZS 1.7bn kila mwezi kupitia mtandao wake mpana wa mawakala zaidi ya  70,000 waliosambaa nchini kote.  

                                                                                 

Biharamulo Wafurahia Huduma za Kisasa Kutoka Duka Jipya la Tigo.

December 08, 2017

Afisa Habari na Mawasiliano wilaya ya Biharamulo, Jonathan Rwekaza akiongea na waandishi na wakazi wa Biharamulo waliohudhuria uzinduzi wa duka la kisasa la Tigo wilayani humo.


Baadhi ya wakazi na Biharamulo wakifuatilia uzinduzi wa Duka jipya la kisasa la Tigo

Meneja Mauzo wa Tigo Biharamulo, Abraham Mchau akiongea na waandishi na wakazi wa Biharamulo waliohudhuria uzinduzi wa duka la kisasa la Tigo wilayani humo.

Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Biharamulo, ambaye ni Afisa Habari na Mawasiliano Biharamulo, Jonathan Rwekaza(kushoto), akikata utepe kuzindua duka jipya la kisasa la kampuni ya Tigo wilayani humo leo. Wanaoshuhudia ni Meneja wa Tigo mkoani Kagera, Sadok Phares (katikati) na Meneja Mauzo wa Tigo Biharamulo, Abraham Mchau


Afisa Mauzo wa Duka hilo, Lucy Ernest akifafanua jambo kwa Afisa Habari na Mawasiliano wilaya ya Biharamulo, Jonathan Rwekaza kuhusu  bidhaa mbalimbali ndani ya duka jipya la Tigo Biharamulo. 
Afisa Mauzo wa Duka hilo, Lucy Ernest akifafanua jambo kwa Afisa Habari na Mawasiliano wilaya ya Biharamulo, Jonathan Rwekaza kuhusu  bidhaa mbalimbali ndani ya duka jipya la Tigo Biharamulo.

Picha ya pamoja

Biharamulo, 7 Desemba, 2017- Katika mwendelezo wa harakati za kuhakikisha kuwa wateja wake wote wanapata huduma bora kwa urahisi, kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali Tigo Tanzania leo imezindua duka kubwa la kisasa wilayani Biharamulo katika Mkoa wa Kagera.

Duka hilo jipya linapatikana katika Jengo la Yusuph Katri lililopo Stendi ya Mabasi ya Biharamulo, mkabala na Kituo cha Polisi na lina uwezo wa kuwahudumia wateja zaidi ya 700,000 wa Tigo wanaopatikana wilayani hapo na viunga vyake.

Akizungumza katika hafla fupi ya kuzindua duka hilo jipya la Tigo, Meneja Mauzo wa Tigo - Biharamulo, Abraham Mchau alisema kuwa ufunguzi wa duka hilo jipya unaendana na mpango wa upanuzi na ukuaji wa kampuni hiyo ya simu unaolenga kuongeza idadi ya vituo vya huduma kwa wateja huku ikihakikisha kuwa bidhaa na huduma zote zinapatikana kwa urahisi na wateja wake nchi nzima.

‘Tigo imejizatiti kufanya uwekezaji utakaohakikisha wateja wetu wanapata huduma kwa viwango vya kimataifa ili waweze kupata suluhisho muafaka kwa mahitaji yao. Ufunguzi wa duka hili la kisasa mjini Biharamulo kunafanya idadi ya maduka yetu ya Tigo kufikia 15 katika Ukanda huu wa Ziwa, huku jumla ya maduka yetu yote ya Tigo nchini ikifikia 75,’ alisema.

‘Uzinduzi huu unaendana na sifa kuu ya Tigo kuwa mtandao unaowaelewa zaidi wateja wake na kuwapa bidhaa na huduma bora, za kibunifu, zinazoendana na mahitaji yao. Tunaendelea kuwekeza katika upanuzi na uboreshaji wa mtandao wetu wa simu, ili kuhakikisha kuwa kila mmoja anakuwa sehemu ya mabadiliko na faida za ulimwengu wa kidigitali unaoongozwa na Tigo,’ Mchau alifafanua.

Kwa upande wao, wakaazi wa Biharamulo wameelezea kufurahishwa kwao na ujio wa duka hilo jipya la Tigo kwani litawapunguzia adha ya kusafiri kwa mwendo mrefu kupata ufumbuzi wa matatizo yao ya simu pamoja na kuboresha upatikanaji wa huduma za simu katika wilaya hiyo.