December 30, 2013
3
Ernest Mangu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Desemba 30, 2013, amemteua Kamishna wa Polisi Ernest Mangu kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.
 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa usiku wa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa Kamishna Mangu anachukua nafasi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini anayestaafu, Saidi Mwema.
 
Kabla ya uteuzi wake unaoanza keshokutwa, Januari Mosi, 2014, Kamishna Mangu alikuwa Mkurugenzi wa Inteligensia ya Jinai (Director of Criminal Intelligence) katika Jeshi hilo la Polisi.
 
Aidha, taarifa hiyo inasema kuwa Rais Kikwete amemteua Kamishna Abdulrahman Kaniki kuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, ambayo ni nafasi mpya katika muundo wa sasa wa Jeshi la Polisi.
 
Kabla ya uteuzi wake, Kamishna Kaniki alikuwa Kamishna wa Uchunguzi wa Kijinai (Commissioner for Forensic Investigations). 
 
 Mkuu wa Jeshi la Polisi mpya ataapishwa kesho, Jumanne,  Desemba 31, 2013 katika Viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam.
December 30, 2013

RAIS KIKWETE AKABIDHIWA RASIMU YA KATIBA (TOLEO LA PILI) LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akipokea Rasimu ya pili ya katiba mpya kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba mpya, Joseph Warioba, wakati wa hafla ya kukabidhiwa rasimu hiyo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo. Akizungumza katika hafla hiyo Rais, aliitaka Tume hiyo kuiweka Rasimu hiyo kwenye mitandao ili wananchi waweze kuisoma na kuielewa na kuweza kutoa maoni yao kwa urahisi kupitia mitandao.
 Naye Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Warioba, alisema kuwa kulingana na idadi ya kura zilizopatikana kutoka kwa wananchi kuhusu uundwaji wa Serikali tatu, alisema kuwa idadi kubwa zaidi ni ya watu walihitaji Serikali tatu kuliko walioipinga, hivyo Serikali tatu haipingiki ambapo kwa sasa itabaki ni kazi ya maamuzi ya Bunge la Katiba linalotarajia kuungwa mapema mwezi Januari mwakani.
 Rais jakaya Kikwete, akimkabidhi raismu hiyo Makamu wake baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume ta katiba mpya.
 Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi Risimu hiyo, Spika wa Bunge, Anne Makinda na baadhi ya viongozi.
 Baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Siasa, waliohudhuria hafla hiyo.
 Baadhi ya waasisi waliokabidhiwa Rasimu hiyo na Rais kikwete, baada ya kukabidhiwa.
 Tundu Lissu, na wenzake wakiangua kicheko baada ya kutaniwa na Rais wakati akisoma hotuba yake kwenye hafla hiyo.
 Zitto Kabwe, akiisoma Rasimu hiyo kwa makini.......
 Jaji Warioba, akimkabidhi Rasimu hiyo, Rais wa Zanzibar, Dkt. Mohamed Shein.
 Rais akipokea Rasimu hiyo.....
 Rais Jakaya Kikwete akihutubia baada ya kupokea Rasimu hiyo.
 Eti na huyu jamaa naye alikuwa akisikiliza kwa makini hotuba ya Rais kuhusu Rasimu hiyo...
 Mtangazaji wa ITV na Redio One, Alfred Masako (kushoto) na Dkt. Kitila, wakisikiliza kwa makini hotuba ya Rais.
 Sehemu ya wananchi na viongozi waliohudhuria hafla hiyo.
 Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Warioba, akizungumza.
 Umakini wa kusikiliza....
 Rais Jakaya akiteta jambo na Jaji Warioba.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Prof. Ibrahim Lipumba.
Picha ya pamoja...... RASIMU YA KATIBA MPYA NA HOTUBA YA RAIS JAKA KIKWETE ITAWAJIA HIVI PUNDE.
December 30, 2013
 WAUGUZI LAWAMANI KWA KUSABABISHA MAMA AJIFUNGULIE  NJE.
Picture
Sabina Mwakyusa (28) anayedai alifukuzwa na wauguzi wodini na kujifungulia nje ya geti usiku huku mvua ikinyesha akiwa na Mama yake mzazi, Rhoda Mwakyusa(50) aliyembeba mwanaye huyo aliyezaliwa.
Na Gordon Kalulunga, Mbeya -- HOSPITALI teule ya wilaya ya Mbeya (Ifisi-Mbalizi), imekumbwa na kashfa ya kufukuza wajawazito wodini kisha wajawazito hao kujifungulia katika mazingira yasiyo na staha nje ya hospitali.

Tukio la hivi karibuni limetokea usiku wa Desemba 19, mwaka huu, ambapo baadhi ya wauguzi waliokuwepo katika chumba cha matazamio ya kujifungua, wanadaiwa kumfukuza na kumpiga mjamzito Sabina Mwakyusa (28) mkazi wa Kijiji cha Iwala, kata ya Utengule Usongwe wilayani humo.

DKT. SHEIN AZINDUA RASMI JENGO JIPYA LA KIWANDA CHA UCHAPAJI ZANZIBAR

December 30, 2013

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akifungua pazia kuashiria ufunguzi rasmi wa Jengo jipya la Kiwanda cha Uchapaji Zanzibar na Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, huko Maruhubi Mjini Unguja, ikiwa ni katika shamra shamra za Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar,(kulia) ni Waziri Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed.
 Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Dr. Aboud Sheikh Rajab, akitoa maelezo kwa  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) alipotembelea jengo jipya la kiwanda cha uchapaji, Maruhubi jana,ikiwa ni shamra shamra za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

BASI JIPYA LA AZAM LAWASILI...KAMA LA KLABU KUBWA ZA ULAYA

December 30, 2013
Hakuna Afrika nzima; Basi jipya la wachezaji wa klabu ya Azam FC ya Dar es Salaam, lililowasili nchini juzi likiwa tayari kusafirishwa visiwani Zanzibar ambako timu hiyo imekwenda kushiriki Kombe la Mapinduzi. Hili ni aina ya mabasi ambayo yanatumiwa na klabu za Ulaya kama Manchester United, Bayen Munich na Barcelona ambalo kwa Afrika Azam inaweza kuwa klabu ya kwanza kulimiliki.
Kitu cha maana
Kila siti ina TV
Kuna friji
Kuna choo i