PICHA ZA MATUKIO STARS NA HARAMBEE

May 29, 2016

Kikosi cha kwanza cha timu ya Soka ya Tanzania -Taifa Stars kilichoanza dhidi ya Harambee Stars ya Kenya Jumapili.

Mshambuliaji wa Taifa Stars, Elias Maguli (Kulia) akichuana na David Odhiambo wakati wa mchezo wa kirafiki wa Kimataifa uliofanyika Uwanja wa Moi Kasarani, Nairobi Kenya. timu hizo zilitosahana nguvu kwa kutoka sara ya 1-1.

Winga wa Taifa Stars, Shiza Ramadhani akichuana na beki Joakins Atudo wa Harambee Stars katika mchezo huo.

BenPol Akonga Nyoyo za maelfu wa mashabiki katika Tamasha la Nyama Choma Jijini Dar es salaam

May 29, 2016
 Mwanamuziki mahiri  wa Rnb hapa nchini  , Bernard Michael Paul, maarufu kama ‘Ben Pol’ akitoa burudani  kwa maelfu ya wakazi wa Dar es salaam waliohudhuria maadhimisho ya miaka mitano ya  Tamasha la Nyama choma 2016,ambapo Tigo ilimdhamini kutumbuiza katika tamasha hilo , mapema jana usiku katika viwanja vya Leaders Jijini Dar es salaam .

BEN POL akicheza na mashabiki zake jukwaani wakati wa tamasha la nyama choma katika viwanja vya leaders Jijini Dar es salaam 
Mashabikiwa muziki wa bongo fleva wakishangilia wakati Benpol anatumbuiza kibao chake cha MOYO MASHINE 

Benpol akihojiwa na mtangazaji wa Clouds fm Askofu Tza baada ya kutumbuiza katika tamasha la Nyama choma mapema jana katika viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam.
Baadhi ya mawakala wa tigo waliokuwepo katika viwanja  vya Leaders kutoa msaada na huduma mbali mbali toka tigo ikiwemo huduma za intaneti ya kasi ya Tigo 4G LTE
Wakala wa tigo akisajili laini ya mteja katika tamasha la Nyama choma mapema jana usiku katika viwanja vya Leaders Jijini Dar es salaam.


Mtangazaji wa Choice fm na mshindi wa Bigbrother 2014 Idris sultan akifurahi jambo na Mcheza kikapu wa kimataifa Hasheem Thabit wakati wa Tamasha la Nyama Choma lililofanyika mapema jana usiku katika viwanja vya leaders jijini Dar es salaam.
Msanii mahiri wa Bongo fleva Vanessa Mdee akiongea jambo na mmoja wa shabiki zake katika viwanja  vya Leaders Jijini Dar es salaam
Mabanda ya tigo yaliyokuwepo uwanjani katika kutoa huduma mbalimbali kwa wateja wa tigo  waliofika katika tamasha la Nyama Choma 

Mmoja wa wapishi wa nyama akichoma nyama wakati wa tamasha la Nyama Choma mapema jana katika viwanja vya leaders Jijini Dar es salaam.

Wadau wakiendelea kufurahia muziki na kula nyama choma katika tamasha liliofanyika mapema jana



Mmoja wa wakala wa Tigo akimsaidia mteja  kufungua intaneti ya tigo katika simu yake katika tamasha la Nyama Choma .liliofanyika mapema jana usiku katika viwanja vya Leaders Jijini Dar es salaam,
Maelfu ya wakazi waliofika katika tamasha wakifurahia muziki toka kwa wasanii mbali mbali waliotumbuiza jukwaani
photo Krantz Mwantepele Founder & CEO , KONCEPT Phone: +255-712579102 /+255-767392840 Email: krantzcharles@gmail.com Blog: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com Website;www.koncept.co.tz IMAGINE INSPIRE INFLUENCE
RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AFANYA ZIARA YA KICHAMA PEMBA

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AFANYA ZIARA YA KICHAMA PEMBA

May 29, 2016

sh1 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein akisalimiana na viongozi alipowasili katika viwanja vya Skuli ya Fidel Castro Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusnini Pemba leo alipofika kuwashukuru wanachama cha Mapinduzi CCM kwa ushindi waliompatia katika uchaguzi wa Marudio uliofanyika mwezi Machi mwaka huu,[Picha na Ikulu.] 29/05/2016.
sh3Wanachama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya chakechake Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akizungumza nao leo, wakati alipofika katika ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro leo kuwapongeza   kwa ushindi alioupata katika uchaguzi wa Marudio uliofanyika mwezi Machi mwaka huu,[Picha na Ikulu.]29/05/2016.
sh4 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akizungumza na wanachama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Chakechake Pemba wakati alipofika katika ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro leo kuwapongeza   kwa ushindi alioupata katika uchaguzi wa Marudio uliofanyika mwezi Machi mwaka huu,[Picha na Ikulu.]29/05/2016.
sh5Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) alipokuwa akizungumza na wanachama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Chakechake Pemba wakati alipofika katika ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro leo kuwapongeza   kwa ushindi alioupata katika uchaguzi wa Marudio uliofanyika mwezi Machi mwaka huu,[Picha na Ikulu.]29/05/2016.
sh6 
Kiembe Ramadhan Khamis kutoka Tawi la Mkoroshoni  akitoa mchango wake wakati  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wakati alipofika katika ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro leo kuwapongeza wanachama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Chakechake Pemba kwa ushindi alioupata katika uchaguzi wa Marudio uliofanyika mwezi Machi mwaka huu,[Picha na Ikulu.]29/05/2016.
sh7 
Balozi Mohamed Kombo Juma (Wawi) akitoa mchango wake wakati  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wakati alipofika katika ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro leo kuwapongeza wanachama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Chakechake Pemba kwa ushindi alioupata katika uchaguzi wa Marudio uliofanyika mwezi Machi mwaka huu,[Picha na Ikulu.]29/05/2016.
sh8Mwenyekiti wa Wilaya ya Chakechake Pemba akitoa taarifa wakati  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein (katikati) wakati alipofika katika ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro leo kuwapongeza WanaCCM kwa ushindi alioupata katika uchaguzi wa Marudio uliofanyika mwezi Machi mwaka huu,(kushoto) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai (kulia),[Picha na Ikulu.]29/05/2016.
sh9Wanachama cha Mapinduzi CCM wialayanya Chakechake akinyanyua mkono juu kuunga mkono maelezo ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein wakati alipofika katika ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro leo kuwapongeza kwa ushindi alioupata katika uchaguzi wa Marudio uliofanyika mwezi Machi mwaka huu,[Picha na Ikulu.

MAONYESHO YA BIASHARA TANTRADE YAFUNGULIWA TANGA LEO

May 29, 2016


 WATUMISHI wa Halmashauri ya jiji la Tanga wakibadilishana mawazo na wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji la TBC wakati wa maonyesho ya nne ya Tan Trade yanayofanyika kwa siku 10 Mwahako nje kidogo ya jiji la Tanga

 Mwandishi wa Shirika la Utangazaji TBC Mkoani Tanga, Betha Mwambellah, akiangalia moja ya bidhaa katika maonyesho ya Kibiashara yanayofanyika Tanga ambayo yamefunguliwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Chales Mwaijage leo.
 Waandishi wa habari Mkoani Tanga, Tunu Ligombe wa Cluud TV  (kulia) na Betha Mwambellah wa Shirika la Utangazaji (TBC) wakishangaa moja ya bidhaa za maonyesho yaliyofunguliwa leo Tanga.


 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Chales Mwijage, akikata utepe kuzindua  maonyesho ya nne ya biashara (Tan Trade) yanayofanyika Mwahako nje kidogo ya jiji la Tanga yanayofanyika kwa siku kumi .



 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Chales Mwijage, akipokea zawadi iliyotolewa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Tanga na Kaimu Meneja wa Bandari Tanga, Tryphone Ntipi  wakati wa maonyesho ya biashara (Tan Trade) yaliyofunguliwa leo Mwahako nje kidogo ya jiji la Tanga yanayofanyika kwa siku 10.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Chales Mwijage akipata Qahwa wakati wa maonyesho ya Biashara aliyoyazindua leo Tanga
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uchukuzi, Chales Mwijage, akiangalia viatu katika moja ya mabanda ya maonyesho ya biashara (Tan Trade) yanayofanyika Mwahako nje kidogo ya jiji la Tanga maonyesho ambayo yanafanyika kwa siku 10 na kufunguliwa leo.



Mwandishi wa Shirika la Utangazaji (TBC) Betha Mwambellah akifurahia jambo wakati wa maonyesho ya nne ya Tantrade yaliyofunguliwa leo na Waziri wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji, Chales Mwijage.

JK AWAFUNDA VIJANA WA CCM VYUO VIKUU JIJINI DAR ES SALAAM LEO JIONI

May 29, 2016
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete akihutubia katika mahafali ya 2016 ya Shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu wa CCM yaliyofanyika viwanja vya Karimjee Dar es Salaam leo jioni.
 Vijana vyuo vikuu Dar es Salaam wakiserebuka katika mahafali yao.
 Vijana hao wakiendelea kuserebuka.
 Hapa ni furaha kwa kwenda mbele.
Ni kama wanasema'  Hapa ni ushindi tu 2020 kwani vijana tumejipanga.
Vijana wakiwa kwenye mahafali hayo.

WADAU WACHANGAMKIA WINDHOEK TAMASHA LA NYAMA CHOMA VIWANJA VYA LEARDERS JIJINI DAR ES SALAAM

May 29, 2016
 Mtaalamu wa kuchoma nyama kutoka mkoani Arusha, Jackson Isaya akionesha ufundi wa kuchoma nyama katika Tamasha la Nyama choma lililofanyika ,viwanja vya Learders Dar es Salaam jana.
 Wadau wa Windhoek wakipata kinywaji hicho katika tamasha hilo.
 Mwonekano mpya wa bia ya windhoek.
 Timu nzima ya kutoa huduma ya Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd wakati wa tamasha hilo.
Wadau wa Windhoek wakionesha kinywaji hicho wakati wakinywa. Kulia ni Meneja wa Kampuni hiyo, Mr Ruta, Kushoto ni mdau wa Windhoek kutoka Kilimanjaro, Nurudin Sagafu na wa pili kulia ni  Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ya Mabibo, Jerome Rugemalira.

WILAYA YA MPWAPWA KUFANYA HARAMBEE YA KUPATA MADAWATI JIJINI DAR ES SALAAM JUNI 4, 2016

May 29, 2016
 Mkuu wa Wilaya  ya Mpwawa iliyopo mkoani Dodoma, Mohamed Utaly (wa pili kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu harambee ya kupata fedha za kununulia madawati itakayofanyika Juni 4 mwaka huu Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Donald Ngwenzi,Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Mohamed Maje na Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi, Samuel Albertus Coy.
 Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Mohamed Maje (kulia), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Donald Ngwenzi, akizungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Mohamed Utaly.

Na Dotto Mwaibale


HALMASHAURI ya Wilaya ya Mpwapwa Dodoma Juni 4 mwaka huu inatarajia kufanya harambe ya kupata fedha za kununulia madawati kwa ajili ya shule za msingi na sekondari wilayani humo ambayo itafanyika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi Mkuu wa Wilaya hiyo Mohamed Utaly alisema wamefikia hatua hiyo ili kukabiliana na uhaba wa madawati katika shule hizo ambapo pamekuwa na changamoto kubwa.

Alisema awali halmashauri hiyo ilikuwa na upungufu wa madawati 16,000 lakini baada ya kuwashirikisha wananchi na kufanya harambee mbalimbali walifanikiwa kupata madawati 6000 na kubaki kiasi cha madawati 10,000 ambayo yanahitaji.

Utaly alisema halmshauri hiyo katika bajeti yake ya mwaka 2015-2016 ilitenga sh. milioni 180 kwa ajili ya madawati ambapo kunamafanikio makubwa ya kupata madawati hayo yaliyosalia hivyo akatumia fursa hiyo kuwaomba wadau mbalimbali wa ndani wa wilaya hiyo na nje kujitokeza katika harambee hiyo ili waweze kufanikisha jambo hilo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Mohamed Maje alisema changamoto kubwa waliyoibaini ni kutokuwa na kitengo cha kufanya ukarabati wa madawati yaliyo haribika ambacho hivi sasa kimeanzishwa.


"Kwa muda mrefu hatukuwa na kitengo cha kukarabati madawati yaliyoharibika lakini sasa tumekianzisha na kitasaidia kupunguza changamoto hiyo kwa kitengo hicho kitakuwa kikisaidia na wajasiriamali waliopo kwenye vikundi vya watu 20 ambavyo vipo sita kwa ajili ya kufanya kazi hiyo" alisema Maje.