RADIO 5 YAMKABIDHI MFUGAJI BORA KANDA YA KASKAZINI PIKIPIKI KUMWEZESHA KUFIKIA MALENGO

August 18, 2015

Meneja Masoko wa Radio 5 ,Sarah Keiya akizungumza kwenye kikao kabla ya kumkabidhi mshindi wa kwanza zawadi ya Pikipiki yenye thamani ya sh. milioni 2 mfugaji bora Kanda ya Kaskazini,John Alfayo ambaye ni mkazi Kijiji cha Olmotony wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha.

Meneja wa Benki ya Akiba Commercial tawi la Arusha(ACB)Issa Hango akizungumza namna mfugaji John Alfayo alivyonufaika na mikopo kutoka benki hiyo ambayo imemfanya kufikia mafanikio makubwa.

Meneja Masoko wa Radio 5 ,Sarah Keiya(kushoto) akipongezana na Meneja wa Benki ya Akiba Commercial tawi la Arusha(ACB)Issa Hango baada ya makabidhiano yaliyofanyika katika ofisi za Taso,Njiro jijini Arusha,wanaoshuhudia ni Bwana na Bi John Alfayo. 

Meneja wa Benki ya Akiba Commercial tawi la Arusha(ACB)Issa Hango (kulia)akimkabidhi Pikipiki mshindi wa kwanza katika ufugaji bora Kanda ya Kaskazini,John Alfayo na mkewe Hilda leo,anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima Kanda ya Kaskazini,Arthur Kitonga.

Meneja Masoko wa Radio 5 ,Sarah Keiya(kushoto) akiwakabidhi John Alfayo na mkewe hati za Pikipiki iliyotolewa na kampuni hiyo ambayo imekua ikiwasaidia wakulima kukabiliana na changamoto mbalimbali.

Maafisa wa Chama cha Wakulima Kanda ya Kaskazini(Taso)wafanyakazi wa Benki ya ACB tawi la Arusha,Radio 5 ,watumishi wa halmashauri ya Arusha DC na mshindi wa ufugaji bora wakiwa katika picha ya pamoja baada ya makabidhiano.
Habari Picha na Filbert Rweyemamu-Arusha

UKAWA WATANGAZA MAJIMBO WALIYOGAWANA KATIKA UCHAGUZI MKUU

August 18, 2015


 Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi,  Nderakindo Kessy (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya chama hicho, Ilala Dar es Salaam jana, wakati akitangaza majimbo yaliyochini ya vyama vinavyounda Ukawa ambayo vyama hivyo vitasimamisha wagombea wao katika uchaguzi mkuu. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha NLD, Masudi Makunjunga.
 Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Shaweji Mketo (wa pili kulia), akizungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari. Kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha NLD, Masudi Makunjunga, Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi,  Nderakindo Kessy na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika.
 Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika, akizungumza katika mkutano huo.
 Viongozi wa vyama hivyo wakiwa meza kuu.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.


Na Mwandishi Wetu


UMOJA wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), umetangaza mgawanyo wa majimbo yake 253 huku majimbo mengi yakienda Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Taarifa ya mgawanyo wa majimbo ilitolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Dk. Nderakindo Kessy jana katika ofisi kuu za chama hicho Ilala jijini Dar es Salaam.

Kessy alisema baada ya majadiliano ya muda mrefu kuhusu kuachiana majimbo ya ubunge, vyama vinavyounda Ukawa vimefanikiwa kuachiana majimbo ili kuhakikisha wanakiondoa Chama Cha Mapinduzi (CCM), madarakani.

Alisema mgawanyo wa majimbo hautahusiana na mgawanyo wa kata za kugombea udiwani na mwongozo wa kuachiana kata ndiyo utatumika katika kuamua namna ya kugombea kata.

“Tunapenda kuchukua nafasi hii kuwatangazia Watanzania majimbo ambayo hadi leo (jana), tumekubaliana kuachiana kuwa ni majimbo 253 na majimbo 12 tutawaambia Jumatano au Alhamis kwani kuna mambo hayajakaa vizuri,” alisema.

Aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Mkoa wa Mara majimbo yote wameachiwa Chadema ambayo ni Rorya, Tarime Mjini, Tarime Vijijini, Musoma Vijijini, Butiama, Bunda Mjini, Mwibara, Musoma Mjini na Bunda Vijijini.

Kessy alisema Mkoa wa Simiyu ambao una majimbo saba, majimbo sita wamepewa Chadema ambayo ni Bariadi, Maswa Magharibi, Maswa Mashariki, Kisesa, Meatu, Itilima na Jimbo la Busega atasimama mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF).

“Mkoa wa Shinyanga majimbo yote sita wameachiwa Chadema na sababu ya msingi ni wao kuwa na mizizi ambapo ni majimbo ya Msalala, Kahama Mjini, Kahama Vijijini, Shinyanga Mjini, Kishapu na Ushetu na Mkoa wa Mwanza ni Ukerewe, Magu, Nyamagana, Buchosa, Sengerema, Ilemela, Misungwi yameenda Chadema na Kwimba na Sumve CUF,” alisema.

Kaimu Katibu Mkuu huyo alisema Mkoa wa Geita majimbo yote yaliachiwa Chadema, ambayo ni Bukombe, Busanda, Nyang’wale, Chato na Mbogwe, Mkoa wa Kagera katika majimbo tisa Chadema imeachiwa majimbo sita ambayo ni Karagwe, Kyerwa, Bukoba Mjini, Muleba Kaskazini, Muleba Kusini na Biharamulo na Nkenge, Ngara yakiachwa kwa NCCR-Mageuzi na Jimbo la Bukoba Vijiji likiachwa kwa CUF.

Mkoa wa Mbeya Jimbo la Lupa, Songwe, Mbeya Mjini, Kyela, Rungwe, Busekolo, Mbozi Mashariki, Momba, Mbeya Vijijini, Vwawa na Tunduma yote yameachiwa Chadema na Jimbo la Ileje NCCR-Mageuzi.      

“Iringa, Jimbo la Ismani, Kalenga, Mufindi Kaskazini, Iringa Mjini, Kilolo, Mufindi Mjini Chadema itasimamisha wagombea na Mufundi Kusini NCCR-Mageuzi, ambapo Mkoa wa Njombe majimbo yote yameachwa Chadema ambayo ni Njombe Kaskazini, Lupembe, Wanging’ombe, Makete, Ludewa na Makambako,” alisema Kessy.

Kessy alisema Mkoa wa Rukwa wamekubaliana kuwaachia Chadema, ambapo ni majimbo ya Nkasi Kusini, Kwela, Nkasi Kaskazini, Sumbawanga Mjini na Kalambo, huku Mkoa wa Tanga CUF wameachiwa majimbo nane ambayo ni Handeni Mjini, Handeni Vijijini, Pangani, Tanga Mjini, Bumbuli, Mlalo, Lushoto na Mkinga. Chadema wameachiwa majimbo manne ambayo ni Kilindi, Muheza, Korogwe Mjini na Korogwe Vijijini. 

Kaimu Katibu Mkuu huyo alisema Mkoa wa Kilimanjaro majimbo saba imeachiwa Chadema ambayo ni Rombo, Same Magharibi, Same Mashariki, Moshi Vijijini, Moshi Mjini, Hai na Siha ambapo Vunjo NCCR-Mageuzi wameachiwa na Jimbo la Mwanga likibakia hadi Alhamis.

Mkoa wa Arusha alisema Chadema wameachiwa majimbo yote ambayo ni Arumeru Mashariki, Arumeru Magharibi, Arusha Mjini, Longido, Monduli, Karatu na Ngorongoro halikadhalika Mkoa Manyara Jimbo la Simanjiro, Mbulu Vijijini, Hanang, Babati Mjini, Babati Vijijini, Kiteto na Mbulu Mjini.

Aidha, Kessy alisema Mkoa wa Dar es Salaam, Jimbo la Ubungo, Kawe, Ukonga, Ilala na Kibamba Chadema itasimamisha wagombea na Kinondoni, Jimbo la Temeke na Mbagala CUF itasimamisha wagombea huku majimbo ya Segerea na Kigamboni yakibakia kiporo hadi Alhamisi wiki hii.

Alisema Mkoa wa Pwani majimbo ya Bagamoyo, Kisarawe, Mkuranga, Mafia, Rufiji Utete na Rufiji Kibiti majimbo hayo yameachiwa CUF na Majimbo ya Chalinze, Kibaha Mjini, Kibaha Vijijini yakiachiwa Chadema.    

Mkoa wa Morogoro Jimbo la Kilosa na Morogoro Kusini Mashariki CUF watasimamisha wagombea huku majimbo ya Mikumi, Morogoro Kusini, Kilombero, Mlimba, Mvomero, Ulanga Magharibi, Ulanga Mashariki na Morogoro Mjini yatakuwa chini ya Chadema.

“Mkoa wa Dodoma Jimbo la Kondoa Mjini, Kondoa Vijijini, Chemba yameachwa kwa CUF, Jimbo la Kibakwe na Mtera wameachiwa NCCR-Mageuzi na Dodoma Mjini, Kongwa, Bahi na Chilonwa Chadema itasimamisha wagombea.

Kessy alisema Mkoa wa Singida majimbo yote saba yameenda Chadema ambayo ni Iramba Magharibi, Iramba Mashariki, Singida Kaskazini, Singida Mashariki, Singida Magharibi, Manyoni Magharibi na Manyoni Mashariki. 

Kwa Mkoa wa Tabora Jimbo la Bukene, Nzega Vijijini, Igalula, Kaliua Tabora Kaskazini na Tabora Mjini watagombea CUF na Nzega Mjini, Igunga, Urambo, Ulyankulu, Manonga na Sikonge Chadema watasimamisha wagombea.

Alisema Mkoa wa Katavi majimbo yote sita ya Mpanda Mjini, Mpanda Vijijini, Katavi, Nsimbo na Kavuu. Mkoa wa Kigoma Jimbo la Buyungu, Mhambwe, Kasulu Mjini, Kasulu Vijijini, Kigoma Kusini na Manyovu NCCR-Mageuzi itasimamisha wagombea na Kigoma Kaskazini na Kigoma Mjini Chadema itasisimamisha wagombea wa ubunge.

Mkoa wa Ruvuma Jimbo la Tunduru Kaskazini, Namtumbo na Tunduru Kusini Chama cha CUF watasimamisha wagombea na majimbo ya Peramiho, Mbinga Magharibi/Nyasa, Mbinga Mashariki/Mbinga, Songea Mjini na Madaba, na Mbinga Mjini NCCR-Mageuzi itasimamisha mgombea.

“Mtwara Jimbo la Newala Mjini, Newala Vijijini, Tandahimba, Mtwara Vijijini, Nanyamba na Nanyumbu CUF itasimamisha wagombea huku majimbo ya Lulindi, Masasi na Ndanda wakiachiwa Chama cha National League Democratic (NLD),” alisema Kessy.

Kessy alisema Mkoa wa Lindi Ukawa kwa ujumla wao wamekubaliana kuwaachiwa CUF katika majimbo yote ambayo ni Mtama, Kilwa Kaskazini, Kilwa Kusini, Lindi Mjini, Ruangwa, Nachingwea, Liwale na Mchinga.
Mketo

Akizungumzia uamuzi huo, Kaimu Naibu Katibu Mkuu CUF, Shaweji Mketo alisema mgawanyo huo umezingatia mambo makuu matano ambao ni kuhusu mbunge aliyeko tangu waka 2010, nafasi ya chama katika uchaguzi huo wa 2010, nafasi ya udiwani, uchaguzi wa Serikali za Mitaa na nguvu na mtandao wa chama hadi sasa.

Mketo alisema lengo la Ukawa si kugawana majimbo kama inavyotafsiriwa ila ni kugawana kwa vigezo ili kuhakikisha wanapata ushindi wa jumla na kushinda uchaguzi ujao.

Makujunga

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mkuu wa NLD, Masudi Makujunga alisema chama chao kipo pamoja kuhakikisha kuwa mabadiliko ya kisiasa, kijamii yanatokea ndani ya nchi wakati huu.

“Lengo si ufahari katika kugawana majimbo, lengo letu ni kuhakikisha kuwa mabadiliko yanapatikana na sisi NLD tupo tayari kushiriki katika mabadiliko hayo kwenye sehemu husika,” alisema.

Mnyika

Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika alisema jitihada za Ukawa zipo katika hali nzuri hivyo wao watahakikisha kuwa wanakuwa wamoja hadi kufikia hatima yao ambayo ni kushinda uchaguzi na kuongoza nchi.

Alisema kilichofanyika ndio makubaliono ya viongozi wao hivyo wana Ukawa wote wanapaswa kukubaliana na hali hiyo ili Taifa liweze kusonga mbele kwa maslahi ya wananchi na wapenda mabadiliko.

Aidha, Mnyika aliitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kutoa ufafanuzi kuhusu kuwepo kwa maelekezo ya kuvitaka na wagombea wao kurejesha fomu Agosti 19, mwaka huu huku ikiamini kuwa sheria inataka mchakato huo kukamilika Agosti 21.

Mnyika aliitaka NEC kutoa ufafanuzi kuhusu kuwepo kwa wanajeshi watatu ambao wanahusika na mfumo wa teknolojia ya habari katika tume hiyo jambo ambalo ni kinyume cha taratibu za tume hiyo.

Mnyika alisema iwapo tume itakuwa kimya itakuwa imethibitisha taarifa hizo ambazo kimsingi zinachochea vurugu na hofu kwa washiriki wa uchaguzi huo.

Ukawa uliasisiwa wakati wa Bunge Maalumu la Katiba mwaka 2014, lengo likiwa kuunganisha nguvu kwa ajili ya kusimamia na kutetea maoni ya wananchi yaliyowasilishwa kupitia rasimu ya pili ya Katiba iliyotayarishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Umoja huo ulihusisha wabunge kutoka vyama mbalimbali vya upinzani na baadhi ya wabunge kutoka kundi lililojulikana kama la 201ambapo baadaye, ulibaki na wabunge na viongozi kutoka vyama vya NLD, NCCR – Mageuzi, CUF na Chadema.

Lowassa

Wakati huo huo, Mgombea urais wa Chadema, Edward Lowasa amelakiwa na maelfu ya watu mjini hapa na kusema yeye ni muumini wa muungano wa serikali tatu na si mbili, ikiwa ni kuhitimisha mchakato wake wa kutafuta wadhamini Zanzibar.

Akihutubia maelfu ya wanachama wa vyama vinavyounda umoja huo na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Demokrasia Kibanda Maiti mjini Unguja, alisema wanaosema yeye si muumini wa serikali tatu ni wazushi na wapuuzwe.

Lowassa alisema alikuwa muumini wa mfumo huo tangu alipokuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu katika miaka ya 90. Alisema wanaosema yeye ni muumini wa serikali mbili na hawezi kubadilika hawamjui.

Alisema yeye na wenzake waliwahi kupendekeza jambo hilo katika vikao vya chama na serikali kwa lengo la kuimarisha muungano, lakini ilishindikana kutokana na viongozi wengi wa CCM kuwa na woga wa mabadiliko.

“Hali hii ya uwoga wa viongozi wengi wa CCM haikuja bure bali ni kutokana na mfumo wa chama hicho ila wanasahau mwalimu aliwahimiza kuwa Watanzania wanahitaji mabadiliko, na kwa mujibu wa Baba wa Taifa kama watayakosa ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM,” alisema.

Lowassa aliongeza, “fursa ya mabadiliko imekuja kupitia Ukawa na ninawaomba Watanzania tuitumie vyema na kuionesha CCM kuwa nchi hii inaweza kuwa na mabadiliko bila ya ubabe wala vitisho.”

Kabla ya mkutano huo alipokelewa na wafuasi wa vyama hivyo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume mjini Zanzibar kisha msafara wake ulioongozwa na mgombea wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.

Alisema muungano kati ya iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar ni watu wa pande hizo mbili, hivyo kuna umuhimu wa kuwepo kwa maridhiano yatakayoondoa manung'uniko miongoni mwa wananchi wa pande hizo jambo ambalo atalisimamia kwa nguvu zake.

“Umaskini wa nchi hii una sababishwa na watu kutojiamini kwa baadhi ya watendaji wa serikali na kutosimamiwa kikamilifu kwa sheria za nchi, miongozo na maamuzi yanayofikiwa ktika vikao vya kitaifa jambo ambalo tukiwa timu moja mimi, babu Duni (mgombea mwenza) na Maalim Seif (mgombea urais wa Zanzibar) tutawapeleka mchaka mchaka ili kuleta maendeleo kwa kasi kubwa na ya ajabu,” alisema.

Aidha, mgombea huyo alikosoa hatua ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) ya kumvua ukamanda wa vijana taifa, muasisi wa Tanu na CCM, Kingunge Ngombare Mwiru na kuitaja hatua hiyo kuwa ni kukiuka haki ya kikatiba ya kutoa maoni na kwamba laana za kiongozi huyo zitakishukia chama hicho.

“Watu makini hamuwezi kukubali kumpoteza mtu kama Kingunge eti kwa sababu alitoa maoni yake hadharani kuhusu jambo la kweli. Wamesahau kuwa mzee huyu ndiye aliyekinusuru chama kisisambaratike wakati Ujamaa ulipokuwa umesambaratika ulimwenguni na yeye kuwa ndiyo msemaji mkuu wa chama. Jambo hili linaashiria mwisho wa zama za CCM na laana za kitendo hicho ni lazima ziwashukie na hawatakuwa na wa kumlaumu,” alisema Lowassa. 

Akizungumza kwa mara ya kwanza tangu ajiunge na Chadema katika ardhi ya Zanzibar, mgombe mwenza wa Lowassa, Juma Duni Haji aliwaomba wananchi wa Zanzibar kuwaunga mkono na kuwapa ridhaa itakayowawezesha kuwaunganisha wananchi wa Tanzania kuelekea katika umoja na maridhiano.  

Maalim Seif

Akihutubia hadhara hiyo,  Maalim Seif alivitahadharisha vyombo vya dola kusimamia ulinzi wa raia na mali zao kwa haki bila ya upendeleo kutokana na kuwepo kwa taarifa za vitendo vinavyoashiria uvunjwaji wa sheria alivyodai vinafanywa na CCM.

“Wenzetu hawa wamekuwa mabingwa wa kuhubiri amani wanapokuwa majukwaani lakini wanaposhuka huwa ndiyo wavunjaji wakubwa wa amani kwani kuna taarifa kuwa wagombea wetu wa ubunge na udiwani katika Jimbo la Shauri Moyo na Wadi ya Kidatu wamevamiwa na kunyang'anywa fomu zao za kusaka wadhamini. Hali hii haiashirii kuwa kuna nia njema,” alisema.
 
Mapema aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga ambaye alijiunga na Chadema, Khamis Mgeja aliwataka wananchi wa Zanzibar kuendelea kuiunga mkono Ukawa kwa kuwa ndiyo yenye uwezo wa kukidhi matakwa ya Wazanzibar na Watanzania.

Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliwashukuru wananchi wa Zanzibar na CUF kwa kumridhia aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho na Waziri wa Miundombinu, Duni Haji kujiunga na Chadema hatua iliyomuwezesha kuteuliwa kuwa mgombea mwenza wa Lowassa.

“Kumekuwa na vitisho dhidi ya watumishi wa vyombo vya dola kuwa mtaachwa pindi mkiwaunga mkono wagombea wa Ukawa, ninawatoa hofu kuwa mtaendelea kuwepo hata baada ya CCM kuondoka kwa sababu nyinyi mpo kwa mujibu wa sheria,” alisisitiza Mbowe na kuahidi kustawisha maslahi yao pindi Ukawa ikishinda.

Mbatia

Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema kupitia umoja wao wamewaagiza wanasheria wa vyama vinavyounda Ukawa kunakili matukio yote ya ukiukwaji wa haki binadamu vitakavyofanywa na watendaji au viongozi wa CCM ili waweze kuwafungulia kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita-The Hague. 


“Hatutavumilia aina yoyote ya uharamia ambayo itafanywa na mtu au taasisi ili kuvuruga harakati za Ukawa kuleta mabadiliko kupitia uchaguzi mkuu ujao, tumewaagiza wanasheria wetu kunakili kila tukio linaloashiria hali hiyo na tutamfikisha kila aliyehusika au atakayehusika kuhujumu matakwa ya demokrasia yasitekelezwe,” alisema.(Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712727062)

CCM YATANGAZA KAMATI YA KAMPENI ZAKE KATIKA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 2015

August 18, 2015


TAMASHA LA MICHEZO LA WAANDISHI WA HABARI ARUSHA KUTIMUA VUMBI AGOSTI 29

August 18, 2015

..Meneja masoko na mauzo wa Kampuni ya Mega Trade  Edmundi Rutaraka, akimkabidhi hundi ya Ts 1.5 Milioni Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo na burudani mkoa wa Arusha,Mussa Juma kwa ajili ya tamasha la  10 waandishi wa habari mkoa wa Arusha, Manyara na Dar es salam na wadau wa habari ambalo litafanyika Agoust 29 uwanja wa sheikh Amri Abeid, hafla hiyo ilifanyika jana, Palace Hoteli Jijini.
 
habari na libeneke la kaskazini blog
Tamasha la 10 la vyombo vya habari  na wadau wa habari mkoa wa Arusha, linatarajiwa kufanyika Agosti 29 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid kwa kushirikisha timu nane ikiwepo  timu ya TASWA kutoka jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Palace Hotel , Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo mkoa wa Arusha(TASWA-Arusha), Mussa Juma, alisema tayari maandalizi muhimu yamekamilika.

Juma alisema Tamasha hilo linaloandaliwa na TASWA na kampuni ya Arusha Media.mdhamini Mkuu ni Kampuni ya Bia nchini( TBL) kwa miaka 10 sasa, litashirikisha michezo ya Soka, Mpira wa pete, kuvuta kamba na kukimbiza kuku.

"tunapenda kutangaza rasmi tamasha la 10 ya TASWA Arusha litafanyika Agosti 29 na kauli mbiu yetu ni Uchaguzi Mkuu bila vurugu inawezekana"alisema

Alisema katika Tamasha hilo, ambalo litashirikisha pia timu za wafanyakazi wa kampuni ya bia nchini(TBL) Taasisi na Faidika na kampuni ya Pepsi litaandamana na ziara ya wanahabari kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Arusha.

Nahodha wa timu ya TASWA Arusha, Ramadhani Siwayombe akikabidhiwa jezi kwa ajili ya tamasha la waandishi wa habari na wadau wa habari mkoa wa Arusha ambalo litafanyika Augosti 29 Sheikh Amri Abeid, anayemkabidhi ni Filbert Masele meneja mikopo ya wafanyakazi wa FAIDIKA na Meneja wa FAIDIKA mkoa wa Arusha Eliya Mlay hafla hiyo, ilifanyika Palace hotel 

Wakizungumza katika kikao hicho, Meneja wa Masoko wa kampuni ya Mega Trade Edmund Rutaraka, Meneja masoko wa kampuni ya SBC(T) Lalit Sharma na Meneja wa Faidika Arusha,Eliya Mlay walisema wamedhamini Tamasha hilo ili kuendeleza michezo.

Rutaraka alisema kampuni yao kwa miaka mitano sasa inadhamini tamasha hilo na wanajivunia mafanikio makubwa.

Tamasha hilo, limedhaminiwa na kampuni ya bia nchini(TBL) Kampuni ya Mega Trade,Shirika la hifadhi za Taifa(TANAPA),Shirika la Nyumba nchini (NHC) Kampuni ya SBC(T) Ltd,Mamlaka hifadhi Ngorongoro(NCAA), Taasisi ya FAIDIKA na Tanzanite One.
Makamu Mwenyekiti wa TASWA Arusha, Adrea Ngobole alisema wadhamini wengine wa Tamasha hilo watatangazwa karibuni sambamba na zawadi na mgeni rasmi.

 Meneja wa masoko na mauzo wa Kampuni ya SBC(T) Lalit Sharma, akimkabidhi mipira Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo na burudani mkoa wa Arusha, Mussa Juma kwa ajili ya Tamasha la kumi la waandishi wa habari mkoa wa Arusha,Manyara na Dar es Salaam na wadau wa habari, ambalo litafanyika Agoust 29 uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
 Makamu Mwenyekiti wa TASWA mkoa wa Arusha,Andrea Ngobole, akipokea  vikombe kutoka kwa Filbert Masele meneja mikopo ya wafanyakazi wa FAIDIKA na Meneja wa FAIDIKA mkoa wa Arusha Eliya Mlay jana Palace Hotel  kwa ajili ya tamasha la waandishi wa habari na ambalo litashirikisha pia wafanyakazi wa taasisi hiyo, ambalo litafanyika Augost 29 uwanja wa Sheikh Amri Abeid
Wadhamini na viongozi wa TASWA Arusha, wakiwa kwenye kikao na waandishi wa habari kuelezea Bonanza la vyombo vya habari na wadau wa habari mkoa wa Arusha,ambalo litafanyika Augosti 29 uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

WATANZANIA WAASWA KUTEMBELEA HIFADHI ZA TAIFA,TANAPA WAZINDUA RASMI LEO MKOANI HAPA

August 18, 2015




 Afisa Utalii Hifadhi ya Taifa Saadan, Anjela Mnyaki, akizungumza wakati  wa kongamano la kampeni  la Uhamasishaji  Watanzania kutembelea vivutio vya ndani  vya utalii  lilofanyika Leo  Tanga.



 Washiriki wa kongamano la Utalii wa ndani lililoitishwa na Hifadi ya Taifa Tanzania wakifuatilia maelezo ya namna ambavyo Watanzania wanashindwa kutembelea vivutio vya ndani vilivyopo vikiwemo vya Hifadhi ya Saadani na Mkomanzi ambazo zote ziko Mkoani Tanga
 Mhifadhi Utalii hifadhi ya Taifa ya Saadan, Pelagy Marandu, akizungumza wakati wa kongamano la kampeni la uhamasishaji Watanzania kutembelea vivutio vya ndani vya utalii lililofanyika leo Tanga.




 Kaimu Mkurugenzi wa Masoko Hifadhi ya Taifa ya Saadan, Victor Ketansi, akizungumza wakati wa kongamano la kampeni la uhamasishaji Watanzania kutembelea vivutio vya utalii lililofanyika jana Tanga.



KESSY HASSANI MWENYEKITI MPYA AFRICAN SPORTS”

August 18, 2015
ALIYEKUWA Makamu Mwenyekiti wa timu ya African Sports
“Wanakimanumanu”katika uongozi uliomaliza muda wake, Hassani Kessy amechaguliwa kushika wadhifa wa Mwenyekiti wa Klabu hiyo baada ya kupata kura 52 ambao ni sawa na asilimia mia moja kwenye uchaguzi mkuu.

Uchaguzi huo ulifanyika kwenye ukumbi wa Spended na kusimamiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la soka nchini (TFF) Wakili Aloyce Komba ambaye aliwataka viongozi ambao wamechaguliwa kuchangia kasi ya maendeleo kwenye timu hiyo ili iweze kurudisha makali yake ya miaka ya nyuma.

Kessy ambaye aliwania nafasi hiyo akiwa hana mpinzani alifanikiwa kupata kura kwa njia ya ndio na hapana ambapo kati ya wajumbe 53 kuwa moja iliharibika kwenye mchakato huo wa uchaguzi.

Kwa upande wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti ilichaguliwa aliyekuwa Meneja wa timu hiyo,Abdul Ahmed ambapo alipata kura za ndio zote ambapo alikuwa hana mpinzani kwenye mchakato huo wa uchaguzi.

Aidha kwa upande wa wajumbe wa kamati ya utendaji walifanikiwa
kuchaguliwa Godias Kimath aliyepata kura (51), Mwinshame Mbwana aliyepata kura (52) na Abdallah Babala aliyepata kura (51)waliopata kuwa za ndio kwenye mchakato huo ambao Kamati hiyo iliiagiza klabu hiyo kuhakikisha inajaza nafasi mbili za wajumbe waliosalia ili iweze kutimia idadi ya watano ambao wataunda kamati ya utendaji.

Akizungumza baada ya kuchaguliwa,Kessy alisema kuwa mipango yake mikubwa ni kuhakikisha timu hiyo inarudisha makali yake ya miaka ya nyuma wakati walipopanda daraja na kufanikiwa kuchukua Ubingwa wa Ligi kuu soka Tanzania bara.

NHIF YAINGIA MKATABA NA Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ

NHIF YAINGIA MKATABA NA Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ

August 18, 2015

unnamed (1)
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bwana Michael Mhando na Mkuu wa Huduma za Matibabu Jeshini Brigedia Denis Raphale Janga wakitia saini mkataba wa ushirikiano ambapo Mfuko utatumia vituo vya matibabu vya Jeshi kutibu wanachama wake.
unnamed
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bwana Michael Mhando na Mkuu wa Huduma za Matibabu Jeshini Brigedia Denis Raphale Janga wakikabidhiana mkataba.
………………………………………………………….
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeingia mkataba na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambapo wanachama wa mfuko huo na wategemezi wao watapata huduma za matibabu katika hospitali za jeshi nchini kote. Mkataba huo wa miaka mitatu uliosainiwa jana unalenga kupanua wigo wa vituo vya matibabu na kuanzisha ushirikiano wa kihistoria baina ya pande mbili hizo. Akizungumza wakati wa kutia saini mkataba huo Mkuu wa Huduma za Afya Jeshini Brigedia Denis Raphael Janga, amesema amepokea kwa furaha mkataba huo kwa kuwa utawapa nafasi ya kutoa huduma bora kwa kundi kubwa la wanachama wa NHIF ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikosa huduma katika vituo vya jeshi vilivyo karibu nao. Ameahidi kushirikiana kwa karibu na uongozi wa NHIF ili kuhakikisha wanachama na wategemezi wao wanapata vipimo na dawa wakati wote watakapokwenda kwenye vituo hivyo. Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bwana Michael Mhando amesema NHIF kwa muda mrefu fursa ya kufanya kazi na JWTZ katika sekta ya matibabu na kwamba mkataba huo unafungua historia mpya ya ushirikiano baina ya taaisi hizo wa kujenga nchi kwa pamoja. Amesema ili kuhakikisha kuwa mkataba huo unakuwa na manufaa kwa pande zote mbili Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya utaandaa mafunzo maalumu kwa watoa huduma wa vituo vya jeshi ili kuhakikisha kuwa kunakuwa na uelewa wa pamoja wa namna ya kuhudumia wanachana wa NHIF watakaokwenda kupata huduma katika vituo hivyo. Mhando ameongeza kuwa NHIF itaendelea kushirikiana na uongozi wa JWTZ ili kukamilisha taratibu za kiutawala zitakazowawezesha wanaejeshi na familia zao kujiunga na kunufaika na matibabu kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya. Aidha ameushauri uongozi wa JWTZ kutumia fursa ya mikopo ya vifaa tiba, ukarabati na dawa na vitendanishi inayotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ili kuhakikisha kuwa vituo vya matibabu vinavyomilikiwa na JWZT vinakuwa na mazingira mazuri na vitendea kazi vinavyotakiwa. Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lina vituo vya matibabu vya ngazi mbalimbali zaidi ya kumi na nane nchini kote.
VILABU VYA UN VYA ELIMU YA JUU VYAZIMISHA SIKU YA VIJA DUNIANI.

VILABU VYA UN VYA ELIMU YA JUU VYAZIMISHA SIKU YA VIJA DUNIANI.

August 18, 2015

2
Mwenyekiti wa vilabu vya UN vya Elimu ya juu Zanzibar Ali Kombo Hassan akisoma risala ya vijana wa vilabu UN katika Mkutano uliofanyika Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.
1
Mlezi wa vilabu vya UN vya Elimu ya juu Zanzibar Dkt. Muhd Makame Haji akiwakaribisha wageni walikwa katika Mkutano wa kuadhimisha siku ya vijana Duniani uliofanyika huko Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.
3
Mjumbe wa vilabu vya UN vya Elimu ya juu Khadija Salum Khamis akitoa hutuba yake kuhusu madhara yanayopatikana kutokana na vurugu za uchauzi, katika Mkutano wa kuadhimisha siku ya vijana Duniani.
4
Afisa elimu ya wapiga kura kutoka Tume ya Uchaguzi Zanzibar Juma Sanifu Sheha akitoa mada juu ya ushiriki wa vinaja katika uchaguzi wa Amani katika Mkutano wa kuadhimisha siku ya vijana Duniani uliofanyika huko Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.
6 
Afisa programu ya maendeo ya Vijana mfuko wa idadi ya watu wa Umoja wa Mataifa ofisi ya Zanzibar Aoife Spengeman akitoa shukrani kwa vijana mara baada ya kumaliza kwa Mkutano huo (kushoto) Mratibu wa vilabu vya UN Zanzibar Maalim Ame Haji Vuai.
5
Baadhi ya Vijana wa vilabu vya UN vya Elimu ya juu wakimskiliza kwa makini mtoa mada Juma Sanifu kutoka Tume ya Uchaguzi (hayupo pichani) wakati akiwasilisha.
Picha na Makame Mshenga Maelezo Zanzibar.