WANANCHI KUWENI MAKINI NA WANAOCHOCHEA CHUKI-BALOZI SEIF IDD

September 07, 2015

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Kwale Wilaya ya Micheweni wakati alipowasili kuzungumza nao.
 Balozi Seif akizungumza na Wananchi na Wana
CCM wa Kijiji cha Kwale Wilaya ya Micheweni akitekeleza ahadi aliyotoa
kwa Wazee Waasisi wa Kijiji hicho ya kufika kusalimiana nao.
 Baadhi ya Wananchi na wanaCCM wa Kijiji cha Kwale
wakifuatilia Hotuba ya Balozi Seif hayupo pichani alipofika Kjijini
hapo kusalimiana nao.
Balozi Seif akiwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa
akiagana na Wana CCM wa Kijiji cha Kwale mara baada ya kuzungumza nao
katika Mkutano wa hadhara.
Picha na –OMPR –ZNZ.
 
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
amewatahadharisha Wananchi kuwa makini na Watu wanaochochea chuki
miongoni mwa Jamii jambo ambalo  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
kamwe haitakubali kuona amani ya Nchi inachezewa kizembe.

Alisema wapo watu waliochoka na amani iliyopo nchini kwa kuanza
kushabikia cheche za kujiandaa kuwashawishi Vijana wawe tayari kufanya
fujo mara tuu baada  ya zoezi la kupiga kura kwenya uchaguzi Mkuu wa
Mwezi Oktoba mwaka huu.

Balozi Seif Ali Iddi ametoa tahadhari hiyo wakati akizungumza na
Wananchi amoja na Wana  CCM wa Kijiji cha Kwale Wilaya ya Micheweni
Mkoa wa Kaskazini Pemba akitekeleza ahadi aliyowapa wazee wa Kijiji
hicho hivi karibuni ya kuwatembelea na kusalimiana nao.

Balozi Seif aliwaonya Vijana kujiepuka na mtego huo ulioandaliwa kwa
ajili yao unaoweza kuwaathiri na akawatolea mfano wa matukio ya
Januari mwaka 2001 ambayo waandaji wakubwa waliwazuia Vijana wao na
kuwaachia Vijana wa wenzao kutumbukia katika balaa.

Akizungumzia Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika siku 49 zijazo
Balozi Seif ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya
Taifa ya CCM aliwakumbusha wana CCM na Wananachi hao wa Kijiji cha
Kwale kuendelea kuiunga mkono CCM ibakie madarakani.

Alisema Dira ya Cahama cha Mapinduzi ni kuwanuganisha Wananachi wote
katika kudumisha Umoja na Mshikamano kwani tabia ya mfarakano
inayoonekana kubebwa na upinzani imepigwa vita hata katika vitabu wa
Dini.

Balozi Seif amewapa pole Wananchi wa Kijiji hicho cha Kwale kutokana
na madhila waliyoyapata kufuatia kitendo cha Upinzani kutaka kupachika
Bendera kwa nguvu ndani ya Kijiji hicho bila ya ridhaa ya Wananchi
wenyewe.

Alisema Wanachama wa Chama cha Mapinduzi kamwe hawakubali kuonewa naUongozi wa Chama hicho katika ngazi zote daima utaendelea kutetea
maslahi yake muda wowote ule.

Katika Mkutano huo Balozi Seif Ali Iddi alipata fursa ya kuizindua
rasmi Maskani ya Chama cha Mapinduzi ya Wazede wa Kijiji hicho cha
Kwale kiliomo ndani ya Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
7/9/2015.
 MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA BALOZI WA INDIA NCHINI TANZANIA KWA MAZUNGUMZO, IKULU DAR ES SALAAM.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA BALOZI WA INDIA NCHINI TANZANIA KWA MAZUNGUMZO, IKULU DAR ES SALAAM.

September 07, 2015
x1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na balozi wa India Nchini Tanzania, Mhe. Sandeep Arya, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Sept 7, 2015 kwa mazungumzo.
x2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na Balozi wa India Nchini Tanzania, Mhe. Sandeep Arya, baada ya mzungumzo yao yaliyofanyika  Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Sept 7, 2015.
Picha na OMR
DR.JOHN POMBE MAGUFULI: WANA HANDENI NIPENI KURA NIMALIZIE MIRADI YA BARABARA NILIYOKWISHA IANZA

DR.JOHN POMBE MAGUFULI: WANA HANDENI NIPENI KURA NIMALIZIE MIRADI YA BARABARA NILIYOKWISHA IANZA

September 07, 2015

????????????????????????????????????
mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akihutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa CCM wa Kigoda mjini Handeni na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi wilayani humo, Dr Magufuli amewaomba wananchi wa Handeni kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu ili Rais na  aweze kuleta maendeleo na kakamilisha miradi mbalimbali ya barabara aliyoanza kuitekeleza wilayani humo akiwa Waziri wa Ujenzi.
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Ndugu Abdallah Bulembo ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi na waangalizi wa kimataifa kutoa tamko kufuatia baadhi ya wagombea kuanza kufanya kampeni chafu wakiingia makanisani na kujinadi na kuomba kura makanisani jambo ambalo sio jema kwa taifa letu kwani siasa haihusiani na masuala ya dini.(PICHA NA JOHN BUKUKU – FULLSHANGWE-HANDENI)
????????????????????????????????????
mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akiwahutubia wananchi katika mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kigoda mjini Handeni.
????????????????????????????????????
Umati wa wananchi ukifuatilia mkutano huo.
????????????????????????????????????
mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli akipanda jukwaani kwenye mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kigoda Handeni.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wazee wa wilayani Kilindi wakiwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika kata ya  Songe Kilindi.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Kilindi.
????????????????????????????????????
Kada wa CCM Ndugu Amon Mpanju akizungumza na wana Kilindi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kijiji cha Songe.
????????????????????????????????????
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Ndugu Abdallah Bulembo akiwahutubia wananchi katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Mzee Yusuf Makamba akiwahutubia wananchi wa kata ya Songe wilayani Kilindi wakati akimnadi Dr. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli akizungumza na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Hery Shekifu katikati nanyekiti wa Wazazi  Ndugu Abdallah Bulembo wananchi wa Kilindi.
????????????????????????????????????
Baadhi ya Akina mama wa wanachama wa CCM wakiimba huku wakiwa wameshika mabango yene picha ya Dr. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Baadhi ya vijana wakimpungia mkono Dr. John Pombe Magufuliwakati akiwa njiani kuelekea wilaya ya Kilindi akitokea mkoani Morogoro.
????????????????????????????????????
Akina mama wakimpungia mkono Dr. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Dr. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi njiani akitokea mkoani Morogoro kwenda Handeni Mkoani Tanga.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Hapa Kazi Tu!
????????????????????????????????????
Lazima tumuone Magufuli
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Baadhi ya wananchi wakiwa wameshika mabango yenye picha ya Sadiq Muradi Mgombea ubunge wa jimbo la Mvomero.
????????????????????????????????????
Mmoja wa wananchi waliohudhuria katika mkutano wa kampeni mjini Turiani akipata tunda la Chungwa huku akiwa amekumbatia picha yake yenye picha ya Mgombea wa jimbo la Mvomero Ndugu Sadiq Murad.
????????????????????????????????????
Wananchi wakiwa na picha za Dr. John Pombe Magufuli katika mkutano wa kampeni uliofanyika Turiani mkoani Morogoro.
????????????????????????????????????
Dr. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi mjini Turiani.
????????????????????????????????????
Kutoka kulia ni Mzee Yusuf Makamba, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro Ndugu Innocent Kalogeres na Ndugu Sadiq Murad mgombea ubunge jimbo la Mvomero.
????????????????????????????????????
Dr. John Pombe Magufuli akizungumza wakati akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Mvomero Ndugu Sadiq Murad.
????????????????????????????????????
Dr. John Pombe Magufuli akisoma moja ya mabango ambayo yaliandikwa na vijana wachoma mahindi wa Dumila. 
????????????????????????????????????
Dr. John Pombe Magufuli akiwasili katika eneo la Dumila akiwa njiani kuelekea mkoa wa Tanga kupitia Kilindi, Handeni mkoani Tanga.

MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA ATAJA VYAMA VYA SIASA VYENYE USAJILI WA KUDUMU AMBAVYO VINASTAHILI KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU

September 07, 2015

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, Monica Laurent (kushoto), akizungumza na wanahabari wakati akimkaribisha msemaji wa mkutano huo kuzungumza na waandishi.
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Nyahoza (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu ambavyo ninastahili kushiriki uchaguzi mkuu. Kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Emmanuel Kayuni. 
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Mwanahabari wa gazeti la Nipashe, Theresia akiwa mbele ya kamera wakati wa mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.


RAIS KIKWETE AWAPA POLE MAJERUHI YA MSONGAMANO WA WANANCHI BAADA YA MKUTANO WA KAMPENI KATIKA UWANJA WA JAMHURI MJINI MOROGORO JANA

September 07, 2015
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya  Mkoa wa Morogoro Dkt. Ritha Lyamuya alipokwenda kuwapa pole majeruhi walioumia katika msongamano mkubwa uliotokea katika mlango wa kutokea nje baada ya mkutano wa kampeni wa CCM katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana Septemba 6, 2015. Watu wawili walipoteza maisha, akiwemo mvulana wa miaka 12 aliyejulikana kwa jina la Ramadhani Abdallah na mwanamama Grace George (42), ambapo jumla ya watu 17 walijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini hapo. Hadi jioni hii majeruhi saba walikuwa wameruhusiwa
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Kaimu Mganga Mku wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro Dkt. Samson Tarimo alipokwenda kuwapa pole majeruhi walioumia katika mlango wa kutokea nje baada ya mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana Septemba 6, 2015.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mweka Hazina wa CCM mkoa wa Morogoro Ndg. Hassan BAntu alipokwenda kuwapa pole majeruhi walioumia katika mlango wa kutokea nje baada ya mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana Septemba 6, 2015.
 Mmoja wa majeruhi Bw. Kokoliko Ramadhani akiwa kitandani pake hospitalini hapo akiuguza bega la kuume aliloumia kwenye msongamano huo
 Rais Kikwete akimpa pole  mmoja wa majeruhi Bw. Kokoliko Ramadhani akiwa kitandani pake hospitalini hapo akiuguza bega la kuume aliloumia kwenye msongamano huo
 Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimpa pole  mmoja wa majeruhi Bi Flora Maduka akiwa kitandani pake hospitalini hapo baad ya kujeruhiwa katika msongamano huo
 Rais Kikwete akimpa pole  mmoja wa majeruhi Bi. Jalia Mohamed akiwa kitandani pake hospitalini hapo akiuguza bega la kuume aliloumia kwenye msongamano huo
 Rais Kikwete akiendelea kutoa pole kwa majeruhi
 "Pole sana...." Rais Kikwete akimfariji mmoja wa majeruhi

 Rais Kikwete alitumia wasaa huo kuwapa pole wagonjwa wengine waliokuwa wamelazwa wodi moja na majeruhi hao. Hapa anamfariji mtoto aliyeungua kwa moto
  Rais Kikwete alitumia wasaa huo kuwapa pole wagonjwa wengine waliokuwa wamelazwa wodi moja na majeruhi hao. Hapa anamfariji mtoto aliyevunjika mguu wakati akicheza kwenye mti
Rais Kikwete akimpa pole mvulana ambaye aligongwa na gari wakati akielekea kumsikiliza mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli katika mkutano wa kampeni Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana 
Rais Kikwete alipata fursa ya kutembelea wodi ya watoto na kuwapa pole kwa kuumwa kwao
Rais Kikwete akiongea na wanafunzi waliokuwepo hospitalini hapo kumtembelea mgonjwa
Rais Kikwete alizongwa na wananchi waliokuwa na hamu ya kuongea naye 
Rais Kikwete akitoa mapendekezo ya kupanua hospitali hiyo ambayo ina eneo kubwa lakini majengo machache ya chini. Alipendekeza uongozi wa hospitali na mkoa ubuni namna ya kuipanua kwa kujenga majengo ya ghorofa ili kuwepo na wodi na sehemu nyingi zaidi za huduma.
Mwishoni Rais Kikwete aliongea na wanahabari wa kutoka vyombo mbalimbali na kueleza masikitiko yake kwa yaliyotokea jana Uwanja wa Jamhuri baada ya mkutano wa kampeni kumalizika.
Rais Jakaya Kikwete akiongea na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya  Mkoa wa Morogoro Dkt. Ritha Lyamuya baada ya kuwajulia hali majeruhi wa msongamano baada ya mkutano wa kampeni uwanja wa Jamhuri Morogoro jana. PICHA NA IKULU