BALOZI WA LUPEMBE AIPA MKONO WA BARAKA AZAM KWENYE MECHI YA MARUDIANO J'PIL

March 17, 2017
BALOZI wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Richard Lupembe, ameweka wazi kuwa Azam FC ni moja ya timu zinazowatia moyo  Watanzania wanoishi nje ya nchi, huku akiipa mkono wa ushindi kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya Mbabane Swallows ya Afrika Kusini.

Lupembe alitoa kauli hiyo wakati alipoitembelea timu hiyo jana kwenye kambi yake katika Hoteli ya Acardia jijini Pretoria, nchini humo ikijiandaa na mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaofanyika Uwanja wa Taifa wa Somhlolo nchini Swaziland Jumapili hii saa 10.30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

“Kwa kweli nimefarijika sana kwa kuiona Azam FC tena kama nakumbuka mlikuja hapa mwaka jana, mlikuja hapa kucheza na  Bidvest nikawa mgeni rasmi na mkono wangu ukawa wa kheri mkashinda, nawahakikishieni nitawashika tena mkono na ninauhakika mtashinda tena,” alisema Lupembe

Alisema kuwa atakuwa pamoja na timu hiyo kwa kipindi chote itakapokuwa jijini hapa hadi Jumamosi itakapoelekea Swaziland huku akiitakia kila la kheri kuelekea mtanange huo unaosubiriwa na mashabiki wengi wa timu hizo.

“Ndio tunafahamu kuwa kuna timu kubwa za Simba na Yanga, lakini Azam FC inatia moyo kwa sisi watu ambao tulioko nje nawatakia kila la kheri, mazoezi mema mimi nipo hapa kama balozi, na nitahakikisha nitakuwa na nyie mpaka siku mtakapoenda kucheza mpira,” alisema,
Lupembe aliitembelea Azam FC jioni wakati ikielekea kwenye mazoezi kujiandaa na mchezo huo.
Mara mwisho Balozi huyo kuishika mkono Azam FC iliichapa Bidvest Wits mabao 3-0 jijini Johannesburg katika mchezo wa raundi kama hii, ambapo kutokana na ushindi wa 1-0 katika mchezo wa kwanza kwa sasa timu hiyo inahitaji ushindi wowote au sare ili iweze kusonga mbele.

Balozi  wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Richard Lupembe akiwa pamoja na wachezaji wa Azam wakati alipoitembelea timu hiyo jana kwenye kambi yake katika Hoteli ya Acardia jijini Pretoria, nchini humo ikijiandaa na mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaofanyika Uwanja wa Taifa wa Somhlolo nchini Swaziland Jumapili hii saa 10.30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.alip
Kocha wa Azam ... akitoa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mazoezi  ya kujiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Mbabane Swallows siku ya Jumapili.
Beki wa Kulia wa Azam, Shomari Kapombe akiwa anagombania mpira na Kingue wakati wa mazoezi ya timu hiyo  kujiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Mbabane Swallows siku  ya Jumapili.
PROF.GABRIEL AMEWATAKA MAAFISA MAWASILIANO SERIKALINI KUJIONGEZEA UWEZO WA KITAALUMA KUTIMIZA MAJUKUMU YAO.

PROF.GABRIEL AMEWATAKA MAAFISA MAWASILIANO SERIKALINI KUJIONGEZEA UWEZO WA KITAALUMA KUTIMIZA MAJUKUMU YAO.

March 17, 2017
sh1
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na Maafisa Mawasiliano wakati wa ufungaji wa Kikao kazi kwa Maafisa hao kilichofanyika Mjini Dodoma.
sh2
Naibu Katibu Mkuu Bibi Nuru Millao akitoa mrejesho wa kikao kazi cha Maafisa Mawasiliano kwa mgeni rasmi wakati wa ufungaji wa hicho kwa Maafisa hao kilichofanyika Mjini Dodoma.
sh3
Mkurugenzi Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi akisisitiza jambo wakati wa ufungaji wa Kikao kazi kwa Maafisa hao kilichofanyika Mjini Dodoma.
sh4
sh5
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akitoa vyeti kwa kwa wadhamini kutoka TSN, TTCL, Multichoice Tanzania, TANAPA, SSRA mara baada ya kumalizika kwa kikao kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kilichofanyika Mjini Dodoma.
sh6
sh7
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa katika poicha ya pamoja na Maafisa Mawasiliano Serikalini na wadhamini wa kikao hicho mara baada ya kufungwa kwa kikao kilichofanyika Mjini Dodoma.

MKWABI SUPERMARKET YATUMIA MILIONI 26 KUDHAMINI TANGA CITY MARATHON

March 17, 2017
Meneja Mkuu wa Mkwabi Group Of Campainers,Kawkab
Hussein akuzungumza na waandishi wa Habari leo kuhusu mashindano ya Riadha ya Tanga Marathon yatakayofanyika Aprili 15 mwaka huu ambayo yamefadhiliwa na Kampuni hiyo kwa kuwekeza kiasi cha sh.milioni 16 kushoto ni Mratibu wa Mashindano hayo Juma Mwajasho na Kulia ni Katibu wa Chama cha Riadhaa Mkoani Tanga(RT)
Hassan Mwagomba
 Katibu wa Chama cha Riadhaa Mkoani Tanga(RT) Hassan Mwago mba akizungumza na waandishi wa habari leo kuishukuru kampuni ya Mkwambi Group of Campainers kufadhili mashindano ya Riadhaa Mkoani Tanga ya Tanga City  Marathon yatakayo fanyika April 15 mwaka huu katikati ni Mratibu wa Mashindano hayo Juma Mwajasho kulia ni Meneja Mkuu wa Mkwabi Group Of Campainers,Kawkab Hussein

Mratibu wa Mashindano hayo Juma Mwajasho akisistiza jambo kwenye mkutano na waandishi wa Habari Mkoanoi Tanga leo
 Sehemu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga wakiwa kwenye harakati za kuchukua matukio
 Sehemu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga wakiwa kwenye harakati za kuchukua matukio
Sehemu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga wakiwa kwenye harakati za kuchukua matukio

KAMPUNI ya Mkwabi Super Market imejitosa kudhamini Mashindano ya Tanga City Marathon kwa kuwekeza kiasi cha sh.milioni 16 ikiwa ni mkakati wa kurudisha hamasa na kuinua mchezo huo mkoani Tanga

Hatua ya Kampuni hiyo ambaye imekuwa mstari wa mbele kusaidia juhudi mbalimbali za michezo mkoani Tanga imelenga kurudisha hamasa na ushindani kwa washiriki.

Akizungumza na wandishi wa habari  leo Mratibu wa Mashi ndano hayo Juma Mwajasho alisema mbio hizo  zitaanza kutimua vumbi Aprili 15 mwaka huu katika Jiji la Tanga.

Mwajasho  alisema mashindano hayo yatasaidia kuongeza ari ya michezo na  kuamsha hamasa za wapenda riadha  katika mkoa wa Tanga na lengo ni kukuza michezo huo ambao utakuwa endelevu.

Alisema washiriki wa mashindano hayo kuanzia watoto wa miaka 12 kuendelea ambao  watakimbia mbio za kilometa tano,10,21, ambapo Mkwabi Super makert  .

Alisema mbio za kilometa tano fomu ya usajili itakuwa shilingi
1000,mbio za kilometa 10 sh 5,000 na mbio za kilometa 20 fomu itakuwa sh 8,000 ambapo mshindi wa kwanza ataondoka na kitita cha Tsh milion 10 na mshindi wa pili shilingi laki 700,000,mshindi wa tatu na wanne watapokea Tsh 500,000 na washindi wengine watapata kifuta jasho kila mmoja laki moja.

Katibu mkuu wa chama cha  riadha mkaoa wa Tanga Hassan Mwagomba alisema mashindano hayo kwao ni faraja  hivyo wameyapokea  kwa moyo nakwamba wataunga mkono juhudi hizo ili kuweza kufanikiwa mbio za Tanga City  marathoni mwaka huu wa 2017 .

Mwagomba alieza kuwa mashindano hayo ya mbio yataanzia  katika eneo la Mkwabi Super Makert  na kuzunguka  kwaminchi,kisha kuishia katika uwanja wa mkwakwani.

Alisema lengo kubwa la mashindano hayo ni kufufua riadha mkoani hapa ili kuweza kuleta mafanikio na yatashirikisha  wananchi wa mkoa mzima kwenye  halmashauri 11 na yatakuwa endelevu.

‘’Tunatarajia kupata wataalam  kutoka jijini Dar es salaam watakao wapima afya zao na usajili tayari umekwisha anza kwani zimebaki siku chache hivyo tuko kwenye hatua nzuri ya maandalizi’’alisema Mwagomba
RAIS DKT MAGUFULI ATOA MAELEKEZO YA KUTATUA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI KIJIJI CHA FUKAYOSI WILAYANI BAGAMOYO MKOA WA PWANI LEO

RAIS DKT MAGUFULI ATOA MAELEKEZO YA KUTATUA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI KIJIJI CHA FUKAYOSI WILAYANI BAGAMOYO MKOA WA PWANI LEO

March 17, 2017
fuka1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisiliza changamoto za wakulima na wafugaji katika kjijiji cha Fukayosi  wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani aliposimama  kwa muda na hatimaye kutoa maelekezo ya namna ya kutatua migogoro hiyo akiwa njia kuelekea Dar es salaam akitokea  katika ziara ya kikazi ya Dodoma leo Machi 17, 2017
fuka2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wanakjijiji wa  Fukayosi  wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani aliposimama  kwa muda na hatimaye kutoa maelekezo ya namna ya kutatua migogoro kati ya wakulima na wafugaji 
 akiwa njia kuelekea Dar es salaam akitokea  katika ziara ya kikazi ya Dodoma leo Machi 17, 2017
fuka3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maagizo kwa Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Mhe. Maggid Mwanga  baada ya kuongea na wanakjijiji wa  Fukayosi wilayani humo aliposimama  kwa muda na hatimaye kutoa maelekezo ya namna ya kutatua migogoro kati ya wakulima na wafugaji   akiwa njia kuelekea Dar es salaam akitokea  katika ziara ya kikazi ya Dodoma leo Machi 17, 2017.
fuka4
Baadhi ya wananchi wakishangilia hotuba ya Rais Dk. John Pombe Magufuli wakati alipoongea nao katika kijiji cha Fukayose wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
fuka5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiongea na wanakjijiji wa  Fukayosi wilayani humo aliposimama  kwa muda na hatimaye kutoa maelekezo ya namna ya kutatua migogoro kati ya wakulima na wafugaji  akiwa njia kuelekea Dar es salaam akitokea  katika ziara ya kikazi ya Dodoma leo Machi 17, 2017.
PICHA NA IKULU
MASHINDANO YA MAJESHI KUTIMUA VUMBI KESHO MACHI 18 ZANZIBAR

MASHINDANO YA MAJESHI KUTIMUA VUMBI KESHO MACHI 18 ZANZIBAR

March 17, 2017
JESHOI
MWENYEKITI wa Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMATA) Brigedia Jenerali Martin Amos Kemwaga, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusiana na mashindano ya vikosi vya ulinzi na usalama Tanzania itakayoanza kesho mjini Zanzibar.
JESHOI 1
 BAADHI ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMATA) Brigedia Jenerali Martin Amos Kemwaga uliofanyika ukumbi wa mikutano katika uwanja wa Amani.
 JESHOI 2
BAADHI ya wajumbe wa Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMATA) wakimsikiliza Mwenyekiti wao Brigedia Jenerali Martin Kemwaga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Picha na Makame Mshenga – Maelezo Zanzibar.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu yatembelea kampuni ya simu za mkononi Tigo.

March 17, 2017
Wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Miundombinu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania wakiwasili kwenye ofisi za Tigo Jijini Dar Es salaam leo


Mkurugenzi Mtendaji  wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez akiwakaribisha wajumbe wa kamati ya kudumu ya Miundo mbinu, mara baada ya kuwasili katika ofisi za Tigo Kijitonyama leo.
Mkurugenzi Mtendaji  wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez akiwakaribisha wajumbe wa kamati ya kudumu ya Miundo mbinu, mara baada ya kuwasili katika ofisi za Tigo Kijitonyama leo.
  Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya  bunge ya Miundo mbinu, Prof. Norman Sigalla  akifafanua jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji  wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez na mjumbe wa kamati hiyo.
  Mkurugenzi Mtendaji  wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez akiongea na wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya miundombinu kwenye kikao kilichofanyika leo ofisi za Tigo jijini Dar Es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji  wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez akifafanua jambo  kwa  wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya miundombinu kwenye kikao kilichofanyika leo ofisi za Tigo jijini Dar Es Salaam.
. Mjumbe wa kamati ya Miundombinu ya bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania Mh. Anna Tibaijuka akiongea na wafanyakazi wa Tigo
Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Ufundi Tigo,Jerome Albou, akifafanua jambo kwa wajumbe wa kamati ya miundombinu ya bunge la Tanzania walipotembelea ofisi za Tigo leo  
. Mjumbe wa kamati ya Miundombinu ya bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania Mh. Anna Tibaijuka akiongea na wafanyakazi wa Tigo
 Mkurugenzi Mtendaji  wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez akiongea na wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya miundombinu kwenye kikao kilichofanyika leo ofisi za Tigo jijini Dar Es Salaam.


VICE CHANCELLOR OF THE OPEN UNIVERSITY OF TANZANIA VISITS UNESCO DAR ES SALAAM OFFICE

VICE CHANCELLOR OF THE OPEN UNIVERSITY OF TANZANIA VISITS UNESCO DAR ES SALAAM OFFICE

March 17, 2017
On the morning of Friday,17thMarch 2017 Prof. Elifas Tozo Bisanda, the Vice Chancellor of the Open University of Tanzania (OUT) visited the UNESCO Office in Dar es Salaam. Prof. Bisanda, who is also the Chairperson of the UNESCO National Commission of the United Republic of Tanzania, had a meeting with the UNESCO Dar es Salaam Head of Office and Country Representative, Ms. Zulmira Rodrigues followed by a meeting with all office staff. UNESCO Dar es Salaam Head of Office and Country Representative Ms. Zulmira Rodrigues talking during the visit of Prof. Bisanda[/caption] During his meeting with staff members, Prof. Bisanda introduced the Open University of Tanzania, and outlined its history, mission, programs and innovative solutions in education and management introduced by the University. These included blended learning (combining online and face-to-face methodologies) and solutions for visually and hearing impaired learners. UNESCO Dar es Salaam Head of Office and Country Representative Ms Zulmira Rodrigues encouraged staff to take advantage of the learning opportunities that the OUT provides. The Open University of Tanzania is a long-time partner of UNESCO Dar es Salaam in implementation of education programs and projects in Tanzania, including the ongoing Chinese funded project, “Enhancing Teacher Education for Bridging the Quality Gap in Tanzania” Prof. Elifas T. Bisanda Vice Chancellor of the Open University of Dar es Salaam and Chairperson of the UNESCO National Commission of the United Republic of Tanzania talking to UNESCO Dar es Salaam staff members.

MASHIRIKA YA UMOJA WA MATAIFA NCHI TANZANIA WAFANYA MKUTANO NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI HAPA NCHINI

March 17, 2017
Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania yamewakutanisha wahariri ambao ni wanachama wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) ili kujadili namna ya kufanya kazi pamoja na mashirika hayo. Mashirika ya umoja wa mataifa yaliyoshiriki kwenye mkutano huo ni UNDP, ILO, FAO, WFP, UNHCR, UN Women, nk.

Akizungumza na wahariri Mwakilishi wa Shirika la Mipango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez amesema umoja wa mataifa uko bega kwa bega na waandishi wa habari ili kuonesha mchango wao kwenye jamii. Hivyo mchango wa waandishi wa habari ni wa msingi kwao na ili kuweza kutekeleza malengo waliyojiwekea hasa kuinua uchumi wa Tanzania.
Mwakilishi wa Shirika la Mipango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez akifungua mafunzo kwa wanachama wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) ulioandaliwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es Salaaam.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Nchini Tanzania Michael Dunford akizungumza  jambo kwenye mkutano uliowakutanisha wahariri wa vyombo kutoka Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliowakutanisha ili kujadili njia nzuri za kufanya kazi kwa pamoja ili kufikisha ujumbe kwenye jamii.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia. Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya akizungumza jinsi wanavyoshirikiana na serikali ya Tanzania pindi wanapoingia wakimbizi kutoka nchi mbalimbali zinazoizunguka nchini ya Tanznaia hasa zile nchi zenye migogogro ya kisiasa.
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UNAIDS Dk.Warren Namara akizungumza jambo pamoja natoa data kuhusu maambukizi ya virusi vya Ukimwi nchini pamoja na duniani na jinsi kiwango hicho kinavyopunguza nguvu kazi ya taifa.
Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Neville Meena akiwasilisha mada  kuhusu mazingira wanayofanyia kazi pamoja na kutolea ufafanuzi kuhusu jukwa la wahariri Tanzania linavofanya kazi hasa kwenye habari za jamii kwenye mkutano wao pamoja na Mashirika ya Umoja wa Mataifa uliofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Viongozi mbalimbali wa Mashirika ya umoja wa mataifa nchini Tanzania wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Neville Meena kwenye mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.

TAASISI YA MKAPA YAKABIDHI KWA WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII MKOANI KATAVI VITENDEA KAZI VYENYE THAMANI YA SH. MIL 33

March 17, 2017
Taasisi ya Benjamin W. Mkapa (BMF) jana imekabidhi vitendea kazi (baiskeli 158, mabegi 150, mabuti 25 na makoti ya mvua 25) vyenye thamani ya Shs 33,985,000 kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mej. Jenerali (Mstaafu) Raphaeli Muhuga kwa lengo la kuwasaidia Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na urahisi zaidi. 

Taasisi ya Mkapa kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto – Mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu na Ukoma pamoja na Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi inatekeleza mradi wa Ukimwi na Kifua Kikuu chini ya Shirika la Save the Children kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa Kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria. 

Mradi huu unaotekelezwa kwa kipindi cha miaka 3 katika mikoa ya Rukwa, Katavi, Tabora na Kigoma unalenga kuisaidia Serikali kupunguza maambukizi ya Kifua kikuu kwa 25% na kupunguza vifo vitokanavyo na Kifua Kikuu kwa 50% mpaka kufikia 2020. Pamoja na hayo mradi unalenga kupunguza maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi, Kupunguza vifo vitokanavyo na Ukimwi, kutokomeza unyanyapaaji na kuongeza upatikanaji wa urahisi wa huduma za Ukimwi hasa upimaji wa VVU. 

Katika kuhakikisha malengo ya mradi yanafikiwa Taasisi ya Mkapa imetoa mafunzo mbalimbali katika ngazi ya jamii ikiwemo mafunzo kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii 183 juu ya ubainishaji na ufuatiliaji wa wagonjwa wa kifua kikuu ndani ya jamii. Pamoja na hayo jana imekabidhi baiskeli 158, mabegi 150, mabuti 25, na makoti ya mvua 25 kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi zitakazotumiwa na wahudumu hao katika utekelezwaji wa majukumu hayo ya ubainishaji na ufuatiliaji wa wagonjwa wa kifua kikuu na ukimwi kwenye jamii husika.

Afisa mradi kutoka Taasisi ya Mkapa Bw. David Magiri akikabidhi nyaraka za vifaa kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mej. Jenerali (Mstaafu) Raphaeli Muhuga, kulia kwake ni Katibu Tawala Katavi, Ndg. Paul Chagonja
Bi. Flora Cosmas, Mhudumu wa Afya ngazi ya Jamii akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mej. Jenerali (Mstaafu) Raphaeli Muhuga, baada ya kupokea baiskeli iliyotolewa na Taasisi ya Mkapa.
Mkuu wa Mkoa Katavi Mhe. Mej. Jenerali (Mstaafu) Raphaeli Muhuga, Katibu Tawala Katavi, Ndg. Paul Chagonja, Afisa Mradi wa Kifua Kikuu na Ukimwi Taasisi ya Mkapa, Ndg. David Magiri katika picha ya pamoja na Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii katika halfa ya kukabidhiwa vitendea kazi kutoka Taasisi ya Mkapa.
Katibu Tawala Mkoa wa Katavi, Ndg. Paul Chagonja akiendesha moja ya baiskeli zilizotolewa na Taasisi ya Mkapa kwa lengo la kuwasaidia ufanyaji kazi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii mkoa wa Katavi
Hafla ya ukabidhishwaji wa vitendea kazi kwa Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii mkoa wa Katavi.

MAMONGÓO: HATUSEMI DILI ZETU KWA KUWA WACHAWI NI WENGI!

March 17, 2017

Vijana kutoka Arusha maarufu kwa ngoma zao kama kimbaumbau na digidigi wanaojulikana kama Mamongóo (vijana washamba), wamesema kuwa jamii ya sasa hivi inawatisha kutangaza mishe zao wanazofanya nje ya muziki.
Mamong’oo wiki hii wakiwa katika ziara yao kikazi Dar es salaam, wamesema kuwa wao wanajihusisha na biashara nyingi ikiwemo kilimo na ufugaji kama zilivyo jamii nyingi mkoani Arusha. Lakini mtangazaji  DJ Tee wa kipindi cha vijana cha Shujaaz alipotaka kufahamu mishe zingine wanazofanya wasanii hao walisema hawawezi kumwaga mchele maana siku hizi wanga ni wengi.
“Sisi pesa zetu hatujahifadhi benki ila tumeziweka sehemu ambayo tunajua zina mzunguko wa kuzalisha, na tumewekeza kwa vijana wenzetu” alisema chalii Jambo kutoka kundi hilo. Hata hivyo, walipoulizwa ikiwa kijana amepata pesa anatakiwa kuwekeza kwenye kitu gani kwanza kati ya shamba, nyumba au ardhi, walisema kwamba ardhi ndio kitu ambacho kinafaa kwa kijana kuwekeza kabla ya kununua gari au hata nyumba maana ardhi inaweza kuleta nyumba na gari.
Wasanii wengi siku hizi wamekuwa na kasumba ya kutumia mishe zao wanazofanya pembeni ya sanaa sio kwa kujiongezea kipato pekee bali kujipatia heshima miongoni mwa fans wao. Mfano mzuri ni msanii Masanja Mkandamizaji ambaye kwa sasa amekuwa akitengeneza mamilioni ya pesa kutokana na biashara ya #KilimoPesa ambapo yeye analima mpunga pamoja na kumiliki mgahawa wa kuuza wali nyama pamoja na biashara zingine tusizozifahamu.
Kipindi cha vijana cha Shujaaz huruka hewani kila Jumamosi saa nne kamili asubuhi kupitia Abood FM ya Morogoro, kisha safari huendelea saa tisa alasiri kupitia East Africa Radio, TBC FM na Chuchu FM ya Zanzibar kwa wakati mmoja, huku KingsFM ya Njombe ikijiunga saa kumi jioni.