SHEIKH MKUU WA TANZANIA MUFTI SHAABAN BIN SIMBA AFARIKI DUNIA

June 15, 2015

SHEIKH mkuu wa Tanzania (Mufti) Shaaban Simba amefariki muda mfupi uliopita jijini Dar es Salaam. Habari za uhakika kutoka ndani ya Baraza Kuu la Tanzania (BAKWATA) zimeifahamisha Saluti5 kuwa Mufti amefariki katika hospitali ya TMJ baada ya kuzidiwa na tatizo la mapafu. INNA LILLAHI WA INNA ILAYHI RAAJI'OON

MAKONDA AONGOZA MAMIA MAZISHI YA BABA YAKE MSANII STEVE NYERERE

June 15, 2015

 Marehemu Francis Festus Mengele, enzi za uhai wake.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Francis Festus Mengele.
 Shangazi wa Msanii, Steve Nyerere, Grace Mengele (katikati), akiwa na wadogo zake Steve Nyerere wakati akiwasili makaburi ya Kinondoni kwa mazishi ya mpendwa wao, Francis Mengele.
 Watoto wa marehemu na dada zake wakiwa kwenye ibada ya maziko makaburi ya Kinondoni.
 Ibada ya maziko ikiendelea.
 Hali ilivyokuwa wakati wa mazishi.
 Jeneza lenye mwili wa marehemu Francis Mengele 
likishushwa kaburini.
  Jeneza lenye mwili wa marehemu Francis Mengele 
likishushwa kaburini.
 Wasanii mbalimbali wakiwa kwenye mazishi hayo.
 Ni huzuni tupu.
 DC Makonda akiwa udongo kwenye kaburi la Francis Mengele wakati wa mazishi.
 Kaburi likijengwe baada ya kuwekwa mwili wa marehemu kaburini.
 Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu Francis Mengele.
 Waombolezaji wakiwasili makaburi ya Kinondoni tayari 
kwa mazishi.
 Hali ilivyokuwa makaburini.
 Hali ilivyokuwa makaburini.

Wasanii  mbalimbali wakiwa kwenye maziko hayo.

Na Dotto Mwaibale



WASANII mbalimbali wa filamu na bongo fleva  wamejitokeza kwa wingi katika mazishi ya baba ya msanii mwenzao Steve Mengele 'Steve Nyerere, yaliyofanyika jana makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.


Msanii Jacob Stephen JB ni miongoni mwa wasanii waliohudhuria mazishi ya marehemu Francis Mengele baba yake na msanii huyo aliyefariki wiki iliyopita kutokana na maradhi ya mapafu.


Wasanii wengine waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Micky, Vicent Kigosi 'Ray' Elizabeth Michael 'Lulu' Chuchu Hans, Kajala Masanja 'Kajala' , Mtunzi na muongozaji wa filamu Myovela Mswaisa na wengine wengi.


Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda aliyeongoza mazishi hayo alisema kifo cha Mengele ni pigo kubwa katika wilaya hiyo ya Kinondoni na familia kwa ujumla.


"Mengele alikuwa na mchango mkubwa katika wilaya yetu ya Kinondoni katika kulipa kodi kutokana na biashara zake alizokuwa akizifanya na wingi huu wa watu waliojitokeza katika mazishi yake inaonesha jinsi alivyokuwa akishirikiana na wenzake hasa waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Usharika wa Kimara alikokuwa akisali" alisema Makonda.



Makonda alitumia fursa hiyo kuiomba Manispaa ya Kinondoni ndani ya miezi mitatu kuhakikisha inajenga choo katika makaburi hayo ya Kinondoni kwani ni aibu kwa eneo hilo kukosa choo hivyo kuwafanya wananchi wanaofika kwa ajili ya maziko kukosa huduma ya choo. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-0712-727062)

BILIONEA DANGOTE ALIDHIA UJENZI WA BANDARI YAKE MTWARA KWA KUSHIRIKIANA NA TPA

June 15, 2015


 Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Dangote, Alhaji Aliko Dangote, akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Hawa Ghasia alipowasili kwenye uwanja wa Ndege mjini Mtwara jana kwa ajili ya kutembelea kiwanda chake cha Cementi kilichoko Msijute, mkoani Mtwara.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Hawa Ghasia akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Dangote, Alhaji Aliko Dangote, alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mtwara leo kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha Cementi cha Dangote. Katikati ni Balozi wa Nigeria Nchini Tanzania, Ishaya Manjanbu.

 Mkurugenzi wa Makampuni ya Dangote, Alhaj Aliko Dangote (kulia), akijadiliana jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka, walipokutana mjini Mtwara jana kuangalia uwezekano wa kujenga kituo cha kusafirisha saruji katika eneo la Bandari ya Mtwara.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Dangote, Alhaji Aliko Dangote, akizungumza na waandishi wa habari baada kuwasili mjini Mtwara jana na kutembelea kiwanda chake cha Cementi, kilichoko Msijute, mkoani Mtwara.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Dangote, Alhaj Aliko Dangote akisaini kitabu cha wageni, baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege mjini Mtwara jana, kwa ajili ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda chake cha saruji. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka.
 Mkurugenzi wa Makampuni ya Dangote, Alhaj Aliko Dangote akiwafuatana na wenyeji wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Hawa Ghasia (wa pili kushoto), Balozi wa Nigeria, Ishaya Manjanbu (wa pili kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Bi. Fatma Salum Ali (kushoto), alipowasili kwenye uwanja wa ndege, mjini Mtwara jana.





Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Dangote, Alhaj Aliko Dangote, akiteta jambo na Mwakilishi mkazi wa Dangote nchini Tanzania, Bi. Esther, mjini Mtwara , baada ya Mkurugenzi huyo kutembelea kiwanda chake cha saruji kinachojengwa mkoni Mtwara.

Serikali kuboresha huduma ya ardhi

Serikali kuboresha huduma ya ardhi

June 15, 2015

01
Balozi wa Ireland nchini Tanzania Bi Fionnuala Gilsenan akisaini kitabu cha wageni alipomtembelea Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (kushoto) ofisini kwake leo jijini Dar es salam.
02
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiongea na mgeni wake Balozi wa Ireland nchini Tanzania Bi Fionnuala Gilsenan (kulia) leo jijini Dar es salam. Kushoto ni Kamishna wa Ardhi nchini Dkt. Moses Kusiluka.
03
Balozi wa Ireland nchini Tanzania Bi Fionnuala Gilsenan akisisitiza jambo wakati alipomtembelea Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (kushoto) ofisini kwake leo jijini Dar es salam.
04
Balozi wa Ireland nchini Tanzania Bi Fionnuala Gilsenan akiwaonesha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (katikati) na Kamishna wa Ardhi nchini Dkt. Moses Kusiluka (wa kwanza kushoto) baadhi ya picha na michoro inayoonesha namna bora ya matumizi ya ardhi kulingana na matumizi husika ikiwemo mipango miji na vijiji.
…………………………………………….
Na EleuteriMangi-MAELEZO
Serikali inadhamira yadhati kuboresha huduma ya ardhi nakuipeleka karibu na wananchi kwa wakati ili iwe na tija kwa maendeleo endelevu. Hayo yamebainishwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alipokuwa akiongea na Balozi wa Ireland nchini Tanzania Bi Fionnuala Gilsenan leo jijini Dra es salam. Akifafanua kuhusu namna huduma hiyo itakavyopelekwa karibu na wananchi, Waziri Lukuvi amesemakuwa wizara yake imeanzisha kanda nane ili kusogeza huduma za ardhi karibu na wananchi badala ya hali ilivyokuwa zamani ambapo huduma hizi zilitolewa makao makuu ya wizara hiyo tu yaliyopo jijini Dar es salaam. “Ili kutoa huduma ya ardhi kwa wakati kwa wananchi, huduma ya utoaji wa Hatimiliki za ardhi sasa ni kwenye kanda ambazo zinasimamiwa na Makamishna wa Ardhi Wasaidizi.” Alisema Lukuvi. Kanda hizo ni kanda ya Dar es salaam inayojumuisha Manispaa za Ilala, Temeke na Kinondoni, kanda ya Mashariki ambapo makao makuu yake yapo Morogoro, kanda ya Magharibi makao yake makuu yapo Tabora, kanda ya Ziwa makao yake makuu yapo Mwanza na kanda ya Kaskazini makao yake makuu yapo Moshi mkoani Kilimanjaro. Kanda nyingine ni pamoja na kanda ya kusini ambayo makao yake makuu yapo Mtwara, kanda ya Kusini Magharibi makao yake makuu yapo Mbeya na Kanda ya Kati ambayo makao yake makuu yapo mkoani Dodoma. Katika kutoa huduma yenye ubora kwa wananchi kwa wakati, Serikali kwa kushirikiana na Halmashauri wataongeza watumishi wakada za wapimaardhi, wapangaji wa miji na vijiji pamoja na wathaminia mbao watafanyakazi kwa pamoja kwenye kanda husika ambapo huduma ya ardhi itakuwa karibu zaidi na wananchi. Naye Balozi wa Ireland nchini Tanzania Bi Fionnuala Gilsenan amempongeza Waziri Lukuvi na watendaji wote wa wizara hiyo kwa kuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma haraka na kwa wepesi zaidi kwa jamii hatua ambayo ni yakupongezwa na kila mpenda maendeleo. Balozi Bi Gilsenan alisema kuwa ardhi nibidhaa muhimu inayoweza kutumika kwa kutoa huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo elimu, maji, barabara, ujenzi wa viwanda na miundo mbinu mingine ili kumfanya mwananchi kupata huduma yenye tija kwa wakati. Aidha, kwa upande wake Kamishna wa Ardhi nchini Dkt. Moses Kusiluka alisema kuwa utoaji wa huduma ya usimamizi wa ardhi umeanza kuboreshwa kwa kubadili mfumo wa utoaji wa huduma kuwa wa kielekroniki kutoka mfumo wa kawaida, yaani‘manual’. Dkt. Kusiluka amesisitiza kuwa mfumo wa kielektroniki utaboresha sana utoaji wa huduma za ardhi, ikiwa ni pamoja nak uondoa tatizo la milkipandikizi (double allocation), kuondoa udanganyifu, kuongeza ufanisi wa watendaji na kuongeza mapato ya Serikali.
KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AITIKISA CHATO MKOANI GEITA

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AITIKISA CHATO MKOANI GEITA

June 15, 2015

1
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasha mtambo wa maji uliojengwa Chato Mlimani kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji utakaohudumia wakazi wa mji huo leo wakati wa ziara yake katika mkoa wa Geita , Kinana anaendelea na ziara hiyo ya kikazi mkoani humo baada ya kumaliza ziara kama hiyo mkoani Kagera jana, Kinana anaendelea  na ziara hiyo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010-2015 na kuhimiza uhai wa chama, kukosoa na kutatua matatizo mbalimbali yanayokabili wananchi kwa maisha na maendeleo yao kwa ujumla akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.(PICHA NA KIKOSI CHA FULLSHANGWE-CHATO-GEITA)
2
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  na Mkuu wa wilaya ya Chato Rodrick Mpogolo kulia wakipiga makofi mara baada ya kuwashwa rasmi kwa mtambo huo.
3
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, Rodrick Mpogolo Mkuu wa wilaya ya Chato na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi pamoja na viongozi wa CCM wilaya ya Chato wakipunga mikono na wanaCCM mbalimbali katika picha ya pamoja.
4
Baadhi ya wananchi wakigombea kupanda gari kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Chato.
5
Baadhi ya akina mama wakiwa na ndoo zao tayari kwa kuchota maji mara baada ya kuzindua rasmi mtambo wa maji Chato Kilimani ambao utahudumia wakazi wa mjini Chato na baadhi ya vijiji.
6
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji Paulina Sabinati mara baada ya uzinduzi wa mradi huo.
7
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na  Mkuu wa wilaya ya Chato Ndugu Rodrick Mpogole, viongozi wa CCM wilaya ya Chato pamija na mafundi wa Tanesco akishiriki kutandaza waya za umeme katika mradi wa umeme vijijini REA katika kijiji cha Mkungo.
8 9
Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ukisimama baada ya wananchi wa kijiji cha Mkaurugusi wilayani Chato wakati akielekea kijiji cha Ihanga.
10
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma mabango ya wananchi waliosimamisha msafara wake wakiomba awasaidia kufanikisha mpango wa kuwawekea umeme katika kijiji chao cha Makurugusi ambacho laini ya umeme kuelekea kijiji cha jirani imepitia.
11
Mwakilishi wa wananchi hao wa kijiji cha Makurugusi Bw. Shampinga David akielezea masikitiko ya wananchi hao kutokana na mpango wa umeme vijijini kupita kijiji chao bila kuwawekea umeme huo Bw. Shampinga amemuomba Kinana kuhakikisha anawasaidia na wao wanapata umeme katika kijiji chao.
12
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi hao.
13
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipeana tano na wananchi hao mara baada ya kuwaahidi kuongea na Waziri wa Nishati na Madini ili kijiji hicho kiwekewe umeme vijiji  REA ambapo wanakijiji hao walijawa na furaha mara baada ya kusikia kauli hiyo kutoka kwa kiongozi huyo wa juu wa CCM.
14
Baadhi ya wananchi wakiwa wamepanda kwenye pikipiki wakielekea kwenye mkutano wa Kinana katika kijiji cha Ihanga ambako alishiriki katika ujenzi wa nyumba ya daktari.
15
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia ngoma mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Ihanga.
16
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika ujenzi wa nyumba ya daktari katika kijiji cha Ihanga wilayani Chato.
17
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi  na Uenezi akipungia mkono wananchi mara baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara mjini Chato.
18
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Chato.
19
Kwaya ikiimba wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM mjini Chato alipowasili katika mkutano wa hadhara.
20
Wananchi wakinyanyua mikono yao juu juu kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
21
Mkuu wa wilaya ya Chato Ndugu Rodrick Mpogolo akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara mjini Chato.
22
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika
23
Baadhi ya wananchi wakiwa juu ya magari wakifuatilia hotuba za viongozi mbalimbali katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika mjini Chato mkoani Geita leo.
24
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akihutubia mkutano wa hadhara mjini Chato.
25
Nape akisisitiza jambo wakati akihutubia mkutano huo.
26
Umati wa wananchi ukiwa katika mkutano huo.
27
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano huo.
28 29 30 31
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo katika mkutano huo.
32
Baadhi ya wananchi wakirejea nyumbani mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo.