KUMUWAKILISHA MAKAMU WA RAIS DKT MOHAMMED GHARIB BILAL HARAMBEE MSIKITI WA PATANDI, JIJINI ARUSHA

May 12, 2015

Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa.

MHESHIMIWA EDWARD LOWASSA KUMUWAKILISHA MAKAMU WA RAIS DKT MOHAMMED GHARIB BILAL KWENYE HARAMBEE YA UCHAGIAJI UJENZI WA MSIKITI WA PATANDI, JIJINI ARUSHA, IJUMAA  MEI 15,2015.
 
Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inapenda kuutaarifu umma kuwa shughuli ya Harambee ya kuchangia ujenzi wa Msikiti wa Patandi uliopo wilaya ya Arumeru jijini Arusha ambao umepangwa kufanyika Ijumaa ya tarehe 15, 2015 na ambayo awali ilitangazwa kuwa mgeni Rasmi katika Harambee hiyo angekuwa Mheshimiwa Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sasa itasimamiwa na Mheshimiwa Edward Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa jimbo la Monduli.
 
Mabadiliko haya yanatokana na Mheshimiwa Makamu wa Rais kukabiliwa na majukumu mengine ya Kitaifa na hivyo kutoa ombi maalum kwa Mheshimiwa Edward Lowassa kumuwakilisha katika shughuli hiyo jambo ambalo amekubali.
 
Kufuatia taarifa hii, tunauomba umma na wananchi wote wenye nia njema kushirikiana nasi pamoja na mgeni Rasmi atakayemuwakilisha Makamu wa Rais katika harambee hiyo inayolenga kukusanya fedha ili kukamilisha msikiti huo ambao ulianza kujengwa mwishoni mwa miaka ya 1990.
 
Msikiti wa Patandi upo katika eneo wanalokaa wananchi wenye imani mbalimbali na waumini wanaoutumia msikiti huu, wamekuwa wakijitoa kwa namna nyingi katika kusaidia kujenga mshikamano baina ya jamii zinazowazunguka bila kuwa na vikwazo na pia wamekuwa wakishiriki katika kuwasaidia watoto yatima na wengine wenye uhitaji katika kukabiliana na maisha yao. 
 
Kufuatia dhima hii na mchango huo wa wanajamii wanaoswali katika Msikiti huu, Mheshimiwa Makamu wa Rais ameona na imempendeza kuwa, shughuli hii ya uchangiaji ujenzi isisogezwe mbele kumsubiri bali iendelee kwa kuwa anaamini Mheshimiwa Lowassa ni mzoefu katika kufanikisha shughuli za aina hii na kwamba mchango wake katika jamii hasa shughuli za harambee ni wa kutiliwa mfano. Tunawakaribisha sana kushirikiana naye katika kufanikisha Harambee hii. Kumbukeni kutoa ni moyo na wala si utajiri!
 
Imetolewa na:  Boniphace Makene
     Mwandishi wa Habari wa Makamu wa Rais
Dar es Salaam: 12 Mei 2015

BREAKIN NEWZZ!!:- RAIS JK AMTEUA MKURUGENZI MPYA WA MAKOSA YA JINAI!!

May 12, 2015

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Kamishna wa Polisi (CP) Diwani Athumani Msuya, kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai (Director of Criminal Investigation).

Kabla ya uteuzi huu CP Msuya alikuwa Kaimu Kamishna wa kamisheni ya Intelijensia ya Jinai. CP Msuya anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Robert S. Manumba ambaye amestaafu kwa mujibu wa Sheria.

Rais Kikwete pia amemteua Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Valentino Mlowola kuongoza Idara ya Intelijensia ya Jinai, kujaza nafasi inayoachwa na Kamishna Msuya.

Kabla ya Uteuzi huu, DCP Mlowola alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza.

Uteuzi huu umeanza tarehe 3 Mei, 2015



Imetolewa na;

Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam.
12 Mei, 2015

NGASSA ASAINI MIAKA MINNE AFRIKA KUSINI, NI KLABU AMBAYO NTEZE JOHN, TSHABALALA NA KENNEDY MWEENE WALICHEZEA

May 12, 2015
Na Mahmoud Zubeiry, BETHELEHEM
KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa amesaini Mkataba wa miaka minne kujiunga na klabu ya Free State Stars ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini leo.
Ngassa, mume wa Radhia na baba wa Farida (8) na Faria (6) aliwasili jana jioni mjini hapa na leo asubuhi baada ya kukamilisha mazungumzo, akasaini Mkataba huo mnono.
“Nimefurahi kusaini timu hii, ambayo kaka yangu Nteze John amewahi kuchezea pamoja na wachezaji wengine wakubwa kama Tshabalala na Mweene,”alisema Ngassa.
“Sasa najiandaa kwa maisha mapya baada ya kucheza Tanzania kwa muda mrefu, hii ni changamoto mpya kwangu, mpira wa Afrika Kusini upo juu sana ukilinganisha na pale kwetu (Tanzania). Nataka kutumia fursa hii kuitangaza soka ya Tanzania, ili klabu zisijifikirie tena kusajili wachezaji wa Tanzania,”amesema Ngassa.
Kocha Kinnah Phiri (kushoto) akimkabidhi Ngassa jezi ya Free State Stars leo, makao makuu ya klabu hiyo, Mtaa wa 22B President Boshoff mjini Bathlehem baada ya kusaini Mkataba wa miaka minne kuichezea timu hiyo
Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa timu hiyo maarufu kama Ea Lla Koto, Mmalawi Kinnah Phiri amesema kwamba amekuwa akimpenda Ngassa kwa muda mrefu na kukutana naye FS ni kutimia kwa ndoto zake za kufanya kazi na kijana huyo siku moja. 
Katika Mkataba huo ambao Ngassa, mtoto wa kiungo wa zamani wa Simba SC, Khalfan Ngassa atakuwa analipwa karibu mara tatu ya mshahara aliokuwa anapata Yanga SC, atapatiwa nyumba ya kuishi na familia yake, gari na huduma nyingine muhimu, ikiwemo bima. 
Ngassa anakuwa Mtanzania wa pili kuichezea Free State, baada ya Nteze John Lungu ‘mwana Mwanza’ pia aliyeichezea timu hiyo enzi hizo inaitwa Qwa Qwa Stars mwaka 1997 hadi 1999.   
Ngassa anatua Free States akitokea Yanga SC, ambayo ameichezea jumla ya mechi 186 katika awamu mbili, na kuifungia jumla ya mabao 86.
Ngassa aliyetimiza miaka 26, Aprili 12 mwaka huu, alijiunga na Yanga SC kwa mara ya kwanza mwaka 2006, akitokea Kagera Sugar iliyomuibua mwaka 2005 kutoka timu ya vijana ya Toto Africans ya Mwanza.
Mwaka 2010 alihamia Azam FC kwa dau la rekodi wakati huo, dola za Kimarekani 40,000 (Sh. Milioni 80). 
Kabla ya hapo, akiwa Yanga SC, Aprili mwaka 2009, Ngassa alikwenda kufanya majaribio klabu ya Ligi Kuu England, West Ham United wakati huo chini ya kocha Mtaliano Gianfranco Zola.
Hata hivyo, pamoja na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Zola kuvutiwa na uwezo wa mchezaji huyo kisoka, akasema Ngassa anahitaji kurejea Afrika kuongeza lishe. 
Julai mwaka 2011, Ngassa alikwenda kufanya majaribio Seattle Sounders FC ya Ligi Kuu ya Marekani na akatumiwa katika mchezo wa kujiandaa na msimu dhidi ya Manchester United ya England.
Hata hivyo, Azam FC haikuwa tayari kumuuza mchezaji huyo. Ngassa alicheza Azam FC hadi mwaka 2012 alipohamia Simba SC kwa mkopo na mwaka 2013 akarejea timu yake kipenzi, Yanga SC ambayo, ameiaga baada ya msimu akiiachia ubingwa wa Ligi Kuu.
Mfungaji huyo bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita, pia amewahi kuwa Mchezaji Bora wa Tanzania mara mbili mwaka 2010.
Mwaka 2005 akiwa Kagera Sugar alishinda Kombe la Tusker wakiifunga Simba SC katika fainali na alipohamia Yanga SC alishinda mataji ya Ligi Kuu katika misimu ya 2008, 2009 na 2015.
Ameshinda pia mataji ya Tusker mwaka 2007 na 2009 akiwa na Yanga SC, wakati akiwa na Azam FC aliiwezesha timu hiyo kushika nafasi ya pili katika Ligi Kuu na Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame mwaka 2012.
Amekuwa Mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2010–2011 akiwa na Azam FC na mfungaji bora wa Kombe la Challenge mwaka 2009.
Huyo ndiye mchezaji bora wa Ligi Kuu mwezi Apirli mwaka huu, ambaye ana nafasi kubwa ya kuwa pia Mchezaji Bora wa jumla wa Ligin Kuu msimu huu.
Amekuwa mchezaji muhimu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars tangu mwaka 2007 na hadi sasa amiechezea timu hiyo mechi 82 na kuifungia mabao 22.
Ngassa aliwaaga Yanga SC baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu


KUHUSU FREE STATE;
Free State Stars ni timu yenye maskani yake mjini Bethlehem, Free State ambayo inacheza Ligi Kuu ya Afrika Kusini, maarufu kama PSL.
Haswa ilianzishwa mwaka 1977 katika mji mdogo wa Makwane katika zama za QwaQwa, na ikafanikiwa kupanda Ligi Kuu mwaka 1986.
Timu hiyo ikashinda Kombe la Ligi, michuano ambayo baadaye ikabadilishwa jina na kuwa Kombe la Coca Cola. 
Baada ya kuteremka daraja kufuatia kuyumba kiuchumi, mwaka 2003 klabu hiyo iliuzwa kwa 
Mike Mokoena na familia yake ambaye aliifufua ikianzia Daraja la kwanza kabla ya kufanikiwa kurejea Ligi Kuu mwaka 2005 baada ya kushinda Kombe la Ligi ya Mvela Golden.
Lakini katika msimu wake wa kwanza Ligi Kuu ilishika mkia na kuteremka tena, lakini ikafanikiwa kurejea tena PSL msimu wa 2007–2008. Pia walifanikiwa kushinda taji la Kombe la Baymed Desemba 2006 baada ya kuifunga FC AK katika fainali.
Tangu hapo, timu hiyo ambayo wamepita nyota kadhaa waliotamba katika soka ya Afrika Kusini kama Bunene Ngaduane wa DRC, Jonathan Mensah wa Ghana, Kennedy Mweene wa Zambia na watoto wa nyumbani, John Tlale, Siphiwe Tshabalala na Thabo Matlaba imekuwa imara katika PSL, msimu huu ikimaliza nafasi ya tisa.
TEITI yawanoa waandishi wa habari za biashara juu ya uwazi katika sekta ya madini nchini

TEITI yawanoa waandishi wa habari za biashara juu ya uwazi katika sekta ya madini nchini

May 12, 2015

41Mwenyekiti wa Mpango wa Uhamasishaji wa Uwazi katika Mapato ya Madini, Gesi asilia na Mafuta (Tanzania Extractive Industries Transparency Initiative (TEITI), Jaji Mstaafu, Mark Bomani akifungua warsha ya siku moja kwa wadau na wandishi wa habari za biashara, mkutano uliofanyika Ledger Plaza Bahari Beach Hotel jijini Dar es Salaam, Mei 7, mwaka huu.

Na Andrew Chale, Modewji blog
Mwenyekiti wa Mpango wa Uhamasishaji Uwazi katika Mapato ya Madini, Gesi Asilia na Mafuta (TEITI) Jaji Mark Boman amewataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi zenye lengo la kuielimisha jamii hasa pindi wanaporipoti habari za sekta ya madini hapa nchini.

Akizungumza wakati wa semina ya waandishi wa habari za biashara na uchumi ya siku moja iliyofanyika hivi karibuni Ledger Plaza Bahari Beach Hotel, jijini Dar es Salaam, Jaji Bomani alisema taarifa sahihi hasa za masuala ya uchumi zinahitajika kwani zikitolewa tofauti zinaweza kusababisha mkanganyiko kwa wananchi.

Alisema taasisi hiyo ilianzishwa kuwa lengo la kufuatilia sekta ya madini kwani hapo awali ilionekana kutowanufaisha wananchi.

“Awali kuliwa na mkanganyiko wa kwamba sekta ya madini haiwanufaishi wazawa hivyo Serikali ilichukua hatua na kuunda kamati ya kushughulikia tatizo hilo kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta hiyo ya madini,”alisema.

Alisema chombo hicho kilianza kutoa ripoti za ufuatiliaji wa sekta za Serikali kwa makini na fedha zinazolipwa. Alisema Ripoti ya nne ambayo ni ya mwaka 2014 inaonyesha kwamba mapato ya Serikali yamekuwa yakiongezeka kila mwaka tofauti na ripoti ya kwanza iliyokuwa na hitilafu ya Dola milioni 30.

Alisema mafanikio ya utaratibu huo umesaidia taasisi za Serikali kuhakikisha kwamba kila fedha inayotoka au kulipwa inakuwa ya maandishi ili kuwa na taarifa sahihi.
1Afisa mahusiano Mkuu wa TEITI, Catherine Mbatia akimkaribisha rasmi Mwenyekit wa TEITI, Jaji Mark Boman kwa ajili ya ufunguzi rasmi wa Warsha hiyo iliyowakutanisha wandishi wa habari za biashara na wadau mbalimbali ikiwemo wadau wa madini.

Naye Mjumbe wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) George Kibakaya alieleza kuwa, kiasi cha gesi asilia kilichogunduliwa ni futi za ujazo tirioni 55 hivyo ni vyema kujipanga vizuri ili kuhakikisha kinakuza uchumi wa nchi.

Aidha, katika semina hiyo wandishi wa habari walipata pia fursa ya kujifunza namna ya upatikanaji wa data kwa njia ya mtandao huku wakishahuriwa kuwa pindi wanahabari watafutapo data, kuweza kuwasiliana na wataalam husika iliondoa mkanganyiko ikiwemo idara za kifedha, wataalamu wa hesabu pamoja na mifumo sahihi ya data hasa kupitia mifumo ya inteneti.

Mafunzo hayo ya kuripoti habari kwa kutumia uchambuzi wa data, yalitolewa na Samuel Osei Bekoe kutoka taasisi ya NRGI ya nchini Ghana ambaye alitoa wito kwa wandishi wa habari wa Tanzania hasa wanaotaka kuandika habari za kiuchunguzi katika uripoti wa mahesabu na data kuzingatia vyanzo vya taarifa vya kina na vyenye uhakika.

Ambapo alishahuri kuwa licha ya upatikanaji wa data hizo kuwa mgumu na wa sili kwa baadhi ya sekta, aliwataka wandishi kutumia vipengele muhimu na kwa ufupi bila kuweka mambo mengi ambayo yataweza kumchanganya msomaji.

Akitolea mfano wa taarifa za kiuchumi kwa Tanzania ama nchi zingine, ambapo endapo wataingia kwenye mitandao ya taasisi ya kifedha, Ikiwemo IMF, Benki kuu na zingine zimekuwa na uwazi hivyo wanaweza kupata huko taarifa ambazo zinaweza kuwasaidia kuripoti na kuleta changamoto katika nchi huku akisisitiza kutaja chanzo cha taarifa ama ripoti hiyo.

Pia wadau mbalimbali wakiwemo wataalamu wa madini na wandishi wa habari walitoa mada mbalimbali zilizojadiliwa kwa kina katika semina hiyo kwa mfumo wa mdaharo.
6
Meneja Mahusiano, Alex Modest, (kulia)akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika semina hiyo watatu kulia ni Meneja mikakati kutoka (TBDC) George Kibakaya (kushoto) Mwenyekiti TEITI,Jaji Bomani,wa pili kushoto mwandishi mchambuzi, John Bwire,(katikati) ni Halfani Halfani kutoka (Oil Gas Association Tanzania-OGAT).

NIDA WATUA TANGA,WAANZA KUWAANDISHA WANANCHI WA JIJI LA TANGA NA MAENEO MENGINE MKOANI HAPA.

May 12, 2015
 Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Abdalla Lutavi, akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi la usajili vitambulisho vya  Taifa, kushoto  ni Afisa Habari Mkuu Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Nchini (NIDA), Rose Mdami.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Abdalla Lutavi, akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika zoezi la usajili vitambulisho vya Taifa, kulia ni Afisa Tawala wa Wilaya ya Tanga, Mashaka Makaku.


 Afisa Habari Mkuu Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa nchini(NIDA), Rose Mdami, akizungumza na waandishi wa habari leo namna ambavyo zoezi la usajili wa vitambulisho vya Taifa linavyoendelea na kusema kuwa hadi sasa hakuna kasoro ambazo zimejitokeza na hivyo kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi.

 Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Abdalla Lutavi, akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake, kuhusu wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la kujisajili Vitambulisho vya Taifa linaloendelea wilayani hapa.


AFRICAN SPORTS WAPITISHA KATIBA YAO,SASA WAPO KAMILI KWA USAJILI

May 12, 2015
WANACHAMA arobaini na tisa waliohudhuria mkutano wa klabu hiyo kati ya sabini na sita wa klabu ya African Sports juzi walipitisha katiba mpya wa klabu hiyo ambayo itawapa dira kuu ya kuelekea ushiriki wao katika Michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara .

Katiba hiyo inaendana na katiba nyengine ya vilabu vinavyoshiriki ligi kuu ikiwemo ile ya shirikisho la soka hapa nchini ambapo ilipitishwa na wanachama hao kwenye mkutano wa wanachama wa klabu hiyo ambao ulifanyika kwenye ukumbi wa Splended jijini Tanga.

Akizungumza mara baada ya kuipitisha katiba hiyo, Mwenyekiti wa Klabu ya African Sports, Hassani Shehe alisema kuwa wanamshukuru mungu kupitisha katiba hiyo ambayo ilikuwa ni muhimili mkubwa kwa maendeleo ya timu yao baada ya kupanda daraja ya Ligi kuu.

Hassani alisema kuwa mkutano huo ulikuwa na mambo muhimu mawili ambapo la kwanza lilikuwa ni kupitisha katiba hiyo ikiwemo kukutana na wanachama kwa ajili ya kutambuana.

Alisema kuwa baada ya kumalizika suala hilo muhimu kwao watajiandaa na taratibu wa uchaguzi mkuu wa viongozi ambao wataiongoza klabu hiyo na usajili kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi kuu hapa nchini.

Awali akizungumza katika mkutano huo,Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tanga(TRFA),Salim Omari aliwataka viongozi na wanachama wa klabu hiyo kuhakikisha wanashikamana ili kurudisha makali ya timu hiyo ya miaka ya nyuma.

      “Tunafahamu vizuri enzi za miaka ya nyuma timu hii ilipokuwa ikifanya mambo makubwa katika michuano ya Ligi kuu hivyo viongozi hakikisheni hili linajirudia msimu ujao lakini kikubwa kuweni na ushirikiano “Alisema Salim.

RC PEMBA ALITAKA SHIRIKA LA BANDARI ZANZIBAR KUFANYA UKARABATI BANDARI YA WETE.

May 12, 2015
Na Masanja Mabula,Pemba.
MKUU wa Mkoa wa kaskazini pemba Mhe Omar Khamis Othman amelitaka Shirika la Bandari Zanzibar kuharakisha ukarabati wa bandari ya wete ili kudhibiti ongezeko na bandari bubu katika Mkoa huo .

Amesema kuwa  ongezeka la Bandari bubu katika mkoa huo inasababishwa na  kutokuwepo kwa chombo cha uhakikisha cha usafiri kutoka Pemba -Tanga , hali ambayo inawafanya wananhi kutumia vyombo na bandari zisizo rasmi .

Kauli hiyo ameitoa huko ofisini kwake wakati akizungumza na ujembe kutoka Shirika la bandari zanzibar ukiongozwa na mkurugenzi wa shirika hilo Abdalla Juma Abdalla .

mkuu huyo wa mkoa pia ametumia fursa  kulitaka shirika la bandari zanzibar  kuandaa utaratibu mzuri wa uondokaji na uingiaji wa abira katika bandari ya wete ili kudhibiti upitishwaji wa madawa ya kulevya .

Naye mkurugenzi wa shirika la bandari zanzibar bw abdalla juma abdalla amesema kuwa shirika limepanga kuifanyia matengenezo bandari ya wete katika kipindi cha bajati ijayo .

Amesema kuwa kukamilika kwa matengenezo hayo yataondoa usumbufu wanaoupata abira wanaosafiri  kutoka Pemba  kwenda Tanga .

Hata hivyo mkurugenzi huyo amekiri kuwa hali ni ngumu kuweza kudhibiti bandari bubu kutokana na tatizo la ukosefu wachombo cha uhakikisha wanachotumia  abiria kusafiri na kusafirishia mazao .

Rais Kikwete aifariji familia ya Nyerere kufuatia kifo cha John Nyerere

Rais Kikwete aifariji familia ya Nyerere kufuatia kifo cha John Nyerere

May 12, 2015

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo leo asubuhi nyumbani kwa Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha mwanaye John Nyerere kilichotokea hivi karibuni.Aliyesimama pembeni ya Rais ni mdogo wa marehemu Makongoro Nyerere. mak2 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiifariji familia ya marehemu John Nyerere nyumbani kwao Msasani jijini Dar es Salaam leo asubuhi. mak3 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha mwanaye John Nyerere kilichotokea juzi .Mwili wa Marehemu John Nyerere rubani wa zamani wa ndege za kivita nchini aliyeshiriki kikamilifu vita vya Uganda kati ya mwaka 1978 na 1979, unatarajiwa kusafirishwa leo kwenda kijijini Butiama mkoani Mara kwa maziko.(picha na Freddy Maro) mak4 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha mwanaye John Nyerere kilichotokea juzi .Mwili wa Marehemu John Nyerere rubani wa zamani wa ndege za kivita nchini aliyeshiriki kikamilifu vita vya Uganda kati ya mwaka 1978 na 1979, unatarajiwa kusafirishwa leo kwenda kijijini Butiama mkoani Mara kwa maziko.(picha na Freddy Maro)
RAIS KIKWETE AHITIMISHA ZIARA RASMI YA ALGERIA, AREJEA NYUMBANI

RAIS KIKWETE AHITIMISHA ZIARA RASMI YA ALGERIA, AREJEA NYUMBANI

May 12, 2015

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipanda ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Houari Boumediene jijini Algiers Jumatatu May 11, 2015 baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo.
PICHA NA IKULU
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiaga wenyeji wake katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Houari Boumediene jijini Algiers Jumatatu May 11, 2015 baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo. kj3 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na Marubani na Wafanyakazi wa Shirika la ndege la Tassili la Algeria baada ya kuwsili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo May 12, 2015  baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku tatu nchini Algeria. kj4 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na viongozi mbalimbali katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo May 12, 2015  baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku tatu nchini Algeria. kj5 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Raymond Mushi alipowasili  kutoka Algeria katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo May 12, 2015  baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku tatu nchini Algeria. kj6 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na  Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es salam Suleiman Kova,  Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Raymond Mushi, Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sophia Mjema na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Paul Makonda  alipowasili  kutoka Algeria katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo May 12, 2015  baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku tatu nchini Algeria.
TOP 3 YA TUZO ZA WATU 2015 KUFANYIKA IJUMAA TAREHE 22/HYATT KEMPISK HOTEL SOMA HABARI KAMILI HAPA LIVE!!

TOP 3 YA TUZO ZA WATU 2015 KUFANYIKA IJUMAA TAREHE 22/HYATT KEMPISK HOTEL SOMA HABARI KAMILI HAPA LIVE!!

May 12, 2015
Tuzo za Watu 2015 zinatarajiwa kufanyika Ijumaa ya May 22 kwenye hoteli ya Hyatt Regency (The Kilimanjaro) jijini Dar es Salaam.  Tuzo za mwaka huu zinahusisha vipengele 13 vilivyopo kwenye muziki, filamu, redio, televisheni na blogs.

Washindi watapatikana kwa asilimia 100 ya kura za wananchi zinazoendelea katika hatua hii ambapo wamebaki washiriki watatu katika kila kipengele.

Kila mshindi atapokea tuzo na zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni moja.

Pamoja na utoaji wa tuzo hizo, hafla hiyo itasindikizwa na burudani moto moto kutoka kwa wasanii watakaotangazwa hapo baadaye. Hakuna kiingilio kwenye tuzo hizo bali itatolewa mialiko kwa baadhi ya watu kwenye tasnia ya burudani na zingine nchini. Pia mialiko 100 itatolewa  kwa wananchi waliopiga kura zaidi.

Haya ndio majina yaliyoingia kwenye fainali ya tuzo za watu:

Mtangazaji wa redio anayependwa 

D’Jaro Arungu - TBC FM - TZW1C
Maryam Kitosi – Times FM - TZW1D
Millard Ayo – Clouds FM - TZW1E


Kipindi cha redio kinachopendwa 

Amplifaya – Clouds FM - TZW2B
Hatua Tatu – Times FM - TZW2C 
Papaso – TBC FM - TZW2D

Mtangazaji wa runinga anayependwa

Abdallah ‘Dullah’ Ambua – EATV - TZW3A
Salama Jabir – EATV/Maisha Magic - TZW3B
Salim Kikeke - BBC Swahili - TZW3C

STARS KWENDA AFRIKA KUSINI KESHO

May 12, 2015

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kesho jumatano inatarajiwa kusafiri kuelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kushiriki michuano ya kombe la COSAFA.

Michuano ya COSAFA inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Mei 17 mpaka Mei 30, 2015 katika viwanja vya Olympia Park na Moruleng  jimbo la North West Province nchini Afrika Kusini ikishirikisha nchi za Kusini mwa Afrika huku Tanzania na Ghana zikiwa ni nchi waalikwa.

Taifa Stars itaondoka jijini Dar es salaam kesho majira ya saa 1 jioni, kwa usafiri wa shirika la ndege la Fasjet na kufika jijini Johanesburg saa 5 usiku.

Mara baada ya kupimwa afya jana na madaktari wachezaji Aishi Manula, Isihaka Hassan, Haroun Chanongo, Kelvin Friday na nahodha Nadir Haroub wamekutwa na majeruhi ambayo yamepelekea kutokuwepo katika kikosi kitakachosafiri kesho, watabakia nchini wakiendelea kufanya mazoezi chini ya ungalizi mpaka timu itakaporejea kutoka Afrika Kusini na kuungana kwa ajili ya maandalizi ya AFCON, huku Amri kiemba akipewa ruhusa kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia.

Msafara wa Taifa Stars utaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa TFF, Ephaphra Swai ukijumuisha wachezaji 20 na benchi la ufundi, timu inatarajiwa kufikia katika hoteli ya Sun City iliyopo pembeni kidogo ya jiji la Rusterburg.

Kesho siku ya Alhamis kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 7 mchana ni muda wa mapumziko, waandishi wa habari mnakaribishwa katika kambi ya timu ya Taifa iliyopo Tansoma Hotel kuweza kuongea na wachezaji, kocha mkuu na daktari wa timu kabla ya kuanza safari jioni.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Best Regards,
 
Baraka Kizuguto
MEDIA & COMMUNICATION OFFICER
A:I P.O.BOX 1574 Karume Memorial Stadium /Shaurimoyo/Uhuru Street I Dar es salaam I Tanzania 

DKT. SEIF RASHID AFUNGUA MKUTANO WA MADAKT DAR ES SALAAM JANA

May 12, 2015

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Ajali na Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI), Dk. Othman Kiloloma akizungumza na wandishi wa habari (pichani hawapo), katika mkutano wa nne wa mafunzo ya upasuaji wa ubongo , uti wa mgongo na mishipa ya fahamu Dar es Salaam leo. Mkutano huo ulifunguliwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Seif Rashid, unao endelea hadi  Mei 15-2015. (PICHA ZOTE  NA KHAMISI MUSSA)
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Tiba MOI,   Dk. Abednego Kinasha akitoa mada katika mkutano huo
 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk, Seif  Rashid (watatu kushoto),  akitetajambo na madaktari hao baada ya kufungua mkutano huo  jijini Dar es Salaam leo  unao endelea hadi Mei 15-2015 ,  (wa kwanza kulia) ni   Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Ajali na Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI), Dk. Othman Kiloloma, wakwanza  kushoto ni  Daktari Bingwa wa Taasisi hiyo,  Anthon Assey na anaye fatia ni Mkuu wa Idara ya upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu Dk.Hamisi Shabani
  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk, Seif  Rashid (kushoto) akisalimiana na  Mkurugenzi wa Fedha na Ugavi katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Ajali na Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Kevin Felix
  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk, Seif (kushoto)  Rashid akisalimiana na Profesa J. Kahamba
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk, Seif  Rashid (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi wa Utawala na Raslimali watu katika Taasisi ya Mifupa Moi
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk, Seif  Rashid (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi wa Uuguzi katika taasisi ya mifupa Moi Flora Kimaro baada ya kufungua  mkutano wa nne wa mafunzo ya upasuaji wa ubongo , uti wa mgongo na mishipa ya fahamu Dar es Salaam leo
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk, Seif  Rashid katika picha ya pamoja na maktari hao
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk, Seif  Rashid (watatu kulia) katika picha ya pamoja baada ya kufungua mkutano huo jijini Dar es Salaam leo
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk, Seif  Rashid (watatu kushoto) akiwa na madaktari, wakurugenzi na maprofesa kutoka New york katika chuo cha weill Cornell na New York Presbyterian Hospital
Madaktari wakiwa katika mkutano huo
Madaktari na baadhi ya wakuu wa vitengo wakisikiliza kwa umakini wakati mada mbalimbali zilikuwa zikitolewa
wakisikiliza kwa utulivu mkubwa madaktari hao

madaktari mbalimbali wakutoka sehemu tofauti wakiwa katika mkutano huo


 Profesa Philip stieg,  kutoka New york katika chuo cha weill Cornell na New York Presbyterian Hospital akiongea na waandishi wa habari (pichani hawapo) baada ya kufunguliwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk, Seif  Rashid
Madaktari wa magonjwa ya ubongo na uti wa mgongo mbele wakiwa na washiriki katika mkutano huo

     Salha Mohamed

SERIKALI imesema inaupungufu wa madaktari bingwa wa upasuaji wa mishipa ya fahamu na ubongo.

Yalibainishwa hayo Dar es Salaam leo, na Waziri wa Afya na ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid wakati wa mkutano wa madaktari bingwa wa mishipa ya fahamu na ubongo na uti wa mgongo waliotoka nchi za Marekani, Ujerumani, Hispania, Uturuki pamoja na Misri na wakishirikiana na madaktari mbalimbali wa Tanzania.

Alisema lengo la mkutano huo ni kuongeza taaluma na kubadilishana uzoefu miongoni mwa madaktari  hao bingwa katika mishipa ya fahamu, ubongo na uti wa mgongo kwenye upasuaji.

"Hili ni eneo muhimu sana, kwani magonjwa haya yanaongezeka sana ikiwa ni kutokana na kuongezeka kwa wagonjwa ya ajali na maradhi yanayopelekea kupata matatizo katika    mishipa hiyo,"  Dk Rashid.

Alisema mkutano huo utawawezesha kufanya kazi kwa umakini na upatikanaji wa vifaa vya kutolea huduma hiyo ili kuweza kuongeza uwezo mkubwa zaidi katika upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu kwa mafanikio makubwa zaidi na kuweka mwelekeo mzuri wa kazi hiyo kwa urahisi zaidi.

Aidha alisema changamoto ya madaktari bingwa ni kubwa zaidi kuliko uwepo wa madaktari hao ambapo wanahitajika zaidi katika taaluma hiyo.


"Juhudi za kutoa fursa kwa madaktari hao ni ndogo kwani bado linahitajio kubwa kwasababu ya mabadiliko ambapo kila siku ajali zimekuwa zikiongezeka," alisema huku akisema zaidi ya asilimia 25 ya wagonjwa ya fahamu na ubongo na uti wa mgongo yanatokana na ajali.

Aidha alisema jengo la Moi litazinduliwa kabla ya uchaguzi ambapo lipo kwenye hatua ya mwisho na kwamba vifaa vitafika baada ya muda mfupi na lipo kwenye hatua za mwisho.

"Jengo hilo jipya litazinduliwa kabla ya uchaguzi mkuu ambapo limekamilika kwa asilimia 90, na litakuwa na vitanda 240 na eneo la kuwezesha wataalamu kutoa huduma bila changamoto zozote.

KUNDI LA VIJANA MARAFIKI WA LOWASSA WAFIKA KILELE CHA MLIMA KILIMANJARO

May 12, 2015

Baadhi ya vijana ambao ni marafiki wa Lowassa wakiwa katika safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Kundi la marafiki wa Lowassa kutoka kana ya Kaskazini wakiwa katika kituo cha Kibo ,wakiwa katika maandalizi ya kuanza kwenda kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro.
Sehemu ya juu ya mlima Kilimanjaro ikiwa imefunikwa kwa theruji.
Kundi la Marafiki wa Lowassa wakiwa katika kituo cha Stella,kikiwa ni kituo cha mwisho kuelkea kilele cha Uhuru .
Mandhari mbalimbali zinayoonekana wakati wa kuupanda Mlima Kilimanjaro.
Safari ya siku tano kwa vijana hao ikahitimishwa katika kilele cha Uhuru Peak wakiongozwa na mratibu wa marafiki wa Lowassa Kanda ya Kaskazini Noel Nnko (mwenye koti jekundu)
Safari ya kurudi kiasi ilikuwa tatizo wakati mwingine baadhi yao walilazimika kupewa msaada kwenye kifaa maalumu cha kushushia wageni waliopata matatizo .

Na Dixon Busagaga wa 

Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.