UMOJA NA MSHIKAMANO NDIO SIRI YA MAFANIKIO BARA LA AFRIKA – NDUGAI

UMOJA NA MSHIKAMANO NDIO SIRI YA MAFANIKIO BARA LA AFRIKA – NDUGAI

May 03, 2016

Na Owen Mwandumbya, Midrand Afrika Kusini.

Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai amesema ili Bara la afrika liweze kuwa Bara lenye nguvu kiuchumi na sauti ya maamuzi duniani halina budi kujikita katika umoja na mshikamono.
Mhe. Ndugai aliyasema hayo alipokuwa akilihutubia Bunge la Afrika (Pan African Parliament) leo kuwasilisha Ujumbe wa Mshikamano kwa wabunge wa Bunge hilo wakati wa Ufunguzi wa rasmi wa Mkutano wa Pili wa Bunge hilo uliofanyika Mjini Midrand Afrika Kusini.
Akizungumzia changamoto zinazolikabli bara la Afrika Mhe. Nduagi alisema nchi nyingi barani Afrika zinakabiliwa na matatizo yanayolingana ambayo ni Vita vya wenyewe kwa wenyewe, ugaidi, umasikini na mengineyo ambayo yanahitaji suluhisho la Pamoja kuyakabili..
“ katika duniani ya sasa ni vyema tukakabiliana na changamoto zinazotukabili kwa pamoja. Matajiri hawawezi kuepuka athari za umasikini na ukosefu wa amani. Kinachotokea eneo moja kinaathiri maeneno mengi mathalani vita vya wenyewe kwa wenyewe Somalia imesababisha wakimbizi katika maeneo mengi duniani” alisema Ndugai
Akizungumzia nafasi ya wabunge katika kupiga vita changamoto zinazolikabili bara la Afrika, Mhe. Ndugai amesema wabunge wa Bunge la Afrika kama wawakilishi wa Manbunge ya Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika wanawajibu wa kutetea maslahi ya Bara la Afrika bila kujali itikadi za kisiasa, maeneo wanayotoka na mambo mengine yanayoweza kuligawa bara la Afrika.
“ Mkiwa Wabunge mnaowakilisha nchi zenu katika Bunge hili, nilazima mhakikishe Umoja wa Afrika unasimamia ipasavyo masalahi ya bara la Afrika ili kutimiza ndoto waliokuwa nayo waasisi wa umoja huu wa Afrika. Kwa mfano baba wa Taifa la Tanzania Mwalimu Julius kambarage Nyerere alisema lazima tukimbie wakati wengine wakitembea” aliongeza Ndugai
Mapema akitoa salamu za Bunge la Lesotho, Spika wa Bunge la Nchi hiyo Mhe. Nthloi Motsamai alisifu juhudi za Mwalimu Julius Nyerere pamoja na waasisi wengine wa bara hili katika kuimarisha umoja wa Afrika na kuwataka wabunge wa Bunge la afrika kuhakikisha mawazo ya viongozi hawa ya kulifanya bara la afrika kuwa moja yanatimia.
Katika hatua nyingine, wabunge wa Tanzania wanaowakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika walikula kiapo cha uaminifu kuwa wabunge wa Bunge hilo baada ya Bunge la Tanzania kuwachagua mapema mwezi Januari.
Wabunge hao ni pamoja na Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile, Mhe. Mboni Mhita, Mhe. David Silinde na Mhe. Asha Abdalah Juma. Mhe. Ndugai anatarajia kurejea nchini kesho jumatano ambapo Bunge la Afrika linaendelea na Vikao vyake hadi tarehe 13 Mei, 2016.
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akilihutubia Bunge la Afrika (Pan African Parliament) kuwasilisha Ujumbe wa Mshikamano kwa wabunge wa Bunge hilo wakati wa Ufunguzi wa rasmi wa Mkutano wa Pili wa Bunge hilo uliofanyika Mjini Midrand Afrika Kusini. Mhe. Ndugai alikuwa miongoni mwa viongozi mashuhuri 12 kutoka Barani Afrika walioalikwa kutoa ujumbe huo kwa wabunge wa Afrika.
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akilihutubia Bunge la Afrika (Pan African Parliament) kuwasilisha Ujumbe wa Mshikamano kwa wabunge wa Bunge hilo wakati wa Ufunguzi wa rasmi wa Mkutano wa Pili wa Bunge hilo uliofanyika Mjini Midrand Afrika Kusini. Mhe. Ndugai alikuwa miongoni mwa viongozi mashuhuri 12 kutoka Barani Afrika walioalikwa kutoa ujumbe huo kwa wabunge wa Afrika.
Spika wa Mhe. Job Ndugai akiwa na baadhi ya Maspika wenzie kutoka mabunge ya Nchi za Bara la Afrika kwenye Mkutano wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament) alikoalikwa kuwasilisha Ujumbe wa Mshikamano kwa wabunge wa Bunge hilo wakati wa Ufunguzi wa rasmi wa Mkutano wa Pili wa Bunge hilo uliofanyika Mjini Midrand Afrika Kusini. Mhe. Ndugai alikuwa miongoni mwa viongozi mashuhuri 12 kutoka Barani Afrika walioalikwa kutoa ujumbe huo kwa wabunge wa Afrika. Kulia kwake ni Spika wa Bunge la Seneta la Lesotho Mhe Seeiso Berenge Seeiso na kushoto ni senate kutoka Bunge la Afrika Mhe. Bennette hayatoe
Wabunge wa Bunge la Afrika wanaowakilisha Tanzania wakila kiapa cha uaminifu. Kutoka kushoto ni Mhe. Asha Abdalah Juma, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile, Mhe. David Silinde na Mhe. Mboni Mhita.

MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BIMA NCHINI (TIRA) YAKUTANA NA WADAU WAKE JIJINI MBEYA

May 03, 2016
Meneja wa Kanda Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini  (TIRA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Ndugu Hiraly Maskini akifungua Mkutano wa  wadau wa soko la Bima kutoka Mikoani ya Nyanda za Juu Kusini  (hawapo pichani) katika ukumbi wa Mikutano Mkapa jijini Mbeya Mei 3 -2016 mkutano ambao unalengo la kujadili na kutambua changamoto mbalimbali wanazo kutana nazo wadau hao katika kutekeleza majukumu yao.(Picha Emanuel Madafa,Jamiimojablogu-Mbeya) 

Wadau wa soko la  Bima Mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juuu Kusini,Mbeya,Iringa,Njombe ,Rukwa ,Songwe na Katavi  wakiwa katika umakini kufuatilia agenda mbalimbali katika mkutano huo ulioandaliwa na  Mamlaka ya usimamizi wa Bima Nchini Kanda ya  Nyanda za Juu Kusini  (TIRA).

Kaimu Meneja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC)Mkoa wa Mbeya Ndugu Victory Mleleu akichangia moja ya maada katika mkutano huo ulihusisha wadau wa soko la Bima Kanda ya Nyanda za Juu Kusini pamoja na Mamlaka ya usimamizi wa Bima (TIRA) semina ambayo imefanyika katika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya Mei 3 mwaka huu.

Mhasibu wa Kanda Mamlaka ya Usimamizi wa Bima  (TIRA)Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Ndugu Kurenje Mbura akiwasilisha moja ya maada katika mkutano wa wadau wa Soko la Bima ulioitishwa na Mamlaka hiyo ya (TIRA ) Mei 3 Mwaka huu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mkapa jijini Mbeya. 

Mmoja wa wadau wa soko la Bima Mkoani Mbeya  Ndugu Masterdy Luvanda akichangia maada katika mkutano wa wadau wa Soko la Bima  ulioitishwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA)  katika Ukumbi wa Mkapa jinini Mbeya Mei 3 mwaka huu, ukiwa na lengo la kujadili changamoto mbalimbali wanazo kutanana nazo wadau hao sanjali na kupeana uzoefu katika sekta hiyo.

Picha ya Pamoja Meza kuu na washiriki wa semina hiyo.

MUONEKANO WA HOTEL KALI YA TANGA CITY LOUNGE LEO

May 03, 2016

Meneja wa Ukumbi huo, Paskal Damas katikati akizungumza na waandishi wa habari kushoto ni mwandishi wa gazeti la Mwananchi Raisa Saidi na kulia ni mwandishi wa gazeti la Mtanzania Sussan Uhinga








RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIKI KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM MKOANI DODOMA

May 03, 2016

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiendesha Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma. Kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kushoto ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein wakifurahia jambo kabla ya kuanza kwa kikao cha cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma.


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipowasili mkoani Dodoma kwa ajili ya kikao hicho cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa.

MAMIA WAJITOKEZA KUMUAGA 'KAMANDA' GABRIEL MWAIBALE

May 03, 2016

 Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Gabriel Peter Mwaibale aliyefariki juzi nyumbani kwao Mabibo jijini Dar es Salaam ambapo mazishi yake yatafanyika leo Kijiji cha Mpuga Wilayani Rungwe mkoani Mbeya.
 Baba mgogo wa marehemu Kulwa Mwaibale (kulia), akitoa maelekezo kwa waombolezaji kabla ya kuanza safari ya kuusafisha mwili huo hadi Tukuyu Rungwe mkoani Mbeya kwa mazishi.
 Babu wa marehemu Mchungaji Ambakisye Mwaibale akitoa heshima za mwisho.
 Rafiki zake marehemu Gabriel wakiwa katika msiba huo.
 Michango mbalimbali ikipokelewa.
 Wakina mama wakiwa katika msiba huo.
 Dada zake Gabriel wakilia katika msiba huo.
 Shangazi wa marehemu Gabriel, Ambwene Anyitike (kulia), akitoa heshima za mwisho wakati wa kuuaga mwili huo.
 Mtoto wa kaka yake Gabriel, Helena Mathias (katikati), akilia kwa uchungu kwa kupotelewa na baba yake mdogo ambaye alikuwa ni kipenzi chake mkubwa.
 Uagaji ukiendelea.
 Rafiki zake Gabriel wakitoa heshima zao.
 Kaka wa marehemu akitoa heshima za mwisho.
 Ndugu jamaa na marafiki wakiwa kwenye msiba huo.
 Dada ya marehemu Elines Mwaibale (kushoto), akiwa na bibi wa marehemu wakati wa kuaga mwili huo.
 Shughuli ya uagaji ikiendelea.
 Dada wa marehemu Neema akiwa ameanguka chini baada ya kupoteza fahamu wakati wa kuaga mwili huo.
 Baba mdogo wa marehemu Kulwa Mwaibale na jirani yake na marehemu wakiweka vizuri mfuni wa jeneza baada ya shughuli ya kuaga mwili huo kukamilika.
 Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Gabriel tayari kwa safari ya kwenda mkoani Mbeya kwa mazishi yaliyofanyika leo kijiji cha Mpuga Lutengano Tukuyu mkoani Mbeya.
Gari likiwa tayari kwa safari hiyo.