TRA, KCMC ZATOSHANA NGUVU MICHUANO YA SHIMUTA TANGA

November 16, 2022


Mshambuliaji wa timu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kulia akiwani mpira dhidi ya timu ya KCMC wakati wa michuano ya Shimuta inayoendelea kutimua vumbi kwenye viwanja vya Mizani Jijini Tanga
Mshambuliaji wa timu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kulia akiwani mpira dhidi ya timu ya KCMC wakati wa michuano ya Shimuta inayoendelea kutimua vumbi kwenye viwanja vya Mizani Jijini Tanga
Mshambuliaji wa timu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kulia akiwani mpira dhidi ya timu ya KCMC wakati wa michuano ya Shimuta inayoendelea kutimua vumbi kwenye viwanja vya Mizani Jijini Tanga








NA Oscar Assenga, TANGA

TIMU za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mabingwa Watetezi kwa upande wa mpira wa Miguu na Hospitali ya Rufaa KCMC ya Kilimanjaro zimetoshana nguvu baada ya kufungana bao 1-1, katika michuano ya Shimuta inayoendelea Jijini Tanga.

Mchezo huo ambao ulifanyika kwenye viwanja vya Mizani Jijini Tanga ulikuwa na upinzani mkubwa kwa kila timu kutaka kupata matokeo mazuri jambo ambalo lilizidisha ugumu wa mchezo huo

Timu ya KCMC ndio walikuwa wa kwanza kupata bao la kupitia Yusuph Madili aliyepiga faulu ya kona iliyotinga moja kwa moja na hivyo kuamsha shangwe na hari kwa mashabiki wao.

Mpaka timu hizo zinakwenda mapumziko KCMC walikuwa mbele kwa bao 1-0 ambapo kipindi cha pili kilianza kwa kasi kutokana na kila timu kufanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji wake na kuingiza nguvu mpya.

Walionekana kujipanga na kujiimarisha katika kipindi hicho timu ya TRA ilianzisha mashambulizi mfululizo lango mwa wapinzani wao huku wakicheza pasi fupi fupi na ndefu .

Kutokana na aina hiyo ya mchezo ambao walikuwa wakicheza iliwapelekea kuweza kupata bao la kusawadhisha kupitia kwa Datram Benzema ambaye alitumia uzembe wa mabeki kupachika wavuni bao hilo na hivyo kuamsha shangwe uwanja mzima.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo Katibu wa timu ya TRA Kamna Shomari alisema kwamba wanamshukuru mwenyezi Mungu kwa kuwawezesha kupata Sare na wana mechi nyengine.

Alisema kwamba hivyo wana matumaini watarekebisha mapungufu na kufanya vizuri Michezo ijayo na kwamba wamepania kuhakikisha wanapata matokeo mazuri kwenye mechi yao


TPDC YAZIGARAGAZA BENJAMINI MKAPA HOSPITALI, TPHPA MICHUANO YA SHIMUTA TANGA.

November 16, 2022

 

Kikosi cha timu ya  Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wanaume 

Kikosi cha timu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wanawake 

Na Oscar Assenga, TANGA

TIMU ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ya kuvuta kamba kwa upande wa wanaume leo wameibuka kidedea kwenye mchezo wa kuvuta kamba baada ya kuwavuta timu ya Benjamini Mkapa Hospitali kwa seti 2-0.

Mchezo huo ambao ulikuwa wa aina yake ulifanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Popatlaly Jijini Tanga ambapo wachezaji wa timu ya kuvuta kamba ya TPDC walionekana kuwa makini jambo ambalo liliwawezesha kuibuka na ushindi huo

Baada ya timu hiyo ya wanaume kumaliza kuvuta kamba iliingia upande wa wanawake ambapo timu ya Shirika hilo nayo iliweza kuibuka kidedea baada ya kuwavuta wanawake wenzao wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viwatilifu (TPHPA) kwa seti 2-0.

Timu ya TPDC ya kuvuta kamba iliwakilishwa vema na wachezaji wake mahiri ambapo kwa upande wa wanaume iliongozwa na Nahodha Joram Ndalahwa,Nnocent Mvamba,Adam Sajilo na Joseph Majebele.

Kwa upande wa timu ya wanawake iliwakilishwa vema na Rehema Saidi,Robi Chambiri,Catherine Madinda na nahodha wao Joyce Kiheka .