WAZIRI MKUU MHE. MIZENGO PINDA ATEMBELEA BANDA LA HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA KATIKA MAADHIMISHO YA NANENANE NYANDA ZA JUU KUSINI JIJINI MBEYA LEO

August 02, 2014


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda akisalimiana na
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Adam Misana
alipotembelea banda la Halmashauri ya Wilaya hiyo leo tarehe 02/08/2014 katika
maonyesho ya wakulima Nanenane nyanda za juu kusini Jijini Mbeya ambapo
alipokelewa na viongozi waandamizi wa Serikali ya Mkoa wa Rukwa wakiongozwa na
Mkuu wa Mkoa huo Eng. Stella Manyanya (Pichani Kulia).
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda (aliyeshika boga
kushoto) akisikiliza maelezo ya kilimo bora cha maboga alipotembelea banda la
Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga leo tarehe 02/08/2014 katika maonyesho ya
wakulima Nanenane nyanda za juu kusini Jijini Mbeya. Kulia kwake ni Waziri
Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Merry Nagu na pichani kulia
ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda akipokea maelezo
kutoka kwa mjasiriamali kuhusu kilimo cha Uyoga alipotembelea banda la
Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga leo 02/08/2014 katika maonyesho ya wakulima
Nanenane nyanda za juu kusini Jijini Mbeya.  Wa pili kushoto ni mwanasiasa nguli nchini na
Mbunge wa zamani wa jimbo la Kwela Dkt. Chrissant Mzindakaya.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda wa pili kushoto
akiangalia mbegu ya uyoga alipotembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya
Sumbawanga leo tarehe 02/08/2014 katika maonyesho ya wakulima Nanenane nyanda
za juu kusini Jijini Mbeya. Wa kwanza kushoto ni mwanasiasa nguli nchini na
Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kwela Dkt. Chrissant Mzindakaya na wa pili kulia
ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya.
Kilimo cha uyoga ni rahisi kwani sio lazima uwe na shamba, kama unavyoonekana pichani.
Picha ya pamoja kati ya Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda, viongozi wa serikali mkoani
Rukwa na wajasiriamali wadogowadogo mara baada ya kutembelea banda la
Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga leo tarehe 02/08/2014 katika maonyesho ya
wakulima Nanenane nyanda za juu kusini Jijini Mbeya.

BASI LA HOOD LAUA WATANO ARUSHA

August 02, 2014

Ajali iliyohusisha basi la HOOD na daladala maeneo ya Usa River mkoani Arusha muda huu..
.Ambapo dereva wa dala dala kafariki hapo hapo 

Maonesho ya Nane Nane yafunguliwa rasmi leo mkoani Lindi

August 02, 2014

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa Maonesho ya kilimo ya nane nane kitaifa mwaka huu katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali wakati alipowasili katika Viwanja vya Ngongo yanapofanyika maonesho ya Kilimo ya nane nane kitaifa Mkoani Lindi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo katika banda la Benki kuu ya Tanzania BOT katika maonesho ya kilimo ya nane nane kitaifa Mkoani Lindi katika viwanja vya Ngongo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo katika banda la sekta ya Afya katika maonesho ya kilimo ya nane nane kitaifa yanayofaanyika Mkoani Lindi katika viwanja vya Ngongo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Dk.Geoffrey Mkamito Mtafiti wa Mazao ya Mizizi, katika banda la Bodi ya Korosho katika maonesho ya kilimo ya nane nane kitaifa yanayofaanyika Mkoani Lindi katika viwanja vya Ngongo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Meneja Biashara na Masoko Numwagile A.Mwaijumba wa Shirika la Nyumbu kuhusu mashine ya utengenezaji wa matofali ya udongo katika maonesho ya kilimo ya nane nane kitaifa yanayofaanyika Mkoani Lindi katika viwanja vya Ngongo.

MANISPAA YA KINONDONI YAFANYA MAKUBWA UTEKELEZAJI ILANI YA CCM JIMBO LA KAWE

August 02, 2014

*Yatekeleza agizo la Rais Kikwete*Ni la jimbo kuwa na hospitali kubwa

 NA BASHIR NKOROMO
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeshuhudia makubwa yaliyofanywa na Manispaa ya wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, katika utekelezaji wa Ilani ya CCM ndani ya jimbo la Kawe.

Miongoni mwa miradi ambayo chama kililazimika kumpongeza Meya wa Manispaa hiyo ya Kinondoni, Yussuf Mwenda, ni utekelezaji wa agizo la Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete ya ujenzi wa Hospitali kubwa katika jimbo la Kawe yenye hadhi kama zilivyo za Mwananyamala,
Amana na Temeke.
Katika uteekelezaji agizo hilo la Rais Kikwete ambayo haikuwemo katika ilani, tayari Manispaa ya Kinondoni imeshaanza ujenzi wa hospitali hiyo katika eneo la Mabwepande, kwa jengo la kupokea wagonjwa (OPD), linalotarajiwa kukamilika mwaka huu, ambapo imeelezwa hadi mwishogharama yake itakuwa sh. milioni 288 ambazo kati yake sh. milioni Sh.153 zimeshalipwa kwa mkandarasi.
Wakiwa katika ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa chini ya Ilani ya CCM ya mwaka 2010-2015 katika jimbo la Kawe, Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Kinondoni, waliokuwa kwenye ziara hiyo jana, walielezwa kwamba, baada ya kukamilika ujenzi wa jengo hilo la kupokea wagonjwa, utaanza ujenzi wa wodi ya kina mama.
“Ndugu wajumbe, wakati Rais Kikwete akiwa katika kampeni zake katika uchaguzi mkuu uliopita, aliagiza kwamba kila jimbo latika mkoa wa Dar es Salaam, lazima liwe na hospitali yenye hadhi kubwa. Sasa ukiangalia agizo hilo ni kama lilikuwa linatulenga sisi wa jimbo la Kawe, maana Jimbo la Kinondoni ipo ya Mwananyamala, Ilala ipo Amana na Temeke pia ipo, ndiyo sababu tumefanya kila jijitahada kuhakikisha sisi Manispaa tunajenga hospitali hii.”, alisema Mwenda.
Wajumbe hao wa Halmashauri Kuu ya CCM, wakiendelea na ziara hiyo, pia walishuhudia mradi mkubwa wa ujenzi wa Shule ya sekondari unaoendelea katika eneo la Mikocheni, unaotekelezwa kwa gharama ya sh. bilioni 1.5 kwenye awamu ya kwanza.
Mwenda alisema, kukamilika kwa shule hiyo kutasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa adha ambayo imekuwa ikiwapata wananchi wa jimbo hilo kwa watoto wao kwenda maeneo ya mbali wanapojiunga na shule ya sekondari baada ya mitihani ya darasa la saba.
Alisema, ujenzi wa shule hiyo ambao sasa upo kwenye hatua ya orofa ya kwanza, unatarajiwa kukamilika mapema na marajio ni kuwezesha watoto watakaomaliza darasa la saba mwaka huu, kuanza kidato cha kwanza kwenye shule hiyo.
Wajumbe hao pia walitembelea mradi wa ujenzi wa soko la kisasa katika eneo la Bunju B, ambalo ujenzi wake unafanyika ili kuwahamishia wafanyabishara ambao wamekuwa wakifanya shughuli zao pembezoni mwa barabara ya Bagamoyo katika eneo hilo la Bunju B na hivyo kuhatarisha maisha yao na pia kuharibu mandhari ya mji.
Ujenzi wa soko hilo umekamilika kwa asilimia 90, na taratibu za kuanza kuwahamishia hapo wafanyabiashara zinaendelea kufanywa na mamlaka zinazohusika.
Baadhi ya miradi mingine ambayo wajumbe hao waliikagua na kuonyesha kuwasisimua, ni ujenzi wa wodi na kina mama na nyumba ya mganga ambavyo vimekamilika, katika zahanati ya Ndumbwi
kwenye jimbo hilo la Kawe.
Pia alikagua na kuridhiwa na hatua iliyopigwa na Manispaa ya Kinondoni katika ujenzi wa barabara za Maandazi iliyopo Masasani, na barabara ya Jourunalism iliyopo eneo la Feza, Mikocheni.
HABARI KATIKA PICHA KUHUSU ZIARA HIYO
 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, wakiwa kwenye Jengo la mapokezi ya wagonjwa (OPD) ambalo linajengwa katika eneo la Mabwepande, likiwa ni sehemu ya Hospitali ya Jimbo la Kawe katika Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam, walipotembelea kiradi mbalimbali ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2010-2015 katika jimbo la Kawe.
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yussuf Mwenda, akizungumza na watumishi wa Manispaa hiyo yeye na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Kinondoni walipofika kwenye mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Jimbo la Kawe unaofanyika Mambwepande, jana.
 Mwenda (wapili kushoto) akikagua ujenzi wa jengo la kupokea wagonjwa (OPD) la hospitali ya Jimbo la Kawe inayojengwa Mabwepande, Dar es Salaam.
 Mwenda akiingia ndani ya chumba cha mapokezi cha jengo hilo la mapokezi ya wagonjwa (OPD) wakati wa ziara hiyo.
 Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Mohammed Cholage akiwaonyesha wenzake eneo aliloona kuwa ni kama kasoro kwenye ujenzi wa jengo la kupokea wagonjwa (OPD) kwenye hospitali hiyo.
 Mwenda akifanya majumuisho na wajumbe baada ya kutembelea jengo la kupokea wagonjwa (OPD) kwenye Hospitali ya jimbo la Kawe inayojengwa mabwepande.
UJENZI WODI YA KINA MAMA NA NYUMBA YA MGANGA ZAHANATI YA NDUMBWI
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yussuf Mwenda akiongozwa jana na Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Ndumbwi, Sophia Kasubi, kuingia kwenye jengo la wodi ya Kina mama ambalo ujenzi wake umekamilika kwa ajili ya zahanati hiyo.
 Mwenda akisaini kitabu cha mapokezi kwenye jengo hilo wodi ya Kina mama kwenye zahanati ya Ndumbwi baada ya kuingia yeye na wageni wenzake
 Mwenda akiongozana na Katibu wa CCM wilaya ya Kinondoni Athumani Sheshe baada ya kukagua nyumba ya mganga kwenye zahanati ya Ndumbwi.
 Mwenda akiagana na watumishi wa zahanati ya Ndumbwi
 Baadhi ya watumishi katika zahanati ya Ndumbwi

UJENZI SHULE YA SEKONDARI KATIKA ENEO LA MIKOCHENI
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda akiongoza msafara kukagua ujenzi wa shule ya sekondari ambayo inajengwa na Manispaa hiyo katika eneo la Mikocheni.
 Mwenda akishiriki ujenzi wa shule hiyo ya sekondari kwa kuchanganya mchanga na saruji wakati wa ziara hiyo.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Kinondoni Pili Chande akishiriki ujenzi Shule ya Sekondari inayojengwa Mikocheni, jana. Kushoto ni Mwenda akishuhudia na aliyesimama kulia ni Katibu wa Itikadi na uenezi Kata ya Kawe, Eddy Mlaponi
 Mwenda akizungumza na wajumbe kufanya majumuisho baada ya kukagua shule hiyo ya sekondari Mikocheni na kuridhika kwamba ni mradi mzuri unaopaswa kupigiwa mfano katika utekelezaji wa ilani ya CCM

UJENZI SOKO BUNJU ‘B’
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuf Mwenda akiongoza msafara kukagua ujenzi wa soko katika eneo la Bunju B jana.
 Mmoja wa wajumbe akilazimika kwenda kukagua hali ya choo kwa ajili ya soko hiyo ipoje kwa ajili ya matumizi ya binadamu?
UJENZI DARAJA MIKOCHENZI FEZA
 Wajumbe wakikagua daraja lililojengwa katika utekelezaji wa ilani ya CCM katika eneo la Mikochezi-FEZA.
Wajumbe wakiwa wameshuka kwenye basi kukagua ujenzi wa barabara ya Maandaazi eneo la Msasani ambayo pia imeboreshwa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya CCM. (Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog)

NOOIJ ATARAJIA MECHI YA WAZI DHIDI YA MSUMBIJI

August 02, 2014
NA BONIFACE WAMBURA,MAPUTO.
Kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij amesema anakiamini kikosi chake ambacho kesho (Agosti 3 mwaka huu) kinacheza mechi ya marudiano ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika dhidi ya Msumbiji (Mambas).

Mechi hiyo ndiyo itakayoamua ni timu ipi kati ya Tanzania na Msumbiji itakayoingia hatua ya makundi ya michuano ya Afrika kwa ajili ya kutafuta tiketi za Fainali itakayofanyika mwakani nchini Morocco.

Katika mechi ya kwanza iliyochezwa jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2. Timu itakayosonga mbele itaingia kwenye kundi lenye timu za Cape Verde, Niger na Zambia.

Akizungumza hapa Maputo, Nooij amesema anaamini kikosi chake kitacheza vizuri zaidi kuliko kilivyofanya jijini Dar es Salaam kwa vile hakitakuwa katika shinikizo la washabiki ambalo mara nyingi hufanya wachezaji wasijiamini.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imefikia katika hoteli ya Pestana Rovuma ikitokea Johannesburg, Afrika Kusini ambapo ilifanya maandalizi yake mwisho, na itafanya mazoezi leo (Agosti 2 mwaka huu) saa 9 alasiri Uwanja wa Taifa wa Zimpeto ambao ndiyo utakaotumika kwa mechi ya kesho.

Kikosi hicho cha timu ya Taifa leo imeandaliwa chakula cha jioni na Balozi wa Tanzania hapa Msumbiji, Shamim Nyanduga.

Wachezaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu nao wameungana na timu leo asubuhi hapa Maputo wakitokea Lubumbashi katika klabu yao ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Mechi itakayochezeshwa na waamuzi kutoka Uganda wakiongozwa na Dennis Batte itaanza saa 9 alasiri kwa saa za hapa ambapo nyumbani Tanzania itakuwa saa 10 jioni.

Wachezaji waliopo katika kiosi cha Taifa Stars hapa Maputo ni Aggrey Morris, Aishi Manula, Amri Kiemba, Deogratias Munishi, Erasto Nyoni, Haruna Chanongo, Himid Mao, John Bocco, Kelvin Yondani, Khamis Mcha, Mbwana Samata, Mwinyi Kazimoto, Mrisho Ngasa, Nadir Haroub, Oscar Joshua, Ramadhan Singano, Said Moradi, Shabani Nditi, Shomari Kapombe, Simon Msuva na Thomas Ulimwengu.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
MAPUTO

LIVE MUDA HUU: WAZIRI MKUU MH. PINDA AZINDUA RASMI MAONESHO YA NANE NANE MKOANI MBEYA, AKAGUA BAADHI YA MABANDA

August 02, 2014