MAADHIMISHO YA MIAKA 52 YA JWTZ, JKT MGULANI YATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE SHIDA KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM

August 29, 2016
 Meja Dora Kawawa wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa 831 KJ Mgulani (kushoto), akimkabidhi msaada wa vyakula, Ofisa Mfawidhi wa Makao ya Taifa ya Watoto wenye shida Kurasini, Beatrice Lawrance, Dar es Salaam leo jioni , ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), ambapo kilele chake kitakuwa Septemba Mosi mwaka huu.
 Maofisa wa Jeshi wa kikosi hicho wakifurahi na watoto wa kituo hicho baada ya kutoa msaada wao.
 Msaada ukitolewa.
 Hapa ni furaha pamoja na watoto hao.
 Watoto wakipata msaada huo.
 Watoto wakipokea msaada.
 Hapa ni furaha tupu kwa watoto kwa kupokea msaada kutoka kwa wazazi wao hao.
Picha ya pamoja na watoto hao na viongozi wao.

Na Dotto Mwaibale

JESHI la Kujenga Taifa Kikosi 831 Kj Mgulani limetoa msaada wa vyakula na sabuni kwa watoto waishio Makao ya Taifa ya Watoto Wenye Shida Kurasini jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa utoaji wa msaada huo kwa niaba ya mkuu wa kikosi hicho Dar es Salam , Meja Dora Kawawa alisema ni moja ya sehemu ya maadhimisho ya kusherehekea miaka 52 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

"Tumeamua kushiriki shughuli za kijamii kama kutoa msaada na kufanya usafi ikiwa ni kuadhimisha siku ya kuanzishwa kwa jeshi letu ambapo kilele chake kitakuwa Septemba mosi mwaka huu" alisema Kawawa.

Ofisa Mfawidhi wa Makao ya Taifa ya Watoto wenye shida Kurasini, Beatrice Lawrance alishuru JKT kwa msaada huo na kueleza ni muhimu sana kwa watoto hao na kuomba taasisi nyingine kuiga mfano huo ili kujenga taifa bora la kesho.

WAKAZI WA MULEBA WALIPOKEA KWA SHANGWE TAMASHA LA TIGO FIESTA USIKU WA JANA

August 29, 2016

Mkuu wa wilaya ya Muleba  Bw Richard Ruyango , akifungua rasmi tamasha la Tigo fiesta kwenye uwanja wa David Zihimbile wilayani humo usiku wa jana, Kulia ni Meneja wa Tigo kanda ya ziwa Edgar Mapande na kushoto mkurugenzi wa vipindi clouds Ruge Mutahaba na mwakilishi kutoka wilayani.

Msanii Christian Bella akipagawisha kwenye Tamasha la Tigo Fiesta wilaya Muleba usiku wa jana lililofanyika uwanja wa David Zihimbile.

Msanii Joh Makini akiwarusha mashabiki wa hip hop kwenye Tamasha la Tigo Fiesta wilaya Muleba usiku wa jana lililofanyika uwanja wa David Zihimbile.





Msanii Raymond akionyesha umahiri wake kwenye Tamasha la Tigo Fiesta wilaya Muleba usiku wa jana lililofanyika uwanja wa David Zihimbile.

Msanii Shilole akiwa na shabiki wake kwenye Tamasha la Tigo Fiesta wilaya Muleba usiku wa jana lililofanyika uwanja wa David Zihimbile.

Msanii chipukizi wa super nyota aliyebahatika kushiriki fiesta ya mwisho litalofanyika jijini Dar Es salaaam
Sehemu ya umati uliohudhuria tamasha la Tigo fiesta Muleba
photo Best Regards Krantz Mwantepele| Managing Director KONCEPT | Mikocheni B, House No 58. Opp Clouds Media. Dar es Salaam, Tanzania | M: + 255 624053989 / +255 712579102 E: Krantz.charles@koncept.co.tz Blog: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com
Vituo viwili vya Redio vyafungwa kwa muda.

Vituo viwili vya Redio vyafungwa kwa muda.

August 29, 2016
MAG1
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akitoa tamko la kufungia vituo viwili vya redio ambavyo ni Kituo cha Redio Five Arusha  na Magic  FM Dar es Salaam kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam, kutokana na  kukiuka Kanuni za Sheria ya Utangazaji ya mwaka 2005 kwa kurusha hewani vipindi vyenye maudhui ya uchozezi,na Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Uratibu wa Vyombo vya Habari Bw. Jamal  Zuberi wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.
MAG2
Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia tamko alilokuwa akitoa Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo  Mhe. Nape Moses Nnauye (hayupo pichani) la kufungiwa kwa Redio  Five  Arusha na Redio Magic FM Dar es Salaam leo Agosti 29,2016 Jijini Dar es Salaam.
………………………………………………………………….
Na Anitha Jonas – WHUSM
Dar es Salaam.
Serikali yafungia vituo viwili vya redio nchini kutokana na kurusha hewani taarifa za kichochezi zinazoweza kuchangia uvunjifu wa amani.
Tamko la kufungwa kwa vituo hivyo vya  redio limetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa akizungumza  na waandishi wa habari.
Aidha,Waziri Nape alivitaja vituo hivyo kuwa ni Kituo cha Redio Five cha Arusha na Kituo cha Redio Magic  FM Dar es Salaam na alisisitiza kuwa utekelezaji wa tamko hilo unaanza leo tarehe Agosti 29, 2016 mara baada ya kutangazwa.
“Uamuzi wa kuvifungia vituo hivyo umefikia baada ya kujiridhisha kuwa kipindi cha MATUKIO kilichorushwa tarehe 25 Agosti ,2016 muda wa 02:00 usiku hadi 03:00 usiku  na Kituo cha Utangazaji cha  Redio Five  Arusha na kipindi cha cha Morning  Magic katika kipengele cha KUPAKA RANGI kilichorushwa tarehe 17 Agosti, 2016 kati ya saa 01:00 asubuhi na saa 02:00 asubuhi vilikuwa na maudhui ya uchochezi unaoweza kuleta uvunjifu wa amani na hivyo kukiuka masharti ya kanuni ya 5 (a),(b),(c) na (d) pamoja na Kanuni ya Huduma za Utangazaji (Maudhui) za mwaka 2005”, alisema  Waziri Nnauye.
Waziri huyo mwenye dhamana na vyombo vya habari nchini alisema vituo hivyo vimefungiwa kwa muda usiojulikana na ameelekeza  Kamati ya Maudhui kuviita vyombo hivyo na  kuwasikiliza kwa kina zaidi na kumshauri hatua zaidi za kuchukua kwa mujibu wa Kanuni za Utangazaji za mwaka 2005.
Pamoja na hayo Waziri Nape alivitahadharisha  vyombo mbalimbali  vya habari ,kutoshawishika kuvunja Sheria na Kanuni  zinazoongoza tasnia ya Habari ili kulinda heshima ya tasnia ya habari  na kuhakikisha nchi inabaki na Amani.
Hata hivyo  Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ya mwaka 2003  Kifungu cha 28 (1) kimempa Mamlaka Waziri wa mwenye dhamana na masuala ya Habari kufungia vyombo vya habari vinavyoweza kurusha hewani habari za uchochezi.
MHE. KAIRUKI AWATA WATUMISHI WA UMMA NCHINI KUJIJENGEA UWEZO KATIKA MAENEO YATAKAYO HARAKISHA MAENDELEO

MHE. KAIRUKI AWATA WATUMISHI WA UMMA NCHINI KUJIJENGEA UWEZO KATIKA MAENEO YATAKAYO HARAKISHA MAENDELEO

August 29, 2016
SONY DSC
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akitoa ufafanuzi wakati wa kipindi cha TUNATEKELEZA kilichorushwa na Runinga ya Taifa (TBC-1). Kushoto ni muongozaji kipindi hicho Bi. Eshe Muhidin.
SONY DSC
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akisisitiza jambo katika  kipindi cha TUNATEKELEZA kilichorushwa na Runinga ya Taifa (TBC-1). Mhe. Kairuki aliainisha kuwa wale wanaotarajia kuomba ajira Serikalini wawe na subira wakati zoezi la uhakiki wa taarifa za kiutumishi likikamilishwa. Kushoto ni muongozaji wa kipindi hicho  Bi. Eshe Muhidin waTBC.
SONY DSC
Muongozaji wa kipindi cha TUNATEKELEZA Bi. Eshe Muhidin (kushoto) akiuliza swali kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) wakati wa kipindi cha TUNATEKELEZA kilichorushwa na Runinga ya Taifa (TBC-1). Miongoni mwa aliyosema Mhe. Kairuki ni wito kwa Watumishi wa Umma kujiendeleza katika maeneo yenye tija kwa Taifa ili kufikia malengo ya nchi.
SONY DSC
TUMEKAMILISHA: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Muongozaji wa kipindi cha TUNATEKELEZA Bi. Eshe Muhidin (kushoto) baada ya kukamilisha kurusha kipindi mmbashara (live) katika studio za Runinga ya Taifa TBC-1.

Wananchi wa Kanda ya Ziwa zaidi ya 750 wapata mafunzo Kilimo Biashara jijini Mwanza.

August 29, 2016

Mwakilishi Msaidizi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon Manyama akitoa salamu kutoka UNDP kwa washiriki wa kongamano hilo (hawapo pichani).

Mkurugenzi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akizungumzia malengo ya Kongamano la Kilimo Biashara kabla ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (katikati) kufungua rasmi.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akitoa hotuba ya kufungua Kongamano la Kilimo Biashara kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa lililofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Rock City Mall jijini Mwanza.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Dk. Charles Mahika akielezea mikakati iliyowekwa na wizara ya kuhakikisha sekta ya kilimo, uvuvi na mifugo inafanikiwa.
Mwezeshaji ambaye pia ni Rais wa vijana wajasiriamali na wataalamu wa miradi ya maendeleo mkoa wa Singida, Philemon Kiemi akitoa mafunzo ya ufugaji kuku wa kisasa kwa washiriki wa Kongamano la Kilimo Biashara lililofanyika mwishoni mwa juma jijini Mwanza katika ukumbi wa Rock City Mall.
Mratibu wa Kongamano kutoka ESRF, Abdallah Hassan akizungumza jambo kwenye kongamano hilo.
 Mwezeshaji Bi. Kalega akitoa mafunzo ya ufugaji Kuku na matumizi ya Azolla kwa washiriki wa Kongamano la Kilimo Biashara lililofanyika mwishoni mwa juma jijini Mwanza katika ukumbi wa Rock City Mall.
Baadi ya wakazi wa Kanda ya Ziwa akiwemo mke wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bi. Mongella waliohudhuria Kongamano la Kilimo Biashara lililofanyika katika ukumbi wa Rock City Mall jijini Mwanza.

Na Mwandishi wetu
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, limesema litaendela kuinua fursa za kiuchumi zinazopatikana hapa nchini kwa kutumia teknolojia za kisasa zinazoendelea kuibuliwa.

Kauli hiyo imetolewa na Programme Specilist- Inclusive Growth UNDP Tanzania, Ernest Salla wakati wa Kongamano la Kilimo Biashara kanda ya ziwa lilofanyika katika ukumbi wa Rocky City Mall Agosti 27 mwaka huu Jijini Mwanza.

Kongamano hilo lililoandaliwa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii  (ESRF) kwa kushirikiana na UNDP/UNEP lililolenga kuzitambulisha fursa katika kilimo biashara, lilihudhuriwa na wananchi mbalimbali zaidi ya 750 kutoka mikoa ya Kagera, Geita, Mara na Mwanza wenyewe.
Katika kongamano hilo Salla alisema kilimo kina fursa nyingi hivyo watanzania hawana budi kuzitumia fursa hizo kwa kuwakumbatia wataalamu ili kiwe mkombozi wa maisha yao.

Akizungumza katika Kongamano hilo la siku moja, Mkurugenzi wa ESRF Dk Tausi Kida alisema licha ya uchumi wa taifa kutegemea kwa kiasi kikubwa kilimo, lakini kilimo hapa nchini bado kipo nyuma  hivyo kuchangia kiasi kidogo katika kumuendeleza mkulima.
“Kwa kutambua upungufu huu, ESRF ikishirkiana na UNDP/UNEP imekuwa ikifanya tafiti mbalimbali ili kusaidia wananchi na taifa kwa ujumla kujikwamua katika vizingiti mbalimbali vya maendeleo ukiwemo umasikini wa kipato,” alisema Dk Kida

Alisema kukua kwa teknolojia duniani, kumeongeza fursa nyigi za kimaendeleo ikiwamo kilimo, kwani wakulima wengi hivi sasa hawategemei mvua na hutumia eneo dogo kwa ajili ya kilimo.

Katika warsha hiyo zilitolewa mada mbalimbali; pamoja na kilimo cha Foda (Hydroponic fodder), kilimo cha mbogamboga (Hydroponic and Aquaponic Vegetables), shamba kitalu (Green house), Azolla na  ufugaji wa samaki na nyuki kutoka kwa wakufunzi mbalimbali waliotoa ufafanuzi kuhusu fursa mpya za kilimo biashara.

Alisema kilimo cha kisasa au “smart farming” ambacho hakihitaji maeneo makubwa kinaweza kufanyika katika maeneo ya mjini tofauti na izaniwavyo kuwa kilimo lazima kiwe vijijini.

Alisema ESRF imeshiriki katika utekelezaji wa miradi ya majaribio inayotegemea teknolojia ya kisasa katika wilaya  za Bunda, Bukoba vijijini, Sengerema, Nyasa, Ikungi na Ileje kupitia miradi ya PEI na CDRBM kwa kipindi cha miaka mitatu.
Pamoja na mambo mengine, alisema matokeo ya miradi hiyo ya majaribio yamethibitisha fursa katika kilimo biashara yanayoweza kuwasadia wananchi katika kujikwamua na ndio miongoni mwa sababu ya kuandaa warsha hiyo.

Akifungua kongamno hilo ambaye alikuwa mgeni rasmi, Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella alisema kilimo pekee ndicho chenye fursa pekee rahisi kuliko sekta nyingine duniani kote.

Mongela aliipongeza ESRF, UNDP, na wadau wengine wa maendeleo, kwa  tafiti hizo na kwamba hatua hiyo itasaidia kuinua uchumi wa watanzania na taifa kwa ujumla.

 Licha ya Mongella kupongeza hatua hizo, lakini alizitaka taasisi mbalimbali kupitia wataalamu wake kuonyesha gharama halisi za kutekeleza miradi hiyo.

“Hizi tekonolojia ni rahisi, watu wakianza nazo kidogokidogo baadaye watapanda na kufika juu, tatizo la wataalamu wanasema gharama ni kubwa za teknolojia, hivyo kuwaogopesha watu,” alisema Mongella

Amoni Manyama kutoka UNDP, alisema kuzingatia maelekezo ya wataaalamu ndio njia pekee ya kufanikisha katika kubuni fursa za kilimo na biashara.

Mwakilishi kutoka Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Dk Charles Mahika alisema wizara yake ikishirikiana nan chi zinazozunguka Ziwa Victoria wanaandaa mwongozo wa kuanzisha ufugaji wa samaki katika vizimba na kwamba mwongozo huo unatarajiwa kukamilishwa jijini Mwanza hivi karibuni.

Katika kongamano hilo wapo baadhi ya wananchi waliotoa shuhuda mbalimbali walionza kunufaika na fursa za kilimo biashara chini ya ufadhili wa UNDP ikishirikiana na ESRF.
KIPAO AMBADILI MUNISHI TAIFA STARS

KIPAO AMBADILI MUNISHI TAIFA STARS

August 29, 2016
Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa, amefanya mabadiliko kwenye kikosi kinachotarajiwa kusafiri Jumatano Agosti 31, 2016 kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017) dhidi ya timu ya taifa ya nchi hiyo, Super Eagles.

Mabadiliko yaliyofanyika ni kwa kumchukua Kipa kinda wa JKT Ruvu, Said Kipao kuchukua nafasi ya Deogratius Munishi ambaye amefiwa na baba yake mzazi katika kifo kilichotokea jijini Dar es Salaam jana Agosti 28, 2016.
Licha ya mchezo huo wa Septemba 3, 2016 kuwa sehemu ya mchuano wa kuwania nafasi ya kucheza fainali hizo za AFCON 2017 huko Gabon, lakini utakuwa ni wa kukamilisha ratiba baada ya Misri kufuzu kutoka kundi G ambalo mbali ya Nigeria na Tanzania, pia ilikuwako Chad ambayo iliyojitoa katikati ya mashindano.
Wachezaji wanaounda kikosi hicho kwa sasa na kuanza kuingia kambini Hoteli ya Urban Rose jijini Dar es Salaam ni:
Makipa-
Said Kipao – JKT Ruvu
Aishi Manula – Azam FC

Mabeki
Kelvin Yondani - Young Africans
Vicent Andrew - Young Africans
Mwinyi Haji - Young Africans
Mohamed Hussein – Simba SC
Shomari Kapombe - Azam FC
David Mwantika - Azam FC

Viungo
Himid Mao - Azam FC
Shiza Kichuya – Simba SC
Ibrahim Jeba – Mtibwa Sugar
Jonas Mkude – Simba SC
Muzamiru Yassin – Simba SC
Juma Mahadhi - Young Africans
Farid Mussa Tenerif ya Hispania

Washambuliaji
Simon Msuva - Young Africans
Jamal Mnyate – Simba SC
Ibrahim Ajib – Simba SC
John Bocco - Azam FC

Mbwana Samatta - CK Genk ya Ubelgiji

WAZIRI MKUU, MAJALIWA AKIWA KWENYE ZIARA NAIROBI.

August 29, 2016

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Rais na Ofisa mtendaji Mkuu wa kampuni ya Sumitomo Corporation ya Japan, Bw. Kunihuru Nakamura  katika Mkutano wa TICAD 6 uliofanyika Nairobi Kenya, Agosti 28, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais na Ofisa mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sumimoto Corporation ya Japan katika mkutano wa TICAD 6 uliofanyika jijini Nairobi Agosti 28,2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Rais na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Sumimoto ya Japan, Bw. Kanihuru Nakamura  (kushoto kwake) baada ya mazungumzo yao jijini Nairobi Agosti 28, 2016. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Profesa James Mdoe na Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt.Adelhelm Meru.  Wanne kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Japan, Mathias Chikawe.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia  Masuala ya Wakimbizi, Fillipo Grand kabla ya mazungumzo yao jijini Nairobi, Agosti  28, 2016. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa TANTRADE, Bw. Edwin Rutageruka (kushoto) wakati alipotembelea banda la Tanzania katika maonyesho yaliyokwenda sambamba na mkutano wa TICAD 6 jijini Nairobi Agosti 28, 2016. 
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
MCHEZO WA LIGI KUU YOUNG AFRICANS V JKT RUVU

MCHEZO WA LIGI KUU YOUNG AFRICANS V JKT RUVU

August 29, 2016
Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imethibitisha kuwa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Young Africans ya Dar es Salaam na JKT Ruvu ya Pwani, ulipangwa kufanyika Jumatano Agosti 31, 2016 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam imeahirishwa mpaka itakapopangiwa tarehe nyingine.

Mechi hiyo imeondolewa kutokana na timu ya Young Africans kuwa na wachezaji wengi kwenye kikosi cha timu ya Taifa (Taifa Stars) kinachosafiri Agosti 31, 2016 asubuhi kwenda Lagos, Nigeria kwa ajili ya mechi ya mchujo ya michuano ya Kombe la Afrika (AFCON Qualifiers) itakayochezwa Septemba 3, 2016.
Mabadiliko hayo hayatavuruga ratiba ya mechi zinazofuata za Ligi Kuu ya Vodacom kwa timu husika.
Tayari wahusika wakiwamo Young Africans na JKT Ruvu SC, wamejulishwa.
RAIS MALINZI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA MUNISHI

RAIS MALINZI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA MUNISHI

August 29, 2016
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za rambirambi Kipa wa Young Africans na timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Deogratius Munishi kutokana na kifo cha Baba yake mzazi, Mzee Boniventur Munishi kilichotokea jana Agosti 28, 2016.

Rais Malinzi amepokea taarifa za kifo cha Mzee Boniventur Munishi mara baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) Young Africans na African Lyon uliofanyika jana Agosti 28, 2016 ambako Deogratius aliongoza timu yake Young Africans kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 bila kufahamu kuwa amepoteza baba.
“Ni ujasiri wa aina yake aliokuwa nao Kipa Munishi kwenye mchezo wa Ligi Kuu bila kuonyesha tofauti,” amesema Malinzi ambaye katika zake za rambirambi kwenda kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki amewataka kuwa na moyo wa subira wakati huu mgumu wa msiba wa mpendwa wao.
Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya marehemu Mzee Boniventur Munishi mahala pema peponi.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe.
MATUKIO MKUTANO WA WAFANYABIASHARA KIGOMA NA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO

MATUKIO MKUTANO WA WAFANYABIASHARA KIGOMA NA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO

August 29, 2016



Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto) akimsikiliza kwa makini Bi. Rehema Kabuye (katikati) aliyekua akilia kwa uchungu, akimsihi Waziri huyo wa Fedha na Mipango, amsaidie ili mume wake ambaye ni Nahodha wa meli ya MV Liemba pamoja na wafanyakazi wengine wa Mamlaka ya Huduma za meli mkoani Kigoma, walipwe mishahara yao ya miezi nane ili kuwaondolea adha ya maisha inayowakabili wao na familia zao
Bi. Rehema Kabuye, (Katikati) ambaye ni mke wa Nahodha wa Meli ya Mv Liemba, inayotoa huduma zake Ziwa Tanganyika, akimwonesha Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), picha za mtoto wake ambaye ana matatizo ya kiafya, akimsihi Waziri huyo amsaidie yeye pamoja na wenzake ili waume zao walipwe mishahara yao ya miezi 8 wanayomdai mwajiri wao, Mamlaka ya Huduma za Meli mkoani Kigoma.
Katibu wa Waziri wa Fedha na Mipango, Edwin Makamba (Kulia), akichukua maelezo ya kina kutoka kwa Bi. Rehema Kabuye, Mkazi wa Kigoma, ambaye amemwomba Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), aingilie kati sakata la waume zao wanaofanya kazi kwenye mamlaka ya huduma za meli mkoani Kigoma, ambao hawajalipwa mishahara yao kwa muda mrefu.
Baadhi ya wafanyabiasha wa Kigoma Mjini, wakimsikiliza kwa makini waziri wa fedha na Mipango, Mhe. Dkt Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani), wakati wa mkutano na Waziri huyo kuhusu masuala mbalimbali ya biashara na ulipaji kodi, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.
Baadhi ya wafanyabiasha wa Kigoma Mjini, wakimsikiliza kwa makini waziri wa fedha na Mipango, Mhe. Dkt Philip Mpango (Mb), wakati wa mkutano na Waziri huyo kuhusu masuala mbalimbali ya biashara na ulipaji kodi, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.

Baadhi ya maofisa wa Wizara ya Fedha na Mipango, wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), wakati wa mkutano wake na wafanyabiashara wa Kigoma Mjini, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), aliyesimama kushoto, akiwahutubia wafanyabiasha wa Kigoma Mjini, kuhusu masuala mbalimbali ya biashara na ulipaji kodi, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.
Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara mkoa wa Kigoma Bw. Raymond Ndabiyegetse (katikati) akichangia hoja katika kikao na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (hayupo pichani) ambaye alipongeza juhudi zinazofanya na Serikali katika kutengeneza mazingira mazuri ya biashara zao.
Mkurugenzi wa kampuni ya Aifola ya Mjini Kigoma, Bw. Zubery Mabie, akiongea kwa hisia kali akishutumu TRA na maafisa wengine wa serikali katika kituo kidogo cha Forodha cha Manyovu kilichoko mpakani mwa Tanzania na Burundi, kujihusisha na rushwa kwa kupitisha maroli yakiwa na mizigo, ikiwemo chokaa anayozalisha, bila kulipia kodi. Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), ameahidi kulifanyiakazi suala hilo.
Mmoja wa wafanyabiashara wa Mjini Kigoma akichangia hoja katika mkutano ulioitishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), kuhimiza ulipaji kodi, matumizi adili ya fedha za umma, matumizi ya Mashine za Kieletroniki na utoaji wa risiti, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.

Askofu Mstaafu wa Kanisa la Anglican, Dkt. Gerard Mpango, akitoa mchango wake wa mawazo ambapo ameitaka serikali kutoa elimu ya kutosha ya biashara na ujasiriamali kwa wafanyabiashara nchini ili waweze kutumia fursa zilizopo katika soko la Afrika Mashariki, kukuza mitaji na biashara zao, wakati wa mkutano wa wafanyabiashara na Waziri wa fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), hayupo pichani, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma

Kamisha Msaidizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, anayeshughulikia masuala ya kodi, Bw. Shogholo Msangi akifafanua kuhusu kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa wafanyabiashara wa Kigoma Mjini wakati wa mkutano na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (mb).
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dokta Philip Mpango (Mb), akizungumza na wafanyabiashara wa Kigoma Mjini, kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo umuhimu wa kulipa kodi na matumizi ya mashine za kieletroniki pamoja na kuwasisitizia kutoa risiti kwa wateja wao. kushoto kwake ni Kamishna Msaidizi anayeshughulikia masuala ya kodi, Wizara ya Fedha na Mipango, Shogholo Msangi, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akionesha rundo la makaratasi yaliyoandikwa hoja na kero mbalimbali za wafanyabiashara wa mjini Kigoma, wakati wa mkutano kati yake na wafanyabiashara hao, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Askofu Dkt. Gerard Mpango, baada ya kumalizika kwa mkutano wake na wafanyabiashara wa Mkoa wa Mjini Kigoma, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto) akifurahia jambo pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Kabwe, wakati wakitoka nje ya ukumbi wa mikutano wa NSSF, ulipofanyika mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango na wafanyabiashara wa mjini Kigoma.


Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Kabwe (kushoto), akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waziri wa Fedha na Mipango,Dkt. Philip Mpango (Mb), baada ya kumalizika kwa mkutano kati yake na wafanyabiashara wa mjini Kigoma, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.




Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (kushoto) akipeana mkono na Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zitto Kabwe, mara baada ya kumalizika kwa mkutano kati ya Waziri huyo na wafanyabiashara wa Mkoa wa Kigoma uliofanyika katika ukumbi wa NSSF, mjini Kigoma.