MGODI WA BULYAHULU WAIPATIA MSALALA ZAIDI YA MILIONI 700 KWA AJILI YA USHURU WA HUDUMA

February 14, 2016
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew akikabidhi hundi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Patrick Karangwa,ikishuhudiwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama Vita Kawawa(katikati)
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kahama wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembelea mgodi wa Bulyanhulu
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Vita Kawawa akizungumza wakati wa ziara yake katika mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu ambapo amesisitiza kuwa kodi ya ushuru wa huduma iliyotolewa na Mgodi wa Bulyanhulu itumike vizuri kujenga miundombinu ambayo wananchi wataiona kwa macho
Afisa Maendeleo na Mahusiano wa mgodi wa Bulyahulu ,Sara Teri akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Kahama Vita Kawawa,kushoto kwake ni Mshauri wa Mahusiano ya Kampuni ya Acacia na Serikali , Alex Lugendo.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Vita Kawawa (Kushoto) akielekea katika eneo la mgodi wa chini ya ardhi Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya kahama Vita Kawawa na ujumbe wake pamoja na mshauri wa mahusiano ya kampuni na serikali wa Acacia aliyesimama katikati mwenye shati ya bluu  Alex Lugendo wakiwa katika picha ya pamoja.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Vita Kawawa Akiwa chini ya archi kilomita moja kutoka uso wa dunia akiwapongeza wafanyakazi wazawa katika mgodi wa Bulyanhulu kwa kufanya kazi ambazo zamani watanzania walikuwa hawawezi, kazi ya kufanya kazi kwa mitambo ya kisasa ya inayojulikana kama Jumbo na mashine zingine za teknolojia ya kisasa zinazotumika katika kuchimba dhahabu kwenye mgodi mkubwa wa dhahabu nchini Bulyanhulu.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Vita Kawawa Akiwa anatoka kwenye lifti kutokea chini ya ardhi baada ya kutembelea mgodi wa dhahabu chini ya ardhi.

Kaimu Meneja wa Uchimbaji katika Mgodi wa Bulyanhulu Salvatory Tesha
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Bw.Graham Crew akifafanua jambo kwa mkuu wa Wilaya ya Kahama Vita Kawawa.
Meneja wa Ufanisi wa Kampuni katika Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu Elias Kasitila akimuonyesha ramani ya uchimbaji mkuu wa Wilaya ya Kahama na ujumbe wake

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Vita Kawawa amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala kuwa fedha zitumike vizuri katika miradi inayoonekana. 

“sitaki masuala ya kusema unajua pesa tuliitumia katika kuweka kifusi barabarani na sasa mvua imekiosha, hapana, hilo litakuwa ni jipu linatakiwa kutumbuliwa, fedha hizi zitumike kujenga miradi inayoonekana kama vila vyumba vya madarasa, zahanati nakadhalika.”
SIKU YA WAPENDANAO

SIKU YA WAPENDANAO

February 14, 2016
Na Mwandishi wetu Washington 
Kila ifikapo tarehe 14 Februari nchini Marekani na sehemu nyengine Duniani husherehekewa Siku Ya Wapendanao "Valentine's Day", au kama ijulikanavyo kwa jina jengine "Siku Ya Mtakatifu Valentine" (Saint Valentine's Day). Katika miaka ya hivi karibuni siku hii pia imeanza kusherehekewa katika maeneo ya Afrika Mashariki. Labda shukrani ziende kwa enzi za utandawazi. Lakini je Siku Kuu hii ilianzia lini?
Asili yake
Hakuna chanzo cha uhakika kuhusu asili na chimbuko la Siku ya Wapendanao. Hata hivyo inaaminika kuwa asili yake inarejea katika enzi za Himaya ya Warumi, na baadaye Kanisa Katoliki kuingiza katika Ukristo.
Kuna watu watatu katika historia ya Kanisa Katoliki ambao wanajulikana kama Mtakatifu Valentine au Valentinus, na wote inasadikiwa walikufa kama mashahidi kwa mujibu wa itikadi za Kikatoliki, na kwa hivyo Kanisa likaamua kuiadhimisha siku waliyonyongwa kama kuwaenzi watumishi hao.
Kuna nganu inayodai kuwa Valentine alikuwa ni Mchungaji aliyehudumu Roma katika karne ya tatu. Wakati huo, Mfalme Claudius Wa Tatu, alipitisha amri ya kupiga marufuku ndoa kwa vijana wa Kiume kwa vile alihisi kuwa wanaume wasio na wake au familia walikuwa askari bora zaidi kuliko waliokuwa kwenye ndoa.
Mchungaji Valentine hakukubaliana na amri hiyo ya Mfalme na akawa naendelea kufungisha watu ndoa kwa njia za siri. Mfalme Claudius alipogundua mpango huo, aliamuru Valentine anyongwe.
Simulizi nyengine zinadai kuwa Valentine huenda alinyongwa kwa kosa la kuwasaidia Wakristo kutoroka katika magereza ya Warumi ambako walikuwa wakiteswa vibaya.
Inadaiwa kuwa Valentine ndiye aliyetuma maamkizi ya mwanzo ya mapenzi (valentine) kumpelekea msichana aliyempenda ambaye alikuwa akimtembelea wakti akiwa gerezani.
Inadaiwa kuwa kabla ya kifo chake, aliandika barua na kuisaini "Kutoka kwa wako Valentine". Maneno hayo bado yanaendelea kutumika hadi leo katika kadi za maamkizi ya siku ya Wapendanao.
WAZIRI UMMY MWALIMU ATEMBELEA MUHIMBILI KUKAGUA UTEKELEZAJI WA AGIZO LA RAIS MAGUFULI

WAZIRI UMMY MWALIMU ATEMBELEA MUHIMBILI KUKAGUA UTEKELEZAJI WA AGIZO LA RAIS MAGUFULI

February 14, 2016
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametembelea hospitali ya Taifa Muhimbili kukagua utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli la kuwataka watumishi wa wizara hiyo waliokuwa wakilitumia jengo la Kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto kuhamisha ofisi zao na kuliacha kwa ajili ya matumizi ya wodi ya wazazi.
Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo katika hospitali hiyo, Waziri Ummy amesema kuwa mpaka kufikia kesho tayari jengo hilo litakuwa limeanza kutumika kwa kuwa watafanya kazi ya kuhamisha makabrasha ya watumishi hao usiku kucha kuhakikisha agizo la Rais John Magufuli linatekelezwa mara moja.
FSA_6533

Picha mbalimbali zinaonesha Waziri Ummy Mwalimu akikagua utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli pamoja na watumishi na vibarua wakihamisha nyaraka na makabrasha mbalimbali kutoka kwenye jengo lililokuwa likitumiwa kama ofisi na watumishi wa wizara hiyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.

FSA_6416 FSA_6443
????????????????????????????????????
FSA_6540
????????????????????????????????????
WAZIRI NAPE AONGEA NA VIONGOZI WA COSOTA NA MKURUGENZI MKUU WA COPYRIGHT MANAGEMENT EAST AFICA BW. PAUL MATTHYSSE

WAZIRI NAPE AONGEA NA VIONGOZI WA COSOTA NA MKURUGENZI MKUU WA COPYRIGHT MANAGEMENT EAST AFICA BW. PAUL MATTHYSSE

February 14, 2016

np1
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Mhe. Nape  Nnauye akiongea na viongozi wa COSOTA na  wa  Kampuni ya  Copyright  Management  Eas t  Africa kuhusu mfumo wa ukusanyaji wa mirahaba utakavyokuwa unafanya kazi. .(Picha na Benjamin Sawe- WHUSM)
np2
 Mkuu wa uendeshaji wa Kampuni ya  Copyright  Management  Eas t  Africa  Bw. Abdi Zagar aliesimama akimuelekeza  Mhe.  Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye jinsi mfumo wa ukusanyaji wa mirahaba utakavyokuwa unafanya kazi, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa  Kampuni ya  Copyright  Management  Eas t  Africa Bw. Paul Matthysse  .(Picha na Benjamin Sawe- WHUSM)
np3
: Mkurugenzi Mtendaji wa  Kampuni ya  Copyright  Management  Eas t  Africa Bw. Paul Matthysse  kulia akimuelekeza Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye jinsi mfumo wa ukusanyaji wa mirahaba utakavyokuwa unafanya kazi.(Picha na Benjamin Sawe- WHUSM)
Stand United kuingia kambini katika Mgodi wa Dhahabu BUZWAGI

Stand United kuingia kambini katika Mgodi wa Dhahabu BUZWAGI

February 14, 2016


images (3)
Timu ya Acacia Stand United fc (CHAMA LA WANA) inayodhaminiwa na kampuni ya uchimbaji madini ya Dhahabu ya ACACIA,mara baada ya kupoteza mchezo wake wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa kufungwa goli 2-1 na  Simba Sc,kesho jumatatu inataraji kuingia kambini katika Mgodi wa Dhahabu BUZWAGI kujiandaa na mchezo wake unaofuata dhidi ya Maafande wa jeshi la kujenga taifa JKT Ruvu.
Afisa habari wa klabu hiyo ISAAC EDWARD amesema kupoteza mchezo wao dhidi ya Simba Sc ni sehemu ya matokeo ya Mpira wa miguu, kwani hivi sasa ligi ni ngumu na kila timu inapambana ili kupata matokeo mazuri.
“tumepoteza mchezo wetu tukiwa nyumbani dhidi ya Simba ni sehemu ya mchezo,tunajipanga na mchezo unaofata nyumbani ambao tutacheza na Jkt Ruvu , timu inataraji kuingia kambini siku ya kesho jumatatu katika Hosteli za Mgodi wa Dhahabu BUZWAGI kujiandaa na mchezo wetu unaofata”
Ameongeza kuwa mchezo ujao timu hiyo ya Acacia Stand United imejipanga kuhakikisha inapata ushindi ili wazidi kujiweka sehemu nzuri kwenye msimamo wa ligi kuu  Tanzania Bara.
“Uongozi pamoja na Benchi la Ufundi tumejipanga vilivyo ili tupate pointi tatu ambazo zitazidi kutuweka katika nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi ”
Isaac amewaomba mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo kuunganisha nguvu kwa pamoja na kuisaidia timu kupata matokeo mazuri nyumbani na Ugenini.
“ mashabiki wetu na wapenzi wa Acacia Stand United (Chama la wana) waendelee kuipa timu ushirikiano katika michezo yetu yote iliyobaki katika mzunguko wa pili ambao ni wa lala salama ikiwa tunacheza nyumbani na hata ugenini pia ”.
Acacia Stand United Fc kwasasa  imejikusanyia pointi 29 katika michezo yake 18 walioshuka dimbani katika msimu huu wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Wafanyakazi wa TBL wapima afya zao na kufanya mazoezi ya viungo

Wafanyakazi wa TBL wapima afya zao na kufanya mazoezi ya viungo

February 14, 2016

tb1
Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group, Roberto Jarrin.(Kulia) akimsikiliza mtaalamu wa mazoezi kutoka Kituo cha Fitness Centre, Payas Moremi (kushoto) jinsi ya kufanya mazoezi wakati wa Siku ya Afya kwanza  kwa wafanyakazi wa kampuni ya bia Tanzania, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki .katikati ni Afisa Mwandamizi wa TBL Oscar Shelukindo.
tb2
Mkurugenzi Mtendaji wa TBL GROUP Roberto Jarrin. Akishiriki mazoezi pamoja na wafanyakazi wenzake wakati wa  siku ya Afya kwanza yaliyofanyika kaitika viwanja vilivyopo eneo la kiwanda hicho  jijini Dar es Salaam,
tb6
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wakiwekea alama za kupimwa afya zao  wakati wa maadhimisho ya  siku upimaji wa Afya , yaliyombatana na mazoezi  kwa wafanyakzi wote  wa kampuni hiyo yaliyofanyika  jijini Dar es Salaam.
tb7
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wakiwekea alama za kupimwa afya zao  wakati wa maadhimisho ya  siku upimaji wa Afya , yaliyombatana na mazoezi  kwa wafanyakzi wote  wa kampuni hiyo yaliyofanyika  jijini Dar es Salaam.
tb8
Wafanyakazi wa kampuni ya bia Tanzania (TBL) wakishiriki katika mazoezi ya viungo wakati wa Maadhimisho ya siku ya Afya Kwanza yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
tb9 tb11 tb12
Waandaaji wa maadhimsho ya siku ya Afya kwanza kwa wafanyakazi wa TBL Tanzania  wakiwa katika picha ya pamoja,

UTT PROMOTED COMPANIES HOLD IT’S FIRST ANNUAL GENERAL MEETING IN DAR

February 14, 2016

Chief Executive Officer, (CEO), with UTT-Project and Infrastructure Development PLC,
Dr.Gration Kamugisha, (First-R), speaks during a joint news conference prior to
the first annual general meeting of UTT promoted companies at Julius Nyerere International
Convention Centre in Dar es Salaam Saturday February 14, 2016. Other sister
companies include UTT-AMIS, and UTT-Microfinance. Others from left to right is UTT
Microfinance’s CEO James Washima, UTT-AMIS’ CEO, Dr. Hamis Kibola, ane Finance
Management Officer from the Office of Treasury Registrar, Edgar Rugaimukamu. 

(Photos:K-VIS MEDIA/Khalfan Said)
Chief Executive Officer with UTT-AMIS, Dr. Hamis Kibola, display the reports of
UTT-PID, and UTT-Microfinance, during a joint news conference prior to the first
annual general meeting of UTT-Promoted companies at Julius Nyerere
International Convention Centre in Dar es Salaam, Saturday February 14, 2016

UTT-PID’s Acting Board Chairperson, Elipina Mlaki, walk- through the meeting agenda
 Participant reads UTT-PID’s  annual report for the year ended 30th June 2014.
 Cross section of participants
 Close follow-up
 Chairman of the Boardof Directors of UTT-Microfinance, Ambassador Fadhili Mbaga, chair the session
 Chairman of UTT-AMIS, Professor Joseph Kuzilwa, speaks during the opening session of the meeting