NAIBU WAZIRI TAMISEMI,JOSEPH KAKUNDA AFURAHISHWA NA MIRADI YA KUWAWEZESHA WANANCHI KUKABILIANA NA ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIA NCHI

December 09, 2017


Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),Joseph Kakunda(kushoto) akipanda ngazi kukagua mradi wa maji wilayani Longido,akiwa na Mkuu wa wilaya ya Longido mkoa wa Arusha,Godfrey Chongolo.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),Joseph Kakunda(kulia) na Mkuu wa wilaya ya Longido(wa pili kulia) wakimsikiliza Mhandisi wa Maji wilayani Longido,Ramadhani Musiba(kushoto) utekelezaji wa miradi ya maji.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),Joseph Kakunda akipanda ngazi kukagua mradi wa maji kijiji cha Eworendeke Kata ya Kimokouwa wilayani Longido.
Ujumbe wa Naibu Waziri  wa Tamisemi,Joseph Kakunda pamoja na maafisa wa halmashauri ya wilaya ya Longodo wakikagua moja ya miradi ya kuwawezesha wananchi kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya Tabia Nchi.
Mhe Joseph Kakunda na Mkuu wa wilaya ya Longido,Godfrey Chongolo wakijumuika na wananchi kuimba wimbo wa kufurahia mradi wa maji.
Mhe Joseph Kakunda na Mkuu wa wilaya ya Longido,Godfrey Chongolo wakiagana na wananchi wa Kijiji cha Ranchi.
Na Mwandishi Wetu,Arusha
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),Joseph Kakunda amepongeza ujenzi wa miradi ya maji inayotekelezwa katika mpango wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabia Nchi katika wilaya za Longido,Monduli na Ngorongoro.

Mradi huo unaosimamiwa kwa pamoja na Ofisi ya Rais-Tamisemi,taasisi ya kimataifa ya maendeleo na mazingira(IIED) na Haki Kazi Catalyst unatarajiwa kuwanufaisha wananchi walio katika wilaya hizo tatu.

Akiwa katika Kijiji cha Eworendeke Kata ya Kimokouwa alipongeza hatua iliyofikiwa ya kuwawezesha wananchi kupata maji safi kwaajili ya matumizi ya nyumbani pamoja na mifugo yao ikizingatiwa wilaya ya Longido asilimia 95 ya wakazi wake ni wafugaji.

Amesema mkandarasi amekua mzalendo kwa kujenga miundombinu ya maji tenki pamoja eneo la kunyweshea mifugo kwa thamani ya Sh 36 milioni na kuonya wakandarasi wasio na uzalendo wanatekeleza miradi kwa gharama kubwa lakini inakua haina ufanisi.

Mkuu wa wilaya ya Longido,Godfrey Chongolo amesema wilaya yake ipo jumla ya miradi 14 inayofadhiliwa na IIED kwa lengo la kuwawezesha wananchi kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Naye Flora Assey ambaye ni mratibu wa mradi huo kutoka Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha amesema lengo la mradi huo ni kuweka mfumo utakaowezesha upimaji wa kiutendaji katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Imeandaliwa na mtandao wa www.rweyemamuinfo.blogspot.com

MAKAMU WA IJA ASHINDA KUKU LUSHOTO

December 09, 2017
 Mr. Fahamu Mtulya Mshindi wa kuku (Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma
 Nazael Mkumbo Mshindi wa kuku
Makamu Mkuu wa Chuo cha uongozi wa mahakama IJA, Fahamu Mutlya leo  alionesha uhodari wa kukimbia baada ya kufanukiwa kumkamata kuku  katika bonanza kuadhimisha siku ya uhuru na kufunga mwaka wa 2017lililofanyika katika uwanja wa chuoni hapo.

Mtulya aliweza kuwashinda wengine waliokuwa kwenye kundi la wahadhiri baada ya kuchomoka kwa haraka na kisha kumdaka kuku huyo wakati kundi la uhasibu mshindi alikuwa Noel Njau wakati Barnaba john alishinda kundi la utawala.

Mpira wa kikapu watumishi waliweza kuwafunga wanafunzi wa chuoni hapo magoli 12 -8 na mpira wa wavu watumishi walifungwa seti 3-2.

Mwenyekiti wa kamati ya Bonanza hilo,Daudi Hemba alisema lilifanyika kwa lengo la kuwaeka pamoja watumishi na wanafunzi katika kujenga afya zao huku wakitafakari kuhusu mambo mbalimbali yahusuyo uhuru wa nchi hii.

“Bonanza hili limefanyika kwa lengo la kuwaweka pamoja watumishi na wanafunzi lakini pia kujenga afya zao huku wakitafakari kuhusu uhuru”alisema Hemba.

Mkuu wa Chuo cha IJA,Paul Kihwelo aliwataka watumishi kujenga tabia ya kufanya mazoezi ya mara kwa mara ili kuimarisha afya zao.

“Bila shaka mnafahamu kwamba anayeshiriki michezo si rahisi
kushambuliwa na magonjwa mbalimbali,na ndiyo maana tumeanzisha IJA joging club ambayo watumishi na wanafunzi wanashiriki kila jumamosi”alisema Kihwelo.
Katika bonanza hilo pia lilifanyika zoezi la upimaji wa afya ambapo watu 25 waliojitokeza kupima virusi vya ukimiwi walionekana kutokuwa na maambukizi wakati waliopima kisukari (Blood Suger) walikuwa 30 ambao walionekana kuwa ya kawaida.

RAIS DKT MAGUFULI AONGOZA SHEREHE ZA MIAKA 56 YA UHURU MJINI DODOMA LEO

December 09, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la heshima wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 56 ya Uhuru katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo Desemba 9, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akipungia wananchi wakati akiwasili kuongoza  sherehe za kuadhimisha miaka 56 ya Uhuru katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo Desemba 9, 2017.

 Sehemu ya viongozi na wageni waalikwa wakishuhudia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza  sherehe za kuadhimisha miaka 56 ya Uhuru katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo Desemba 9, 2017.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa, Mama Janeth Magufuli na Mama Mwanamema Shein kwenye sherehe hizo

 Marais Wastaafu Mhe Benjamin Mkapa na Dkt Jakaya Mrisho Kikwete wakiteta jambo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 56 ya Uhuru katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo Desemba 9, 2017.
 Viongozi mbalimbali katika Jukwaa kuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 56 ya Uhuru katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo Desemba 9, 2017

  Gwaride lililoundwa na vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama vikipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 56 ya Uhuru katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo Desemba 9, 2017
 Kikosi cha Komandoo wa JWTZ kikitoa heshima mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 56 ya Uhuru katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo Desemba 9, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 56 ya Uhuru katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo Desemba 9, 2017. Picha na Ikulu
RAIS MAGUFULI ASAMEHE WAFUNGWA 8157

RAIS MAGUFULI ASAMEHE WAFUNGWA 8157

December 09, 2017
22
Na Lilian Lundo na Beatrice Lyimo- MAELEZO, DODOMA
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesamehe jumla ya wafungwa 8,157 katika maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika leo katika uwanja wa Jamhuri, Mjini Dodoma.
Msamaha huo umehusisha wafungwa 1828 ambao watatolewa kaunzia leo na wengine 6329 wamepunguziwa muda wa vifungo vyao, aidha kati ya wafungwa watakaoachiwa huru wafungwa 61 ni wafungwa ambao walihukumiwa kunyongwa.
“Kuna wafungwa ambao wamehukumiwa kunyongwa wana umri wa miaka 85 na wapo waliokaa gerezani zaidi miaka ya miaka 45, ambao wametubu na kukiri makosa na wapo ambao hawakuwauwa maalbino wala hawakuwa majambazi,” amesema Dkt. Magufuli.
Dkt. Magufuli ametoa mfano wa mfungwa anayejulikana kama Mganga Matonya mwenye umri wa miaka 85 yupo kwenye orodha ya wafungwa watakaoachiwa huru  leo ambapo amekaa gerezani kwa miaka 37 na mahabusu miaka saba (7)  kabla hajahukumiwa.
Katika hatua hiyo, Rais Dkt. Magufuli amewaachia huru Nguza Viking na  Johson Nguza (Papii Kocha) waliohukumiwa kifungo cha maisha.
Aidha Mhe. Rais amesema kuwa msamaha huo alioutoa leo umetokana na mamlaka aliyonayo kutoka kwenye Ibara ya 45 (a) (b) (c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayomruhusu Mhe. Rais kutoa msamaha, kumuachia huru, kubadilisha adhabu au kufuta adhabu kwa mtu yoyote aliyehukumiwa kwa kosa lolote.
Wakati huo huo, Rais Magufuli ametoa wito kwa watanzania wote kuenzi na kudumisha tunu na amani zilizoachwa na waasisi wa Taifa.
Aidha, Rais Magufuli ameeleza kuwa tangu nchi ipate uhuru kumekuwa na maendeleo katika nyanza mbalimbali ikiwemo barabara, madaraja, vituo vya afya, shule za msingi na shule za sekondari.
“Wakati nchi inapata uhuru kulikuwa na jumla ya kilometa 32,600 za barabara ambapo kilometa 1360 zilikuwa katika kiwango cha lami, lakini mpaka sasa nchi inapotimiza miaka 56 ya uhuru kuna jumla ya kilometa 122,500 za barabara ambapo kati ya hizo kilometa 12,679.55 zipo katika kiwango cha lami, kilometa 2,480 zinaendelea kujengwa katika kiwango cha lami na kilometa 7087 zipo kwenye hatua mbalimbali za maandalizi za kujengwa katika kiwango cha lami” anasema Rais Magufuli.
Aidha, Rais Magufuli amesema kuwa, Mfalme wa Morroco amemtuma Spika wa nchi hiyo kuja kuangalia eneo litakalojengwa uwanja mkubwa wa Kimataifa Mkoa wa Dodoma ambapo unatarajiwa kuwekwa jiwe la msingi mwezi Machi au Aprili mwaka 2018.
Mbali na hayo Sherehe hizo zilipambwa na gwaride kutoka Majeshi ya Tanzania, onesho la kikundi cha Komando, onesho la gwaride la Uzalendo la wanafunzi, vikundi mbalimbali vya kwaya, ngoma za alisi na Tanzania Allstars.