MAKAMU WA RAIS, SAMIA SULUHU AZINDUA MPANGO WA KUWAONGEZEA UWEZO WANAWAKE LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

February 24, 2016

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amezindua Programe maalum ya Mwanamke na wakati ujao (Female Future) ambayo itawajengea uwezo wanawake katika bodi za wakurugenzi wa taasisi na makampuni mbalimbali.

Uzinduzi huo uliofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency  jijini Dar es Salaam leo na kuhudhuliwa na watu mbalimbali wakiwepo wakenya, waganda na watanzania na watu kutoka bara la Ulaya na Asia.

Makamu wa Rais, Samia Suluhu amesema kuwa wanawake ni watendaji wazuri na wanamaamuzi mazuri katika uongozi na uendelezaji wa makamuni pamoja na Tasisi mbalimbali.

Mpango huo uliozinduliwa leo umefanywa wanachana chama cha  waajili Tanzania ambao unalenga kuwajengea uwezo wanawake ili kuongeza ufanisi katika biashara zao na kujenga mtandao ambao utaongeza juhudi na maarifa kwa wanawake.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza wakati wa kuzindua Programe maalum ya Mwanamke na wakati ujao (Female Future) ambayo itawajengea uwezo wanawake katika bodi za wakurugenzi wa taasisi na makampuni mbalimbali iliyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Hyatt Regency  jijini Dar es Salaam leo.
Makamu Mwenyekiti wa kampuni ya ATE, Zuhura Muro akizungumza na wanawake kutoka kutoka makampuni mbalimbali leo wakati Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizindua mpango malumu wa kuwafundisha wanawake ili waweze kuwa na uwezo wa kuleta mawazo yenye kuinua kampuni au taasisi mbalimbali kuwa kubwa.
Mtumbuizaji akitumbuiza katika uzinduzi wa mpango wa kuinua wanawake katika uongozi wa juu katika makampuni au taasisi mbalimbali, uzinduzi  huo umefanyika leo katika hoteli Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker akitoa ushuhuda alioufanya katika taasisi hiyo ya fedha kwa maendeleo ya wanawake waliokusanyika leo ili kuzindua mpango wa kuwaundisha wanawake uongozi katika makampuni na Tasisi mbalimbali katika uzinduzi uliofanyika leo katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu, sera na Uratibu wa bunge, Jenister Mhagama akizungumza leo katika uzinduzi wa Programe maalum ya Mwanamke na wakati ujao (Female Future) ambayo itawajengea uwezo wanawake katika bodi za wakurugenzi wa taasisi na makampuni mbalimbali iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency  jijini Dar es Salaam leo.
Wadau mbalimbali wakisikiliza shuhuda mbalimbali za wadau wa uongozi kwa wanawake kutoka hapa nchini, Uganda na Kenya leo katika uzinduzi wa Programe maalum ya Mwanamke na wakati ujao (Female Future) ambayo itawajengea uwezo wanawake katika bodi za wakurugenzi wa taasisi na makampuni mbalimbali iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency  jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiteta jambo na Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu, sera na Uratibu wa bunge, Jenister Mhagama leo katika uzinduzi wa Programe maalum ya Mwanamke na wakati ujao (Female Future) amayo itawajengea uwezo wanawake katika uongozi wa juu wa taasisi na makampuni mbalimbali katika uzinduzi uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency  jijini Dar es salaam leo. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja baada ya kuzindua Programe maalum ya Mwanamke na wakati ujao (Female Future) katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam leo.

Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

Vodacom yaendelea kusogeza huduma zake karibu na wateja wake

February 24, 2016

Meya wa jiji la Arusha,Kalisti Lazaro (Wa tatu toka kushoto) akisaini kitabu cha wageni kabla ya kuzindua duka jipya la kisasa la Vodacom Tanzania eneo la Florida jijini humo,(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya Kaskazini,Henry Tzamburakis na Mkurugenzi wa duka hilo Theobald Mworia.
Meya wa jiji la Arusha Kalisti Lazaro (kushoto) akipongezana na Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya kaskazini, Henry Tzamburakis(kulia) pamoja na Mkurugenzi wa duka la kampuni hiyo,Theobald Mworia (katikati)ikiwa ni ishara ya kufurahia uzinduzi wa duka hilo lililopo eneo la Florida jijini humo jana.
Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya Kaskazini,Henry Tzamburakis (kulia),akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi wa duka la kampuni hiyo jana lililopo eneo la Florida jijini Arusha,(katikati ) ni Meya wa jiji hilo,Kalisti Lazaro na Mkurugenzi wa maduka ya Vodacom jijini humo,Theobald Mworia.
Meya wa jiji la Arusha Kalisti Lazaro (katikati) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa maduka ya Vodacom Tanzania jijini Arusha,Theobald Mworia (kushoto) na Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya kaskazini, Henry Tzamburakis wakati wa halfa ya Uzinduzi wa duka jipya la kisasa la kampuni hiyo jana lililopo eneo la Florida jijinihumo.
Mgeni rasmi Meya wa jiji la Arusha,Kalisti Lazaro(kushoto) akikata keki kuashiria Uzinduzi wa duka jipya la kisasa la Vodacom Tanzania lililopo eneo la Florida jijini humo,watatu toka kushoto ni Mkurugenzi wa maduka ya Vodacom Tanzania jijini humo,Theobald Mworia.

Waziri Muhongo aitaka TPDC na wabia kuongeza kasi katika uwekezaji wa Kiwanda cha Gesi Kimiminika

February 24, 2016

Na Greyson Mwase, Dar es Salaam 

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Muhongo ametaka kasi iongezwe katika mradi wa ujenzi wa kiwanda cha uchakataji na usindikaji wa gesi kimiminika unaotarajiwa kuanza mkoani Lindi mara baada ya taratibu za maandalizi kukamilika.
Profesa Muhongo alisema hayo katika kikao kwa ajili ya kujadili hatua iliyofikiwa  ya maandalizi  ya ujenzi  wa kiwanda hicho kilichoshirikisha watekelezaji wa mradi huo ambao ni Shirika la Maendeleo  ya Petroli Nchini (TPDC) na makampuni yanayojishughulisha na shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi  nchini.

Makampuni ya utafiti wa mafuta na gesi yanayotekeleza mradi huo ni pamoja na Shell, Statoil, Ophir Energy, Pavilion na Exxon Mobil. Pia kikao hicho kilishirikisha watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST)

Mara baada ya kupokea  taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kuchakata na kusindika  gesi kimiminika Profesa Muhongo alilitaka shirika la TPDC kushirikiana kwa karibu na makampuni ya  utafiti wa mafuta na gesi yanayotekeleza mradi huo na kwa kasi  ya haraka ili mradi huo uweze kukamilika kwa wakati.

Profesa Muhongo alisema  Tanzania ina utajiri mkubwa wa gesi hivyo ni vyema watekelezaji  wakachangamkia  fursa hiyo ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata na kusindika gesi kimiminika ambayo  mahitaji yake ni makubwa  duniani hususan katika  bara la Asia.

“Ifikapo mwaka 2025 inategemewa kuwa mahitaji  ya  gesi  duniani  yatakuwa ni kiasi cha tani milioni 440 kwa mwaka hususan katika nchi za Asia ambazo ni karibu na Afrika, hii ni fursa ambayo tunatakiwa kuichangamkia ili kuendana na  soko  itakapofika kipindi hicho,” alisema Profesa Muhongo.

Profesa Muhongo aliendelea kusema kuwa  gesi  ya kimiminika imekuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi zinazoendelea huku akitolea mfano wa Algeria ambayo ni nchi ya kwanza duniani kwa kuwa na kiwanda cha kuchakata na kusindika  gesi  kimimika ambayo kwa  sasa imepiga hatua kubwa  kimaendeleo.

Katika maandalizi ya awali ya mradi huo, Profesa Muhongo aliagiza uundwaji wa timu kwa ajili ya maandalizi ya mradi huo  ikishirikisha wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya  Fedha, Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), taasisi mbalimbali pamoja na wawakilishi kutoka katika makampuni  yanatofanya utafiti wa gesi na mafuta nchini ambayo ni mtekelezaji wa mradi huo.

Alisisitiza kuwa ni vyema timu hiyo ikawa na wataalam wenye uzoefu mkubwa watakaofanya kazi kwa weledi na kukamilisha kazi hiyo kwa wakati.

Aliagiza kuwa timu hiyo kukamilisha taratibu zote za maandalizi kabla ya mwezi Novemba, mwaka huu.

Naye Mkurugenzi Mtendaji kutoka Shirika la Maendeleo  ya Petroli  Tanzania (TPDC) Dkt. James Mataragio alisema kuwa shirika  lake limekuwa likishirikiana na wabia wa ujenzi wa kiwanda hicho  katika hatua zote za maandalizi  ya awali na kuahidi kuongeza kasi  ili kazi hiyo iweze kukamilika kwa wakati.

MH. LUKUVI ATOA MSAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO IDODI, MKOANI IRINGA

February 24, 2016

Na MatukiodaimaBlog

MBUNGE wa jimbo la Isimani Bw Wiliam Lukuvi amewapa pole waathirika wa mafuriko wa kata ya Mapogolo tarafa ya Idodi wilaya ya Iringa mkoani Iringa kwa kuwakabidhi msaada wa pesa zaidi ya Tsh milioni 9 kwa ajili ya kusaidia mahitaji mbali mbali ikiwa ni pamoja na kurejesha miundo mbinu ya maji safi iliyoharibiwa na mafuriko.
Bw Lukuvi ambae pia ni waziri wa Ardhi ,nyumba na maendeleo ya makazi alikabidhi msaada huo jana baada ya kutembelea waathirika hao waliopo kambi ya Kitanewa pamoja na kutembelea eneo la barabara ya kutoka Iringa kuelekea hifadhi ya Taifa ya Ruaha ambayo kwa sasa imekarabatiwa baada ya awali barabara hiyo kukatika kutokana na mafuriko hayo , alisema kuwa lengo lake kama mbunge wa jimbo hilo la Isimani na serikali ni kuona wananchi waliokumbwa na mafuriko wanaendelea kusaidiwa .
 
Mbunge wa jimbo la Isimani Bw Wiliam Lukuvi ambae ni waziri wa Ardhi ,nyumba na maendeleo ya makazi (kulia) akimpa maelekezo mwenyekiti wa kijiji cha Mapogolo baada ya kumkabidhi fedha kiasi cha Tsh milioni 2 za kulipa fidia ya ardhi kwa wananchi watakaohamishiwa makazi mapya kutoka kitongoji cha Kitanewa Idodi ambao nyumba zao zilisombwa na mafuriko.

Alisema kuwa awali aliomba msaada wa mahindi tani 100 kutoka serikali kwa ajili ya waathirika hao wa mafuriko Idodi na Pawaga ikiwa ni pamoja na kuwasaidia msaada wa fedha kiasi cha zaidi ya Tsh milioni 3 kwa ajili ya kuwawezesha waathirika hao wa mafuriko kupata mahitaji mengine kama mboga na pesa ya kusagia mahindi hayo .
Bw Lukuvi alisema kuwa kwa ajili ya kurejesha huduma ya maji kijijini hapo amewasaidia kiasi cha Tsh miliobni 4 ambazo wameomba kwa ajili ya kuboresha miundo mbinu hiyo ,pia kiasi cha Tsh milioni 2 kwa ajili ya kukiwezesha kijiji kulipa fidia ya ardhi kwa wananchi waliotoa ardhi yao kwa ajili ya wakazi wa kitongoji cha Kitanewa ambao wanapaswa kuhamishwa eneo hilo la mafuriko la kupewa makazi mapya . 
Wananchi wanaotakiwa kuhamishwa kwenda makazi mapya baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko wakimsikiliza kwa makini mbunge wao Lukuvi.

" Waambieni watu wenye mashamba ambayo yatachukuliwa kwa ajili ya viwanja mwaka huu wavune mazao yao na baada ya hapo kila mmoja muweze kumlipa fidia ya Tsh 200,000 na baada ya hapo waitini wataalamu wa ardhi ili waweze kupima viwanja na mpanfgilio mzuri zaidi kwa ajili ya makazi mapya .......pia nataka hata mashamba ya kawaida ya wananchi kupimwa ili kupata hati za ardhi zitakazowawezesha kutumia kupata mikopo ....ila nitawaletea mashine za kufyatulia tofari ambazo unaweza kuzijengea bila kuchoma "
Alisema kuwa kwa ajili ya kuhamasisha ujenzi wa nyumba bora mwananchi atakayekuwa wa kwanza kupandisha jengo atamchangia bati japo kwa sasa amekwisha toa bati zaidi ya 300 kwa mkuu wa wilaya ya Iringa kwa ajili ya waathirika hao.
 
Lukuvi kushoto akiwa na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela katikati jana.
Bw Lukuvi pia amewapongeza wadau mbali mbali zikiwemo taasisi za dini ,watu binafsi ,taasisi ya kifedha pamoja na mifuko ya hifadhi za jamii kwa kujitolea misaada mbali mbali kwa ajili ya waathirika wa mafuriko na wagonjwa wa Kipindupindu Pawaga .
Pamoja na kuwashukuru wadau hao Lukuvi alimpongeza waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa kuwatembelea waathirika hao wa Mafuriko na wale wa Kipindupindu Pawaga .
Hata hivyo Lukuvi alimpongeza mkuu wa wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela na viongozi wote akiwemo mkuu wa mkoa Amina Masenza kwa kusimamia shughuli mbali mbali ikiwemo ya urejeshaji wa miundo mbinu ya barabara iliyokuwa imekatika katika barabara ya Iringa - Ruaha .
Katika hatua nyingine Bw Lukuvi aliagiza serikali ya kijiji cha Mapogolo kutowabagua wananchi katika kugawa chakula hicho cha msaada na kutaka hata ambao si waathirika wa mafuriko ambao wana njaa wapewe chakula hicho cha msaada kwa waathirika wa mafuriko .
Wakati huo huo Waziri Lukuvi alisema kuwa serikali inakusudia kuijenga barabara ya Iringa- kuelekea hifadhi ya Ruaha kwa kiwango cha lami kama mbavyo Rais Dr John Magufuli alivyoahidi wakati wa kampeni kupitia ilani ya uchaguzi ya CCM
Pia kwa ajili ya kuwafanya wananchi kunufaika watalii wanaotembelea hifadhi hiyo ya Ruaha Iringa alisema tayari jitihada za kujenga viwanja vidogo vya ndege nje ya hifadhi ya Ruaha zimeanza na kuwa lengo la serikali ni kuwahamisha wafanyakazi wanaoishi ndani ya hifadhi hiyo na kujumuika na wananchi nje ya hifadhi ili waweze kupata mahitaji kama wananchi wengine.
 Lukuvi akizungunza na waathirika wa mafuriko ambao kwa sasa wanaishi katika mahema 
 
Mkazi wa Kitanewa akifurahia baada ya Lukuvi kuwapatia misaada mbali mbali.
 
Mmoja kati ya wakazi wa KItanewa ambao walikubwa na mafuriko aliyepata kusoma na waziri Lukuvi darasa moja shule ya msingi akimsikiliza mbunge wake 

 
Lukuvi akitoa maelekezo kwa wananchi wa Kitanewa Idodi.
 
Mkazi wa Kitanewa akilalamika kunyimwa msaada wa mahindi ya msaada wakati yeye ni mlemavu japo si mlengwa wa msaada huo wa waathirika wa mafuriko 
 
Lukuvi akielezwa jambo na mmoja kati ya waathirika wa mafuriko Idodi.
 
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akimweleza jambo mbunge Lukuvi 
 
MKazi wa kitanewa Idodi akimpongeza mbunge wake Lukuvi kwa kuwajali wananchi.
 
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela Katikati na kamati yake ya Ulinzi na usalama wakitazama daraja la Iringa -kuelekea hifadhi ya Ruaha ambalo awali lilikuwa halipitiki baada ya kusombwa na mafuriko na sasa linapitika.

ZAKIA MEGHJI AFUNGUA BARAZA LA WAFANYAKAZI MOI JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

February 24, 2016

 Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini Taasisi ya Tiba ya Mifupa ,Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI)  Zakia Meghji (wa kwanza kulia) akifungua Baraza la tatu la Wafanyakazi Taasisi hiyo sambamba na utoaji vteti kwa wafanyakazi bora na pesa taslimu kwa kila mfanyakazi, Dar es Salaam leo katika Ukumbi wa NIMR. wa katikati ni  Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi  Dkt, Othman Kiloloma na anayefatia ni Katibu wa Baraza la wafanyakazi hilo Dkt. Clement Mugisha
 (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)












STATEMENT BY HEAD OF UN MISSION IN TANZANIA ON THE OCCASION OF THE 50TH ANNIVERSARY OF UNDP

STATEMENT BY HEAD OF UN MISSION IN TANZANIA ON THE OCCASION OF THE 50TH ANNIVERSARY OF UNDP

February 24, 2016
Alvaro Rodriguez
UN Resident Coordinator in Tanzania and UNDP Resident Representative, Mr. Alvaro Rodriguez.
Today marks the 50th Anniversary of the United Nations Development Programme (UNDP). Founded in 1966, UNDP now works in some 170 countries and territories to help eradicate poverty and reduce inequalities and exclusion.
In Tanzania, UNDP support began in May 1978. Since then, UNDP has continued to serve as a critical member of the UN team in the country, which has collectively supported the government in achieving its development agenda through aligning its support specifically to the national development priorities. In addition, UNDP has helped strengthen the government’s capacity to manage and coordinate international development assistance through the development of strategies, action plans and an improved aid management system to facilitate national leadership.
UNDP in particular has supported the development of a national framework for reducing emissions from deforestation and forest degradation, as well as of local capacity to manage forest carbon projects. In addition, UNDP continues to support the government to integrate environment and energy issues into national policy, as well as build local and regional capacity. Through a UNDP and Global Environment Facility (GEF) initiative some 8,400 households in the northern region of Mwanza were given solar energy systems. Following this success, the Government now requires all local authorities in Tanzania to include solar planning in their budgets, and has removed all taxes and duties on solar energy appliances.
In terms of democratic governance, capacity development has been provided to the National Assembly of the United Republic of Tanzania and to the Zanzibar House of Representatives, thereby ensuring that MPs can better exercise their interrelated functions of law making, oversight and representation of citizens.
UNDP has over the last two decades strengthened the institutional capacity of the Tanzania Commission for AIDS (TACAIDS) and the Zanzibar AIDS Commission (ZAC) to respond to HIV/AIDS and its impact as well as social-economic factors that lead to the epidemic.
Allow me, in this context, to thank our Development Partners and to acknowledge the spirit of active engagement and collaboration which has characterized the process through which our support to Tanzania has progressed. Indeed, I would like to take this opportunity and to renew our readiness to strengthen further the cooperation with all our partners.
Last year, the world seized a unique opportunity to set a transformational global agenda for sustainable development, by reaching global agreements on financing for development, the post-2015 development agenda, and climate change. These 17 new Sustainable Development Goals (SDGs) will continue the journey towards progress for everyone that aims at going even farther to focus the world on ending poverty, hunger and major health problems, among others. I believe we will achieve substantial results by taking on the many interconnected challenges we face together.
UNDP’s new strategy in Tanzania to 2021 builds on an established and strong relationship with the Government of Tanzania over the past three decades. The Country Programme Document (CPD) followed the imperative of national ownership, with our actions firmly determined by country needs and will be delivering on three major pillars: inclusive economic growth, environmental sustainability and inclusive democratic governance. Reaching out to women and youth of this country remains a top priority for UNDP and shall guide our focus and energy.
Going forward, partnerships and co-ordination will be critical, especially through increased engagement with South-South and triangular co-operation; deeper co-operation with emerging partners on shared development priorities; and partnerships with other stakeholders, including regional bodies, civil society organizations, and private sector entities. In doing this we will also seek to support the data revolution necessary to inform policymaking, monitor progress, and enhance accountability.
To celebrate these achievements, on 29 February 2016, we will organize a Youth Symposium, aimed at discussing how to mainstream youth perspectives and youth-related issues in development planning processes. These youth will be the biggest beneficiaries when the SDGs are accomplished. We invite you to reflect on our shared history, and take part in the great work ahead—crafting strategic interventions where development assistance can be most effective.

Tigo yafikisha upatikanaji wa huduma ya 4G LTE Moshi

February 24, 2016
Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata (katikati)  akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) katika uzinduzi wa huduma ya 4G LTE jijini Dodoma, kushoto ni Meneja wa huduma ya 4G LTE, Benedict Mponzi na kulia kwake ni Meneja Masoko wa kanda ya kaskazini  Kephar Kileo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mapema leo mjini Moshi.

Meneja wa huduma ya 4G LTE, Benedict Mponzi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) katikati ni Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata na kulia kwake ni  Meneja Masoko wa kanda ya kaskazini  Kephar Kileo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mapema leo mjini Moshi.


Moshi, Februari 24 2016. Wateja wa Tigo waishio Moshi sasa wanaweza kupata mtandao wa intaneti wenye kasi kubwa zaidi kufuatia upanuzi wa upatikanaji wa huduma ya 4G LTE hadi kufikia jiji hilo lilopo kaskazini mwa Tanzania Teknolojia ya 4G LTE ina kasi mara tano zaidi kuliko teknolojia ya 3G inayopatikana nchini kwa sasa.

‘’Upanuzi huu umetokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika majaribio ya awali ya utoaji huduma ya 4G jijini Dar es Salaam kuanzia mapema mwaka jana,’’ amesema Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini, George Lugata.
Akizungumza leo na waandishi wa habari mjini Moshi, Lugata amesema: "uzindu wa 4G ni kielelezo cha jinsi ambavyo Tigo imedhamiria kufanikisha kuleta mabadiliko ya dijitali katika maisha ya watanzania na pia kuwa katika msitari wa mbele wa kutumia teknolojia ya kisasa na kibunifu nchini Tanzania."

Mtandao wa 4G LTE una kasi kubwa zaidi katika kuperuzi na kupakua kwa urahisi kutoka kwenye mtandao wa intaneti na pia katika kufanya mawasiliano kwa njia ya Skype. Huduma hii pia inaharakisha urushwaji wa picha za video na ubora hali ya juu na kufanya mikutano kwa njia ya mtandao. 

“Tunapenda kuwahakikishia wateja wetu waishio Moshi kwamba sasa wanaweza kufurahia huduma bora zaidi za mawasiliano kutoka Tigo na Intaneti yenye kasi zaidi,” Lugata amesema. Moshi ni moja wapo ya miji mikubwa Tanzania, na pia inajivunia bandari ndani ya Afrika Mashariki na kwa sababu ya bahari ya Hindi ni kivutio cha utalii nchini.
Wateja wote wa Tigo 4G LTE watanufaika na promosheni; kila atakapo ongeza salió la shilingi  elfu moja au zaidi, atapata mb 500 bure kama bonasí.

Ametaja miji mingine katika mikoa sita ambapo 4G inapatikana kuwa ni Moshi, Dodoma, Morogoro, Tanga na Arusha, “jambo ambalo linaifanya Tigo kuwa na mtandao mkubwa wa 4G nchini Tanzania.” Lengo kuu ni kufikisha huduma ya 4G katika kila kona za nchi ifikapo mwaka ujao, Lugata ameongeza kusema.

MKALI WA NDONDI THOMAS MASHALI KUTAFUTIWA MBABE PASAKA

February 24, 2016

 Bondia Salum Nassoro akipasha na kocha wake, Maneno Abdallah katika gym yao iliyopo Mazense Midizini.

 Promota wa mchezo huo, Haruna Musa katika picha ya pamoja na bondia, Salum Nassoro.

Kampuni ya Dippo Boxing Promotion ya jijini Dar inayoongozwa na promota, Haruna Musa imeandaa pambano la Uzito wa Kati ‘Middle Weight’ kati ya bondia Salum Nassoro wa Dar na Benson Mwakyembe wa Ruvuma mchezo utakaopigwa Siku Kuu ya Pasaka, Machi 28 mwaka huu.

Pambano hilo la kukata na shoka litapigwa kwenye uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma ambapo kwa mujibu wa promota huyo alisema kuwa mshindi wa siku hiyo atazichapa na bingwa wa Afrika  ‘WBF, Thomas Mashali.

Mabondia hao ambao kila mmoja alitamba kumchapa mwenzake, waliwataka mashabiki wa ndondi kujitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo huo ili waone ladha ya ndondi ya asili.

      

Mafanikio ya kipindi cha Radio cha Walinde Watoto katika kupunguza ukatili kwa watoto

February 24, 2016
Mratibu wa kipindi cha walinde watoto Neema Kimaro akiongea na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya kipindi hicho pembeni yake ni  Mwandaaji wa kipindi cha Walinde Watoto Kimela Billa katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika mapema leo katika studio za True Vision  ambao ndio waandaaji wa kipindi hicho chini ya udhamini wa  UNICEF na uratibu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ushirikiano ofisi hizo zipo  Mikocheni, Jijini Dar Es s salaam"
Mwandaaji wa kipindi cha Walinde Watoto Kimela Billa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari  kuhusu mafanikio ya kipindi hicho   katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika mapema leo katika studio za True Vision  ambao ndio waandaaji wa kipindi hicho chini ya udhamini wa  UNICEF na uratibu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ushirikiano ofisi hizo zipo  Mikocheni, Jijini Dar Es s salaam.
Mwandishi wa habari kutoka kituo cha Luninga EATV David Gumbo akiuliza swali kwa mwandaaji wa kipindi cha Walinde Watoto mapema leo  kuhusu mafanikio ya kipindi hicho   katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika mapema leo katika studio za True Vision  ambao ndio waandaaji wa kipindi hicho chini ya udhamini wa  UNICEF na uratibu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ushirikiano ofisi hizo zipo  Mikocheni, Jijini Dar Es s salaam.

Mwandaaji wa kipindi cha Walinde Watoto Kimela Billa akijibu maswali kutoka kwa   waandishi wa habari  kuhusu mafanikio ya kipindi hicho Katikati ni  Mratibu wa kipindi cha walinde watoto Neema Kimaro na kulia kwake ni Mshauri Nasaha Mwandamizi kutoka CSEMA Fatuma Kauramba  katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika mapema leo katika studio za True Vision  ambao ndio waandaaji wa kipindi hicho chini ya udhamini wa  UNICEF na uratibu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ushirikiano ofisi hizo zipo  Mikocheni, Jijini Dar Es s salaam.


Waandishi wa habari wakisikiliza makini maelezo ya waaandaji  wa kipindi cha Walinde Watoto mapema leo  katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika mapema leo katika studio za True Vision  ambao ndio waandaaji wa kipindi hicho chini ya udhamini wa  UNICEF na uratibu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ushirikiano ofisi hizo zipo  Mikocheni, Jijini Dar Es s salaam.




Na Krantz Mwantepele, Dar es salaam

Kuhusu Kipindi cha Walinde Watoto
Ndugu waandishi wa habari, katika jitihada za kutoa elimu kuhusu maswala ya Ukatili dhidi ya Watoto, UNICEF na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ushirikiano na True vision production, walianzisha kipindi cha redio cha Walinde Watoto, ambacho kilianza kuruka hewani kupitia redio mbalimbali hapa nchini mwezi Novemba mwaka 2014. Kipindi hiki kinarushwa na redio 19 nchini Tanzania, bara na visiwani, zikiwemo TBC na ZBC.

Malengo ya Kipindi

Malengo ya Kipindi

Ndugu waandishi wa habari, kipindi cha redio cha Walinde Watoto kilianzishwa kwa malengo yafuatayo;


  1. Kutoa elimu juu ya ulinzi kwa watoto, kufuatia ripoti iliyotolewa mwaka 2011 ambayo ilionyesha ukatili dhidi ya watoto ni tatizo kubwa nchini Tanzania
  2. Kutoa fursa kwa jamii kujadili mazingira salama ambayo mtoto anapaswa kuishi mahali popote atakapokuwa iwe ni nyumbani, shuleni na hata barabarani
  3. Kuelimisha jamii kuhusu umuhimu na  mbinu za kuripoti matukio ya ukatili kwa watoto.
Mafanikio ya Kipindi
Ndugu waandishi wa habari, tangu tumeanza kurusha kipindi cha Walinde Watoto tunajivunia mafanikio mengi;

  • Kwanza kabisa ni kwa vituo vya redio vipatavyo 19 kukubali kushiriki kampeni hii kwa kurusha kipindi cha elimu kwa umma bila malipo. Tulianza na redio 14 zikiwemo TBC na ZBC na miezi michache baadaye ziliongezeka redio nyingine 5 baada ya kuvutiwa na maudhui ya kipindi. Kwa ujumla kipindi cha Walinde Watoto kinasikika nchi nzima.

  • Tumefanikiwa pia kutembelea wilaya zaidi ya 12 nchini Tanzania ili kuhakikisha kwamba tunatoa fursa kwa watu mbalimbali wakiwemo wazazi na walezi kupaza sauti zao katika mambo yahusuyo ulinzi kwa watoto. Miongoni mwa wilaya tulizotembelea ni pamoja na Shinyanga, Magu, Musoma, Geita, Kasulu na Kahama. Nyingine ni Kilosa, Kigoma, Kasulu, Kisarawe, Hai na zile za Zanzibar.

  • Ndugu waandishi wa habari tumefanikiwa kutengeneza na kurusha vipindi zaidi ya 60 vikiwemo vipindi maalum kuhusu mada mbalimbali kama vile ukatili wa aina mbalimbali wanaofanyiwa watoto wakikiwa nyumbani, shuleni, na hata barabarani wakienda na kutoka shule, watoto ulemavu wa ngozi ama albino pamoja na watoto wakimbizi. Tumetoa elimu umuhimu wa kutoa taarifa katika ngazi tofauti pamoja na namba maalum ya msaada wa watoto ya 116.


  • Ndugu waandishi wa habari, jukumu la kuwalinda watoto ni letu sote. Kwa kutambua hili tumefanikiwa kufanya mahojiano na viongozi mbalimbali wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa taasisi na mashirika binafsi, wafanyabiashara, wadau mbalimbali, wanaharakati n.k yote ikiwa na lengo la kupata mitazamo tofauti ya wadau hawa muhimu katika maendeleo ya taifa letu.

  • Ndugu waandishi wa habari, wakati wa uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, tulifanikiwa kufanya vipindi maalum vinavyohusu uchaguzi, tuliandaa midahalo iliyowaleta pamoja wananchi na watoto katika meza moja na wagombea wao wa ngazi za ubunge na udiwani, ili wasikilize ajenda za watoto katika uchaguzi mkuu na kuwaeleza ni kwa namna gani wamejipanga kukabiliana na changamoto zinazohusu ulinzi wa watoto.

  • Kama mnavyofahamu swala la kubadili tabia linahitaji nguvu zetu wote na ni mchakato wa muda mrefu, kwa upande wetu, kupitia kipindi hiki cha redio, kwa asilimia kubwa tumefanikiwa kuongeza uelewa wa jamii kuhusu maswala yahusuyo ukatili kwa watoto na namna mbalimbali za kuwalinda watoto. Tunatumaini mtatuunga mkono katika jitihada hizi.

  • Ndugu waandishi wa habari, tulifanikiwa kufungua tovuti maalumu ya www.walindewatoto.org ambayo imekuwa ikirusha vipindi hivi vya watoto. Tumeweza kufungua akaunti katika mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook, Twitter na Whatasapp na kwa kupitia mitandao hiyo tumeweza kufikia maelfu ya watu. Pia tumeanzisha namba maalum ya simu ambayo watu wanaweza kupiga na kutoa maoni yao kuhusu vipindi.

  • Ndugu waandishi wa habari, kwa kutambua mchango wa redio katika kupiga vita ukatili dhidi ya watoto, mnamo mwezi Februari mwaka 2015 tuliweza kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka redio zote washirika wa kipindi hiki. Mafunzo hayo yaliweza kuwajengea uwezo ili waweze kuzungumzia ukatili kwa watoto, namna mbalimbali ya kuwahoji watu ili kuibua changamoto za watoto, na namna ya kufanya jamii ibadilike na kuona matatizo ya watoto ni yetu sote.

  • Kutokana na ubora wa kipindi, wasikilizaji wengi wameongezeka kitendo ambacho kimewashawishi wamiliki wa vituo binafsi kuongeza muda wa kipindi kutoka nusu saa hadi saa nzima na hivyo kupokea maswali na mijadala yahusuyo watoto kutoka katika maeneo yao.

  • Tumefanikiwa pia kuanzisha vikundi vya wasikilizaji kutoka maeneo mbalimbali nchini ambao husikiliza kipindi kila kinaporushwa na kisha kutupa mrejesho wa yale waliyojifunza. Makundi haya husambaza elimu waliyoipata kwa watu wengine wakiwemo ndugu na marafiki zao.


Tunafanyaje kazi?
Kipindi cha Walinde Watoto kinapata maudhui (content??) kwa kuandaa midahalo mbalimbali, mikutano katika vijiji, mahojiano na wadau, kutembelea wilaya na mikoa mbalimbali pamoja na kupitia mitandao ya kijamii.

Tangu tumeanza kurusha kipindi, tumeandaa nyimbo mbili maalum kwa ajili ya kampeni.
Kama motisha kwa wasikilizaji wetu, tunaandaa mashindano mbalimbali ambapo washindi hupata zawadi mfano fulana (Tshirts), redio n.k

Nini malengo yetu?
Ndugu waandishi wa habari, mwezi wa kwanza mwaka huu tumeanza msimu wa pili wa kipindi cha Walinde Watoto. Tunakusudia kufanya yafuatayo;

  • Kushawishi redio mbalimbali nchini zishiriki kampeni na kurusha kipindi cha elimu kwa umma. Tunakusudia kuongeza idadi ya redio kufikia walau 25 ili tuweze kufikia wasikilizaji takribani milioni 24 nchini Tanzania.

  • Kama tunavyofahamu, maswala ya ukatili kwa watoto yanazidi kushika hatamu. Awamu hii itajikita zaidi kwenye kuzungumzia adhabu mbalimbali za watoto zikiwemo vipigo, matusi, manyanyaso, ukatili wa kisaikolojia na nyingine nyingi.

  • Tunakusudia kutumia namba maalum ya simu kutoka UNICEF kufanya utafiti kuhusu usikilizaji wa kipindi hiki ili kupata mrejesho kutoka kwa wasikilizaji

  • Kuendeleza na kuyajengea uwezo makundi ya wasikilizaji wa kipindi katika jamii ‘community listening groups’

  • Kuongeza nguvu katika matumizi ya mitandao ya kijamii ili kufikia watu wengi zaidi pamoja na kutembelea Wilaya nyingine nyingi.
Wito
  • Tunatoa wito kwa serikali na taasisi mbalimbali kuendelea kutoa ushirikiano ili tuweze kuwahabarisha na kuwafikia watanzania wengi zaidi katika kuhamasisha kuwalinda watoto.

  • Tunatoa wito kwa wazazi na walezi kuendelea kuwajali na kuwalinda watoto wao kama njia mojawapo ya kutimiza majukumu yao kama wazazi.

  • Pia tunatoa wito kwa watanzania kwa ujumla kushirikiana kwa karibu na kamati za ulinzi na usalama wa mtoto katika kulisukuma gurudumu hili la ulinzi na usalama kwa mtoto

  • Endapo utaona mtoto anafanyiwa kitendo cha ukatili basi usisite kupiga namba 116 kwa msaada zaidi, namba hii ni bure kabisa.

Redio zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto
Zifuatazo ni redio zinazoshirikiana nasi katika kurusha kipindi cha Walinde Watoto:
1.     Radio Faraja- Shinyanga
2.     Radio Huruma- Tanga
3.     Country FM –Iringa
4.     Ice FM- Makambako
5.     Radio Boma Hai- Hai
6.     Zenji FM –Zanzibar
7.     Bomba FM –Zanzibar
8.     Radio Maria- Dar Es Salaam
9.     Radio Quran- Dar Es Salaam
10.  Best FM – Ludewa
11.  Radio Victoria –Musoma
12.  Dodoma FM – Dodoma
13.  Zanzibar Broadcasting Cooperation ZBC- Zanzibar
14.  TBC Taifa- Dar Es Salaam
15.  Radio FADECO- Karagwe
16.  Radio Jamii Kilosa- Kilosa
17.  Radio Kwizera- Ngara
18.  Radio Upland- Njombe
19.  Radio Kitulo- Makete.
Mwisho
Ndugu waandishi wa habari narudia tena kusisitiza, jukumu la kuwalinda watoto ni jukumu letu sote. Vyombo vya habari tuna nafasi kubwa sana ya kufikia watu wengi zaidi, tutumie taaluma yetu kutetea na kulinda haki za watoto.
Asanteni sana kwa kunisikiliza.