PPF YAKUTANA NA WAFANYAKAZI WA NOKIA JIJINI DAR ES SALAAM
Mwanachama
mpya wa PPF, akijaza fomu za mpango wa uchagiaji wa hiari wakati wa
utoaji huduma kwa wafanyakazi wa kampuni ya NOKIA pale Mlimani City
jijini Dar es Salaam, Agosti 21, 2015. Kulia ni Afisa wa Kanda wa PPF,
Upendo Singinika Sasi
Meneja Masoko wa PPF, Elihuruma Ngowi (kushoto), akimkabidhi zawadi mwanachama wa Mfuko huo, Raymond Ndambo
Elihuruma
(kushoto) na mtaalamu wa mifumo ya comuter wa PPF, (Kulia), wakiangalia
jinsi wanachama wa mfuko huo wanavyopata taarifa za michangu yao
kupitia simu zao
Afisa Masoko mwandamizi wa PPF, Nelu Mwalugaja, (kulia), akimpatia maelezo ya huduma za Mfuko huo, Mwanachama wa PPF.
Meneja Masoko wa PPF, Elihuruma Ngowi, akizungumza na waandishi wa habari.
Msimamizi
wa Kanda wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Upendo Walter Mazula, (kulia),
akimkabidhi zawadi mwanachama mpya wa PPF, Raymond Ndambo, (katikati),
huku Meneja Masoko wa PPF, Elihuruma Ngowi, wakati wa siku ya
wafanyakazi wa kampuni ya NOKIA.
Wataalamu wa mifumo ya computer wa PPF, wakifuatialia taarifa za Mwanachama (wapili kushoto)
Afisa wa Kanda wa PPF, Upendo, (kushoto), akimpatia zawadi Mwanachama wa Mfuko huo baada ya kupatiwa huduma
Msimamizi
wa Kanda wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Upendo Walter Mazula, (aliyekaa),
akimpatia maelezo Mwanachama wa Mfuko huo, (kushoto), wakati wa utoaji
huduma kwa wafanyakazi wa NOKIA pale Mlimani City jijini Dar es Salaam
Khalfan Said Photojournalist.
WIZARA YA AFYA YAWANOA WAANDISHI WA HABARI JINSI YA KUKABILIANA NA MAGONJWA YA MLIPUKO DAR
Daktari
Mwandamizi Dharura na Maafa kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
Dkt. Mary Kitambi akitoa mada jana jijini Dar es salaam wakati wa semina
ya waandishi wa habari jinsi ya kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa
kipindupindu.
Mmoja
wa waandishi wa habari akiuliza swali jana jijini Dar es salaam
wakati wa semina ya waandishi wa habari jinsi ya kukabiliana na mlipuko
wa ugonjwa wa kipindupindu.
Mtaalamu
wa Ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa kutoka Wizara ya Afya na Ustawi
wa Jamii Dkt.Vida Mmbaga akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari jinsi
ya kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu katika Semina
iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa wanahabari.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Gain Marc Van Amengen (kulia) akitoa ufafanuzi
kwa waandishi wa habari(hawapo pichani ) jana jijini Dar es salaam juu
ya kuweka madini joto kwenye vyakula. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Michael John.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Michael John(kushoto)
akijibu maswali ya wanahabari (hawapo pichani ) jana jijini Dar es
salaam juu ya kuweka madini joto kwenye vyakula. Kulia ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Gain Marc Van Amengen.
Mkurugenzi
Msaidizi huduma ya lishe kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt.
Vincent Assey (kushoto) akifafanua kwa wanahabari juu ya umuhimu wa
madini joto jana jijini Dar es salaam .Kulia ni Mkurugenzi wa Kinga
kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Neema Rusibimayila.
Mmoja
wa waandishi wa habari David John swali jana jijini Dar es salaam
wakati wa semina ya waandishi wa habari jinsi ya kukabiliana na mlipuko
wa ugonjwa wa kipindupindu.
Picha zote na Anitha Jonas -MAELEZO-Dar es salaam.
MAKONDA AWAHIMIZA WASANII KUJIUNGA NA BIMA YA AFYA
Picha ya Pamoja ya DC Makonda, Viongozi wa BASATA, Viongozi wa NHIF na Wasanii
Baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Wasanii waliokabidhiwa kadi za NHIF wakiwa na Mgeni rasmi DC Makonda
Baadhi ya wasanii wakifuatilia mada
Mkuu wa Wilaya ya Kindondoni akihutubia wasanii
……………………………………………………………………………
Awataka kutumia taaluma yao kuhamasisha wengine kujiunga:
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul
Makonda amesema wakati sasa umefika kwa wasanii kujiunga na Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya, badala ya kuendelea kuchangishana fedha za
matibabu kila wanapougua.
Amesema kutokana na kupanda kwa
gharama za maisha hivi sasa zikiwemo za matibabu, wasaani wana kila
sababu ya kuona umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
ili wanapougua watibiwe kwa kutumia kadi badala ya kuhangaika kutafuta
fedha taslimu.
Makonda alikuwa akizungumza
wakati wa ufunguzi wa semina kuhusu huduma za matibabu kupitia mpango
maalumu wa bima ya afya kwa wajasiliamali na vikundi vilivyosajiliwa
unaojulikana kama KIKOA.
Amesema hivi sasa wasanii wengi
wanahangaika kupata matibabu katika mazingira yasiyoridhisha kwa kuwa
hawana bima za afya hivyo ni muhimu kwao wachangamke fursa hiyo ambayo
itawawezesha kuchangia kabla ya kuugua na hivyo kuwa na uhakika wa
kutibiwa hata kama hawana fedha mfukoni.
Naye Mwakilishi wa Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Eugen Mikongoti
amesema NHIF imeanzisha utaratibu huo wa kuchangia kwa kundi la
wajasiliamali ili kuwapa uhakika wa matibabu wakati wote wanapokua
katika shughuli zao za kuelimisha na kuhamasisha jamii katika masuala
mbalimbali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Amesema kwa kuchangia 76,800
mwanachama wa KIKOA atakuwa na uhakika wa kutibiwa mwaka mzima katika
vituo vya matibabu zaidi ya 6000 vilivyosajiliwa na Mfuko nchini nzima.
Mikongoti amesema NHIF itawatumia
wasanii hao katika kuelimisha umma ili kuhakikisha kuwa ujumbe wa
umuhimu wa wananchi kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya unaenea
nchini nzima.
Katika semina hiyo iliyoandaliwa
kwa pamoja na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Baraza la Wasanii
Tanzania (BASATA), viongozi wanne wa Shirikisho la Wasanii
walikabidhiwa kadi zao za bima ya afya zinazowawezesha kupata matibabu
wakati wowote watakapougua.
Mpango wa bima ya afya kwa
wajasiliamali – KIKOA- unawalenga wajasiliamali walio katika vikundi
vilivyosajiliwa, ambapo hadi sasa zaidi ya vikundi mia moja vyenye
wanachama zaidi ya elfu ishirini vimejiunga na Bima ya Afya.
MKURUGENZI MKUU WA AGPAHI AAGANA RASMI NA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika lisilo la Kiserikali la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI), Laurean Bwanakunu aliyekwenda kumuaaga ofisini kwake baada ya Rais Jakaya Kikwete kumteua kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD). (Picha na Francis Dande)
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga (katikati) akizungumza na uongozi wa Shirika lisilo la Kiserikali la AGPAHI uliokwenda ofisini kwake wakati Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo alipokwenda kumuaga.
Meneja Miradi wa Shirika la AGPAHI kwa Mikoa ya Shinyanga & Simiyu, Dk. Gastor Njau (kushoto) akifafanua jambo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la AGPAHI anayemaliza muda wake, Laurean Bwanakunu akifafanua jambo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akisisitiza jambo....
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi Mkuu wa AGPAHI akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga akifafanua jambo wakati uongozi wa Shirika la AGPAHI ulipomtembelea ofisini kwake.
Mkurugenzi Mkuu wa AGPAHI anayemaliza muda wake.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la AGPAHI, Laurean
Bwanakunu (kushoto) akimkabidhi cheti cha shukrani Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga, Ally Rufunga, wakati alipokwenda kumuaga ofisini kwake baada
ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD).
BALOZI MTEULE MAKAKALA WA NCHINI ZIMBABWE AKUTANA NA DR.SHEIN
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akisalimiana na Balozi mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini
Zimbabwe Lt.Gen.Mstaafu Charles Makakala alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha leo,[Picha na Ikulu.]
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(kushoto) akifuatana na Balozi mteule wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Nchini Zimbabwe Lt.Gen.Mstaafu Charles Makakala baada ya
mazungumzo yao leo alipofika Ikulu Mjini Zanzibarkujitambulisha ,[Picha na Ikulu.]
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(kulia) akizungumza na Balozi mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Nchini Zimbabwe Lt.Gen.Mstaafu Charles Makakala alipofika kujitambulisha
Ikulu Mjini Zanzibar leo,[Picha na Ikulu.]
RAIS KIKWETE APOKEA HATI YA UTAMBULISHO WA BALOZI WA DENMARK NCHINI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kushoto)
akipokea hati ya utambulisho ya Balozi wa Denmark nchini Tamzania Einar
Hebogard Jensen (kulia) leo Ikulu jijini Dar es salaam wakati
alipokwenda kujitambulisha.
Balozi
wa Denmark nchini Tamzania Einar Hebogard Jensen akisaini kitabu cha
wageni wakati alipokuwa anaenda kukabidhi hati ya utambulisho na
kujitambulisha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya
Kikwete leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kushoto)
akisalimiana na Balozi wa Denmark nchini Tamzania Einar Hebogard Jensen
(kulia) wakati alipokwenda kujitambulisha na kukabidhi hati ya
utambulisho leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kulia)
akisalimiana na Balozi wa Denmark (kushoto) nchini Tamzania Einar
Hebogard Jensen mara baada ya kukabidhi hati ya utambulisho leo Ikulu
jijini Dar es salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kulia)
akibadilishana mawazo na Balozi wa Denmark nchini Tamzania Einar
Hebogard Jensen (kushoto) wakati alipokwenda kujitambulisha na kukabidhi
hati ya utambulisho leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Balozi
wa Denmark nchini Tamzania Einar Hebogard Jensen (kulia) akisalimiana
na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Dkt.
Maadhi Juma Maalimu (wa pili kushoto) leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Balozi
wa Denmark nchini Tamzania Einar Hebogard Jensen (katikati mstari wa
mbele) akiwa amesimama wakati nyimbo za taifa za Tanzania na Denmark
zikiimbwa leo Ikulu jijini Dar es salaam alipokwenda kujitambulisha kwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete.
Bendi
ya Jeshi la Polisi nchini ikipiga nyimbo za taifa za Tanzania na
Denmark wakati Balozi wa Denmark nchini Tamzania Einar Hebogard Jensen
(katikati mstari wa mbele) alipokuwa anakwenda kujitambulisha kwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
PINDA ATETA NA WAZIRI MKUU WA UGANDA
*Asema Tanzania kuadhimisha miaka 100 ya Maskauti mwaka 2017
……………………………………………………………
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda
amekutana na Waziri Mkuu wa Uganda, Dk. Ruhakana Rugunda na kufanya naye
mazungumzo kuhusiana na masuala mbalimbali yahusuyo nchi hizi mbili.
Akizungumza na mwenyeji wake jana
jioni (Alhamisi, Agosti 20, 2015), kwenye kikao kilichofanyika Ofisi ya
Waziri Mkuu wa Uganda jijini Kampala, Waziri Mkuu alisema amefurahishwa
na juhudi zinazofanywa kwenye mipaka ya nchi hizo mbili na hasa mpaka
wa Mutukula.
“Nimearifiwa kwamba juhudi za
ujenzi wa one-border-post pale Mtukula zinaendelea vizuri. Tunachotakiwa
kufanya kwa sasa ni kuangalia kwa kiasi gani tunaweza kutumia kituo
hiki kama fursa ya kukuza biashara baina ya nchi zetu mbili,” alisema.
Alisema masuala ya kuimarisha
uchumi ni ya msingi na hayana budi kupewa kipaumbele katika kipindi hiki
cha sasa. “Kikubwa ni kwa nchi zetu kuendelea kuimarisha amani iliyopo
kwa faida ya wananchi wake, maana bila amani hakuna kitakachofanyika,”
alisema.
Waziri Mkuu Pinda alitumia fursa
hiyo kumtakia heri yeye na wananchi wa Uganda wakati wakijiandaa kufanya
Uchaguzi Mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika Februari, 2016.
Pia alimwalika Waziri Mkuu wa Uganda aje kutembelea Tanzania pindi apatapo nafasi ya kufanya hivyo.
Naye Waziri Mkuu wa Uganda, Dk.
Rugunda alisema nchi yake bado inatambua na inathamini mchango wa
Tanzania katika kuleta amani nchini mwao.
“Tanzania itaendelea kukumbukwa
na Waganda kwa mchango mlioutoa katika harakati za kuikomboa Uganda
kutoka kwenye makucha ya Iddi Amin Dada. Maneno aliyokuwa akiyasema
mwalimu Nyerere bado yamo akilini mwetu na yanaendelea kuishi mioyoni
mwa Waganda wengi,” alisema.
“Waganda wengi wanaiona Tanzania
kama ni nyumba yao ya pili (second home) na wanafurahia wanapokuja huko
akiwemo Rais wetu, Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni. Sote tunathamini
mchango wa Tanzania na tutaendelea kuuezi,” alisema Dk. Rugunda.
Alisema yeye binafsi anafurahi
kwamba Tanzania na Uganda zimeunganishwa kwa njia ya kieletroniki
(mtandao na mawasiliano ya simu); lakini akaongeza kuwa kiasili, nchi
hizo zimeunganishwa kwa njia ya barabara na maji kupitia Ziwa Victoria
na kwamba ana imani uhusiano uliopo utaendelea kudumu vizazi na vizazi.
Wakati huohuo, Waziri Mkuu
amesema Tanzania itaadhimisha miaka 100 ya Chama cha Maskauti cha
Tanzania ifikapo Agosti, 2017. “Hivi sasa tunao maskauti wapatao 800,000
nchi nzima lakini lengo letu ni kufikisha maskauti milioni moja ifikapo
mwaka 2017 kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 nchini kwetu,”
alisema.
Waziri Mkuu Pinda aliwasili
nchini Uganda Jumatano usiku kwa ziara ya siku moja akimwakilisha Rais
Jakaya Kikwete kwenye maadhimisho ya miaka 100 ya Chama cha Maskauti cha
Uganda (Uganda Scouts Association – USA). Amerejea nchini jana usiku.
Rais Yoweri Museveni ndiye mlezi wa chama hicho na alikuwa amemwalika Rais Kikwete kwenye maadhimisho hayo.
Subscribe to:
Posts (Atom)