Rais Malinzi, alifungua kikao kwa ajenda ya kumuengua Angetile na Wajumbe wakaafiki, lakini wanamng’oa kistaarabu.
Angetile amepewa likizo ya hadi atakapomaliza Mkataba wake mwezi ujao na kwa sasa, aliyekuwa Ofisa Habari wa shirikisho hilo, Boniface Wambura Mgoyo atakatimu nafasi yake.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamati
ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemteua Bw.
Boniface Wambura kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF. Uteuzi huo ni kuanzia
Novemba 2 mwaka huu.
Aidha aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah ameagizwa aende likizo ya malipo hadi atakapomaliza mkataba wake.
Kamati
ya Utendaji inaviomba vilabu, vyama vya wilaya, vyama vya mikoa, vyama
shiriki na wadau wote kumpa ushirikiano Bw. Boniface Wambura katika
utekelezaji wa majukumu yake.
Jamal Malinzi
Rais, Dar es Salaam
Novemba 3, 2013