WIKI YA AZAKI 2024 KUIMARISHA USHIRIKIANO BAINA YA SERIKALI NA WADAU WA MAENDELEO

WIKI YA AZAKI 2024 KUIMARISHA USHIRIKIANO BAINA YA SERIKALI NA WADAU WA MAENDELEO

August 23, 2024










Na: Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM

Washiriki zaidi ya 500 kutoka Asasi za Kiraia (AZAKI), Sekta Binafsi, Serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo wanatarajiwa kushiriki maadhimisho ya Wiki ya AZAKI 2024, itakayofanyika kuanzia Septemba 9 hadi 13 Jijini Arusha.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Agosti 23, 2024 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa The Foundation for Civil Society (FCS), Justice Rutenge, amesema kuwa, wiki hiyo imebebwa na kauli mbiu ya Sauti, Dira na Thamani, ikiendana na wakati uliopo na matukio yanayoendelea nchini, ambayo ni pamoja na uchaguzi wa Serikali za mtaa utakaofanyika mwaka huu, uchaguzi mkuu wa mwakani na Dira ya Taifa ya Maendeleo.

“Tupo kwenye kipindi muhimu sana kwenye demokrasia yetu kama nchi, kwa sababu mwaka huu tuna uchaguzi wa serikali za mtaa, wote mnafahamu, pia mwakani tuna uchaguzi mkuu, lakini la jambo la kipekee sana, mwakani tunatarajia kuzindua dira ya maendeleo ya Taifa ya 2050 ambayo ni fursa adimu sana inayokuja mara moja kwa muda mrefu. Fursa hii kutokana na umuhimu wake si budi sauti za wananchi zikasika kuchangia maoni yao wenye, kwani dira ya Taifa inapaswa itokane na sauti, mawazo, mitazamo na maoni ya wananchi”. Amesema Rutenge.

Aidha, Rutenge ameongeza kuwa, wiki hiyo pia itakuwa na mijadala mbalimbali inayohusu shughuli za AZAKi nchini, maendeleo ya jamii na ushirikiano baina ya Asasi za Kiraia, Serikali na sekta binafsi.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kimataifa linaloshughulika kusaidia na kuwezesha watu wenye ulemavu wa macho nchini (CBM), Nesia Mahenge, ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya wiki ya AZAKi 2024, amesema kuwa kuelekea katika wiki hiyo maandalizi yamekamilika, ambapo amewashukuru wadau wote waliojitokeza kudhamini na kuwezesha maadhimisho hayo.


Aidha, Mahenge ameeleza kuwa, katika wiki hiyo itayaleta pamoja makundi mbalimbali ikiwemo vijana, jamii, makundi maalum na wadau mbalimbali watakaojadiliana kwa pamoja mada zinazohusiana na kaulimbiu ya maadhimisho hayo.

Maadhimisho ya wiki ya AZAKi 2024 ni ya sita kufanyika tangu kuanzishwa kwake mwaka 2018.
RAIS WA ZANZIBAR ALHAJJ DK.HUSSEIN MWINYI AZUNGUMZA NA VIONGOZI WA BARAZA LA MAULAMAA ZANZIBAR IKULU LEO

RAIS WA ZANZIBAR ALHAJJ DK.HUSSEIN MWINYI AZUNGUMZA NA VIONGOZI WA BARAZA LA MAULAMAA ZANZIBAR IKULU LEO

August 23, 2024

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Uongozi wa Baraza la Maulamaa Zanzibar, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 23-8-2024, na (kushoto kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi na (kulia kwa Rais) Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Othman Hassan Ngwali.(Picha na Ikulu) 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Baraza la Maulamaa Zanzibar,baada ya kumaliza mazungumzo , walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha leo 23-8-2024, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)

Rais Samia amesikiliza kilio cha wakazi wa Ngorongoro.

August 23, 2024

 Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza kurejeshwa kwa huduma za kijamii ikiwemo za elimu na afya zilizokuwa zimesitishwa katika Tarafa ya Ngorongoro.


Hayo yamesemwa leo Ijumaa Agosti 23, 2024 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri (Sera, Bunge na Uratibu), William Lukuvi akizungumza na wananchi wa kata 11 zilizopo Tarafa ya Ngorongoro, akiwasilisha maagizo ya Rais aliyewatuma kuwasilikiza wananchi hao waliokuwa wamekusanyika na kukesha kwa siku 5 wakitaka kujua hatima ya malalamiko yao.

Aidha amesema Rais ameagiza uchaguzi katika tarafa hiyo kwa kutumia mipaka ya zamani, ufanyike kama unavyofanyika maeneo mengine nchini.



Furahia Kila Ushindi na Pilsner Mbili

August 23, 2024

Pilsner Lager inakuletea kampeni mpya kabisa ya "Furahia Kila Ushindi na Pilsner Mbili"