"MICHEZO INAWEZA KULETA TIJA KUBWA KUONGEZA UFANISI KAZINI"

December 15, 2016
 MKURUGENZI wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko akizungumza leo wakati akifungua mashindano ya tano ya  Bandari nchini (Interports) kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly kushoto kwake ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,Donald Ngaire kushoto ni Mkurugenzi Rasilimali Watu TPA,Getrude Maseko
 Mkurugenzi Rasilimali Watu TPA,Getrude Maseko akitoa neno wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo
 Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,Donald Ngaire wa kwanza kushoto ni  MKURUGENZI wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko na Mkurugenzi Rasilimali Watu TPA,Getrude Maseko
  PRO wa Mamlaka ya Bandari ya Tanga,Moni Jarufu akitoa maelekezo wakati wa ufunguzi wa mashindani hayo leo
 MKURUGENZI wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko akiteta jambo na watumishi wa Bandari ya Tanga kabla ya kuzindua mashindano ya Bandari
 MKURUGENZI wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko akikagua timu za mpira wa miguu zinazoshiriki mashindano hayo
  MKURUGENZI wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko akikagua timu za mpira wa miguu zinazoshiriki mashindano hayo
  MKURUGENZI wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko akikagua timu za mpira wa miguu zinazoshiriki mashindano hayo katikati akifurahia jambo na waamuzi wa mpira wa pete wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo

Wachezaji wa timu ya Makao Makuu ya Bandari Tanzania wakipita na bango lao kwa mgeni rasmi

TIGO YAZINDUA DUKA LA 'TEAM LEADERS' DEVIS CORNER TANDIKA TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM ILI KUKUZA UJASIRIAMALI

December 15, 2016
 Msimamizi wa Biashara wa Kampuni ya Simu Tigo Dar es Salaam na Zanzibar, Nderingo Materu (wa pili kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa  duka dogo la Tigo Tandika Devis Corner leo.  Kutoka kulia ni Meneja Mauzo wa Tigo Wilaya ya Temeke, Fadhila Saidi, Mwendeshaji wa duka hilo, Khadija  Matambo na kushoto ni Meneja Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo, Isack Shoo.
 Hawa ndio waendeshaji wa duka hilo. Kutoka kushoto ni Victor Juma, David Ngwale na kiongozi wao Khadija Matambo.
 Meneja wa Tigo Uendeshaji wa huduma za Wateja , Isaack Shoo akihojiwa na wanahabari.
 Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa duka hilo.


Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya  Tigo inayoongoza kwa maisha ya kidijitali Tanzania,  leo imezindua rasmi mpangbo mdogo wa maduka ya huduma kwa wateja  unaofahamika  kama maduka ya Team Leaders ambayo  yatatoa huduma za kampuni  moja kwa moja kutoka maeneo wanayokaa wateja. 

Kwa mujibu wa Meneja wa Tigo Uendeshaji wa huduma za Wateja , Isaack Shoo maduka hayo kimsingi yatakuwepo katika maeneo ya makazi  na yatatoa huduma zote  za Tigo na miongoni mwake ni pamoja na  kurudisha  kadi za simu  zilizopotea, mauzo ya muda wa maongezi, huduma za Tigo Pesa, mauzo ya kadi za Tigo na mauzo ya simu za kisasa (Smartphones).

Katika mkutano huo wa waandishi wa habari  uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Shoo alisema, “Kupitia maduka ya team leaders Tigo imejikita kuhakikisha kuwa bidhaa zakehuduma zake zimo karibu na  wateja, kuwezesha wateja wetu  kufurahia huduma  namba moja  ambayo  imo moja kwa moja  katika kujikita  kwetu  katika mabadiliko ya kuboresha mtindo wa maisha ya kidijitali.”

Shoo alisema kuwa kila  duka litakuwa na mawakala watano wa  huduma kwa mteja  ambao watakuwa wamepata mafunzo  yanayohusiana na huduma kwa mteja  kutoka Tigo  ili kukidhi mahitaji ya wateja.

Aliongeza kuwa hadi sasa maduka  yapo maduka matano  ambayo yapo Mbande, Tandika, Tabata, Segerea na  Ukonga (yote yapo Dar es Salaam) na tayari yanafanya kazi. 

Shoo aliongeza, “Maduka zaidi yanatarajiwa kuanzishwa  jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki  ambapo yatakuwa katika maeneo ya Kawe, Mawasiliano Towers, Kimara, Kigogo na Mwananyamala.”

Mbali na mafunzo Tigo pia itatoa  vifaa  muhimu kwa ajili ya biashara kwa mawakala wake katika hatua ya mwanzo ya kuanzisha biashara  katika maduka, jambo ambalo ni muhimu na linalothibbitisha  kujikita kwa kampuni hiyo ya simu katika  kuisaidia serikali  kstiks juhudi zake za kiupunguza  ukosefu wa ajira nchini.

Hivi sasa Tigo ina maduka maduka makubwa 50  kwa ajili ya huduma kwa wateja yaliyoasambaa  kote nchini  yakiwa na uwezo wa kuhudumia wateja kati ya 200 na 300 kwa siku.


BODI YA FILAMU NCHINI YAENDELEA KUWANOA WANATASNIA WA FILAMU MKOANI MARA.

December 15, 2016
Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba, akiongozana na Naibu Katibu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi.Nuru Milla pamoja na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fisso, kwenye ufunguzi wa Mafunzo ya siku tatu kwa Wanatasnia wa Filamu na michezo ya kuigiza mkoani Mara, yaliyoanza jana kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari Mara Mjini Musoma.

Mafunzo hayo yamelenga kukuza weledi kwa wazalishaji wa filamu na maigizo ikiwemo kuzingatia uandishi bora wa miswada ili kuendana na ushindani wa soko la ndani na nje ya nchi.
#BMGHabari
Naibu Katibu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi.Nuru Milla (kulia) akiteta jambo na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fisso, kwenye ufunguzi wa Mafunzo ya siku tatu kwa Wanatasnia wa Filamu na michezo ya kuigiza mkoani Mara.
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fisso (kushoto), pamoja na Kaimu Afisa Utamaduni mkoani Mara, Shekudadi Said (kulia), wakiwa kwenye ufunguzi wa Mafunzo ya siku tatu kwa Wanatasnia wa Filamu na michezo ya kuigiza mkoani Mara.
Naibu Katibu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi.Nuru Milla (kulia), Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fisso (kushoto) pamoja na wanatasnia wa filamu na maigizo mkoan Mara wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo.
Mmoja wa Wakufunzi wa mafunzo hayo, Richard Ndunguru kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam idara ya Sanaa, akitoa mafunzo kwa wanatasnia wa filamu na maigizo mkoani Mara. Amewapa miongozo bora kuhusiana na uandishi wa miswada ya filamu, upigaji wa picha mnato pamoja na nyongevu kwa ubora zaidi ili kuongeza mvuto wa kazi zao.
Wanatasnia wa filamu na maigiozo mkoani Mara, wakifuatilia kwa umakini mafunzo kutoka kwa Richard Ndunguru ambaye ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam idara ya Sanaa.
Wanatasnia wa filamu na maigiozo mkoani Mara, wakifuatilia kwa umakini mafunzo hayo.
Wanatasnia wa filamu na maigiozo mkoani Mara.
Wanatasnia wa filamu na maigiozo mkoani Mara wakiwa kwenye mafunzo ya filamu na maigizo mkoani humo, yanayotolewa na Bodi ya Filamu nchini.
Taswira ndani ya ukumbi wa mafunzo hayo.
Soma Zaidi HAPA

UNICEF YAADHIMINISHA MIAKA 70 TANGU KUANZISHWA, SERIKALI YAIPONGEZA KWA KUSAIDIA WATOTO

December 15, 2016
Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) limeadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa (1946-2016) likiwa na kauli mbiu ya Kwa Kila Mtoto, Tumaini. Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Bi. Maniza Zaman alisema shirila lao kwa kipindi cha miaka 70 limekuwa likifanya kazi za kuwasaidia watoto ambapo malengo yao ni kuhakikisha watoto wanaishi maisha bora na kuwawezesha kufikia malengo ambayo wanatamani kuyafikia. 
Mwakilisha wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini, Bi. Maniza Zaman akielezea kazi ambazo UNICEF imekuwa ikizifanya kwa miaka 70 tangu kuanzishwa na mafanikio ambayo wameyapata.

"Hii ni siku muhimu kwetu kufikisha miaka 70, ni muhimu kwa sababu ya malengo ambayo yamewekwa ya kujenga dunia ambayo kila mtoto atapata haki zake za kimsingi bila kumuacha hata mmoja nyuma ni muhimu sababu ya uwepo wenu kujadili umuhimu wa watoto ambao utatoa matumaini mapya kwa kila mtoto Tanzania, "Kwa miaka 70 UNICEF imekuwa ikiwatetea watoto, kwa pamoja tukishirikiana na wadau wetu kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha tunaboresha maisha ya kila mtoto duniani kote. Mpango wetu upo wazi kuwa kuhakikisha kila mtoto anapata nafasi ya kufikia malengo yake," alisema Zaman. Nae Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema UNICEF ni washirika wazuri wa serikali kutokana na programu ambazo wamekuwa wakitoa kwa watoto na kuwaomba kuendelea kushirikiana na serikali ili kuboresha maisha ya watoto nchini. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza faida ambazo Tanzania imepata kutokana na uwepo wa UNICEF nchini pamoja na kumshukuru Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi kwa kusaini mkataba ambao uliwaruhusu UNICEF kuingia nchini kwa ajili ya kuwasaidia watoto.

"Serikali ya Tanzania itaendelea kulinda na kutetea haki za watoto na katika utekelezaji wa hili tunawashukuru sana UNICEF kwa programu ambazo wamekuwa wakizifanya, watoto wa Tanzania wamefaidika sana na programu ambazo UNICEF mnazitoa na serikali itaendelea kushirikiana na UNICEF kuwasaidia watoto nchini," alisema Mwalimu. Kwa upande wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN), Alvaro Rodriguez alisema UNICEF imesaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha maisha ya watoto duniani kote tangu ilipoanzishwa na kupitia mpango wa SDGs ni matumaini ya UN kuwa serikali ya Tanzania kwa kushirikiana nanyi zitaendelea kushirikiana ili kuwasaidia watoto. 
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN), Alvaro Rodriguez akielezea jinsi UNICEF ambavyo natekeleza mipango ya Umoja wa mataifa kwa kuanza na mpango wa kwanza wa Millenium Development Goals (MDGs) ambao ulimalizika mwaka 2015 na mpango wa sasa wa maendeleo endelevu (Sustainable Development Goals - SDGs).

"Mchango wa shirika hili la watoto ni mkubwa, muhimu na wenye thamani kubwa sana katika dunia ya leo na kesho, kwa miaka 15 iliyopita tulikuwa na mpango wa MSDs ambao ulishughulikia changamoto ambazo zinawakabili watoto na sasa kuna mpango wa SDGs ambao tumekusudia ufanye mageuzi makubwa kwa maendeleo ya baadae ya binadamu wakiwepo watoto, na Tanzania kama mwanachama wa UN ina wajibu wa kuhakikisha inafanikisha hilo," alisema Rodriguez. 
Rais wa pili wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi akitoa pongezi kwa UNICEF kwa kazi ambazo wanafanya za kuwasaidia watoto ili waishi katika mazingira bora.

Nae mgeni wa heshima katika maadhimisho hayo, Rais wa pili wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi aliipongeza UNICEF kwa kufikisha miaka 70 na kusema kuwa "Nilihusika kukubali UNICEF kufanya kazi nchini na leo sijuitii hilo kwa kazi ambayo mnaifanya, niwatie moyo muendelee na kufanya kazi kwa kuwasaidia watoto." 
Baadhi ya watu waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 70 ya kuanzishwa shirika la UNICEF.

MASHINDANO YA SCOUT KANDA YA AFRIKA MASHARIKI YAFANYIKA ARUSHA

December 15, 2016






Skauti wa TZ na wengine wa nchi za Afrika Mashariki wakipita
mbele ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa kambi ya mashindano ya
skauti nchi za afrika mashariki inayoendelea mkoani Arusha
Skauti Tz na wengine kutoka nchi za afrika mashariki
wakimsikiliza mgeni rasmi wakati wa ufunguzi rasmi wa kambi ya
mashindano inayoendelea mkoani Arusha
Skauti kutoka Kenya na wengine wa nchi za Afrika Mashariki
wakipita mbele ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa kambi ya
mashindano ya skauti nchi za afrika mashariki inayoendelea mkoani
Arusha
.


Na Woinde Shizza,Arusha
Vyama vya scout kanda ya Afrika Mashariki vimekutana mjini hapa kuanza mashindano ya  mascout  yenye lengo la kuwezesha vikosi vya scout kushindana pamoja ili kujipima katika utekelezaji wa programu ya vijana ya stadi za kiscout katika vikosi na jumuiya ya afrika mashariki ambazo
wamekuwa wakijifunza katika maeneo yao.

Akizungumza katika mashindano hayo yalioanza jana meneo ya kisongo jijini hapa,kamishna mkuu wa chama cha skauti tanzania Rashidi Mchata alisema kuwa mashindano hayo yameshirikisha  vijana wa kiscout kutoka nchi tano za
jumuiya ya afrika mashariki.

Mchata alisema kuwa mashindano hayo yatahusisha makundi ya mascout wadogo ,mascout wakubwa na masouti vijana  kutoka kila nchi yatashindana kutengeneza stadi za kiskauti kwa kutumia mbinu zao ambazo wamekuwa
wakifundishwa katika vikosi vyao   kwa ajili ya kuwawezesha kuhudumia jamii na kuwafanya wawe wazalendo.

"Vyama vya mascout kutoka jumuiya ya afrika tumekutana hapa arusha kwa malengo matatu ikiwemo mashindano ,jukwaa la vijana mascout lakini pia
tumekuwa na mkutano mkuu wa makamishna wa skauti kutoka nchi za jumuiya na hii inasaidia kwa pamoja kuhakikisha kuwa vijana wetu wanakuwa wazalendo na
kupitia haya mashindano tutaweza kuwapata washindi ambao wanawakilisha nchi zao walizotokea"alisema Mchata.

Rehema Ramadhani mwanascout kutoka  dar es salaam ambae anawakilisha tanzania katika mashindano hayo alisema kuwa mashindano hayo yanajumuisha mambo yote waliokuwa wanafundishwa kuanzia ngazi ya wilaya na kwamba
yanawapa uzoefu wa stadi zao kutoka kwa mascout wa nchi nyingine za jumuiya ya afrika mashariki.

Alisema kuwa katika vikosi vyao wamekuwa wakifundishwa mambo mbali mbali ikiwemo utunzaji wa mazingira kama ilivyo kauli mbiu ya rais magufuli lakini pia jinsi ya kutoa huduma ya kwanza kwa mtu au jamii pale inapopata janga na hivyo wanaamini kuwa wataiwakilisha tanzania kuwa mshindi katika
mashindano

Kwa upande wake mwenyekiti wa jukwaa la vijana wa  kiscout katika jumuiya ya afrika mashariki Murtadhwa Abdallah alisema kuwa taasisi mbali mbali zinatakiwa kujitokeza na kushirikiana katika kufadhili scout kwani vyama
hivyo vimekuwa vikikabikiwa na changamoto ya fedha hivyo kushindwakujiendesha vyenyewe.
MAMBO 8 YA KUZINGATIA PINDI UNAPOTAKA KUSAFIRI

MAMBO 8 YA KUZINGATIA PINDI UNAPOTAKA KUSAFIRI

December 15, 2016

Na Jumia Travel Tanzania

HAKUNA jambo linalokera kama kugundua kuwa umesahau kitu fulani ambacho kilikuwa kina umuhimu mkubwa sana kwenye safari yako uliyokwishaianza.

Hali kama hii huwa inawatokea watu wengi hivyo kupelekea kuchelewa au wakati mwingine kuachwa kabisa na usafiri.

Kuepukana na usumbufu huu hasa ukizingatia asilimia kubwa ya watu wako kwenye pilikapilika za kusafiri kipindi hiki cha sikukuu na shamrashamra za mwaka mpya, Jumia Travel (www.travel.jumia.com) ingependa kukutahadharisha kuzingatia yafuatayo ili safari yako iwe ya raha mustarehe.

Tafiti kuhusu mahali unapokwenda
Ni muhimu kufahamu mahali unapokwenda hasa umbali wake, itakugharimu kiasi gani kufika, hali ya hewa, gharama za maisha pamoja na mila na utamaduni za watu wanaoishi huko. Kama unasafiri mkoa ambao haujawahi kufika hapo awali ni vizuri ukafanya tafiti au ukaulizia kutoka kwa marafiki, ndugu na jamaa ili usiende kupata tabu ukifika.

Tambua usafiri utakaokufikisha huko
Zipo njia nyingi za usafiri za kuweza kukufikisha mahali unapotaka inategemea chaguo, uharaka au uwezo ulionao. Kama unataka kuwahi mahali unapokwenda kutokana na shuguli nyingi au kuepuka uchovu basi usafiri wa anga (ndege) utakuwa ni sahihi kwako. Na kama hautojali kuwahi au uchovu njia ya barabarani kwa kutumia basi itakufaa kwani utaweza kuwa na muda wa kutosha kujionea vitu vingi njiani vitakavyopelekea kunogesha safari yako.

Kata tiketi mapema siku moja kabla ya safari
Usipendelee kukata tiketi siku ya safari kwani unaweza kukuta usafiri haupatikani, nafasi zimejaa, bei imebadilika au kupata basi ambalo halikuridhisha na hadhi yake. Kata tiketi siku moja kabla ya safari kwani itakuondolea hofu ya kutokuwa na uhakika wa kusafiri na kukupa muda wa kupanga mambo mengine vizuri zaidi.

Panga vitu unavyovihitaji kwa ajili ya safari mapema
Kutojipanga mapema na safari mara nyingi hupelekea mtu kusafiri huku akiwa ameacha vitu muhimu huko mbele aelekeapo. Na kamwe usijidanganye kwamba utaweza kumudu kukumbuka na kupanga vitu vyako vyote unavyovihitaji siku ya safari kwani unaweza ukachelewa kuamka na ukahamaki mwishowe ukajikuta unasahau kubeba vitu vya msingi. Hivyo tunakushauri weka kila kitu unachokiona ni muhimu kwa safari yako ndani ya begi siku moja kabla ya safari bila ya kusahau kuiweka tiketi yako sehemu ambapo unaiona kwa urahisi.

Fahamu mahali utakapolala pindi utakapowasili
Siku hizi huhitaji kusumbukaili kufahamu sehemu ya malazi kwa sababu taarifa zote zinapatikana kwa njia ya mtandao. Kwa mfano, ukitembelea mtandao wa Jumia Travel (www.travel.jumia.com) utaweza kuperuzi orodha ya hoteli na sehemu mbalimbali za malazi nchini, utafahamu mahali ziliko, hadhi zake, gharama, upatikanaji na namna ya kulipia.

Amka mapema na wahi kituoni siku ya kusafiri
Kama una mazoea ya kuchelewa kuamka asubuhi ni vema ukaweka kengele ikuamshe asubuhi kupitia simu au kifaa ulichonacho au kumtaafiru ndugu au rafiki akuamshe mapema. Kuamka mapema kunakuwezesha kujiandaa vya kutosha kwa safari hata kukupa kuda wa kukumbuka vitu ambavyo pengine ulivisahau pamoja na kuwahi kituoni tayari kwa kusafiri.

Kuwa makini na vyakula unavyokula njiani
Huna budi kuzingatia aina ya vyakula utakavyokuwa unakula njiani kwani vinaweza kukudhuru kiafya. Vyakula vinavyopikwa na kuuzwa njiani huna uhakika vinaandaliwa vipi na kupikwa katika mazingira gani hivyo umakini mkubwa unahitajika. Hata hivyo, kutokana na maboresho ya miundombinu siku hizi safari nyingi hazichukui muda mrefu kwa hiyo unaweza ukala vyakula vikavu kama vile keki au mikate pamoja na vinywaji kama maji, soda au juisi mpaka utakapofika ndipo ule chakula cha kutosha.

Jihadhari usiachwe na basi njiani
Kuna matukio kadhaa ambapo abiria huachwa na usafiri hususani kwenye vituo vifupi vinavyowekwa njiani kuwapa fursa abiria kujisaidia au kununua chakula. Kama unajijua ni mzito kula kituoni ni vema ukanunua, ukabeba chakula na kwenda kulia ndani ya basi vilevile kwa kujisaidia nakushauri jisaidie mahali ambapo utaliona basi au abiria unaosafiri nao ili isiwe rahisi kuachwa.

Tunatumaini kwamba mbinu hizi chache zitakusaidia pakubwa katika safari yako unayoitarajia msimu huu wa sikukuu.

IOP WAMEMA NDOA ZA UTOTONI ZINAZIDI KUONGEZEKA MKOANI IRINGA

December 15, 2016
 hawa ni baadhi ya wananchi wa kabila la kimasai ambalo linakaliwa na tuhuma za kuozesha wasicha wenye umri mdogo.
hili ni jengo la shirika lisilo la kiserikali la Ilula Ophan program (IOP)

na fredy mgunda,Iringa
Shirika lisilo la kiserikali la Ilula Ophan program (IOP) limeendelea kukemea na kutoa elimu juu ya ndoa za utotoni kwa kuwa zinarudisha maendeleo nyuma ya wasichana wa jamii ya kimasai.

Akizungumza na blog hii Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Ilula Ophan program (IOP) Edson Msigwa alisema kuwa tatizo la ndoa za utotoni katika kabila la wamasai bado ni kubwa.

Msigwa alieleza jinsi gani wanavyofanya shughuli za kukemea na kutoa elimu juu ya ndoa za utotoni katika jamii ya wamasai

“Tunajitahidi kuwafikia jamii zote za wilaya ya kilolo mkoani iringa kwa lengo la kutoa elimu lakini tunakumbana na changamoto kutoka kwa wazazi ambao bado wana mila potofu hasa huku umasaini”alisema Msigwa

Aidha Msigwa alisema kuwa kila siku ndoa za utotoni zinaongezeka huko vijijini  na kuitaka serikali kukubali takwimu wanazozitoa kwa kuwa zinaukweli.

“Sisi hapa Ilula Ophan program (IOP) tunaishi na wasichana wa kabila la kimasai wafanikiwa kukimbia kuozeshwa wakiwa na umri mdogo hebu mwangalie huyo motto joyce alivyo alitakiwa aolewe na umri huu wa miaka kumi nan ne je unafikiri ni haki jamiii inatakiwa kubadili na serikali inatakiwa kuongeza juhudi kulitatua hili”alisema Msigwa

Naye mmoja wa wasichana wa kimasai aliyekimbia kuolewa akiwa na umri mdogo Joyce Hassani alisema kuwa msichana wa kimasai wakimaliza elimu ya msingi wanalazimishwa kuolewa na familia yake.

“Mimi na mwenzangu tumemaliza shule tu wametupeleka kucheza ngoma kisha kutaka kutuozesha lakini mungu mwema tulifanikiwa kukimbia na kufika hapa Ilula Ophan program (IOP) japo kuwa wanaume wa kimasi wanakuja hapa kituoni mara kwa mara kutaka kutuiba turudi kule umasaini ili tukaolewe hasa kaka zangu”alisema joyce

Joyce ameiomba serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali kusaidia kupambana na mila potofu zinazowapotezea malengo wasichana wa kimasai.

“Angalia tunavyoteseka saizi tunaishi kama watoto yatima wakati wazazi wetu wapo na wana afya zuri kabisa lakini tatizo kubwa sisi wasichana wadogo wa kimasai tunaolewa tukiwa na umri mdogo sana tunaomba jamii iamuke na kutusaidia kutatua tatizo hilo.”alisema Joyce

Zipo sababu nyingi na ushahidi mwingi wa kisayansi, unaonyesha kuwa, ndoa na mimba katika umri mdogo ni hatari kwa afya na mstakabali wa maisha yake na mtoto wake.

Wasichana wanaopata ujauzito na kujifungua katika umri mdogo wengi wao pia hupata tatizo la fisitula - Vescovaginal fistula.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na chama cha waandishi wahabari wanawake (TAMWA) umeonesha kuwa katika mwaka 2012-2013 matukio 228 ya mimba na matukio 42 ya ndoa za utotoni yaliripotiwa nchini tanzania.

UNESCO YAFANYA UZINDUZI WA KOZI YA MAADILI KWA WALIMU WA VYUO VYA AFYA NA SAYANSI

December 15, 2016
Shirika la Umoja wa Matifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limefanya uzinduzi wa kozi ya maadili kwa walimu ambao wanafundisha vyuo vya afya na sayansi kutoka ndani na nje ya nchi. Akizungumza katika ufunguzi wa kozi hiyo, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO, Zulmira Rodrigues alisema UNESCO imeandaa kozi hiyo ili kuwajengea uwezo kuhusu maadili mema ya kazi walimu hao ili hata wanafunzi wanaowafundisha wawe na maadili mema sasa na hata baada ya kuhitimu masomo yao. 

Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO, Zulmira Rodrigues akitoa neno la ufunguzi katika kozi ya siku nne kwwa walimu wa vyuo vya afya wa ndani na nje ya nchi.

"Kwenu wanufaika wa kozi hii ambao itafanyika kwa siku nne, ni matumaini yangu kozi hii ya siku nne itatumika kikamilifu katika maisha yenu ya kila siku, ikiwa kama ni mkufunzi, mwanafunzi au katika tafiti zenu za kisayansi, na utakuwa balozi wa UNESCO kwa kusambaza elimu kwa wengine, "Jambo la muhimu ni kujenga uelewa ili kuhakikisha kama nchi inapambana na changamoto kubwa za kimaadili ambazo zinaikabili kwa sasa na baadae. UNESCO itaendelea kushirikiana na Muhimbili na wadau wengine wa ajili ya kusaidia Tanzania," alisema Zulmira. 
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO, Zulmira Rodrigues akizungumza na washiriki wa kozi ya maadili kwa walimu wa vyuo vya afya.

Kwa upande wa Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi cha Muhimbili, Prof. Ephata Kaaya alisema mafunzo hayo ni muhimu kwa walimu hao na kuwahakikishia kuwa kila mshiriki hataondoka bure kwani watapewa mafunzo na wakufunzi wenye uwezo mkubwa. "Niwahakikishie washiriki wote wa kozi hii ambao mnatoka ndani na nje ya nchi kuwa mafunzo haya yatawaongezea uelewa kuhusu maadili mema, hili tatizo sio la Tanzania pekee hata Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda wote wanakabiliwa na hili tatizo kama ilivyo kwetu," alisema Prof. Kaaya. 
Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi cha Muhimbili, Prof. Ephata Kaaya akizungumza kuhusu kozi ya maadili kwa walimu wa vyuo vya afya na kuahidi kuwa mafunzo hayo yatakuwa bora na ambayo yatakuwa msaada mkubwa kwao.

Aidha Prof. Kaaya aliishukuru UNESCO kwa kutoa mafunzo hayo na kuwaomba kuendeleza ushirikiano uliopo kati yao. 
Baadhi ya washiriki wa kozi ya maadili ya siku nne iliyoandaliwa na UNESCO.

Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.
Click here to Reply or Forw