BREAKING NEWS : YANGA WAMTIMUA KOCHA BRANDTS

December 23, 2013



IMEWEKWA DESEMBA 23 2013
Na.
Timu ya Yanga imetangaza rasmi kumtimua kocha wake mkuu raia wa Uholanzi Ernie Brandts ikiwa ni siku chache baada ya kula kibano cha mabao 3-1 kutoka kwa mahasimu wao Wekundu wa Msimbazi Simba kwenye mchezo wa hisani wa Nani Mtani Jembe.

Akitangaza maamuzi magumu yaliyofikiwa na kamati ya utendaji Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya klabu hiyo ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya usajili Abdallah Binkleb amesema wamefikia uamuzi wa kumtimua kazi Brandts kwakuwa tayari uwezo wake ulifikia mwisho.

BOSI TRBA ATAKA UMAKAMU WA RAIS TBF.

December 23, 2013
IMEWEKWA DESEMBA 23
 Na Oscar Assenga,Tanga.
MWENYEKITI wa Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Tanga(TRBA)Hamisi Jaffary amejitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi ya Umakamu wa Rais wa Shirikisho la mpira wa Kikapu nchini (TBF) unaotarajiwa kufanyika Desemba 29 mwaka huu.

Akizungumza jana,Jaffary alisema ameamua kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo kwa lengo la kuleta mabadiliko kwenye mchezo huo kwenye mikoa mbalimbali hapa nchini.

DIWANI WA CCM AFARIKI KWA AJALI YA PIKIPIKI YAKE SHINYANGA

December 23, 2013

IMEWEKWA DESEMBA 23.SHINYANGA, Tanzania 
DIWANI wa Kata ya Nyida wilayani Shinyanga kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Shindiko Masele(40) amekufa papo hapo baada ya kupinduka na pikipiki aliyokuwa akiendesha.
Akizungumza na waandishi wa habari Mjini hapa, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Sosteness Ngassa alisema diwani huyo alipata ajali hiyo juzi saa 2.30 usiku wakati alipojaribu kumkwepa mwendesha baiskeli na kusababisha pikipiki yake kupoteza mwelekeo na ikagonga mti uliokuwa kando ya barabara.
Ngassa alisema baada ya pikipiki hiyo kugonga mti diwani huyo alianguka chini na kufa papo hapo huku abiria aliyekuwa amebebwa aliyetambuliwa kwa jina la Silasi Ngoni alijeruhiwa kidogo kwa kupata michubuko ambapo hata hivyo alikimbizwa katika hospitali ya serikali mkoani Shinyanga alikotibiwa na kuruhusiwa.

BONANZA LA TWANGA PEPETA SUGU JANA LIVE AT LEADERS CLUB KILA JUMAPILI NI KAMA KAWA WAPO SO CHECK THEM OUT!!

December 23, 2013







WATU SABA WAKAMATWA KWA KUTUHUMIWA KUWEKA MABOMU YALIYOKUSUDIWA KULIPUA NYUMBA MBILI WILAYANI KOROGWE.

December 23, 2013
Imewekwa Desemba 23,2013 saa 2:13 mchana.
 Na Oscar Assenga,Korogwe.
JESHI la Polisi mkoani  hapa kwa kushirikiana na wakazi wa Kijiji cha Maili kumi wilayani Korogwe wamefanikiwa kuwakamata watu saba kwa tuhuma za kuhusika na kuweka mabomu  yaliyokuwa yameandaliwa tayari kwa kulipuka kwenye nyumba mbili tofauti za ibada.
Pamoja na mabomu hao watuhumiwa hao ambao majina yao yanahifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi wanatuhumiwa kuhusika na kukutwa na vifaa mbalimbali vya kutengenezea milipuko ya mabomu hayo pamoja na silaha za jadi ambazo pia zilikuwa zimefichwa katika nyumba hizo za ibada huku katika Kijiji cha Maili kumi wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.
Watu hao walikamatwa wakiwa na chupa 10 ambapo tano zilikuwa na  Petrol zikiwa na tambi zake ndani,gololi 103 ambazo hutumiwa kwa milipuko,galoni kubwa mbili zilizokuwa na lita nne za petrol,majambia,mishale yenye sumu,soksi za kuzuia uso(mask)upinde,Daftari lenye mafunzo ya kijeshi kuhusu namna kufungua na kufunga silaha.

WATU SABA WAKAMATWA KWA KUTUHUMIWA KUWEKA MABOMU YALIYOKUSUDIWA KULIPUA NYUMBA MBILI WILAYANI KOROGWE.

December 23, 2013
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Coastatine Massawe akiwaonyesha waandishi wa habari ambao hawapo pichani silaa mbalimbali zilizokuwa zikutumiwa na watuhumuiwa waliokamatwa





TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI TFF.

December 23, 2013
Release No. 212
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Desemba 23, 2013

MECHI YA MTANI JEMBE YAINGIZA MIL 422/-
Mechi ya Nani Mtani Jembe kati ya Yanga na Simba iliyochezwa juzi (Desemba 21 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 imeingiza sh. 422,611,000.

Mapato hayo ni kutokana na washabiki 52,589 waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 40,000. Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo walikuwa 19,044.

Asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa kutokana na mapato hayo ni sh. 64,466,084.75 wakati gharama za kuchapa tiketi ni sh. 7,488,000.

Mgawo mwingine ilikuwa kama ifuatavyo; kila klabu imepata sh. 117,470,066.61, asilimia 15 ya uwanja ni sh. 52,598,537.29, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 35,065,691.53 wakati gharama za mchezo zilikuwa sh. 28,052,553.22.

MALINZI, MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atakuwa na mkutano na waandishi wa habari utakaofanyika kesho (Desemba 24 mwaka huu).

Mkutano huo utafanyika saa 6 kamili mchana kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).


Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)