Benki ya CRDB yawakaribisha Wanahisa kwenye Mkutano wake Mkuu wa 28

May 16, 2023

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wapili kushoto), Kahumbya Bashige, Mjumbe wa Bodi ya CRDB Bank Burundi (wapili kulia), Katibu wa Kampuni Benki ya CRDB, John Rugambo (wakwanza kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa (wakawanza kulia) wakionyesha Taarifa ya Mwaka 2022 ya Benki ya CRDB wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuwakaribisha wanahisa wa benki hiyo katika Mkutano Mkuu wa 28 utakaofanyika siku ya jumamosi ya tarehe 20 Mei 2023. Picha zote na Othman Michuzi.
---
Arusha 16 Mei 2022 - Benki ya CRDB inatarajia kufanya Mkutano Mkuu wa 28 wa Wanahisa siku ya Jumamosi tarehe Mei 20 kuanzia saa 2 asubuhi katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).


Mkutano huo unafanyika kufuatana na Sheria ya Makampuni namba 212 ya mwaka 2002, ambapo kila mwaka Benki ya CRDB imekuwa ikiandaa mkutano huo unaowapa Wanahisa fursa ya kujadili masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupitisha au kuidhinisha maamuzi mbalimbali yenye maslahi kwa Benki.



Akizungumzia katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hoteli ya Mount Meru jijini Arusha, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay amesema mkutano huo utafanyika kwa njia mseto “Hybrid Meeting” ili kutoa fursa kwa wanahisa wengi zaidi kushiriki kwa njia ya kidijitali.


Dkt. Laay alisema katika Mkutano Mkuu wa 27 wa Wanahisa waliadhimia Mkutano wa 28 wa ufanyike Makao Makuu ya Benki ya CRDB jijini Dar es Salaam, lakini kwa kuzingatia mkakati mpya wa Benki wa 2023-2027, Bodi ya Wakurugenzi ilipitia na kuidhinisha mabadiliko ya eneo la Mkutano kwenda Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) jijini Arusha.


“Bodi ya Wakurugenzi ilipendekeza mabadiliko hayo ya sehemu ya kufanyika Mkutano Mkuu kwa Wanahisa wanaomiliki zaidi ya 50% kulingana na Katiba na Mkataba wa Benki (MEMARTS) na Sheria ya Makampuni Na. 12 ya 2002, na Wanahisa walikubali mabadiliko haya,” alisema Dkt. Laay huku akiwakaribisha wanahisa katika Mkutano huo.

Dkt. Laay alisema Mkutano huo pia utafanyika kupitia mtandaoni Wanahisa wataweza kujiunga kuanzia saa 2:00 asubuhi kupitia link https://escrowagm.com/crdb/login.aspx au kupitia SimBanking App, ambapo imewekwa sehemu ya ya kujisajili kushiriki Mkutano Mkuu.

“Tumeweka muongozo wa jinsi ya kushiriki mkutano mkuu kwa njia ya mtandao kupitia tovuti yetu ya www.crdbbank.co.tz, mitandao yetu ya kijamii, lakini pia maelekezo yametumwa kwa ujumbe mfupi kwa Wanahisa,” alisema Dkt. Laay huku akiwahakikishia kuwa Benki hiyo vizuri katika kuhakikisha wanashiriki bila chanagamoto yoyote.

Mkutano Mkuu wa 28 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB utatanguliwa na semina maalum kwa wanahisa na umma yenye kauli mbiu ya “Ushirika wa Serikali na Benki ya CRDB kuwezesha Vijana na Wanawake kupitia programu ya IMBEJU”. Semina hiyo ambayo pia itaambatana na maonyesho ya vijana wabunifu itafanyika siku ya Ijumaa tarehe 21/05/2022 kuanzia saa 3 asubuhi katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).

Mgeni Rasmi katika semina hiyo anatarajiwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mh. Mwigulu Nchemba ambapo mada mbalimbali zitawasilishwa na wataalamu wa masuala ya fedha, sheria na uwekezaji katika masoko ya mitaji.

Ajenda mbalimbali zitajadiliwa katika Mkutano Mkuu wa 28 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB ni pamoja na uchaguzi wa wajumbe huru wa bodi, kuteua wakaguzi wa hesabu, na kujadili na kupokea Taarifa ya Bodi ya Wakurugenzi, na Taarifa ya Hesabu zilizokaguliwa, pamoja na gawio kwa mwaka 2022 ambapo pendekezo la gawio la Sh 45 kwa hisa litawasilishwa.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, alisema pendekeo hilo la ongezeko la gawio kwa hisa linatokana na Benki ya CRDB kuendelea kupata matokeo mazuri sokoni ambapo mwaka wa fedha ulioisha ilipata faida baada ya kodi ya Shilingi 351.4 bilioni ukilinganisha na Shilingi 268 bilioni mwaka 2021.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema katika mkutano mkuu wa 28 wanahisa wa benki hiyo watapata nafasi ya kujadili juu ya mkakati mpya wa biashara wa muda wa kati wa miaka mitano 2023 – 2027.


Mkakati huu ambao umebebwa na kaulimbiu ya “Mageuzi Tahabiti” una lenga katika kuimarisha utendaji wa Benki ya CRDB na kuifanya kuwa kinara katika ukanda wa Afrika ya Mashariki na Kati.


Nsekela alitumia fursa hiyo pia kuwahamasisha wanahisa wa Benki ya CRDB kujitokeza kwa wingi kwani ushiriki wao utaiwezesha Bodi na Menejiment kupata maoni yao ya namna bora ya kuboresha utendaji wetu.

Akielezea kauli mbiu ya Mkutano wa mwaka huu wa Wanahisa wa Benki ya CRDB ya “Mageuzi Thabiti” Mkurugenzi wa Mawasiliano wa benki hiyo, Tully Mwambapa alisema inaelezea namna inavyoimarika katika utendaji kutokana na mabadiliko ya kimkakati yanayofanywa kila mwaka na kuifanya iwe na ukuaji endelevu wenye thamani ya uwekezaji.



-- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 735 997 777 www.kajunason.blogspot.com "Everything is Possible Through Peace & Stability'' >>> DO YOUR PART TO PREVENT COVID-19: • Wash your hands frequently • Avoid touching face • Cover coughs and sneezes • Disinfect surfaces regularly • Limit handshaking • Consider postponing travel plans • Avoid large gatherings

MIFUMO MBALIMBALI YA VYOMBO VYA MOTO KUTENGENEZWA TANGA MWAKA 2024

May 16, 2023


 Mkurugenzi wa Taasisi ya TAASISI ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) Shaukatali Hussein akiendesha pikipiki inayotumia umeme
Mkurugenzi wa Taasisi ya TAASISI ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) Shaukatali Hussein akiendesha bajaji inayotumia umeme




Mmoja wa vijana walionufaika na mafunzo akiendelea na shughuli zake kama alivyokutwa
Mkurugenzi wa Taasisi ya TAASISI ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) Shaukatali Hussein  akizungumzia maendeleo ya mradi huo
Ruta Venance- ambaye ni mhitimu wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari Usagara  ambayo ni mmoja wa wanufaika na mafunzo hayo akizungumza namna yalivyomsaidia


Na Oscar Assenga, TANGA

TAASISI ya Tanzania Open Innovation Organization imesema kwamba itaanza mchakato wa kutengeneza mifumo mbalimbali ya vyombo vya moto mkoani Tanga ambavyo zitasaidia kurahisisha suala la usafirishaji

Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Shaukatali Hussein wakati akizungumza na waandishi wa habari katika shule ya Sekondari ya Tanga Ufundi ambalo kunaendelea na mafunzo kwa vijana kuhusu namna ya ubadilishaji wa pikipiki,baiskeli kwenda kwenye mfumo wa kutumia umeme.

Mafunzo hayo yanaendeshwa na Taasisi hiyo na Robotech Labs chini ya ufadhili wa Shirika la Botnar Foundation ambao wamedhamiria kutoa ujuzi kwa vijana ili waweze kujikwamua kiuchumi.

“Kwa kweli tunawashukuru Jiji la Tanga na wafadhili wetu Botnar Foundation sasa tumeweza kuwapa ujuzi vijana kuhusu namna ya kuzibadilisha pikipiki,baiskeli kutoka kwenye mfumo wa awali na kuziingiza kwenye ule wa kutumia umeme hii ni hatua kubwa Alisema

Mkurugenzi huyo aliwataka vijana kuchangamkia fursa ya kupata mafunzo hayo ambayo yatawawezesha baadae kuweza kujiajiri na hatimaye kuweza kuinua uchumi wao na jamii kwa ujumla kwani mpaka sasa ni vijana 30 katika Jiji la Tanga ndio wamenufika na mafunzo hayo na tumetembelea kata mbalimbali mwako ulikuwa ni mkubwa lakini kufika kwenye eneo hilo ni changamoto.


Mkurugenzi huyo alisema kwamba hivyo wanaiomba jamii na Serikali kuwahamasisha vijana kuchangamkia fursa hiyo muhimu. Lengo likiwa ni kuwapatia vijana hao fursa za kuweza kunufaika na mradi wa kutengeneza pikipiki,baiskeli za umeme ambazo zinatumia betri na mota ya kawaida.

Akielezea kuhusu umuhimu wa vyombo hivyo ambavyo vinatumia umeme alisema ukipa hesabu lita moja ya mafuta ni 2700 unapata kilomita 30 mpaka 40 lakini ukichajisha kwa kutumia umeme ni unit mbili hata 1500 haifiki na unatembea kilomita 90 hivyo inapunguza gharama kwa madereva na inawapatia mtaji mkubwa.

Hata hivyo alisema pamoja na hayo hivi sasa wanaendelea na matengenezo ya Bajaji za umeme walianzia na baiskeli na wakaishia kwenye baiskeli za walemavu na mwakani wataelekea kwenye magari na center ndogo za kutumia umeme.

Awali akizungumza wakati wa mafunzo hayo ni Ruta Venance- ambaye ni mhitimu wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari Usagara alisema anashukuru kwamba amenufaika na mradi huo na ujuzi wakutosha alioupata anaweza kutengeneza mwenyewe.

Alisema alimua kutumia muda ambao alikuwa akisuburi kuingia kidato cha tano na sita amejua mfumo mzima wa kutengeneza pikipiki na wanawashauri vijana waliopo mtaani waende kupata mafunzo hayo ni mazuri

Naye kwa upande wake Mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya Sekondari Tanga Ufundi Saidi Kasim a,lisema kwamba mradi huo wa utengenezaji wa pikipiki za umeme yatamsaidia yeye na wenzake kuweza kupata ujuzi mbalimbali.

Aidha alishauri kwamba mafunzo hayo yawe endelevu ili waweze kupata ujuzi zaidi huku akiiomba serikali waweze kufadhili mafunzo hayo maana wakifanya hivyo watasaidia kupunguza vitu vingi vinavyoingia nchini kutokana na uwepo wa wataalamu ambao watakuwa na uwezo kuvitengeneza hapa nchini.

Mwisho.

MRADI WA BBT KATIKA CHUO CHA MLINGANO MATI MUHEZA KUWANUFAISHA VIJANA

May 16, 2023



Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Tanga Ramadhan Omary katika akipata maelezo mara baada ya kufika katika Chuo cha Mati Mlingano kushoto ni Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Tanga Theresia


vijana wanaonufaika na mradi wa BBT katika chuo cha Mlingano Mati Muheza wakimsikiliza Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Tanga Ramadhani Omary ambaye hayupo pichani


Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Tanga Ramadhani Omary katika akielekea shambani


MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga(UVCCM) Ramadhan Omary kulia akiwa na jembe akishiriki kulima na vijana kwa niaba ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Mohammed Kawaida wakati alipotembelea Chuo cha Kilimo (Mati Mlingano )ambacho ni Miongoni mwa Vituo vya Mradi wa jenga kesho yako iliyo bora (BBT).
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga(UVCCM)  Ramadhan  Omary kushoto akiangalia namba vitalu vya miche vilivyopandwa na vijana  kwa niaba ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa  Mohammed  Kawaida wakati alipotembelea Chuo cha Kilimo (Mati Mlingano )ambacho ni Miongoni mwa Vituo vya Mradi wa jenga kesho yako iliyo bora (BBT).


Na Oscar Assenga, MUHEZA 



MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga(UVCCM)  Ramadhan  Omary leo aliongoza  ziara ya kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Mkoa wa Tanga kwa Niaba ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa  Mohammed  Kawaida kutembelea Chuo cha Kilimo (Mati Mlingano )ambacho ni Miongoni mwa Vituo vya Mradi wa jenga kesho yako iliyo bora (BBT).

Katika Ziara hiyo iliyofanyika  aliwataka  Vijana kuitumia Fursa hiyo ya uwepo wa chuo hicho kwa manufaa yao binafsi na jamii inayowazunguka kwasababu serikali imetumia gharama kubwa kujenga kwaajili ajili ya kuwanufaisha na kuwaajiri Vijana kwenye sekta ya Kilimo,

"Mradi huu wa BBT ni moja kati ya miradi iliyotupa heshma kubwa vijana tuufanyeni kwa kwa ustadi na uwaminifu mkubwa"Alisema Omary 

Mwenyekiti hiyo alitumia fursa hiyo kuushauri Uongozi wa Chuo kuwa na utaratibu wa kutoa mafunzo kwa wakulima wa maeneo ya hayo na maeneo ya karibu kwa ajili ya kuwanufaisha wakulima wa Maeneo hayo na kuweza kukuza kilimo bora kwa jamii inayokuzunguka,

"Mkoa wetu unafursa nyingi za kilimo kaimu mkuu wa chuo angalieni namna chuo hiki kitaweza kuwanufaisha vijana/ jamii inayo wazunguka ili tuwe na kilimo chenye tija"Alisisitiza Omary 

Aidha katika hatua nyengine Omary aliwataka  Makada wa CCM na Vijana wa Chuo cha Mati Mlingano kwa niaba ya vijana wote wa Tanga kuwa namna pekee ya Kumlipa  Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt.Samia  kuyasema mazuri anayoyafanya na kuyatangaza mema anayoyafanya kwa Watanzania wote kiujumla kwani ameyafanya mengi kwa ajili ya Watanzania.


"Kwa kweli sisi kama vijana katika mkoa wa Tanga tunapongeza kazi kubwa inayofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu hivyo kama vijana lazima tuzitangaze kazi hizo tusiishie kusema mama anaupiga mwingi "Alisema Mwenyekiti huyo 

"Lakini pia tumuombe Mungu atujalie viongozi wengi mithili ya Bashe kwa sababu unamuona kabisa anaguswa na changamoto za vijana na jamii ya Kitanzania"Alisema 


Mwisho