WLAC WAENDELEA KULILIA SHERIA KANDAMIZI KWA WANAWAKE NA WAJANE

June 22, 2016
Mkurugenzi mtendaji wa WKAC Tanzania Bi THEODOSIA NUHULO akiizungumza na wanahabari leo Jijini Dar es salaam kuhusu maswala mbalimbali yanayohusu ukandamizwaji wa wanawake hususani wajane nchini Tanzania ikiwemo sheria kandamizi ya mirati ya kimila nchini sheria ambayo imetajwa kuwaumiza wajane wengi .PICHA ZOTE NA EXAUD MTEI MSAKA HABARI
Na Exaud Mtei

Serikali ya Tanzania imetakiwa kufanya marekebisho makubwa ya sheria ya mirathi ya kimila sheria ambayo imetajwa kuwa ni kandamizi na inawanyima haki wanawake na wasichana ikiwa ni utekelezaji wa mkataba wa CEDAW ambao nchi imesaini mwaka 1986 ambapo ulikuwa unawaelekeza wanachama kuondoa ubaguzi dhidi ya wanawake katika ngazi za kisiasa,kiuchumi,na kijamii ili kuletwa usawa.

Wito huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na kikosi kazi cha kamati ya mkataba wa kuondoa aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake CEDAW ambacho kinaundwa na mashirika tisa yanayotetea haki za wanawake Tanzania kwa namna mbalimbali.
Akizungumza kwa niaba ya mashirika hayo yote mkurugenzi mtendaji wa kituo cha msaada wa kisheria kwa wanawake WLAC ambao wameyaongoza mashirika hayo katika tamko hilo Bi Theodosia Nuhulo ameeleza kuwa mnamo mwaka 2005 WLAC  kwa kushirikana na wadau wengine watetezi wa haki za wanawake walifungua kesi mkakati katika mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Dar es salaam kupinga vipengele kandamizi katika sheria hiyo ya mirathi (Tamko la Mirathi la kimila) la mwaka 1963 lakini mnamo mwaka 2006 ilitupilia mbali kesi hiyo huku ikitamka wazi kuwa vifungu vilivyolalamikiwa ni vya kibaguzi kweli lakini haiwezi kufanya mabadiliko ya kimila katika tamko la kisheria.
Mkurugenzi wa umOja wa wajane nchi i Tanzania ROSE SARWAT akizngumza na wanahabari wakati Tanzania ikiingia kuadhimisha siku ya wajene nchini ambapo amewataka wajene na watanzania kujitokeza kwa wiingi kesho katika viwanja vya mnazi mmoja kuadhimisha siku hiyo ili kupata Fursa ya kujadili kwa pamoja kuhusu haki zao hususani sjheria hiyo kandamizi kwa wajane.
Ameeleza kuwa WLAC kwa kushirikiana na wadau mbalimbali walifanya jitihada zote za kukata Rufaa dhidi ya uamuzi huo lakini mnamo 2010 rufaa hiyo ilitupiliwa mbali tena kwa kigezo kwamba uamuzi na amri iliyotolewa na mahakama kuu ilikuwa na tarehe mbili Tofauti yani tarehe 8/9/2006 na tarehe 7/12/2006.
Amesema kuwa baada ya jitihada zote hizo kugonga mwamba juu ya sheria hiyo kandamizi ameeleza kuwa serikali ya Tanzania kuzingatia ukubwa wa swala hilo kufanya marekebisho ya haraka kwani ndio chanzo kikubwa cha wanawake wajane nchini Tanzania kushindwa kupata haki zao za msingi zikiwemo za mirathi baada ya vifo vya wenzi wao
Mkutano huo ukiendelea
Bi Theodosia ameendelea kusema kuwa pamoja na jitihada nyingi mbalimbali zinazofanywa na WLAC na wadau mbalimbali watetezi wa haki za wanawake bado serikali haijaonyesha jitihada za maksudi za kutekeleza Taarifa /maamuzi ya kamati ya mkataba wa CEDAW kuhusu sheria ya miradhi ya kimila na hali ya wajane Tanzania ili kuhakikisha kwamba wajane wanapata haki zao.
Aidha WLAC wameitaka serikali ya Tanzania kuwajengea uwezo majaji na waendesha mastaka na watumishi wa mahakama na wanasheria kuhusu mkataba wa CEDAW na umuhimu kwa kuzingatia haki za binadamu katika maamuzi yao.
Wanahabari mbalimbali wakisikiliza kwa makini-PICHA ZOTE NA EXAUD MTEI MSAKA HABARI WA HABARI24 BLOG
Pamoja na hayo WLAC wameitaka serikali kuchapisha taarifa hiyo ya kamati ya CEDAW na kutoa elimu kwa jamii ili kuondokana na mila potofu dhidi ya wanawake na kuwatendea haki badala ya kuwanyanyasa kwa namna mbalimbali.

Hata hivyo WLAC wameitaka serikali kutoa fidia ya kutosha kwa wajane waliohusika katika kesi mkakati kutokana na ukiukwaji mkubwa wa haki zap.

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS NA MCHUMI MKUU WA BENKI YA DUNIA MSTAAFU, AHUDHURIA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA BENKI KUU YA TANZANIA

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS NA MCHUMI MKUU WA BENKI YA DUNIA MSTAAFU, AHUDHURIA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA BENKI KUU YA TANZANIA

June 22, 2016

p1 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na aliyekuwa Makamu wa Rais na Mchumi Mkuu wa Benki ya Dunia Profesa Justin Yifu Lin aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016
p2 p3 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa katima mazungumzo na aliyekuwa Makamu wa Rais na Mchumi Mkuu wa Benki ya Dunia Profesa Justin Yifu Lin aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016. Kushoto ni Balozi wa China nchini Dkt. Dkt. LU Younqing,
p4 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana  na Balozo wa China nchini Dkt Lu Younqing baada ya kuwa na mazungumzo na aliyekuwa Makamu wa Rais na Mchumi Mkuu wa Benki ya Dunia Profesa Justin Yifu Lin aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016. Kushoto ni Katibu Mkuu Wizarta ya Viwanda na Biashara Dkt. Adelhem James Meru na Kulia ni Mkurugenzi Idara ya Asia katika Wizara ya Mambo ya Nje Bw. Mbelwa kairuki.
p5 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na katibu Mkuu Wizara ya fedha na Mipango Dkt Servacius Likwelile alipowasili kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016
p6 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisimama kwa ukakamavu wakati wimbo wa Taifa ukipigwa akiwa na  Mkuu Wizara ya fedha na Mipango Dkt Servacius Likwelile, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndullu, na Mkuu wa Mkoa wa Dar e3s salaam Mhe Paul Makonda  kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016
p14 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia wakati wa  maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016
p13
p7 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akibofya kitufe kuashiria uzi8nduzi rasmi wa  maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016
p8
p9 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akizindua sarafu maalumu ya shilingi 50,000/- kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016
p10 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akizindua Kitabu kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016
p11 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akizindua Kitabu kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016
p12  
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akatika picha ya pamoja na Magavana na Manaibu Magavana na menejimenti ya BOT kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016
KAMISHNA MSTAAFU SULEIMAN KOVA AAGWA RASMI KIJESHI BAADA YA KUSTAAFU

KAMISHNA MSTAAFU SULEIMAN KOVA AAGWA RASMI KIJESHI BAADA YA KUSTAAFU

June 22, 2016

KOV1 
Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova akipunga mkono kwa Maofisa, wakaguzi, Askari na wageni mbalimbali waliohudhururia sherehe za kumuaga rasmi Jeshini baada ya kustaafu utumishi zilizoongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki katika Chuo cha Polisi Moshi (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
KOV2 
Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova akikagua gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili yake wakati wa  sherehe za kumuaga rasmi Jeshini baada ya kustaafu utumishi zilizoongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki katika Chuo cha Polisi Moshi (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
KOV3 
Maofisa wa Polisi wakisukuma gari maalumu lililombeba Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi Suleiman Kova kutoka katika viwanja vya Chuo cha Polisi Moshi wakati wa  sherehe za kumuaga rasmi Jeshini baada ya kustaafu utumishi zilizoongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki. (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
KOV4 
Gari maalumu lililombeba Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi Suleiman Kova likipita katika ya gwaride ikiwa ni ishara ya kumuaga zilizofanyika katika Chuo cha Polisi Moshi nakuongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
KOV5 
Gwaride Maalumu la Kumuaga Kamishna Mstaafu Suleiman Kova likipita mbele yake kwa mwendo wa haraka wakati wa Sherehe za kumuaga rasmi baada ya kustaafu utumishi.Sherehe hizo zilifanyika katika chuo cha Polisi Moshi (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
KOV6 
Gwaride Maalumu la Kumuaga Kamishna Mstaafu Suleiman Kova likipita mbele yake kwa mwendo wa haraka wakati wa Sherehe za kumuaga rasmi baada ya kustaafu utumishi.Sherehe hizo zilifanyika katika chuo cha Polisi Moshi (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)

PROF. MBARAWA AZINDUA MKUTANO WA19 WA SADC WA KAMATI YA USAFIRI WA ANGA

June 22, 2016

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea wakati wa uzinduzi wa mkutano 19 wa SADC wa kamati za usafiri wa Anga uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.wapili kushoto ni mwakilishi wa SADC ICAO Raphael Bokango, Mwenyekiti wa SADC kamati ya usafiri wa Anga Geoffrey Moshabesha na Mkurungenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari (Kulia).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamalaka ya usafiri wa Anga Tanzania Hamza Johari akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa mkutano 19 wa SADC wa kamati za usafiri wa Anga uliofanyika kwenye ukumbi waKimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Mwenyekiti wa SADC kamati ya usafiri wa Anga Geoffrey Moshabesha na mwakilishi wa SADC ICAO Raphael.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Kushoto) akisalimiana na Mkurungenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari (Kulia) mara baada ya kuzinduzua mkutano 19 wa SADC wa kamati za usafiri wa Anga uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.wapili kushoto ni mwakilishi wa SADC ICAO Raphael Bokango, Mwenyekiti wa SADC kamati ya usafiri wa Anga Geoffrey Moshabesha.
Baadhi ya wajumbe wa wakiwa kwenye mkutano 19 wa SADC wa kamati za usafiri wa Anga uliofanyika kwenye ukumbi waKimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo. Uliozinduliwa na i Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa.